Thursday, March 28, 2019
APPLE YATOA SASISHO LA PROGRAM ENDESHI YA iOS 12.2
Apple wametoa Sasisho la Program Endeshi ya iOS 12.2 kwa ajili ya iPhone, iPad, and iPod toleo ambalo litawezesha wenye vifaa vya hivyo kunufaika za Apple zilizotambulishwa jumatatu ya Machi 25 mwaka huu nchini Marekani ikiwemo huduma ya kupata habari iitwayo Apple News+
Apple pia wameongeza imoji,ambapo iOS 12.2 itamwezesha mtumiaji wa huduma ya Siri iliyopo katika vifaa hivyo kuongoza Apple TV kwa kutumia iPhone au iPad.
Miongoni mwa madiliko yaliyokuja na sasisho la iOS 12.2 ni kukusianisha kwa Apple News+ na Apple News iliyokuwepo mwanzo,
ambapo huduma hii ya kulipia itawawezesha watumiaji wa vifaa vya Apple waliopakua sasisho hili jipya kupata zaidi ya magazeti mtandao 300,na machapisho mengine ya habari ya kidigitali.
Labels:
Habari
Monday, April 30, 2018
WAKUU WA TEKNOHAMA WAKUTANA KENYA
Watunga sera na sheria mbali mbali wamekua wakifanya maamuzi ya TEKNOHAMA bila kushirikisha wadau wa TEKNOHAMA – Hii imekua moja ya changamoto inayo leta mkinzano wa utendaji wenye manufaa kwa wana TEKNOHAMA maeneo mengi barani Afrika.
Mjadala
ulioangazia umuhimu wa udhibiti na uangalizi wa watendaji katika sekta ya
TEKNOHAMA umeonekana kua mzuri ila umegubikwa na changamoto kadhaa kutokana na ushirikishwaji
mdogo wa wadau ili kuweza kuleta mabadiliko kwenye sekta husika.
Mjadala
huu umejadiliwa kufuatia kuwepo kwa sera mpya nchini Kenya itakayo rasimisha
Wana TEKNOHAMA na kuwataka watambulike kabla ya kuweza kuhudumu maeneo mbali
mbali. Hili litafanana na tulicho nacho nchini Tanzania kwa wanasheria pamoja
na wataalam wa maeneo mengine kadhaa.
Kinachotegemewa
katika urasimishaji wa sekta ya TEKNOHAMA na kumfanya mwana TEKNOHAMA
atambulike na kuhudumia katika sekta ya TEKNOHAMA ni pamoja na kupitia
hatua kuu tatu ambazo ni, Kusomea – Usaili – Kupatiwa leseni ya kutoa huduma
katika sekta husika.
Changamoto
iliyo onekana ni pamoja na uwezekano wa kuua vipaji vya wabunifu wa TEKNOHAMA
ambao wamekua wakija na ubunifu wenye manufaa pasi na kua na ujuzi rasmi katika
sekta husika.
Tumeshudia
kuwepo kwa vijana walio somea fani nyingine tofauti na TEKNOHAMA ila baadae
kuja na Mifumo mizuri ya Kitehama iliyoweza kutatua changamoto mbali mbali
katika maeneo yetu tofauti na wengine waliosomea fani husika na kushindwa kuwa
wabunifu wa kuleta mabadiliko katika jamii zetu.
Kuna
baadhi ya Mifumo tuko nayo maeneo mengi ambayo wabunifu wake hawakua na elimu
ramsi katika sekta ya TEKNOHAMA. Aidha, Swali kuu matumizi ya TEKNOHAMA ya
mekua kuna ulazima mhusika kua na elimu rasmi? Ilhali kila sekta inategemea
TEKNOHAMA na kuna uwezekano kila mwenye ujuzi wa fani yoyote akawa na uwezo wa
kufanya vizuri kwenye mifumo ya TEKNOHAMA.
GDPR
(General Data Protection Regulations) Nchi za umoja wa ulaya wana mategemeo ya
kuanza rasmi matumizi ya GDPR mwishoni mwa mwezi wa tano mwaka huu wa 2018 –
Lengo kuu ni kulinda faragha za raia wake.
