Mapenzi ya watu kwa simu za kisasa za mikononi ( smartphone) yameendelea kupanda kwa mwaka
2013 ambapo watu walinunua simu hizo zaidi ya bilioni moja hii ni kutokana na
makadilio yaliyotolewa na shirika la kimataifa linalofanya utafiti wa masoko
katika masuala ya mawasilino ya simu, wanunuzi wa bidhaa,teknolojia ya habari
na Mawasiliano (IDC) katika utafiti wake lililoutoa Februari 7,mwaka huu
Idadi hiyo ambayo inahusisha smartphone mpya kwa mtu mmoja kati ya watu
saba duniani,hii inavutia ikilinganishwa na mwaka 2012 ambapo jumla ya simu
milioni 725 zilisafirishwa kwenye masoko ambapo inaonesha kuwepo kwa ongezeko
la simu milioni 275 zilizouzwa ambalo ni ongezeko la asilimia 39 ikilinganisha
na mwaka 2012.
“Nafikiri kuna taarifa zingine kubwa ambapo mwaka jana
tumeona ukuaji mkubwa katika soko la simu “Anasema Ramon Llamas mchambuzi toka
IDC
IDC inakadilia kuwa asilimia 79 ya simu zilizopelekwa katika
masoko toka viwandani mwaka 2013 simu nne kati ya tano ni zilizotengenezwa
katika mfumo wa Android.
Katika soko la dunia simu za Apple hazikuonekana kusambazwa
sana kwani kulikuwa na vifaa vya Mawasiliano vya mfumo huo kwa zaidi ya asilimia 15 tu ikiwa ni kupelekwa
sokoni kwa simu milioni 153 ambalo ni ongezeko la asilimia 13 ukilinganisha na
mwaka 2012.
Takwimu za IDC pia
zinaonesha habari njema kwa kampuni ya Microsoft kwa simu zake za Windows
ambapo usambazwaji wa simu hizo ulikuwa na kufikia milioni 33,ambalo ni
ongezeko mara mbili ilivyokuwa mwaka 2012.Simu za BlackBarry zilionekana
kushuka kwa asilimia 40 kwakuwa na idadi ya simu milioni 19 zilizosambazwa sokoni.
Mtandao PC world umeeleza kuwa pamoja na kupigiwa chapuo kwa
kwa matoleo mapya ya simu za iPhone, Samsung
Galaxy Note 3, HTC One na zingine
watengenezaji wa simu bado watapanga kutoa simu za bei rahisi ili kuwa na wigo
mkubwa wa ukuaji wa soko hasa simu zilizengenezwa katika mfumo wa android
Chanzo:PC World
.