Thursday, February 28, 2013

BOT YATOA MSIMAMO KUHUSU WIZI WA FEDHA KATIKA ATM

Wakati matukio ya wizi wa fedha katika mashine maalumu za kutolea fedha katika benki maarufu kwa jina la ATM yakiendelea kuripotiwa na vyombo vya usalama nchini Tanzania,Benki Kuu ya Tanzania (BOT) imesema kuwa licha ya kuwepo kwa wizi huo kamwe haitazuia huduma hiyo kwani ni mkombozi mkubwa kwa wateja.

Gavana wa BOT  Profesa Benno Ndulu amekaririwa na Gazeti la Jambo leo akieleza kuwa huduma hiyo haiwezi kufutwa badala yake wataendelea kutafiti njia za kuwabana wahalifu hao.

Kauli hiyo ya gavana Ndulu imekuja siku moja baada ya jeshi la polisi wilayani Rungwe, mkoani Mbeya,kuwanasa watu wanne akiwamo mwanafunzi aliyemaliza kidato cha nne mwaka jana, wilayani Bunda, mkoani Mara, baada ya kukutwa wakiiba fedha Benki ya NMB tawi la Tukuyu kupitia mashine za kutolea fedha (ATM).

Watuhumiwa  walikutwa wakiwa na kadi bandia za ATM 150 za watu tofautitofauti  na kwamba, hadi wanatiwa mbaroni tayari walikuwa na Sh20.5 milioni mkononi, kadi zote ni za NMB na kwamba, zilikuwa zinaonyesha  wateja wote ni walimu kutoka wilayani Mbozi.
 

Popular Posts

Labels