Hatua
hii inaweza kuathiri maeneo mengi duniani Afrika ikiwemo kwani tumeendelea
kufanya biashara na kuhudumia mataifa ya umoja wa ulaya ambapo inahusisha
taarifa za wana jumuia ya ulaya kupatikana kwetu.
Mjadala
mzito wa nini tutegemee pale umoja wa Ulaya watakapo anza rasmi matumizi ya
GDPR katika taasisi zetu hususan za kifedha. Namna bora ya kuweza kulinda
(faragha) za watumiaji mifumo ya kitehama katika taasisi zetu ili kuondokana na
tunachoweza kukabiliana nacho baada ya kuanza rasmi matumizi ya GDPR barani
ulaya.
CSIRT
(Computer Security Incidence Response Team) – Tumekua na changamoto ya uwepo wa
vitengo mahususi vya kukabiliana na matukio ya kihalifu mtandao katika taasisi
na kampuni mbali mbali. Hili linatokana na uelewa mdogo juu ya umuhimu wa
vitengo hivi mahsusi vyenye jukumu la kukabiliana na uhalifu mtandao.
Umuhimu
wa CSIRT, namna ya kuanzisha na majukumu yake katika kila kampuni na taasisi ni
mjadala nilio uongoza kuhakiki kila mmoja anafahamu hili.
Matukio
ya kihalifu mtandao katika mataifa yetu yanayopelekea upotevu wa Fedha, upotevu
wa taarifa, udukuzi wa mifumo na kadhalika yamekua yakijitokeza mara kwa mara
yanayo acha athari kubwa kwa taasisi za serikali na binafsi maeneo mengi
duniani.
Ni
wajibu wa kila taasisi na kampuni kujua ina jukumu la kujilinda dhidi ya
uhalifu mtandao na namna pekee ya kufikia hapo ni pamoja na kua na kitengo
wahususi chenye jukumu la ulinzi mtandao pekee ambapo kitengo husika kitaweza
kuhakiki usalama mtandao unakuwepo.
Aidha, kumekua na mijadala mingine mingi sana
ambayo yote ilikua na lengo la kuhakiki tuna tambua namna sahihi ya kukabiliana
na changamoto nyingi zinazotokana na uwepo matumizi makubwa ya mifumo ya
TEKNOHAMA yanayo rahisisha utendaji kazi katika taasisi na kampuni
Labels:
Habari
Friday, September 15, 2017
APPLE YAZINDUA SIMU MPYA YA iPHONE X INAYOFUNGUKA KWA KUTUMIA USO

Kampuni ya Apple imezindua simu mpya aina ya iPhone X ambayo hutumia utambulisho wa uso wako badala ya kidole kufunguka.
Apple imesema kuwa simu hiyo inayojulikana kama Iphone 10 pia inaweza kutumia utambulisho huo wa uso nyakati za usiku kufunguka na kwamba ni vigumu kuidanganya ikilinganishwa na mfumo wa kutumia kidole.
Ndio simu ghali zaidi kuzinduliwa na Apple.
Ikiwa na ukubwa wa kuhifadhi Gigabait 64 simu hiyo itagharimu £999 nchini Uingereza wakati itakapoanza kuuzwa rasmi mnamo mwezi Novemba tarehe 3.
Simu yenye ukubwa wa kuhifadhi Gigabait 256 itauzwa kwa £256 nchini Uingereza.
La kushangaza ni kwamba kampuni ya Samsung inauza simu yake ya aina ya Note 8 kwa £869 nchini Uingereza ikiwa na uwezo wa kuhifadhi Gigabait 64.
Kabla ya uzinduzi huo, Simu ya Apple iliokuwa ghali zaidi ni ile ya iPhone 7 Plus ambayo inagharimu $969 nchini Uingereza.
Mtaalam mmoja alisema kuwa uwezo wa Apple kuwashawishi wateja wake kugharamikia zaidi simu zake aina ya smartphone ni kitu cha heshima.
