Serikali ya Tanzania kupitia Menejimenti ya Utumishi wa
Umma Ofisi ya Rais imesema haitagharamia gharama zozote za kuendesha vikao kazi
na watendaji wake kuanzia sasa, badala yake vikao hivyo vitaendeshwa kwa
kutumia Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEKINOHAMA).
Wahusika wakuu wa vikao kazi
hivyo ni pamoja na Wakurugenzi, Makatibu Tawala wa Mikoa na Maafisa Utumishi wa
Mamlaka za Serikali za Mitaa.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini
Dar es Salaam, Florence Temba, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini na
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, amesema kuwa,
kupitia utaratibu huo washiriki wa vikao hivyo watabaki katika maeneo ya kazi
ambapo wataunganishwa na mtandao wa pamoja kwa mfumo wa kuonana na kuongea uso
kwa uso.
Aidha amewatoa hofu watumishi Kuhusu
miondombinu ya mawasiliano kwa kusema Mfumo huo ni salama hakuna haja ya
kuhofia kuhusu kukatika kwa umeme au hali ya hewa kwani mpango huo unaratibiwa
na serikali hivyo ikitokea hali kama hiyo kutakuwepo na umeme wa ziada au kwa
kutumia mkongo wa Taifa wa mawasiliano.
Meneja Mauzo wa mkoa wa Tanga kutoka Tigo Bw.Daniel Mainoya akiongea na waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali , kuhusu uzinduzi wa kifurushi kilichoboreshwa cha University Pack kutoka Tigo katika Uwanja wa chuo cha Utumishi wa Umma, Kange, mjini Tanga.
Mwanafunzi kutoka chuo
cha Utumishi wa Umma, Kange,mjini Tanga, Bi.Stella Mwakiliku akiongea na waandishi
wa habari kutoka vyombo mbalimbali kuhusu vipi wanafunzi wamekikubali kifurushi
hicho kilichoboreshwa cha University Pack kutoka Tigo.
Mwanafunzi kutoka chuo
cha Utumishi wa Umma, Kange, Bw.Albert Risala akiongea na waandishi wa habari kutoka
vyombo mbalimbali kuhusu vipi wanafunzi wamekipokea kifurushi hicho
kilichoboreshwa cha University Pack kutoka Tigo.
Kikundi cha sarakasi kikitumbuiza wanafunzi katika uzinduzi wa kifurushi cha University
pack kilichoboreshwa katika uwanja wa chuo cha Utumishi wa Umma,Kange, mjini
Tanga.
Msanii wa kizazi kipya
Roma Mkatoliki akiwatumbuiza wanafunzi wa chuo cha Utumishi wa Umma,Kange,
mjini Tanga,katika uzinduzi wa kifurushi cha University pack kutoka Tigo kilichoboreshwa.
Kampuni ya simu za mkononi ya Tigo imezindua
kifurushi maalum kinacho wawezesha wanafunzi, ambao ni wateja wa Tigo, kuweza kupigiana
simu bure.
Huduma hii imeboreshwa zaidi baada ya kifurushi
hicho kwa jina maarufu kama Tigo Uni Pack kuzinduliwa mwaka jana, ukilinganisha
na kifurushi cha zamani, kifurushi hichi kipya cha wiki kitawapatia wanafunzi
wepesi wa kujiunga wakiwa popote ndani ya nchi, hii ni kwa mujibu wa taarifa
iliyotumwa kwa vyombo vya habari na kampuni ya Tigo leo.
Kinachohitajika ili wanafunzi waweze kutumia
huduma hii,ni kuhakiki kwamba wamesajiliwa kama wateja wa Tigo katika Vyou
vyao, ujumbe huo ulisema.
Akizungumzia kifurushi hicho kilichoboreshwa,
Meneja wa Bidhaa kutoka Tigo Edwin Mgoa,alisema kifurushi hicho cha Uni Pack,
kinadhirisha vipi Tigo inavyowasaidia wanafunzi kwa ajili ya kuwawezesha kuweza
kupata huduma za mtandao za maisha ya kidijitali.
