Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Mawasiliano,Sayansi na Teknolojia imesema gharama za kupiga simu kutoka mtandao wa kampuni moja ya simu za mkononi kwenda mwingine nchini humo zinapaswa kushuka kuanzia Machi 1,2013 kutoka shilingi 115 hadi shilingi 34.92 kwa dakika huku gharama za mwingiliano kwa kampuni zote zikiwa sawa.
Naibu Waziri wa Mawasiliano,Sayansi na Teknolojia wa Tanzania,January Makamba amesema ni jambo zuri kupunguza gharama hizo kwani mwaka 2008 hadi 2009 baada ya kujengwa Mkongo wa Taifa,bei za simu zilipungua,lakini za muingiliano zilibaki kama zilivyokuwa.
Hatua hiyo inatokana na uamuzi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) baada ya kufanya mapitio ya gharama za simu nchini Tanzania mwaka 2013.
Makamba amesema ili kuhakikisha punguzo hilo linafika kwa wateja,kuanzia mwezi juni mwa huu wizara hiyo itajenga mtambo wa kufuatilia mfumo wa mawasiliano nchini ambao utakuwa ukihakikisha kampuni za simu nchini zinatoa huduma bora ikiwemo kudhibiti kukatika kwa simu na kutopatikana ili kampuni hizo zichukuliwe hatua