Siku hizi, katika kila watu kumi wanaotumia mtandao, basi angalau watano kati ya hao wanatumia mitandao jamii. Kuna baadhi ya watu wamegeuza mitandao hii kuwa kama ni sehemu ya mawasiliano, ama ya mtu kwa mtu au ya kibiashara. Siku hizi, si kitu cha kushangaza kusikia mtu maarufu au kiongozi fulani atakuwa kwenye Facebook saa fulani kwa ajili ya kujibu maswali ya wananchi / mashabiki wake. Mitandao hii ni kama vile Facebook, Twitter, Jamiiforums nk, hivyo basi, hatuwezi kuepuka ushawishi wa mitandao jamii katika jamii yetu.
Matumizi bora ya mitandao jamii huweza kuleta faida nzuri
sana, ila huwa kinyume pale inapotumika sivyo, ama kwa kutokujua ama kwa
kuamua. Hivyo leo hii tuangalie mambo kadhaa ya kuepuka unapotumia mitandao
jamii.
1. EPUKA KUJIACHA WAZI KWENYE MITANDAO JAMII.
Kuna baadhi ya watu wamegeuza mitandao jamii ni dunia yao
nyingine kabisa, wao kila kitu wanachokifanya utakiona kwenye mitandao jamii,
kala nini, anamchumbia nani, kavaa nguo gani nk. Mitandao jamii ni uigaji (Simulation) ya
maisha ya halisi.Tukiwa kwenye maisha halisi, sio watu wote wanaoweza kujua
maisha yako kwa undani,kwani kuna vikomo, kuanzia wale mulio nyumba moja,
munaofanya kazi pamoja nk.
Ingawa kwenye mitandao jamii wengi wanaweza kuchunga kwa
kutumia michungo ya ufaragha (Privacy setting) lakini si wote
wanaojua hilo, pia tumeona mamia ya akaunti za watu zikivamiwa na wavamizi wa
mtandao (Hackers) na kuweka hadharani taarifa zao nyingi. Hivyo epuka kuweza
kila kitu kwenye mitandao jamii, kula na kikomo na pia anza kuchunga marafiki
zako juu ya nani anaweza kuona nini. Unaweza kuangalia Video HAPA jinsi
ya kuchunga ufaragha kwenye Facebook.
2.
JICHUNGE KWENYE UTUMAJI.
Je ushawahi kusikia mtaani wanasema jamaa ana gubu (anaongea
sana?), kwenye mitandao jamii pia kuna watu wana gubu, wanachonga sanasana.
Hawa ni wale watu ambao kila dakika wametuma kitu kipya, hii sio tu hufanya
kupoteza mvuto kwa wanaokufuatilia, bali pia umuhimu wa makala zako hupungua.
Binafsi huondoa watu aina hii kwenye mlisho wa maboresho (activities
feeds) bila hata kujiuliza.
Hivyo, ili kuepuka kutengwa au kuonekana unachonga sana,
chunga idadi ya maboresho unayotuma kwa siku.
3.EPUKA KUTUMA MAKALA ZA NGONO, DINI AU SIASA KAMA WEWE SI
MUHUSIKA.
Hivi ni vitu ambavyo huathiri watu wengi sana, chukulia
mfano wewe ni rafiki wa bwana X, unafungua Facebook au Twitter yako unakutana
na picha ya ngono imejaa kwenye mlisho wa maboresho toka kwa rafiki yako.
Ukweli ni kuwa utajisikia vibaya mno ama kama na wewe ni wa aina hiyo. Hii
pia ni sawa na kwa mambo ya dini na siasa.
Tanzania ikiwa ni nchi isiyo na dini, ila watu wake
wamechanganyika mnomno, kwenye kila marafiki zako wawili, kuna mmoja ni wa dini
nyingine, hivyo epuka kutuma makala za dini zinazoudhi, zenye kebehi au kuudhi
wengine. Jaribu kuwa mtu ambaye utaweza kuishi na watu wote. Mfano huu pia
tuuchukue kule uraiani, kuna baadhi ya watu hukimbiwa, hivyo chukua tahadhari
kabla ya kukimbiwa.
