Baada ya kikao
kilichofanyika juma liliyopita katika Chuo Kikuu cha Stafford ambapo Rais Obama
wa Marekani alikutana na wafanya biashara, Wanasheria na wasimamizi
washeria kujadili hali ya mtikisiko wa maswala ya usalama mitandao,
Inadhihirisha wazi bado kuna safari ndefu kukabiliana na wimbi hili la
uhalifu mtandao duniani kote.
Hii
ni kutokana na ukweli kwamba Tishio la uhalifu mtandao na utayari wa
kukabiliana nao bado kuna kutowiana ipasavyo ingawa jitihada bado ni
kubwa kuweza kukabiliana na uhalifu huu unaokua kwa kasi ya pekee
duniani kote.
Wakati haya yakijiri na
mikakati zaidi ikiendelea ya kukabiliana na wimbi kubwa la uhalifu
mtandao hivi sasa makampuni yanayojihusisha maswala ya fedha yameonekana
yakiathirika zaidi na uhalifu mtandao – Hii ni kwamujibu ya ripoti
maalum iliyotolewa na kampuni ya Kaspersky Lab.
Taarifa
inaeleza kwamba genge la wahalifu mtandao limefanikiwa kuiba Mamilioni
ya Dola za kimarekani kutoka kwenye akaunti za wateja wa mabenki 100
katika mataifa 30 kati ya mwaka 2014 na 2015.
Ripoti
hiyo inaelezea mbinu mpya za wahalifu mtandao wanazotumia kudukua
nambari za akaunti za wateja za siri kabla ya kuingia na kuiba pesa.
Kaspersky
imesema kuwa wizi huo ulianza mwaka wa 2013 na bado unaendelea hata leo
kwani mabenki yote yalioathirika hayana uwezo wa kuwazuia wezi hao.
Hadi kufikia sasa ripoti hiyo inadai kuwa takriban dola bilioni moja zimeporwa kutoka kwenye akaunti za wateza.
Genge hilo la wezi, lililoanzia shughuili yake nchini Urusi, Ukraine na pia Uchina ndilo linalolaumiwa kwa wizi huo.
Kampuni
hiyo ya Kaspersky inasema inafanya juhudi za kuzima wizi huo kwa
ushirikiano na polisi wa kimataifa Interpol na polisi wa bara ulya
Europol.
Kwa
mujibu wa ripoti hiyo mabenki katika mataifa 30 yakiwemo, Russia,
Marekani , Ujerumani , Uchina, Ukraine na Canada yameathirika pakubwa.
Kamanda
wa kikosi cha polisi wa kimataifa Interpol bwana Sanjay Virmani,
amesema kuwa wezi wataendelea kutumia upungufu wa miundo msingi katika
sekta ya uchumi wa mataifa husika hadi pale kutaibuka umoja wa kuzuia
mapengo.
Kaspersky hata hivyo inasema kuwa genge hilo linalenga mabenki bila ya kuwaibia watu binafsi.
genge
hilo kwa jina Carbanak, linatumia mbinu ya kuambukiza virusi kwenye
mashine za benki ikiwemo kamera za CCTV ilikunakili kila kitu
kinachoandakiwa kwenye kompyuta.
Kutokana
na uweledi wao genge hilo lilituma pesa kwenye account zao huku wengine
wakiamrisha mmitambo ya kutoa pesa ATM kumimina pesa bila kikomo.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo kila tukio la wizi lilihusisha takriban dola milioni kumi.
Kwa
Tanzania Hali inaweza kubadilika kabisa siku za usoni kwani tayari
mipango na mikakati ya dhati ya kukabiliana na uhalifu huu wa kuibia
watu pesa zao kupitia ATM inaendelea kwa kasi na hatima ya kupata muarobaini stahiki unategemewa kutatua hali husika.
Na:Yusuph Kileo