Baadhi ya huduma za kidijitali zinazotelewa na
Tigo ni upatikanaji wa muziki bila kikomo kwa kupitia huduma ya Tigo Music,
Facebook ya Kiswahili, Tigo Pesa App, Tigo Backup- huduma inayowawezesha wateja
wa Tigo kuweza kurudisha simu na
zinapoibiwa au kupotea.
Kujisajili
kwa kifurushi cha Uni Pack, mwanafunzi atahitajika kupiga *148*01*20#, namba
ambazo kwa mujibu wa taarifa hiyo, imejumuisha vifurushi vingine muruwa kutoka
Tigo.
Baadhi ya Kompyuta zilizotolewa na Kampuni ya Vodacom kama msaada wa shule ya sekondari ya Shimbwe iliyopo wilayani Moshi vijijini.
Mkuu wa Vodacom kanda ya Kaskazini ,Henry Tzamburakisi akizungumza jambo na mkuu wa shule ya sekondari Shimbwe,Jacob Costantine alipotembelea darasa la Kompyuta shuleni hapo.
Mmoja wa wafanyakazi wa shirika lisilo la kiserikali la Learning Insync akijaribu kuunganisha nyaya katika darasa la kompyuta lilopo shule ya sekondari Shimbwe iliyopo Uru wilaya ya Moshi vijijini.
Mkuu wa Vodacom kanda ya Kaskazini,Henry Tzamburakisi (kushoto) akiwa katika darasa la Kompyuta katika shule ya Shimbwe Sekondari ,wengine ni baadhi ya walimu katika shule hiyo ambao wamepatiwa mafunzo ya kompyuta.
Lisa Wolker akitoa maelekezo kwa walimu na wanafunzi.
Walimu na wanafunzi katika shule hiyo wakisikiliza kwa makini.
Mafunzo juu ya matumizi ya Programu maalumu ya kufundishia na kujifunzia yakiendelea katika darasa la Kompyuta katika shule ya sekondari ya Shimbwe.
Mkuu wa Vodacom Kanda ya Kaskazini Tzamburakisi akielekeza jambo kwa wanafunzi.
Jumla ya Kompyuta 30 zimetolewa na Vodacom kupitia mfuko wa Vodacom Foundation kwa shule ya sekondari Shimbwe ikiwa ni pamoja na upatikanaji wa wataalamu wanao toa mafunzo ya matumizi ya Programu maalumu za kufundishia katika shule hiyo.
Msemaji
Mkuu wa Serikali ya Tanzania, Assah Mwambene amekanusha taarifa zinazosambaa
katika mitandao ya kijamii kuhusu Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa kuwa amefariki
Dunia.
Akizungunza na waandishi wa habari Hii leo
katika ukumbi wa Habari Maelezo jijini Dar es Salaam, Mwambene amesema Rais
Mkapa yupo salama na mzima wa afya na hakuna maradhi yoyote yanayomsumbua.
Mwambene
amewaasa watumiaji wa mitandao mbalimbali hasa Blogs kuacha kuitumia mitandao
hiyo kwa kupotosha umma na kuandika mambo yasiyo na ukweli ili kuepusha mifumuko
ya habari za upotishaji.
Aidha
amesema Serikali italishughulikia hili na tayari imeshaanza kukamata baadhi ya
watu mbalimbali ambao wanatoa taarifa za uongo zinazopelekea umma kupotoka.
Amesema
kuwa vyombo vya habari vifanye kazi kwa uweredi ili kazi ya uandishi wao iwe ya
usawa na kufuata misingi ya uandishi, jambo ambalo wengi hukiuka kutokana
kutofuata weredi wa kazi zao.