Simu hiyo inaweza kujichaji bila kutumia waya na haingii maji wala vumbi.
Labels:
Habari
Wednesday, August 9, 2017
MFUMO MPYA WA ULIPAJI KODI YA PANGO LA ARDHI NCHINI.
![]() |
|
Wataalamu kutoka Wizara ya Ardhi,
Nyumba na Maendeleo ya Makazi wakitoa elimu jinsi ya kutumia mfumo wa Government electronic Payment Gateway
kwa watendaji wa Halmashauri ya Kinondoni.
|
![]() |
|
Elimu ya jinsi ya kutumia mfumo mpya wa
kielektroniki ikitolewa kwa watendaji wa manipaa ya Temeke jijini Dar es
Salaam.
|
![]() |
|
Watendaji wa Baraza la Ardhi na Nyumba
la Wilaya ya Kinondoni wakipewa mafunzo jinsi mfumo mpya wa ukusanyaji maduhuli
ya Serikali utakavyokuwa unatumika.
|
Wizara
ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imeanza rasmi kutumia mfumo wa
kielektroniki wa Government electronic Payment Gateway (GePG) katika makusanyo ya kodi ya pango la ardhi pamoja na tozo
nyingine zinazotokana na sekta ya ardhi nchini.
Mfumo
huu utamrahisishia mwananchi kulipa kodi ya pango la ardhi popote alipo, ikiwa
ni pamoja na kulipia tozo nyingine mbalimbali za sekta ya ardhi. Pia mfumo wa
GePG, utamuwezesha mwananchi au mmiliki wa kipande cha ardhi, kujua anadaiwa
kiasi gani cha kodi ya pango la ardhi na kulipia popote alipo bila kusumbuka
kufuata huduma hizo katika vituo vya makusanyo.
Majaribio
ya ukusanyaji kodi ya pango la ardhi kwa kutumia mfumo wa kielektroniki
yalifanywa katika mikoa ya Dar es Salaam na Pwani, baada ya mafanikio makubwa
kuonekana elimu ikatolewa kwa watendaji wote wa sekta ya ardhi katika
Halmashauri zote za mkoa wa Dar es salaam kabla ya zoezi hilo kuhamishiwa
mikoani.
Mwananchi
yeyote anayemiliki kiwanja au shamba lililopimwa na kuwa na hati, ataweza
kutumia simu yake ya mkononi kujua kiasi cha kodi ya pango la ardhi anachodaiwa
na kukulipa kwa kutumia simu yake ya mkononi pia.
Kwa
zile huduma nyingine za sekta ya ardhi ambazo zinahusisha malipo kama vile
upekuzi katika daftari la msajili (official
serach), mwananchi atapaswa kutembelea ofisi za Wizara ya ardhi zilizo
katika eneo lake na kupatiwa makadirio ya kulipia huduma husika pamoja na namba
ya malipo itakayomuwezesha kulipia aidha kwa njia ya benki au simu ya mkononi.
Kwa
sasa kikosi kazi kinachotoa mafunzo juu ya matumizi ya mfumo huu kimeshaanza
kuelemisha mikoa mingine baada ya kupata mafanikio mazuri katika mkoa wa Dar es
Salaam. Lengo kubwa la kutumia mfumo huu ni kuongeza ufanisi katilka ukusanyaji
wa maduhuli ya serikali pamoja na kurahisisha ulipaji kodi ya pango la ardhi
nchini,
Labels:
Habari
Monday, August 7, 2017
MAAMUZI TOKA KWA MKUTANO WA GAiN 2017 BRAZIL

Mkutano Mkuu wa Mifumo ya utunzaji na usimamizi wa washiriki wa Kanisa la Waadventista wa Sabato Ulimwenguni umemalizika katika jiji la Sao Paulo, Brazil Agosti 6 2017 ukiwa umefanya maazimio yafuatayo.
