Wednesday, August 28, 2013
Tuesday, August 27, 2013
TAHADHARI KWA WATUMIAJI WA KOMPYUTA ZENYE WINDOW XP
Watumiaji wa programu ya komputa iitwayo Window XP wamepewa tahadhari na kampuni ya Microsoft ambayo ndiyo iliyotengeneza program hiyo kuwa hapatakuwa na matoleo mapya (updates) zaidi kuhusu Window XP Service Pack 3 baada ya mwezi wa nane mwaka 2014.
Akizungumza na wataalamu mbalimbali wa masuala ya ulinzi mtandao Agosti 16,mwaka huu Mkurugenzi wa kitengo kijulikanacho kwa jina la Microsoft Trustworthy Computing,Tim Rains anasema kuwa ingawa Window XP wakati inatolewa ilikuwa na ubora huku ikipendwa na watumiaji wengi wa kompyuta,kwa sasa imeonekana kuwa dhaifu kutokana na kuongezeka kwa uhalifu wa kimtandao.
Amesema kumekuwepo na wimbi kubwa la wahalifu wanaotumia mianya mbalimbali kuingilia kompyuta za wateja wanaotumia Window XP na kuongeza kuwa hali hiyo ya uhalifu itaendelea hasa kwa wale wataoendelea kutumia aina hiyo ya window.
Rains amesema wanaendelea kutafuta ufumbuzi pale itakapobainika wahalifu wameweza kupenya katika kompyuta za wateja wao wanaotumia aina mpya za window ambapo kwa sasa kupitia kituo cha kuangalia usalama wa kompyuta cha kampuni hiyo kinaendelea kutoa maelezo ya jinsi ya kuwalinda wateja wao.
Amesema kampuni ambazo bado zitakuwa zinatumia Window XP,zitasababisha wahalifu kutafuta mapungufu katika window hiyo na kuleta athari ambapo kampuni ya Microsoft haitakuwa na msaada ama wa bure au wa kulipia dhidi ya hali hiyo,kwani itakuwa imeshaacha kutoa msaada wa kuhusu Window XP
Chanzo:Gazeti la Mwananchi
Sunday, August 25, 2013
Saturday, August 24, 2013
WASHA YA TEKNOHAMA NA VYOMBO VYA HABARI YAFANYIKA COSTECH JIJINI DAR ES SALAAM
Mwezeshaji wa kipindi cha Maisha na Teknohama cha Morning Star Radio,Johnson Mziray akichangia jambo kwenye warsha hiyo,pembeni yake mwenye miwani ni Mtangazaji wa Kipindi cha Maisha na Teknohama,Mtangazaji Maduhu |
Sama toka Kampuni ya E Media akifundisha jinsi ya kupiga picha za Video |
Saturday, August 17, 2013
TWITTER YAONESHA KUWAVUTIA VIJANA
Facebook ni mtandao wa kijamii ambao unaendelea kuongoza kwa kuwa na watumiaji wengi duniani hata hiyo utafiti unaonesha kuwa vijana sasa wanahama kutoka mtandao huo na kujiunga na mtandao wa kijamii wa Twitter .
Kuna mamia ya watu ambao haiwezi kupita siku bila kutembelea facebook,lakini sasa inaonekana twitter ikipata watumiaji kutoka facebook hasa ikiwavutia zaidi vijana ambao wengi wao wanatumia facebook.
Twitter inaruhusu mtumiaji kufahamu kile ambacho hadhira katika mtandao huo inakizunguzia na kuruhusu kufahamu kinachoendelea na kumpatia anachokihitaji.
Mtandao wa solidtechreview umeeleza kuwa mwishoni mwa mwaka 2012, inakadiliwa kuwa asilimia 21 ya watumiaji wa intaneti duniani walikuwa walikuwa wamejiunga na twitter na kila mwezi kulikuwa na watu milioni 288 waliokuwa wanajiunga na mtandao huo.
Utafiti unaonesha kuwa facebook ina asilimia 34 ya watumiaji ambao umri wao ni chini ya miaka 30 na asilimia 45 zaidi ya miaka 45. Wakati ni asilimia 30 tu ya watumiaji wa twitter ambao wanaumri zaidi ya miaka 45.