Dr John Pombe Magufuli leo Oktoba 29,2015 alitweet kwenye account yake ya twitter ya https://twitter.com/MagufuliJP @MagufuliJP kabla ya kutangazwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, miongoni mwa wagombea 8 waliokuwa wakigombea nafasi hiyo katika uchaguzi Mkuu wa Tanzania uliofanyika Oktoba 25,2015
Katika account yake Dr John Pombe Magufuli ambaye anakuwa Rais wa Tanzania awamu ya tano alitweet kwa mara ya mwisho Oktoba 24 ukiondoa zile alizoretweet za account ya twitter ya chama chake cha Siasa.
Polisi nchini Ujerumani wameonya wazazi dhidi ya kuweka picha za watoto wao hadharani katika mtandao wa kijamii wa Facebook.
Katika ujumbe kwenye ukurasa wao wa Facebook, polisi wa eneo la Hagen
wametahadharisha wazazi kuwa picha hizo zinaweza kunakiliwa au
kubadilishwa na kutumiwa vibaya na watu wanaovutiwa kimapenzi na watoto.
Aidha, watoto wahusika huenda wasipendezwe na picha hizo kuwa wazi
mitandaoni watakapokomaa na kuwa watu wazima. Wazazi wameshauriwa
kuhakikisha kuwa picha hizo, ikilazimu, zinatazamwa na marafiki zao
pekee na si kila mtu mtandaoni.
Ushauri huo wa polisi hao umeenezwa sana mtandaoni na kuvutia hisia
mseto. Afisa msemaji wa Polisi wa Hagen ameiambia BBC kwamba
walishangazwa na jinsi ujumbe huo wa tahadhari ulivyopokelewa. Amesema
wanakadiria kuwa umesomwa na watu zaidi ya milioni 12.
Bw Hanki ameongeza kuwa ujumbe huo haujaongozwa na matukio yoyote mapya
ya kesi za uhalifu au watu wanaovutiwa na watoto kimapenzi huko Hagen.
Picha zilizobadilishwa
Shirika la kujitolea linalohusika na ulinzi wa watoto NSPCC katika
taarifa yao wamesema: " Wazazi wote wanapaswa kujisikia huru na
kufurahia kuchukua picha za watoto wao na kushirikiana nao na marafiki
na familia. Hata hivyo, tunapaswa wote kuwa makini wakati wa kuziweka
picha hizo mitandaoni.
"Tunajua kwamba wahalifu wa ngono wana uwezo wa kubadilisha picha za
watu wasiokuwa na hatia, na maendeleo katika programu za kuhariri picha
zimefanya hili kuwa rahisi sana.
" Hivyo kama wazazi watachapisha picha za watoto wao kwenye mitandao,
wanapaswa kuchukua hatua ili kuhakikisha kwamba wanachunguza hali yao ya
faragha na kuhakikisha wanaridhishwa na watu watakaotazama picha hizo."