Kuna baadhi ya watu, wakishauziwa nyumbani, hasira zinaishia
kwnye mitandao jamii,amini usiamini, mitandao jamii haiwezi kukusaidia kutuliza
hasira zako zaidi ya kukupotezea muda na kujidhalilisha. Ni sawa na yule mtu
mwenye ugomvi na mke / mume wake halafu anapita kila nyumba kutangazia
mapungufu ya mwenza wake, jamii nzima inajua, siku mutakaporudiana, watu wote
washajua mapungufu ya mwenza wako, je utafuta toka kwenye vichwa vyao? Kwenye
mitandao jamii vilevile, kuna baadhi ya watu kuhifadhi kila unachotuma na siku
ya siku watatumia kuja kukashambulia. Kaa mbali na mitandao jamii kama unaona
hauwezi kuchunga mhemuko (emotion) wako.
5.SIYO KILA MTU LAZIMA AWE RAFIKI YAKO.
Chukulia mfano mitaani tunamoishi, kuna watu wa aina
mbalimbali, na siyo kila mtu ni rafiki yako, kuna baadhi ya watu hata hautaki
kuwasogelea kutokana na tabia zao, hii ni sawa kwenye mitandao jamii. Epuka
kukubali maombi ya urafiki toka kwa kila mtu, haswaa ambao hauwafahamu.
Marafiki sio tu huweza kutumika kujenga taswira yako, bali kuna baadhi ya
marafiki si marafiki, hivyo chunga marafiki zako la sivyo ipo siku utakuja
kujuta.
6 . UHIFADHI WA HISTORIA
Uhifadhi wa historia - Ni vizuri kujua kila unachofanya kwenye
mitandao ya kijamii haswa kutumia account yako kama ni email au nini
kinahifadhiwa sehemu , kama umekashifu mtu , kama umejiunga kwenye
vikundi vya kiharamia au kama umetafuta kitu kinachohusiana na ugaidi au
kutengeneza mabomu yote hii huwa inahifadhiwa usishangae siku moja
ukagongewa mlango kuonyeshwa kile ulichokuwa unafanya na rumande moja
kwa moja .
7.KUJIUNGA KWENYE VIKUNDI AU UKURASA
Kuna
watu wanapenda kulike kurasa za facebook za watu , vikundi na nyingine
nyingi bila kufuatilia vizuri , unaweza kulike leo kwa nia nzuri tu kwa
sababu ana habari nzuri baada ya siku kadhaa kupata watu wengi mtu huyu
au kikundi kinaweza kuanza kuweka mambo yake yaliyojificha na inaweza
kukuweka katika nafasi mbaya kama ni katika familia , kazini , utumishi
wa umma au sehemu za harakati ingawa una uhuru wa kuchagua .
8 - KUHUSU TABIA ZA MTU
Kutumia mitandao
ya kijamii kama facebook na myingine unaweza kujua tabia za mtu , vile
anavyopenda , rafiki zake , wanafamilia wake , mke wake , mume , watoto ,
wafanyakazi wenzake na tabia nyingine za ajabu au nzuri na vile vile
kwenye tekinologia ya mawasiliano siku hizi kuna mfumo wa tabia za watu
kujulikana - kile ambacho unapenda kutafuta au kuongelea ndicho
utakachokuta kwenye email yako kama tangazo au kurasa yako ya facebook
kama TAG
Hayo ni mambo muhimu kwa ajili ya afya ya utumiaji wa
mitandao jamii, usisahau kulike Kurasa yetu ya Facebook kwa makala mbalimbali
za IT kila wiki https://www.facebook.com/dudumizi
Imeandikwa na Yona Msuya toka tovuti ya dudumizi na Yona Maro wa wanabidii forum