Saturday, November 17, 2012

TANESCO WASHINDI HUDUMA MBOVU

Shirika la Ugavi wa Umeme nchini Tanzania (TANESCO)  limeibuka mshindi wa jumla wa kero kwa wateja wa huduma mbalimbali na  bidhaa hapa nchini kupitia mchakato unaoendelea kupitia mitandao ya kijamii ya Twitter na Facebook.

 Nafasi ya pili ilishikiliwa na Kampuni ya mawasiliano ya Tigo na ya tatu kuchukuliwa na kampuni ya mawasiliano ya Vodacom.

Katika mzunguko wa kwanza jumla ya makampuni 29 yaliingia katika kinyanganyiro na kufanikiwa kuchukua ushindi katika makundi mbalimbali .

Katika kundi la huduma za usafiri wa Anga , Shirika la Ndege la Precision ndio liliongoza kwa kero na huduma zisizo na uhakika huku kundi la huduma za maji likishikiliwa na Dawasco.

Kwa upande wa usafiri wa mabasi Kampuni ya Happy Nation iliongoza kwa malalamiko kutoka kwa wateja huku kundi la ving’amuzi vya Televisheni likiongozwa  na Star Times.
 
Kwa upande wa huduma za maegesho ya magari , eneo la Magogoni Ferry limelalamikiwa na wateja kwa huduma mbovu na kufanikiwa kushika nafasi za juu katika kundi hilo.

Kwa upande wa wateja wanaolipia huduma za Televisheni kituo cha TBC pekee ndicho kimelalamikiwa kwa kutokuwa na huduma za uhakika kwa watazamaji wake.

Katika kundi la huduma za mawasiliano ya simu za mkononi , Kampuni ya Tigo ndiyo iliibuka  mshindi ikifuatiwa na Kampuni ya Vodacom.

Zoezi hili la kukusanya kero linafanywa na Wananchi  kupitia akaunti ya Twitter inayopatikana kupitia @hudumambayatz na facebook group iliyopewa jina la HUDUMA BONGO ambapo huduma na bidhaa zote zinazolipiwa na wateja mfano Burudani, Elimu, Hospitali, Hoteli, n.k zinazowakera wateja zitaingia katika kinyanganyiro hicho.

Washauri wa kibiashara wa Huduma Bongo wanatoa wito kwa viongozi wa juu wa Mashirika yote 29 yaliyotajwa kuchukua hatua madhubuti za kuhakikisha wateja wao wanapata huduma bora kulingana na fedha wanazotoa ili kuweza kuleta maendeleo ya Taifa.

Zoezi hili linaendelea ambapo katika mzunguko wa kwanza jumla ya kero 119 ziliwasilishwa na wateja endapo msomaji una kero iliyoshindwa kupatiwa ufumbuzi na watoa huduma hawa unahitajika kuwa na akaunti inayotambulika ya Twitter au Facebook na kujiunga na Huduma Bongo kisha ueleze kero yako. Ukweli na Haki kuzingatiwa

  Chanzo:wavuti.com
 

Friday, November 16, 2012

ELIMU YA TEKNOHAMA YAHIMIZWA

Wadau kutoka kampuni na mashirika mbalimbali nchini Tanzania wameshauri kutolewa elimu zaidi kuhusu matumizi sahihi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Teknohama) na ufanisi wake ili kuleta tija kwa watanzania wengi.

Wakizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa warsha ya Teknohama iliyotolewa na ubalozi wa Marekani nchini Tanzania,wadau hao walisema ni muhimu kwa wadau wengine ikiwamo serikali kuandaa mafunzo kama hayo kwani kuna mambo mengi ya msingi ambayo bado yanasumbua katika matumizi sahihi na ufanisi wa Teknohama.

Mmoja wa maofisa wa ubalozi wa Marekani Jeffrey Shrader alisema waliandaa warsha hiyo kwa sababu ya kukua kwa kiasi kikubwa kwa Teknolojia ulimwenguni hivyo ni vyema kuwaelimisha wengine ambao hawafahamu.

