Mamlaka
ya mawasiliano Tanzania (TCRA) inakusudia kuanza awamu ya pili ya uzimaji wa mitambo ya
mfumo wa utangazaji wa analojia kwenda dijitali katika miji ya Singida na Tabora
mwishoni wa mwezi Machi 2014.
Miji mingine katika awamu ya pili itakuwa
Musoma, Bukoba, Morogoro, Kahama, Iringa, Songea na Lindi. Awamu hiyo inategemewa
kukamilika mwishoni mwa mwezi Oktoba 2014.
Taarifa
ya TCRA kwa vyombo vya habari ilitolewa jana na Mkurugenzi wa Mamlaka hiyo Prof
John Nkoma inasema nia ya Mamlaka ni
kuona zoezi la uhamaji kutoka mfumo wa utangazaji wa analojia kwenda mfumo wa
kidijiti linakamilka nchini humo kabla ya kufikia ukomo wa matangazo ya
analojia kama ilivyoelekezwa na Shirika la Umoja wa Mataifa linalosimamia
Mawasiliano Duniani (ITU) juni 17,2015.
Tanzania
ni nchi ya kwanza kuzima mtambo ya analojia Barani Afrika, Zoezi la uzimaji
mitambo kwa awamu ya kwanza iliyoanza disemba 31,2013 ambalo lilifanyika kwenye
miji saba lilikuwa na changamoto nyingi, kwani liligusa nyanja mbalimbali zikiwemo
za kijamii, kibiashara, kiufundi na Kisiasa.