Shirika hilo limeongeza kuwa iwapo wazazi wana wasiwasi kuwa picha ya
mtoto wao imeanguka mikononi mwa watu wabaya, wanapaswa kuwasiliana na
Internet Watch Foundation, Child Exploitation na Online Protection
Centre (Ceop) au kuwasililiana na NSPCC kupitia numbari ya msaada ya
simu ya 0808 800 5000 ambapo watapokeza usaidizi.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Dk. Kamugisha Kazaura (kulia) akikata keki katika moja ya tawi la ofisi za kampuni hiyo jijini Dar es Salaam kuzinduwa wiki ya huduma kwa wateja. Kampuni ya simu ya TTCL leo imezinduwa wiki ya huduma kwa wateja ambayo ilianza Oktoba 12 hadi 16, 2015.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Dk. Kamugisha Kazaura akisaini kitabu cha wageni katika moja ya tawi la ofisi za kampuni hiyo jijini Dar es Salaam kwenye hafla ya uzinduzi wa wiki ya huduma kwa wateja. Kampuni ya simu ya TTCL leo imezinduwa wiki ya huduma kwa wateja ambapo inaanzia Oktoba 12 hadi 16, 2015.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Dk. Kamugisha Kazaura akisalimiana na mmoja wa wateja waliofika kupata huduma katika tawi la ofisi za kampuni hiyo jijini Dar es Salaam lililopo Makao Makuu ya kampuni hiyo, kabla ya kumlisha keki kwenye hafla ya uzinduzi wa wiki ya huduma kwa wateja.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Dk. Kamugisha Kazaura (kushoto) akimlisha keki mmoja wa wateja wa kwanza waliofika kupata huduma katika moja ya tawi la ofisi za kampuni hiyo jijini Dar es Salaam kwenye hafla ya uzinduzi wa wiki ya huduma kwa wateja. Kampuni ya simu ya TTCL imezinduwa wiki ya huduma kwa wateja ambapo ilianza Oktoba 12 hadi 16, 2015.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Dk. Kamugisha Kazaura (kushoto) akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya uzinduzi wa wiki ya huduma kwa wateja leo jijini Dar es Salaam. Kampuni ya simu ya TTCL imezinduwa wiki ya huduma kwa wateja ambapo inaanzia Oktoba 12 hadi 16, 2015.
Meneja wa Kanda ya TTCL Dar es Salaam Kati, Jane Mwakalebela (kushoto) akimlisha keki Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Dk. Kamugisha Kazaura kwenye hafla ya uzinduzi wa wiki ya huduma kwa wateja.
Ofisa Mkuu wa Mauzo na Masoko wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Peter Ngota akifafanua jambo kwa wageni waalikwa kwenye hafla fupi ya uzinduzi wa wiki ya huduma kwa wateja jijini Dar es Salaam.
Hapa ni wakati wa kugonganisha glasi za mvinyo kutakiana afya njema na utendaji bora...!
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Dk. Kamugisha Kazaura (kulia) akitoa zawadi kwa mmoja wa wateja wa kwanza waliofika kupata huduma katika moja ya tawi la ofisi za kampuni hiyo leo jijini Dar es Salaam kwenye hafla ya uzinduzi wa wiki ya huduma kwa wateja.
Baadhi ya wateja wa kwanza wa TTCL waliofika kupata huduma leo katika matawi ya huduma kwa wateja ya jijini Dar es Salaam wakiwa katika picha ya pamoja na zawadi zao na Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Dk. Kazaura (katikati) kwenye hafla ya uzinduzi wa wiki ya huduma kwa wateja.
Akizungumza na baadhi ya wateja wa TTCL, maofisa na wafanyakazi jijini Dar es Salaam Mkuu wa Idara ya Huduma kwa Wateja TTCL, Laibu Leonard alisema ndani ya maadhimisho hayo maofisa wa TTCL watapita kuwatembelea wateja ofisini na majumbani kuwasikiliza maoni yao ikiwa ni pamoja na kupata mrejesho juu ya huduma wanazozitoa.
Alisema maofisa waandamizi wa kampuni hiyo watashiriki moja kwa moja katika zoezi hilo la kutoa huduma pamoja na kuwatembelea wateja kupata maoni yao na pia kutoa shukrani kwa wao kukubali kuhudumiwa na kampuni hiyo ya simu ya kizalendo nchini Tanzania.
"...Mbali na kutoa huduma zetu katika matawi mbalimbali katika kipindi hiki maofisa waandamizi wa TTCL watawatembelea wateja moja kwa moja katika ofisi zao au majumbani kwa ajili ya kuwasikiliza na pia kupokea naoni yao," alisema Leonard akizungumza katika hafla hiyo.
Katika uzinduzi wa hafla hiyo TTCL ilitoa zawadi kwa wateja watano wa mwanzo waliofika katika vituo vya huduma kwa wateja leo asubuhi kuhudumiwa na kampuni hiyo pamoja na kuwazawadia maofisa wa TTCL waliofanya vizuri zaidi katika idara ya huduma kwa wateja ya kampuni hiyo, ikiwa ni motisha ya kuchochea utendaji bora zaidi.
