Saturday, December 28, 2013

NAMNA YA KUWEKA ULINZI WA KUKIFUATILIA KIFAA CHAKO CHA MAWASILIANO CHA APPLE KILICHOPOTEA

Umepoteza  iPhone ama kifaa chochote cha mawasiliano cha  Apple iOS? Kabla yakutoa taarifa kwa vyombo vya usalama ama kufanya lolote unapaswa ufuate hatua za kiulinzi ambazo zimewekwa na Apple ili kukusaidia kufahamu iPhone, iPad na iPod iliyopotea.

 iPhone 5S iliyotoka mwaka huu imetengenezwa mfumo wa kiusalama wa utambuzi wa alama za vidole,inahitaji kidole cha mmiliki kufungua simu,mfumo huu unasaidia kuzuia mwizi kuifungua simu ili kuitumia,simu hiyo pamoja na vifaa vingine vya mawasiliano vya Apple vinapopotea waweza kufahamu vilipo kwa kufuata hatua zifuatazo

Hatua # 1 – Seti na uactivate “Find My iPhone” katika kifaa chako

Hatua hii inahitajika uifanye mara unaponunua kifaa chako iwe ni Iphone,Ipad n.k.
Hakikisha umepada ID yako ya Apple ambayo inahusiana na kitambulisho cha kifaa ulichokinunua,ID ambayo pia itakusaidia wakati wa matumizi katika iCloud na upakuaji wa program tumishi toka Apple.
Nenda Settings ==> iCloud ==> angalia kama “Find My App” iko ON


iphone_find_my_iphone


 ipad_find_my_iphone

Utakapoweka ON “Find My iPhone” kama kifaa chako kitaibwa ama kupotea kitakusaidia kukutafuta na kufahamu kilipo .

Hatua #2 – Jiunge na  iCloud.com kwa kutumia  Apple ID yako

Unaweza kukitafuta na kukipata kifaa chako kilipo kwa kutumia iCloud.com iwapo utakuwa umefanya setting ya kwanza ya hatua ya kwanza kwa kufungua tovuti hiyo kwenye komputa yako na kuingia kwa kutumia Apple ID ile uliyosajili kifaa chako.Inakubali katika komputa za Window na Mac


 sign_in_icloud

Hatua   #3 –Fungua “Find My iPhone” na chagua palipoandikwa Device to Track

Bofya kwenye alama ya  “Find My iPhone” katika ukurasa wa  iCloud.com


 icloud_find_my_iphone

Hatua # 4 – Tafuta eneo kilipo kifaa chako. Kama ni eneo la karibu na ulipokipoteza ama ni ofisini,nyumbani n.k bofya palipoandikwa "play sound to find"

Chagua picha ya miongoni mwa kifaa kilichopotea Iphone,iPad n.k mahali palipoandikwa  “My Devices”. Baada ya kuchagua hapo, itaonekana ramani ya mahali kifaa kilipo ama muda wa mwisho kifaa hicho kilipokuwa.
icloud_select_device

Hatua # 5 – Ruhusu “Lost Mode”. Subiri mlio wa simu na endelea kuifuatilia ilipo

Baada ya kuchagua  “Find My iPhone”  program tumishi kwenye  iCloud itakuonesha mwongozo mwingine wa hatua zifuatazo,
# Play Sound – Hapa kifaa kitaanza kitatoa mlio na kama umepoteza nyumbani,ofisini n.k utausikia mlio
# Lost Mode –Kama unauhakika kuwa umeisahau simu yako ya iphone mahali utakaoruhusu hatua hii itumike itakuomba uweke namba ya simu ambapo watu watakupata,ama unaweza kuweka sentensi ama kuacha vivyo hivyo na kubofya "Done" na ujumbe utatokea kwenye simu yako iliyopotea hata kama umeifunga na utasomeka "Hii Iphone imepotea tafadhari nipigie "Namba yako"
# Erase iPhone – Hatua ya mwisho.Kwa kutumia iCloud na Find My iPhone unaweza kufuta ama kuondoa taarifa zako katika kifaa chako kilichoibwa ambapo utaondoa email zako,program tumishi ulizoweka n.k Kumbuka hatua hizi zote zinahitaji upatikanaji wa intaneti




TFF KUANZA KUTUMIA TEKETI ZA ELEKTRONIKI

 
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) litaanza kutumia tiketi za elektroniki kwenye uwanja wa Azam uliopo Chamazi,Dar es salaam wakati wa mechi za Ligi Kuu za Ashanti United na JKT Ruvu  zitakazopambana Januari Mosi 2014, kati moja ya mechi za kujaribio ya  matumizi ya mfumo huo nchini Tanzania.