Twitter inaelezwa kuwa ni rahisi kutumiwa na watu ambao hawana muda mwingi wa kukaa na kuandika mambo mengi kwenye mitandao ya kijamii,rahisi kukuunganisha na watu wengi maarufu duniani, rahisi kuwasilianana kubadilishana mawazo mbalimbali kuliko facebook.
GOOGLE YAANZISHA HUDUMA YA KUKUPATIA RATIBA YA USAFIRI WA NDEGE
Kampuni ya Google kupitia huduma yake ya kutafuta jambo sasa imeanzisha utaratibu wa kutoa majibu ya moja kwa moja kwa maswali kuhusu ratiba ya ndege unayotaka kuitumia kwa kusafiri.
Huduma hiyo ambayo mtumiaji anaweza kuuliza swali na akapata jibu kwa mfano Je ndege yangu ni ya hadhi gani moja moja google itakuonyesha juu ya ukurasa ndege unayohitaji kusafiri nayo.
Google inaeleza kuwa kipengele hiki kinatoa majibu ya haraka kwa mtumiaji kuliko kusoma ujumbe wa barua pepe ama kalenda.
Huduma hii ilianza huko Marekani kwa ajili ya kuweka booking ya ndege ama hoteli kwa kutumia sauti ama kwa kuandika.Hata hivyokipengele hiki kimeelezwa kuwa si vyema kukitumia kwa watu ambao wanahitaji faragha katika mambo yao.
Huduma hii ilianza huko Marekani kwa ajili ya kuweka booking ya ndege ama hoteli kwa kutumia sauti ama kwa kuandika.Hata hivyokipengele hiki kimeelezwa kuwa si vyema kukitumia kwa watu ambao wanahitaji faragha katika mambo yao.
Friday, August 16, 2013
JINSI YA KUONDOA UJUMBE USIOKUHUSU KWENYE WASIFU WAKO WA FACEBOOOK
Je, Unasumbuliwa na MESSAGE
usizozitaka kuziona, hususani toka kwa watu usiowajua ?
Nenda sehemu ya Settings, kisha chagua kuwa Unataka kupokea message za Walio FRIENDS zako tuu.
Message nyingine zote zitaingia kama SPAM, hivyo hazitokuja INBOX yako. Zitapelekwa kwa Folder maalum la SPAM, ni mpaka ulitafute hilo folder la Spam ndio utaziona message nyingine kama hizo za kukusumbua.
Kama unataka kuangalia Messages ambazo zimeingizwa kwenye folder la SPAM,
unachotakiwa kufanya ni kuenda sehemu ya MESSAGE (Kushoto mwa profile
yako), kisha bofya hapo juu kama unavyoona kwenye kielelezo hapa chini
Unaweza kufanya hivi, kwani pengine kuna mtu muhimu ambaye si rafiki yako
amekutumia ujumbe ambao ungependa kuusoma. -
chanzo:Mbuke blog
TAHADHARI:USITUMIE SIMU YAKO IKIWA KWENYE CHARGER
Ma Ailun, mdada mwenye miaka 23 alikuwa akitumia iPhone5, na mara baada ya kifo chake dada yake aliamua kuwapa onyo watumiaji wengine wa iPhone kuhusu hilo tatizo kupitia weibo ambayo ndio kama twitter ya China na baada ya habari kusambaa Apple ambao ndio watengenezaji wa iPhone walitoa pole kwa familia na kuahidi kufuatilia tatizo lilikuwa nini, mwanzoni msemaji wa Apple alisema alisema inawezekana charger iliyotumika ilikuwa feki lakini ikathibitika kuwa simu ilinunuliwa kwa wakala aliethibitishwa na ilikuwa haina muda mrefu.
Chanzo:tanganyikan blog
Friday, August 9, 2013
SONY NA PANASONIC WAUNGANA KUTEGENEZA CD YENYE UWEZO WA HIFADHI YA GB 300.