*Imeandaliwa na www.thehabari.com
Tukio la kipekee katika anga ya
usalama mitandao ambalo limekualiki azimishwa kila mwaka katika mwezi
wa Oktoba ambapo mataifa yanaadhimisha siku ya uelewa wa maswala ya
usalama mitandao duniani kote.Na imani
Mwaka huu Tanzania itauchukulia mwezi huu kinamna ya kipekee ili
kuweza kukuza uelewa kwa watu wake Tukio ambalo nategemea makampuni
mbali mbali na maeneo mengine yataandaa program mbali mbali za kukuza
uelewa wa maswala ya usalama mitandao ili kuweza kufikiwa malengo
yaliyokusudiwa na wanausalama wote mitandao duniani kote. Aidha, inaaminika kama ilivyo katika uhalifu mwingine wowote ni vigumu kumaliza kabisa
tatizo ila kuna njia kadhaa ambazo kwa umoja wake zikifanyiwa kazi vizuri
zinaweza kabisa kupunguza kwa kiasi kikubwa sana tatizo la uhalifu mtandao.
Tatizo
kubwa kubwa ni kuwa njia hizi zimekua zikiishia katika maandishi baada ya
kujadiliwa na wanausalama mitandao ambapo mimi binafsi nilikua miongoni mwao.
Kwa
kupata
elimu hii wale wote waliokua wakifanya uhalifu mtandao pasi na kujua
wanakua na ufahamu wa kutosha na hatimae kundi hili linakua limeondokana
na
uhalifu mtandao. Aidha, kundi la pili ambalo ni lile linalofanya
uhalifuu huu wa mtandao wakiwa hawana namna kwa kutokujua athari zake
baada ya kujua athari za uhalifu mtandao kwao
na kwa wengine na pia kujua njia mbadala wanazoweza kutumia kuepukana na
uhalifu huu kupitia elimu ya uelewa ya usalama mitandao kundi hili
linaweza pia likapunguzwa hadi asilimia 84% kwa mujibu wa wataalam
wa usalama mitandao.
Kundi
la mwisho ambalo ni wahalifu wanaofanya uhalifu huu makusudi ingawa wanajua
wakifanyacho na hawana utayari wa kuepukana na uhalifu huu mtandao nalo
linapunguzwa nguvu kwani watumiaji mitandao wanakua na uelewa wa namna wahalifu
hawa wanavyo fanya uhalifu na njia sahihi za kujilinda hatimae kundi hilipia
linakosa watu wengi wanaoweza kuingia katika mtego wao wa uhalifu mtandao na
kupungukiwa kasi na nguvu ya usambazaji wa uhalifu huu.
Inaaminika
asilimia zaidi ya 37% ya wahalifu wa kundi hili la tatu wanapokosa watu
wanoweza kuingia mtegoni wanajikuta wanakata tama na kujishughulisha na mambo
mengine tofauti na uhalifu mtandao.
Kumekua
na wimbi kubwa la makampuni mengi mbali na kua na teknolojia nzuri ya kuzuia
uhalifu mtandao bado yameendelea kugubikwa na uhalifu mtandao kutokana na
kutowekea mkazo swala hili la kukuza uelewa wa maswala haya ya usalama
mitandao. Pia mataifa mengi yameendelea kujipanga kwa kua na vitengo kadhaa vya
udhibiti uhalifu pamoja na kua na sharia sahisi za kudhibiti uhalifu huku bado
wimbi kubwa la wahalifu mtandao bado likiendelea kua kubwa.
Tatizo
ni kukosekana na njia sahihi na namna madhubuti ya kuendea njia hii ya kukuza
uelewa wa maswala ya usalama mitandao ambapo kama nilivyo fafanua awali
ingeweza kabisa kupunguza kwa kiasi kukubwa swala hili la uhalifu mtandao.