Taarifa ya TFF kwa vyombo vya habari imeleza kuwa
Viingilio katika mechi hiyo itakayoanza saa 10 kamili jioni ni sh. 1,000 na sh. 2,000 ambapo tiketi zinapatikana kupitia M-Pesa na mawakala wa CRDB Fahari Huduma. Tiketi zitaendelea kuuzwa hadi kipindi cha kwanza cha mechi hiyo kitakapomalizika.


Mawakala 18 wa Fahari Huduma wanaouza tiketi hizo ni ABC Computer- Mtaa wa Samora, Abraham Anangisye Mwampetele- Maji Matitu, Apex Security Services- Mtaa wa Mibega, Kinyerezi, Athuman Fakhi Adam- Kongowe Mbagala, Fedha Investment Limited- Pamba Road na Fuya Godwin Kimbita- Tegeta Block.


Ghomme Health & Education Limited-Bahari Beach, Herman Arbogast Tarimo- Kigamboni, K- Finance Limited- Shekilango, Sinza, Koli Finance Limited- Mtaa wa Samora, LB Pharmacy- Mtoni Kijichi, Lista Phares Barnabas- Tabata Segerea na Maly Investment Company Limited- Mtaa wa Sikukuu, Kariakoo.


Wengine ni Micu Enterprises- Mtaa wa Congo, Kariakoo, S&D Collection Company Limited- Mikocheni, Shoppers Plaza, Therry Investment Limited- Tegeta Kibaoni, TSHS Distributors Limited- Mtoni kwa Aziz Ali na Wemerick Independent Vehicle- Mtaa wa Boko.


Pia mshabiki anaweza kununua tiketi kwa njia ya simu- mtandao wa Vodacom kwa kupiga *150*03*02# ambapo atapata namba atakayoitumia kufanya malipo kupitia MPESA. Katika MPESA namba ya malipo kwa TFF ambayo ndiyo mshabiki ataitumia kufanya malipo ya tiketi (business number) ni 888800. Vilevile mteja wa CRDB aliye katika mtandao anaweza kufanya malipo kupitia CRDB simbanking.


Baada ya kufanya maombi kupitia njia yoyote ya hizo tatu; MPESA, Fahari Huduma na CRDB simbanking, mshabiki atapata namba ambayo ataitumia ku-print tiketi yake kupitia mashine maalumu za kuchapia Tiketi ya TFF zilizo katika ATM za CRDB kwenye maeneo yafuatayo;


Benki ya CRDB tawi la Azikiwe, tawi la Holland House ambapo kuna mashine mbili, tawi la Vijana, tawi la Kariakoo, ATM ya Mtaa wa Shaurimoyo ambapo kuna mashine mbili na ATM ya CRDB iliyoko kituo cha mafuta cha Kobil Sabasaba, Mtoni kwa Aziz Ali.

HACKER NI NINI?

 
KAMA HAUKUJUA BASI JUA
Na MBUKE TIMES
Neno HACKER makusudio yake haswa sio kumaanisha mtu anayefanya vitendo vya kihalifu kwa kutumia kompyuta, yaani kama vile kuiba password za watu, kusoma emails za watu n.k. Bali neno HACKER kiasili lina maana ya mtu mwenye uwezo wa kipekee wa kutafuta suluhu ya tatizo kwa haraka, kwa mbinu za ubunifu ambazo pengine si mbinu rasmi, ila zinaleta suluhu ya haraka.

--Hata hivyo kwakuwa HACKER ana ujuzi wa hali ya juu wa matumizi ya kompyuta na ni mtundu, basi wapo Hackers walioamua kutumia ujuzi huo kufanya uhalifu, na ndipo jina lilipoharibika.

--Hata hivyo jamii ya hackers na wanateknolojia wengi wameendelea kuelimisha matumizi sahihi ya jina HACKER na neno HACKING. Mifano ya wazi ni :-
1. Facebook: Kuta za ofisi za FB zimeandikwa neno HACK. Kusisitiza umuhimu wa kuandika codes kwa haraka na kutafuta kwa ubunifu na kwa haraka suluhu ya matatizo.
Hata mfumo mzima wa uendeshaji wa FB umepewa jina THE HACKER WAY.

2. Makampuni mengi yamekuwa yakiandaa mikutano ya siku moja au zaidi kwa ajili ya kukutanisha HACKERS ili kubuni bidhaa na kutatua matatizo mbalimbali. Mikutano hiyo huitwa HACKATHONS
-- Kwa maelezo zaidi search Google maneno HACKER, FACEBOOK THE HACK WAY na HACKATHONS.