Katika warsha hiyo wakufunzi mbalimbali walitoa mada zinazohusiana na Teknohama ikiwemo ulinzi wa mawasiliano kama vile komputa na simu,mfumo wa uendeshaji wa mambo ya kuchukua na kutumia taarifa katika mitandao.

MATUMIZI YA KADI MOJA YA SIMU KWA MITANDA TOFAUTI YAJADILIWA DAR ES SALAAM

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania jana ilianza kuendesha mkutano wa kimataifa kuhusu usimamizi na utekelezaji wa huduma ya simu za mkononi kwa kutumia kadi moja ya simu kwa mitandao yote bila kuwa na simu kadi nyingi za mitandao tofauti.

Akizungumza kwenye ufunguzi wa mkutano huo wa siku mbili Mkurugenzi Mkuu wa TCRA,Profesa John Nkoma, alisema kadi moja ya simu ya mkononi inaweza kutumika katika zaidi ya mtandao mmoja wa simu kama mteja atataka kuhama kutoka mtandao mmoja kwenda mwingine bila kununua kadi nyingine ya simu kama ilivyozoeleka.

Alisema lengo la mkutano huo ni kutaka kujadili kwa kina utekelezaji na usimamizi wa huduma maalum ya mawasiliano ya simu ambapo mtumiaji wa simu ya mkononi anaweza kutumia kadi moja tu kama atataka kujiunga na mtandao mwingine.

Huduma hiyo inatarajiwa kuanza mapema mwakani baada ya maandalizi na michakato yote,Huduma hii imeshaanza kutumika nchini Kenya tangu Aprili mwaka jana

TATIZO LA UDANGANYIFU NA WIZI KWA KUTUMIA TEKNOHAMA LIMEKUWA KUBWA DUNIANI

TAARIFA YA TCRA KUHUSU MFUMO MWINGINE WA NAMBA ZA SIMU TANZANIA HII HAPA

Wednesday, November 14, 2012

WATEJA WA SIMU TANZANIA KUHAMA MTANDAO BILA KUBADILIA NAMBA

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) inaandaa utaratibu wa kuanzisha mfumo mpya wa kuhama mtandao bila ya kubadili namba ya simu(MNP) na kuhamia mtandao mwingine.

Mkurugenzi Mkuu wa TCRA,Prof.John Nkoma anasema mfumo huo utawasaidia watu wote wanaotumia simu nchini humo waliokuwa wanashindwa kuhamia mtandao mwingine kwa hofu ya kubadili namba ya simu,lakini baada ya kuzindua mfumo huu watu watahama mitandao kwa urahisi bila kubadili namba za simu.

Anafafanua kuwa mfumo huo utasaidia kuleta ushindani kwa makampuni ya simu na kuleta faida kwa wateja,pia makampuni hayo yataweza kuongeza ubora wahuduma kwa wateja wao.

TCRA imeandaa makutano wa kimataifa ambao utahudhuriwa na watu zaidi ya 100 wa kuzungumzia suala hilo ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa Mawasiliano,Sayansi na Teknolojia nchini Tanzania,Prof.Makame Mbarawa.

Mkutano huo wa siku mbili unaotarajiwa kuanza kesho umeandaliwa kwa ushirikiano na Umoja wa Mawasiliano Duniani (ITU) na utahudhuriwa na wawakilishi mbalimbali kutoka duniani kote zikiwemo nchi za Afrika Mashariki

Katika hatua nyingine Mkurugenzi huyo aliwataka wananchi kununua vinga'amuzi mapema ili kuondokana na usumbufu ambao unaweza kujitokeza baada ya kuhamia katika mfumo wa digital Disemba 31 mwaka huu.

TIGO VS OUR SAFETY



Tigo Tanzania - Dar es Salaam, Tanzania

A failure in contingency planning and disaster recovery
Today, on November 14, 2012 in Tanzania, the TIGO network was completely not accessible. It was not possible to make calls or send messages. TCRA reports that in June 2012 TIGO had Subscriber base of 5,613,330 and 5,509,337 Registered Subscribers (http://tcra.go.tz/publications/telecomStatsJune12.pdf). This means, the outage of the TIGO network today has affected a big number of subscribers, related business and corporate as well and individual networks. A typical example is when one wants to communicate on behalf of his/her organization. It is also possible that individuals want to communicate and do their businesses or need to access their TIGO Pesa accounts. This has not been possible through TIGO.

