Friday, February 21, 2014

FACEBOOK KUINUNUA WhatsApp KWATENGENEZA MABILIONEA WAPYA KATIKA TEKNOHAMA

 


Mtandao wa kijamii wa Facebook umenunua programu tumishi ya huduma za ujumbe mfupi wa maneno ya WhatsApp kwa dola za marekani bilioni 19 (TSh 30.9 trilioni) katika taarifa iliyotoka mapema Februari 19,2014.

Ununuzi huo wa WhatsApp umetengeneza mabilionea wapya angalau watatu, akiwemo mwanzilishi wa WhatsApp, Jan Koum, ambaye atajiunga na bodi ya wakurugenzi ya Facebook.

Mwanzilishi mwenza wa WhatsApp, Brian Acton, naye anaingia katika orodha ya mabilionea wapya vijana.

Miaka 4 iliyopita, Acton alijaribu kuomba kazi Facebook na Twitter baada ya kupunguzwa kutoka Yahoo,inaandika  blogu ya teknolojia ya Techcrunch.
 .
Leo hii, program aliyoitengeneza na rafikiye wa Yahoo, Koum, inagombaniwa na kampuni zilezile zilizomkataa na hatimaye, imenunuliwa kwa mabilioni ya dola na Facebook.

Wengine walioula ni wawekezaji wa kwanza wa WhatsApp toka kampuni ya uwekezaji ya Sequoia.

Techcruch inaripoti vijana wa Sequoia wametengeneza zaidi ya dola bilioni 3 (TSh 4.9 trilioni) – mara 50 ya pesa waliowekeza – katika ‘dili’ hilo.

Facebook, ambao ni mtandao wa kijamii  mkubwa kuliko yote duniani ukiwa na wanachama zaidi ya bilioni 1, inaamini kuwa WhatsApp itasaidia kuongeza uwepo wake katika masoko mbalimbali duniani, hasa katika nchi zinazoendelea za Afrika, Asia na Amerika Kusini ambapo teknolojia ya simu za mkononi imeshika hatamu.

Uamuzi huo unaipa Facebook nafasi ya kuongeza idadi ya watumiaji wa mtandao wake, itarithi zaidi ya watumiaji milioni 450 wa WhatsApp.

Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa Facebook, Mark Zuckerberg anaamini uamuzi wa kuinunua WhatsApp kwa dola bilioni 19 ni wa busara, kwa kuwa “[WhatsApp] ni mtandao unaokuwa kwa haraka, ambayo itafikia watumiaji zaidi ya bilioni moja hivi punde.”
 
WhatsApp iliyoanza kutumika mwaka 2009,hadi kufikia  November 10, 2013, ilikuwa na watumiaji milioni 190 kwa mwezi,wakiwa wametumiana picha milioni 400 kila siku, ambapo iliweza kuhifadhi ujumbe wa maandishi bilioni 10  kwa siku.

Desemba 2013 WhatsApp ilieza kuwa ilikuwa na watumiaji milioni 400 kila mwezi. 

Program huyo tumishi kwa sasa inatumika katika vifaa vya mawasiliano yaani tabiti,simu na kompyuta zenye mifumo ya iOS,Android,BlackBerry,Simbiani na Windows
 
Chanzo:Gazeti la Mwananchina na Wikipedia org

Popular Posts

Labels