UTAFITI:FACEBOOK YAKIMBIWA NA VIJANA HUKO UINGEREZA




Utafiti unaonesha kuwa Vijana kati ya miaka 16-18 nchini Uingereza wanaonekana kutovutiwa na mtandao wa kijamii wa facebook  kutokana na kukerwa na mtandao huo. 

Tovuti ya yahoo imesema kuwa Vijana hao sasa wameonekana kuvutiwa  Zaidi na mitadao ya kijamii mingine ambayo ni  Twitter, Instagram, Snapchat  na WhatsApp.

Profesa Daniel Miller kutoka Chuo Kikuu cha London ambaye alisaidia kufanya utafiti kuhusu jambo hilo amesema wakati ambapo wazazi wamekuwa na wasiwasi kuhusu watoto wao kujiunga na face book lakini watoto wanaeleza kuwa ni familia zao ndizo zinazosisitiza wawepo kwenye mtandao huo kwa ajili ya mawasiliano.

Utafiti huo ulifadhiliwa na umoja wa ulaya na kuwahusisha vijana wenye umri wa miaka 16-18 umeonesha kuwa mitandao mingine ya kijamii na program tumishi zinaonekana si bora katika miongozo ya namna ya  kuitumika  kuliko facebook.

Utafiti huo unaonesha kuwa Facebook inawaunganisha watumiaji vyema,inatoa mpangilio mzuri wa picha na mpangilio wa mahusiano miongoni mwa watumiaji.

 WhatsApp inaonekana ni bora kwa ujumbe wa maandishi ambapo kwa sasa inaonekana kuipiku facebook na kutokana na kuonekana bora katika huduma ya ujumbe mfupi wa maneno . 

Miongoni mwa vijana wengi nchini Uingereza  sasa wanatumia  Snapchat,ambao hukuwezesha kutuma picha ambazo huondoshwa sekunde chache baada ya kuzituma.

Kumekuwa na lawama kuhusu faragha katika mtandao wa facebook hasa baada ya mwaka huu kuelezwa kuwa Wakala wa Ulinzi wa Marekani (NSA) imekuwa ikifanya  udukuzi wa taarifa zilizoko katika mtandao huo.

Utafiti huo pia unaonesha kuwa vijana hao sasa wanajiunga na Instagram mtandao unaotoa huduma ya kubadilisha picha,Mike Butcher kutoka Techcrunch.com ameiambia Sky News kuwa Facebook ilikuwa mahali tulivu na faradha hasa kwa wanafunzi wa vyuo vikuu na wahitimu kwa ajili ya kutengeneza kipato na imekuwa maarufu.
Anaeleza kinachotokea sasa ni vijana kutafuta mitandao mbadala ambayo ni  Instagram na Twitter.

Monday, December 16, 2013

TANZANIA IMEJIPANGAJE KATIKA KUKABILIANA NA UDUKUZI?

UDUKUZI NI NINI ?

Ni uchukuaji wa taarifa za mwingine kwa njia ambazo sio halali kwa kutumia vyombo vya mawasiliano anavyotumia mtu husika kama email , simu , kompyuta , tv na vingine vingi .

Taarifa hizi zinaweza kuwa kwa njia ya nyaraka zilizohifadhiwa , zinazofanyiwa kazi ( kama ziko shared ) , kusikiliza mawasiliano ya sauti kama kupiga au kupokea simu , ujumbe mfupi yaani sms na Mawasiliano ya email mtu anayofanya na watu wake au makundi .

Katika siku za karibuni wigo umepanuka kidogo sasa hivi mpaka kwenye anuani za watu kwenye mitandao ya kijamii kama facebook watu wanaouwezo wa kuiba taarifa au kuingia na kupotosha , kwenye majukwaa ya majadiliano pia watu wanaweza kuingia kuvuruga au kuiba taarifa za mtumiaji fulani bila wenye jukwaa kujua .

Kwa mataifa yaliyoendelea Aina hii ya Ujasusi ni njia moja wapo ya kujilinda dhidi ya adui wa nje na wa ndani , adui huyo anaweza kuwa gaidi , jasusi mwenzake , biashara za kimataifa , teknolojia , uuzaji na usambazi wa silaha , taarifa za afya , viwanda na nyingine nyingi .

MATUKIO MAARUFU YA UDUKUZI KIMATAIFA
1 – Miezi kadhaa iliyopita tumesikia na kusoma kwenye vyombo vya habari kuhusu Udukuzi uliokuwa unafanywa dhidi ya viongozi mbalimbali wa nchi za ulaya na amerika ya kusini na mashirika ya ujasusi ya kimarekani .

