Watumiaji wa simu za Nokia na Windows wamekuwa wakitamani kutumia huduma ya ujumbe wa maneno ya BlackBerry (BBM) huduma hiyo sasa itapatika katika simu hizo.
Nokia na BlackBerry wamethibitisha mapema leo kuwa huduma hiyo ya ujumbe wa bure imekubalika na na itatumika katika simu za Nokia na Lumia zenye mfumo wa Windows na katika simu mpya ya Nokia iitwayo Nokia X ambayo imetengenezwa katika mfumo wa Androd.
BlackBerry imesema kuwa huduma hiyo itaanza kutumika miezi michache ijayo na itaanza kupatikana katika Nokia Store.
Hatua hii iliyochukuliwa na BlackBerry,Nokia na Microsoft wakati ambapo Facebook imetumia dola $19 kununua programa tumishi ya ujumbe wa maneno ya Whatsapp.
Huduma za BBM na Whatsapp) zimepata umaarufu sana katika mawasiliano kwa watu mbalimbali kwa urahisi zaidi.