|
Yusuph Kileo akitoa mada kwenye mkutano huo |
Mazungumzo
ya awali kabla ya mkutano wa wanausalama mitandao uliokamilika jijini
Johannesburg nchini Afrika Kusini yanaweza kusomeka kwa "KUBOFYA HAPA" Mkutano
ambao uliokua na vuta nikuvute kupata suluhu ya changamoto tulizo nazo za
kiusalama mtandao duniani kote zinazoendelea kukua kila kukicha huku ikionekana
dhahiri kabisa wahalifu mtandao wanaelekea kuzidi nguvu huku Tanzania ikiorodheshwa kuwa ya sita kwa
nchi zinazotegemewa kuathirika zaidi na uhalifu mtandao barani Afrika.
Akitolea
ufafanuzi wa takwimu hizi Bwana Vernon Frye, Mkuu wa Usalama mitandao wa
kampuni ya Vodacom ya Afrika Kusini, alielezea kuhusiana na uhalifu mpya wa
Ransomware ambapo tayari athari zake zimesha onekana Nchini huku akiibua
mjadala mzito wa wapi tume jikwaa.
Aidha
Mjadala mrefu kutoka kwa aliyekua Mkurugenzi wa wakala wa usalama wa Marekani
(National Security Agency – NSA) Bwana William Binney pamoja na Raisi na
muanzilishi wa kivinjari cha aina ya Tor kinachotumika sana na jumuia ya wana
usalama mitandao waliibua changamoto ya ufaragha baina ya watumiaji wa mitandao
na namna ya kuendelea kuhakiki kunapatikana uthibiti wa faragha hizi kutotumika
vibaya na wahalifu.
Akiwasilisha
mada ya changamoto tulizo zazo barani Afika na nini kifanyike ili kujikwamua
katika hali mbaya tuliyo nayo hivi sasa ya wimbi la uhalifu mtandao barani
afrika ambapo umeendelea kugharimu bara katika Nyanja za kisiasa, kijamii
pamoja na kiuchumi. Yusuph Kileo toka Tanzania alielezea kwa kina mambo ya msingi tunayo takiwa kuyafanyia
kazi ili kuhakiki Bara linabaki salama.
Katika
mjadala huu ambapo wanausalama mtandao kutoka maeneo mbali mbali ya dunia
waliunga mkono alichozungumza kuwa bado kuna kusua sua katika ushirikiano wa
pamoja katika kutokomeza uhalifu mtandao huwa wahalifu mtandao kuonekana
niwenye ushirikiano ulimkubwa kabisa.
Aidha alifafanua kuhusiana na mipango isiyo endelevu ya kukuza vipaji vya wana
usalama mtandao wa ndani pamoja na kuwa na program za kukuza uelewa kwa jamii
juu ya matumizi salama mitandao ambazo hazionyeshi athari kutokana na uhaba wa
maandalizi sahihi na kujua walengwa stahiki.
Makubaliano
yamsingi yalikua ni mengi na kwa uchache ni pamoja na kuhakiki kunakua na
program endelevu za kuwa kukuza uelewa wa matumizi salama ya mitandao sanjari
na kukuza wataalam wa ndani. Pia Ushirikiano baina ya wanausalama si tu katika
ngazi ya kitaifa na kibara bali kidunia imeonekana ni muhimu sana. Aidha
makampuni kuhakiki yanatumia teknolojia zinazoweza kuendana na hali ya uhalifu
hivi sana na kuhakiki wanaziba mianya ya kihalifu kuanzia kwa wafanyakazi wao
imeonekana ni jambo muhimu sana.
Aidha
mkutano huo ulitoa fursa ya washiriki kupata kubadilishana mawazo kwa
nyakati tofauti ambapo mtaalamu huyo wa masuala ya usalama katika mitandao alitumia fursa hiyo kuweza kujifunza mengi
kutoka kwa mkongwe wa fani hii na aliyeweza kuongoza wakala kubwa ya
usalama mitandao ya nchi ya Marekani kama inavyo onekana pichani.