2 – siku kadhaa kabla ya mkutano wa G20 NA hata wakati mkutano huo unaendelea baadhi ya wajumbe walipokea barua pepe ambazo zilikuwa na program maalumu zilizojiingiza kwenye kompyuta zao na hapo hapo walianza kufuatiliwa na kuibiwa taarifa zao haswa kile walichokuwa wanafanya na kuandika kutumia kompyuta zao na simu , uchunguzi ulipofanyika iligundulika uvamizi huu ulitokea uchina .

3 – wajumbe wa mpango wa nyuklia wa irani walipoenda uingereza kwa ajili ya mkutano Fulani nao waliingiziwa virusi walipowasha tu vifaa vyao vya mawasiliano , virusi hivi vilisambaa mpaka kwao mpaka kwenye vinu vyao vya nyuklia matokeo yake ni kwa baadhi ya vitu kutokufanya kazi sawasawa .
Hili suala kwa Irani pamoja na vikwazo ndio limesababisha uongozi mpya kutaka muafaka na mataifa yaliyoendelea , pia lilisababisha baadhi ya wanasayansi wao kuuwawa kwa njia za kigaidi haswa wale waliokuwepo kwenye mradi huu .

MATUKIO MAARUFU YA UDUKUZI NCHINI
Kwa hapa nchini kuna matukio 3 ambayo ni maarufu lakini hayajawahi kuongelewa sana .
1 – Waziri mmoja na kundi lake walikuwa wanaenda nchi Fulani ya ulaya kwa ajili ya warsha na alitarajiwa kutoa msimamo Fulani , basi alivyofika hotelini kuwasha kompyuta yake kuanza kupekua vitu hapo maharamia wa mtandao walimvamia na kuharibu hiyo kitu aliyokuwa anafanyia kazi siku zote .

2 – Mara kadhaa kumewahi kutokea udukuzi kwenye taasisi zetu zinazosimamia maswala ya mawasiliano haswa TCRA na ilipochunguzwa ikagundulika waingiliaji wengi walitokea nchi ya China , china imekuwa nchi inayongaa ulimwenguni kwenye masuala ya Udukuzi .
3 – Udukuzi uliwahi kufanywa dhidi ya shirika moja la ndege nchini halafu wahalifu wakavamia kwa nia ya kuharibu utaratibu wa urushaji ndege na uhifadhi mwingine wa taarifa , hii ilisababisha ndege moja kukaa uwanjani bila kufanya safari kwa mwezi mmoja kwa sababu za kiusalama na ndege hiyo ilikuwa inaendeshwa na mitambo maalumu kutoka nchi nyingine .

HALI YA TANZANIA
Hali ya Tanzania kusema za ukweli sio ya kuridhisha sana kutokana na mambo 3 makuu .
1 – Sheria za Mawasiliano – Sheria zetu za mawasiliano hazijitoshelezi na wahalifu wengi wanatumia fursa hiyo kufanya uhalifu wao kutoka hapa kupiga wengine au kupitia hapa kupiga wengine wa mbali , tunapenda kuwa na sheria nzuri za mawasiliano zinazoendana na wakati wa sasa na kila idara serikalini itengeneze sheria zake kwa kunukuu sheria mama .

2 – Utumiaji wa Vifaa chakavu – Tunaona watu haswa wenye fedha zao wakinunua vifaa chakavu vya mawasiliano haswa toka nchi za mbali kwa ajili ya kuja kutumia hapa nchini vifaa hivi vingi vimesababisha utengenezwaji wa njia za kivamizi na kwa sababu teknologia zake za kizamani imekuwa rahisi wa wahalifu kuzichezea na kufanya wanachojua .
3 – Vifaa visivyokidhi viwango – Tumeona watu wananunua simu ambazo hazina viwango na kuzitumia kwenye shuguli za uhalifu , simu nyingine zinapunguzwa baadhi ya vitu ili ziweze kufanya kazi nchini , watu maofisini wanaingiza programu kwenye kompyuta zao ambazo hazina leseni au leseni bandia yote hii haitakiwi .

4 – Kutokufuata taratibu za manunuzi – Hapo juu nimesema hatuna sheria za mawsiliano na tumezoea kununua vifaa chakavu , tukiwa na hivyo viwili tutaweza kuwa na utaratibu mzuri wa kununua vifaa haswa vya mawasiliano maofisini na kwenye idara za serikali utakaofuata vitu hivyo viwili .

