Rais wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dr Jakaya Mrisho Kikwete amezindua Mtambo Maalum wa Usimamizi na Uhakiki wa Mawasiliano ya Simu, Februari 27,2014 jijini Dar es salaam,uzinnduzi uliofanyika yalipo makao makuu ya Mamlaka ya Mawasilino Tanzania (TCRA)
TCRA kupitia Mkurugenzi wake Profesa John Nkoma ameeleza mtambo huo utakuwa na faida zifuatazo;
1.Kuwa na uwezo wa kujua mapato yanayopatikana kwenye simu za kimataifa zinazoingia nchini.
2.Kuongeza mapato kwa sekta ya mawasiliano kutokana na wapigaji wa simu waliopo nje ya nchi ili kuweka uwiano ulio sawa kati ya makampuni ya hapa nchini na yale ya nje ya nchi.
3.Kuwa na utaalamu wa kuweza kuzuia matumizi ya simu zinazopigwa nchini na makampuni yasiyo na leseni kwa ajili ya kuunganisha simu za kimataifa na hivyo kuikosesha serikali ya Tanzania na Makampuni ya simu mapato halali.
4.Kuongeza uwazi na uwajibikaji katika sekta ya mawasiliano.
5.Kuipa serikali kwa kupitia TCRA uwezo wa kuweza kusimamia sekta ya mawasiliano vizuri,kwa kuwa sekta inakuwa kwa kasi na inatoa huduma nyingi sana zikiwemo za benki mtandao.
Makampuni yenye leseni za kutoa huduma za simu za kimataifa na nchini Tanzania ni Airtel,MIC (Tigo),Sixtelecoms,TTCL,Vodacom na Zantel