1. Taarifa rasmi na sahihi za idadi ya washiriki wa kanisa zitapatikana kupitia mfumo wa ACMS pekee.
2. Anwani za makanisa yote ya Waadventista zinapaswa zipatikane kupitia mfumo wa ACMS
3. Kila mwezi karani wa kanisa atatuma taarifa ya washiriki kwenda konferensi, ambayo itaendelea kutumwa mpaka ngazi ya juu.
4. Division ya Amerika kusini inajaribiwa na mfumo mpya wa 7ME ambao unaruhusu kila mshiriki kujaza takwimu zake mwenyewe na ukifanikiwa ndio utatumika rasmi ulimwenguni kote ifikapo mwaka 2018.
5. Idara zote za kanisa zitatumia mfumo wa ACMS kutoa taarifa za idara.
Mkutano huu ulikuwa na wajumbe 31 kutoka ulimwenguni kote na Divisheni ya Afrika Mashariki na kati iliwakiliswa na wajumbe wawili
Friday, June 9, 2017
TEKNOHAMA YAKUZA UFANISI MAMLAKA YA USIMAMIZI WA BANDARI TANZANIA (TPA)
Serikali Mtandao inarahisisha utendaji kazi na utoaji wa huduma kwa umma. Usikose kuangalia kipindi hiki cha Seikali Mtandao katika Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) uone jinsi wanavyotumia mifumo mbalimbali ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano katika kazi zao za kila siku.
Thursday, June 8, 2017
INTANETI INAVYOCHOCHEA UKUAJI WA UTALII BARANI AFRIKA
Afrika ni Bara la pili kwa kuwa na idadi kubwa ya watu ambapo inafikia takribani bilioni 1.2 (wengi wao wakiishi mijini) na inatarajiwa kongezeka mpaka bilioni 2.5 kufikia mwaka 2050 (25% ya watu wote duniani).
Kwa mujibu wa ripoti ya utalii kwa Afrika mwaka 2017 iliyofanywa na Jumia Travel imebainisha kwamba mtu mmoja kati ya watatu ni sehemu ya watu wa daraja la kati (watu wanaofanyakazi kwenye taaluma na biashara mbalimbali pamoja na familia zao) na wanatarajiwa kuongezeka mara mbili zaidi kufikia 2050. Watu wa daraja la kati ni muhimu katika uchangiaji wa ukuaji wa utalii wa ndani na ukanda mzima tuliopo.
Saturday, May 13, 2017
MAELFU YA KOMPYUTA YADUKULIWA NA KUTEKWA NA KIRUSI CHA 'WANACRYPT'
Udukuaji huo umetumia program ya udukuaji iliyotengenezwa na shirika la usalama wa taifa la Marekani (US National Security Agency-NSA) ambalo nalo lilibiwa program hiyo na wajanja.
Wadukuaji hao wanaojiita The Shadow Brokers ndio wanaodai kuwa waliiba program hiyo na kuiweka hadharani katika mitandao ya internet.
Kampuni ya Microsoft ilitengeneza ngao ya kuzuia udukuaji kwa kutumia program hiyo na kuiweka hadharani mwezi Machi, lakini ni wazi watu wengi hawakutumia nafasi kuweka ngao hiyo.
Kampuni mbalimbali kutoka nchi 99 zinasemekana mitandao yao imetekwa, kumekuwa na malalamiko kutoka Uingereza, Marekani, China, Urusi, Hispania, Italia,Taiwan na nchi nyingi nyingine.
Kampuni ya ulinzi wa mitandao (Cyber-security) ya Avast imesema imeweza kupata malalamiko 75,000 ya madai ya kuhusu kirusi cha WannaCrypt, kutoka karibu pande zote duniani.
![]() |
| Hivi ndivyo kompyuta inavyosomeka ukishadunguliwa na kirusi cha Wannacry |
Urusi imesema imeweza kugundua chanzo na inakishughulikia. Huko Ujerumani kampuni ya kuuza tiketi za treni imekubwa na kadhia hiyo wakati maabara ya chuo kikuu kimoja Italy imekutana na tatizo hilo.
