Monday, November 18, 2013

GOOGLE NA MICROSOFT KUDHIBITI PICHA ZA KUDHALILISHA WATOTO



Kampuni za Google na Microsoft zinazoongoza duniani kwa mitandao yao kutumika kutafuta taarifa mbalimbali zimekubaliana kuchukua hatua za kuhakikisha inakuwa vigumu kupata picha zinazowadhalilisha watoto katika mitandao.

Maombi kufikia 100,000 yakitafuta picha hizo, hayatapata matokeo yoyote ya utafutaji picha za kudhalilisha watoto na taarifa nyingine zilizo kinyume cha sheria.

Waziri mkuu wa Uingereza David Cameron, ambaye alitoa wito kwa kampuni hizo kuchukua hatua za kuwanusuru watoto kutokana na udhalilishaji huu, amepongeza hatua hiyo.

Lakini ameonya kuwa lazima hatua hiyo itoe matokeo mazuri, vinginevyo ataleta sheria mpya ya kuyabana makampuni hayo ya mawasiliano.

Mwezi Julai, 2013, Bwana Cameron alizitaka kampuni za Google na Microsoft ambazo kwa pamoja zinachangia asilimia 95% ya utafutaji wa taarifa mbalimbali kwa njia ya mtandao, kuchukua hatua zaidi ili kuzuia watu kupata picha mbaya.

Alisema kwamba wlitakiwa kuhakikisha kuwa maombi yanayotumwa kutafuta taarifa ambazo zinalenga kupata picha chafu, yasitoe majibu yoyote.

Kwa sasa kampuni zote mbili zimeanzisha "programu mpya ya kompyuta" ambayo itazuia utafutaji wa picha zinazowadhalilisha watoto.

Akiandika katika gazeti la Uingereza la Daily Mail, mwenyekiti mtendaji wa Google Eric Schmidt amesema: "Mabadiliko haya yameondoa maombi zaidi ya 100,000 ambayo huenda yalihusishwa na udhalilishaji wa watoto.

"Likiwa jambo muhimu, hivi karibuni tutaweka mabadiliko haya katika zaidi ya lugha 150, hivyo matokeo ya hatua hii kuwa ya dunia nzima."

Ameendelea kueleza kazi ya kuzuia picha za udhalilishaji watoto, kwa kusema:"Sasa tunaonyesha - kutoka mtandao wa Google na mengine, juu ya chumba cha kutolea maombi ya kutafuta taarifa mbalimbali kwa maombi zaidi ya 13,000.

"Maonyo haya yanaonyesha wazi kwamba udhalilishaji wa watoto ni kinyume cha sheria na kutoa ushauri wa mahali pa msaada."

Jumahili, kampuni mbili hizo za Google na Microsoft zitaungana na kampuni nyingine za internet katika ofisi za waziri mkuu wa Uingereza zilizopo Downing Street, kwa ajili ya Kikao cha Usalama wa Internet.
chanzo:BBC

Popular Posts

Labels