It is possible to extend this thinking to other aspects of our nation including security and safety both physically and in the cyber space. These issues may need further

discussion.

Few questions are relevant though:

1. Did TIGO think of business continuity and disaster recovery?
2. Can we rely on TIGO for mission critical activities at a national, organizational, and individual levels?
3. Is it possible to now establish a customer compensation mechanism in situation like this?
4. Is it possible that what happened to TIGO can also happen to other providers?
5. Can this situation happen to all providers in Tanzania at once?
6. What is our national Business Continuity plan?
Source:Jim Yonaz on facebook.

Saturday, November 10, 2012

MITANDAO YA KIJAMII KUMTAFUTA BINGWA WA KERO KWA WATEJA TANZANIA


  Jumuia ya watumiaji wa huduma mbalimbali nchini Tanzania kupitia mitandao ya kijamii ya Facebook na Twitter imezindua rasmi shindano la kusaka kampuni zinazotoa huduma na bidhaa mbovu kwa wateja nchini Tanzania. Jumuiya hiyo inawajumuisha watu wa kada mbalimbali wakiwemo wanasheria, wanaharakati, waandishi wa habari, viongozi wa kisiasa, wafanyabiashara na wateja wa huduma na bidhaa mbalimbali nchini Tanzania.

Lengo la jumuiya hiyo ni kushinikiza wafanyabiashara nchini kutoa huduma na bidhaa bora kwa wateja na kuwakumbusha umuhimu wa wateja. Kauli mbiu ya wanajumuiya hao ni Mteja ni Mfalme. Katika wiki ya kwanza tangu jumuiya hiyo kuzinduliwa jumla ya makampuni 21 yameingizwa katika shindano hilo kwa wateja wao kuwasilisha malalamiko yao. Kwa taarifa zaidi kuhusu ni fuatilia akaunti ya Twitter @hudumambayatz au kundi la Facebook linalojulikana kama HUDUMA BONGO.

Ili kuweza kupiga kura yako unahitajika kuwa na akaunti hai (yenye mawasiliano mara kwa mara) katika mtandao wa Twitter au Facebook na kujiunga na jumuiya hiyo. Mara tu utakapowasilisha kero yako utaifanya kampuni unayoilalamikia kuingia katika mchuano mkali wa kumsaka bingwa wa huduma mbovu kwa wateja nchini.

Huduma Bongo inatoa wito kwa makampuni yote kuboresha huduma na bidhaa zao ili kuweza kuwapatia wateja kilicho bora zaidi katika soko hili la ushindani. Imetolewa na Mshauri wa Habari wa Huduma Bongo hudumabongo@gmail.com
Chanzo:thehabari

Friday, November 9, 2012

HOW CAN YOU KNOW IF YOUR CELL/PHONE IS FAKE?


How can you know if your cell/mobile phone is fake? In which country was it manufactured? Simple, through your IMEI number. 

Tested on iPhone, Nokia, Samsung, LG, Sony Ericsson and Motorola phones. However, it should work on any brand.

Press *#06# on your phone and the International Mobile Equipment Identity (IMEI) number appears. Then check the 7th and 8th digit.

1 2 3 4 5 6 7th 8th 9 10 11 12 13 14 15
 Phone IMEI No. x x x x x x ? ? x x x x x x x
 

IF the Seventh & Eighth digits are 02 or 20 this means your cell phone was assembled in China which is of low quality.

IF the Seventh & Eighth digits are
08 or 80 this means your cell phone was manufactured in Germany which is of fair quality.

IF the Seventh & Eighth digits are
01 or 10 this means your cell phone was manufactured in Finland which is of very good quality.

IF the Seventh & Eighth digits are
00 this means your cell phone was manufactured in original factory which is the best phone quality.

IF the Seventh & Eighth digits are
13 this means your cell phone was assembled in Azerbaijan which is of very bad quality and may also be dangerous for your health.
 Source:esoftnetonline








Popular Posts

Labels