Spain imejikuta ikipata tatizo hilo kwenye kampuni yake kubwa ya simu ya Telefonica, kampuni ya umeme ya Iberdrola na kampuni ya kusambaza gesi ya Gas Natural, wafanyakazi wa kampuni hizo walielekezwa kuzima kompyuta zote.
Kampuni ya simu ya Portugal Telecom, na kampuni ya kusafirisha mizigo ya FedEx, ofisi moja ya serikali ya mtaa huko Sweden na kampuni ya simu za mkononi ya Megafon ya Urusi ni kati ya wahanga wa tatizo hili.
Nani hasa waliosababisha hili? Wataalamu wengine wanasema wahusika inawezekana waligundua mapungufu katika program ya Microsoft, NSA waliliona hilo pia na walitengeneza program iliyokuwa inaweza kuteka kompyuta zote zinazotumia Microsoft, program hiyoikaibiwa na wezi wanaojiita (The Shadow Brokers), wezi hawa walianza kuinadi program hiyo katika mtandao na hatimae tarehe 8 April 2017, wakaigawa bure kwa kusambaza password mtandaoni. Wakidai wamefanya hivyo kama njia yao ya kumpinga Rais Donald Trump.
Microsoft tayari wameshatengeneza program ambayo itakuwa inaweza kutoa taarifa kama kompyuta yako imeingiliwa na udukuzi wa WannaCrypt.
CHANZO:theiringa.blogspot.com
Friday, May 12, 2017
WANAOASAJILI LAINI ZA SIMU BILA UTARATIBU KUKAMATWA

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imesema kuanzia sasa itakamata mtu yoyote anayesajili laini za simu kwa kuchakachua au bila kufuata utaratibu na kumfikisha kwenye vyombo vya sheria.
Agizo hilo pia limeelekezwa kwa kampuni ya simu ambayo itaunganisha laini ambayo haijasajiliwa itaunganishwa kwenye mashtaka na mtu aliyesajili laini feki.
Mwanasheria Mwandamizi Mkuu wa TCRA,Johanes Karungura amesema mamlaka iko makini katika kulinda usalama wa mitandao na usalama wa nchi.
Thursday, May 11, 2017
WATUMIAJI BILIONI MOJA WA GMAIL HATARINI KUDHURIWA KIMTANDAO
Watumiaji wa Gmail takribani bilioni moja duniani wako hatarini kudhuriwa na uhalifu mtandao aina ya Phishing ambao umelenga programu tumishi ya Google Docs.Yusuph Kileo mtaalamu wa makosa ya Kidigtali nchini Tanzania anazungumza na BBC.
Popular Posts
-
Mkurugenzi Msaidizi anayeshughulikia masuala ya Simu katika Wizara ya Ujenzi ,Uchukuzi na Mawasiliano Ndugu John Mwera akizungumza ...
-
Kanisa la Waadventista Wa Sabato mwaka huu litashiriki mkutano wa Waadventista watalaamu wa mawasilino ya Intaneti duniani (GAiN) kwa k...
-
Katibu Mkuu Kiongozi wa Tanzania,Balozi Ombeni Sefue amesema tatizo la wizi katika mashine za kutolea fedha (ATM), la dunia nzima. Sefu...
-
Mkuu wa Huduma za Fedha kwa njia ya simu wa Tigo Ruan Swanepoel (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam...
-
Waatalamu wa afya nchini Tanzania wakiwamo madaktari, wataanza kupata huduma ya kupiga simu na kutuma ujumbe mfupi wa maneno bila malip...
-
Watu wasiofahamika wameukata Mkongo wa Taifa kati ya Masasi na Mchinga mkoani Mtwara.Mkongo huo wa taifa ambao ni miundo mbinu ya tekno...
-
Kampuni ya Simu nchini Tanzania (TTCL) jana imekabidhi mradi wa mawasiliano utaotumiwa katika mikoa 12 ya Tanzania kwa ofisi ya Mkaguzi na ...
-
If you've already bought a smart phone, you'll know the importance of choosing a good OS for it. With the versions of all the giant...




