Wednesday, March 13, 2013

WIZARA HAIJAPOKEA MAOMBI YA KUSITISHA MATANGAZO YA TELEVISHENI

Waziri wa Mawasiliano,Sayansi na Teknolojia  Profesa Makame Mbarawa amesema hajapokea maombi ya Chama cha Wamiliki wa Vyombo vya Habari Tanzania nchini Tanzania (MOAT) kuhusu kusitisha kurusha matangazo ndani ya mwezi mmoja kuanzia sasa kutokana na kushindwa kumudu gharama za uendeshaji wanazodai zinatokana na urushaji wa matangazo kwa njia ya dijitali.

Kupitia kipindi cha Radio One asubuhi ya leo,Waziri Mbarawa amesema hajapokea ombi hilo ambalo hafahamu linaeleza nini na atakapolipokea wizara italifanyia kazi japo amesema wamiliki wa vituo vya televisheni nchini walikubaliana na wizara katika uhamishaji wa masafa ya utangazaji kutoka analojia kwenda dijitali mchakato ambao ulianza mwaka 2005  na vyombo hivyo vilikubali kutumia teknolojia hiyo. 

Kabla ya kuanza kwa zoezi la kuzima mitambo ya analojia disemba 31,2012 vyombo vyote vya utangazaji viliitwa na kusaini makubaliano ya kuzima mitambo na kuanza kurusha kwa njia ya dijitali.



Nayo Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imesema haitarudi nyuma kwenye suala la kutumia mfumo wa matangazo kupitia njia ya dijitali na kwamba mfumo huo utaendelea kutumika.
 


TCRA ilizima mitambo ya analojia na kuhamia dijitali, Desemba 31, mwaka jana kitendo ambacho Chama cha Wamiliki wa Vyombo vya Habari Tanzania (MOAT) wanadai kimepunguza mapato yanayotokana na matangazo.






Popular Posts

Labels