Na Brown Nyanza
Kampuni mbili maarufu duniani SONY
Corporation na PANASONIC Corporation kupitia tovuti zao wametangaza kuwa wameingia
katika makubaliano ya kutengeneza CD (compact disk/Optical Disc) zenye uwezo wa
kuhifadhi GB 300 za data ifikapo mwaka 2015.
Kampuni
zote mbili zimeongeza kwa kusema kwamba hii itakuwa ni mara ya kwanza katika
historia ya CD duniani. Katika miaka ya karibuni CD zimesifika kuwa na uwezo wa
kuhifadhi data kwa ulizi wa hali ya juu, hii ni kutokana uwezo mkubwa wa
kuhimili mabadiliko mbalimbali ya kimazingira,
vumbi, joto, na pia CD inaweza kuhifadhi data kwa kipindi kirefu sana iwapo
ikihifadhiwa sehemu nzuri.
Kampuni
hizo zimekaririwa kwa kusema kwamba wateja wao hasa wamelengwa kuwa makampuni
makubwa ya kutengeneza filamu nchini marekani na duniani kote, Pia makampuni
makubwa ya utangazaji, Pia (Cloud based Data centes) zinatarajiwa kuwa ndio
soko kubwa katika teknolojia hii mpya ya kuhifadhi data. Katika miaka ya
karibuni Kampuni ya SONY ilitengeneza
CD zenye zinazotumia teknolojia ya BluRay zenye uwezo wa kutunza data kwa kiasi
cha GB 25 hadi GB 50 katika CD moja
tu.
HUAWEI YAIPATIA NM-AIST DOLA 30,000 ZA MAREKANI
Kampuni ya Huawei ya Tanzania imesaini makubaliano na Chuo cha Sayansi na Teknolojia cha Nelson Mandela (NM-AIST) kuhusu kukijengea chuo hicho uwezo zaidi wa kufanya tafiti katika masuala ya teknolojia ya habari na mawasiliano (TEKNOHAMA).
Katika makubaliano hayo,kampuni itakuwa ikitoa Dola 30,000 za Marekani kila mwaka ndani ya miaka mitatu,ili kusaidia chuo nyanja hiyo na hasa kwa wanachuo wa ngazi za uzamili na uzamifu.
Balozi wa China nchini Tanzania,Lu Youqing amesema moja ya mahitaji ya vyuo vinavyofanya tafiti duniani ni kupata vitendea kazi na wataalamu waliobobea.
Katika makubaliano hayo,kampuni itakuwa ikitoa Dola 30,000 za Marekani kila mwaka ndani ya miaka mitatu,ili kusaidia chuo nyanja hiyo na hasa kwa wanachuo wa ngazi za uzamili na uzamifu.
Balozi wa China nchini Tanzania,Lu Youqing amesema moja ya mahitaji ya vyuo vinavyofanya tafiti duniani ni kupata vitendea kazi na wataalamu waliobobea.
Wednesday, August 7, 2013
MWENYEKITI WA MAKAMPUNI YA IPP,DR REGINALD MENGI AWAPONGEZA WASHINDI WA TWEET YA JULAI 2013
Dr
Reginald Mengi amewapongeza washindi wa tweet bora ya julai 2013 ambao
aliwakabidhi zawadi ofisi kwake jijini Dar es salaam jana ambapo
miongoni mwa waliopata zawadi ni mshindi wa tatu ambaye ni mtangazaji wa
kipindi cha Maisha na Teknohama cha Morning Star Radio ambaye alijibu
swali lililoulizwa na Dr Mengi kupitia twitter ambalo liliuliza "Kijana
asiyekuwa na ajira wala fedha anawezaje kuanza kujijenga kiuchumi?Ambapo
jumla ya tweet 1225 zilizojibu swali hilo mwezi julai.
Dr
Mengi amekuwa akiuliza swali la uchumi kupitia twitter toka mwezi mei
mwaka 2013 na kuchagua tweet tatu zinazojibu swali na kutoa zawadi ikiwa
ni njia ya kuibua mawazo mapya katika kuondoa umaskini nchini Tanzania
Swali la tweet bora Agusti 2013 ni: Je, Nini kifanywe kuzalisha ajira nyingi kwa vijana hapa Tanzania?