Unapomblock mtu kwenye viber
inamaana umezuia kuwasiliana na mtu yoyote kwa njia yoyote katika mtandao wa
kijamii wa viber,hutapokea ujumbe wa maneno ama kwa kupiga simu.
Hii inamaanisha kuwa
Hii inamaanisha kuwa
- Hutaweza kupiga simu ama kuwasiliana kwa ujumbe wa maneno.
- Picha ya wasifu wako na hali yako vitaonekana kwa uliyemblock.
- Ukijaribu kurudisha tena mawasiliano hutaona ujumbe ama kumbukumbu ya simu ulizopiga kabla ya kublock.
- Kublock hakutafuta ujumbe na historia ya mawasiliano yaliyofanyika mwanzo kabla
- Kumblock mtu hakutamzua mtu huyo kukuongeza kwenye mawasiliano ya makundi anayowasiliana nayo yaliyoundwa katika mtandao wa Viber
Nawezaje kublock mawasiliano?
Kuna njia mbalimbali.
Kuna njia mbalimbali.
- Unapopata ujumbe toka kwa mtu usiyemfahamu,ukurasa wa mawasiliano utaonesha chaguzi mbili,unaweza mwongeza katika orodha ya unaowasiliana nao ama unaweza kumblock When receiving a message from an unknown contact.
- Unapoblock mtu kwenye kundi,unaweza kufanya hivyo kwa watu waliopo kwenye kundi hilo nenda kwenye kundi chagua contact > chagua menu ya kifaa chako > nachagua "Block".
- Uliyemblock ataendelea kuona unachokifanya kwenye kundi husika na wewe unaona pia.
- Njia hii itatumika moja baada ya mawasiliano mengine unayoyafanya.
- Unaweza kublock kwa ukurasa wa maelezo ya mawasiliano kwa kupeleka kushoto mwa kioo cha kifaa chako cha mawasiliano chagua menu > Chagua "Block"
- Unaweza kuweka namba kwa kufuata hatua hizi settings > Privacy > Block List > Block number. Kumbuka kuweka namba kwa kufuata utaratibu huu + namba ya nchi – Namba ya eneo – Namba ya simu. Mfano kwa namba ya Tanzania itaonekana + 255 123 456 789
Unawezaje kurudisha ulichokiblock?
- Chagua menu ya More Options
- Chagua Settings
- Ingia Privacy
- Chagua Block List
- Tafuta namba unayotaka kuirudisha
- Chagua Unblock
Kumbuka namba unayoirudisha haitarejesha ujumbe uliotumwa wakati ilipoiblock
Unapoblock namba ya mtu katika
wasifu wako wa viber,mhusika hatagundua hili ataendelea kukutumia ujumbe na
ujumbe huo hautaupata.
Kwa ajili ya kuwa na faragha hakuna
njia moja inayoonesha kuwa mtu amekublock ama la,inabaki tu kwamba ukiblock
namba ya mawasiliano mtu hata jua na hata wewe ukifanyia hivyo hutajua.