NINI KIFANYIKE
Ni wakati mzuri sasa kwa Taasisi muhimu nchini kama Mabenki , Polisi , Tume ya mawasiliano , Kampuni za Mawasiliano ya Simu na Intaneti , taasisi za elimu kama vyuo na shule kuwa na taratibu za kufundisha watu matumizi salama ya vifaa vya mawasiliano , ununuzi mzuri wa vifaa vya mawasiliano na uuzaji mzuri wa vifaa vya mawasiliano .

Tufanye hivi huku tukingoja sheria mama wa mawasiliano iboreshwe na wengi wataboresha masomo yao kuzingatia sheria mama ya mawasiliano nchini kulingana na hali tuliyonayo .

Ningependa kuona sheria mama ikiandikwa kutokana na mila na tamaduni za mtanzania sio nje ya hapo , hata pale mtu akisoma itoe harufu ya utanzania au uafrika mashariki .

Kupambana na udukuzi wote sio rahisi lakini tunaweza kupunguza uwezo wa kufanyiwa udukuzi kwa kuhakikisha tuna vifaa vizuri vya mawasiliano na kufuata taratibu za utumiaji .
YONA FARES MARO
0786 806028

Saturday, December 14, 2013

MUONGOZO WA KUTENGENEZA TOVUTI HUU HAPA

 

Kitabu hiki kipo tayari. Wasiliana kwa namba 0713 309 314 au 0763 309 314 na Mushi Richard, Mpesa: 0755872462, Tigopesa: 0713643703 lipia kitabu chako mtumie email yako kisha akihakiki hela imeingia anakutumia kitabu kilicho katika mfumo wa Soft Copy. Ni TSHS. ELFU KUMI NA MBILI TUU (12,000/=). Hata kama upo mkoani.

MICROSOFT KUWASAIDIA WANAFUNZI WA VYUO KUPITIA STUDENT ADVANTAGE




Kampuni ya Microsft Corporation imeanzisha programu mpya ambayo itawawezesha wanafunzi kufanya mazoezi yote wanayopewa shuleni kupitia teknolojia ya habari na mawasiliano.

Kampuni hiyo imebuni programu mpya ya Student Advantage ambayo itawawezesha wanafunzi kupeana kazi za shule,mazoezi ya nyumbani na masuala yote muhimu ya kitaaluma.

Mpango huo uliotangazwa hivi karibuni wakati kampuni hiyo ikitambulisha programu ya Microsoft Office 365 Education ambayo inakadiriwa kutumiwa na zaidi ya wanafunzi milioni 110 wa vyuo 35,000,idara na wahadhiri mbalimbali duniani.

Programu hiyo itawapa fursa wanafunzi kuitumia kupitia huduma zilizopo ambazo ni Microsoft Word na OneNote ambazo zinafanana na huduma za PowerPoint na Excel.

Mpango huo umeanza rasmi Desemba Mosi mwaka huu,huku vyuo mbalimbali duniani vikipewa leseni ya Office 365 ProPlus kwa wanafunzi wahadhiri pamoja na wakuu wa idara watakuwa wanatumia programu yenye leseni ya Office Proffesional Plus bila gharama zozote.Huduma hizo zote zitawapa wanafunzi nafasi wanafunzi kupata maarifa mbalimbali kupitia mtandao wakiwa nyumbani na huduma nyingine ambazo zipo kwenye programu hiyo yenye vitu vingine vitakavyomwezesha mwanafunzi kuwasiliana na wanafunzi wengine waliopo katika vyuo mbalimbali duniani.

Mkuu wa Kampuni hiyo katika nchi za Afrika Mashariki na Kati Mark Chaban anasema wamefanikiwa kutembelea vyuo 30 binafsi na vya umma pamoja na Wizara mbalimbali za elimu ili kutoa mafunzo kuhusu utumiaji wa programu hiyo ambayo ipo chini ya International Data Corporation (IDC) ambayo itakuwa ikikusanya taarifa za maendeleo ya wanafunzi watakaokuwa wakitumia ili waweze kupata ajira na kuboresha maisha yao.

Kampuni hiyo imesema inakusudia kufuatilia uwezo wa wanafunzi katika kutumia huduma hiyo ambapo watakaoonekana kuwa na kiwango cha juu watachukuliwa na kupelekwa kwenye makampuni mbalimbali na kulipwa mishahara minono.

Microsoft imepanga kutengeneza ajira kwa asilimia 28 ifikapo mwaka 2020 ambapo miongoni mwa wanafunzi milioni 115 watakaoajiriwa kwa vigezo vilivyowekwa .

Popular Posts

Labels