Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imetangaza kuzima rasmi mitambo ya kurusha matangazo ya televisheni kupitia mfumo wa utangazaji wa analojia katika baadhi ya maeneo mkoani Mwanza kuanzia Machi 1,mwaka huu na kuwasha digitali.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Huduma za Utangazaji wa TCRA,Habi Gunze,mitambo hiyo itazimwa februari 28,mwaka huu majira ya saa 6:00 usiku katika maeneo ya jiji la Mwanza,Wilaya ya Sengerema,Wilaya ya Ukerewe na Kijiji cha Kisesa.
Amesema maeneo mengine ya mkoa huo yataendelea kutumia mfumo wa analojia hadi mitambo ya digitali itakapofungwa rasmi katika maeneo hayo na mamlaka hiyo imekamilisha maandalizi yote ili wateja wa mawasiliano ya televisheni kwa njia ya analojia waingie katika mfumo mpya wa digitali.