Tuesday, February 12, 2013
MADAKTARI NCHINI TANZANIA KUWASILIANA BURE KUPITIA VODACOM
Waatalamu wa afya nchini Tanzania wakiwamo madaktari, wataanza kupata huduma ya kupiga simu na kutuma ujumbe mfupi wa maneno bila malipo yoyote kwa wataalam wenzao popote nchini humo na kupokea taarifa, maelekezo na ushauri unaohitajika kupitia mtandao wa mawasiliano ya simu za mkononi wa Vodacom.
Mtandao kwa ajili ya mawasiliano ya wanataaluma wa afya Health Network Programme, umeanzishwa kwa lengo la kurahisisha utendaji kazi wa madaktari na kuboresha kiwango cha mawasiliano ya wenyewe kwa wenyewe.
Usajili wa mtandao huo kuanzia sasa unatarajia kuhusisha wataalam wa afya wapatao 9,000 nchi nzima, wakiwamo madaktari wa meno na wasaidizi wao, tabibu na tabibu wasaidizi popote alipo, serikalini na binafsi.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Vodacom Foundation, Yessaya Mwakifulefule, kwa vyombo vya habari jijini Dar es Salaam jana, ili mtaalam wa afya ajiunge kwenye programu hiyo, atatakiwa kutumia simu yake ya mkononi ambayo itakuwa na kadi ya simu (simcard) ya Vodacom.
Akizungumza katika uzinduzi wa huduma hiyo jijini Dar es Salaam, Mwakifulefule, alisema huduma hiyo muhimu na yenye tija siyo tu itawanufaisha madaktari na sekta ya afya, bali pia Watanzania wote mijini na vijijini.
Alisema mbali ya kupiga simu bure, wanachama wa mtandao huo kwa kushiriki katika programu hiyo watakuwa na uwezo wa kutuma ujumbe mfupi wa maneno 50 bure kila mwezi kuwasiliana na wenzao waliojisajili ndani ya programu hiyo.
Awali, Taasisi ya Kimataifa inayoshughulika na huduma za mawasiliano (Switchboard) kupitia taarifa yake kwa vyombo vya habari, imewasihi madaktari kujumuika katika program hiyo ili kutathmini mafanikio ya utendaji wao kama wadau na wataalamu ndani ya sekta ya afya.
Alisema suala la upungufu wa madaktari na wataalam wa afya katika mataifa mengi limesababisha daktari au muuguzi mmoja kujikuta akihudumia wagonjwa kati ya 5,000 hadi 150,000.
Programu hiyo inadhaminiwa na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Switchboard na Kampuni ya simu za mikononi ya Vodacom.
Popular Posts
-
Watafiti toka kampuni ya utafiti ya Zscalar wamegundua kuwa,tovuti za kichina zenye picha za ngono zimekuwa zikisamb...
-
Wizara ya Ulinzi wa Uingereza imetoa Nguo za kisasa kwa ajili ya wanajeshi wake wa miaka ijayo . Picha unayoiona ni mfano wa nguo hizo...
-
Mbunge wa Moshi vijijini,Philemon Ndesambulo (CHADEMA) amezushiwa kifo kutokana na baadhi ya watu kusambaza habari hizo kupitia ujumbe mfup...
-
Watu wengi wameshaona filamu ambazo wahalifu wakidukua simu za mikononi hata kama zimezimwa. Kama ili...
-
Serikali ya Tanzania imeomba mkopo wa Dola za Marekani milioni 154 ambazo ni takribani shilingi za kitanzania bilioni 246 kwa India kuwezesh...
-
Almost everyone takes lots of pictures and posts some of them online. With a little more planning of shots and editing, these pictures can ...
-
1.Kutune Gitaa /Kutafuta Ufunguo wa Sauti ya Gitaa Kulikuwa na wakati ambapo bei ya vifaa vya umeme kwa ajili ya kutafuta ...