Kumekua
na jitihada nyingi za kuhamasisha kuanzia ngazi ya mtu binafsi, Makapuni ,
Nchi, Bara na hatimae Dunia nzima kujenga tamaduni ya kukuza uelewa wa matumizi
salama ya mitandao ili kukabiliana na wimbi kubwa la uhalifu unaoendelea kukua
kwa kasi hivi sasa.
Swali
linaloulizwa ni kwamba pamoja na jitihada nyingi za wanausalama mtandao ambapo hadi sasa pamoja
na mambo mengine, tayari kuna mwezi wa Kumi ambao unafahamika kama mwezi maalum
wa maswala ya uelewa wa usalama mitandao yaani “OCTOBER" – Cybersecurity
Awareness Month” na kupatikana kwa
tamthilia maalum ambazo zipo kukuza uelewa wa usalama mitandao.
Jibu
ni kwamba, Jitihada hizi zimebaki kwa wanausalama mitandao na wananchi
wakawaida bado imekua ni vigumu sana kufikiwa na kuelewa pamoja na kua miongoni
mwa jitihada hizi.
Wengi
bado wamebaki wakijua swala la ufahamu na uelewa wa maswala ya usalama mitandao
ni swala la wanausalama mitandao pekee huku wengine wakiamini pia wana TEKINOHAMA
ndio pia wanausika.
Inasahaulika
kabisa swala la kubaki salama kimtandao ni swala linalo takiwa kuanzia katika
ngazi ya mtu binafsi sawa kabisa na swala la ulinzi wa uhalifu mwingine wowote.
Tumekua na utamaduni wa pamoja na mambo mengine, kufunga milango, kuwa na
walinzi katika nyumba zetu na kuweka taa za nje tukiamini zinauwezo wa kusaidia
upungufu wa uhalifu majumbani mwetu.
Cha
kushangaza zaidi, Jitihada hizi binafsi huzioni zikiamishiwa katika udhibiti wa
uhalifu huu wa mitandao ambapo vitu kama Antiviruses, Maneno ya siri na
mengineyo ni ya kuanzia katika ngazi ya mtu binafsi.
Kuna
Kila namna ya kufahamu kua pale swala la uelewa wa maswala ya usalama mtandao
litakapoweza kufanyiwa kazi kwa kiwango kizuri basin i wazi kabisa linaweza
kusaidia kila mmoja kuelewa na kuhimili ipasavyo uhalifu huu mtandao katika
ngazi ya mtu binafsi, pamoja na kukuza utamaduni wa kila mmoja kujua anajukumu
ssi tu la kujilinda binafsi kimtandao bali na kulinda wengine ipasavyo kuhakiki
taifa, bara na hatimae dunia inabaki salama kimtandao.
Kwa
ufupi nimefafanua kwa kina faida zinazoweza kupatikana pale uelewa sahihi wa elimu
ya usalama mtandao itapatikana kwa jamii zetu na katika maofisi yetu (Makampuni)
Maelezo hayo yanawea kusomeka kwa ku “BOFYA HAPA” Wakati huo huo nilipozungumzia
mambo muhimu yanayo paswa kuenda sambamba na uwepo wa sharia mpya ya usalama
mitandao niliainisha kwa kina swala la uelewa sahihi wa maswala ya usalama
mitandao pamoja na ujuzi wa kufanyia kazi uchunguzi wa uhalifu mtandao na
ushirikiano kama inavyoweza kufatiliwa katika video hii hapo chini.
Leo
nitaangazia njia ambayo imeshika nafasi ya juu na imeonekana na uwezo mkubwa wa
kuhimili uhalifu mtandao ambapo imeaminika inauwezo wa kupunguza aina mbili za
wahalifu mtandao pamoja na kusababisha aina ya tatu kupungua makali. Kwa ujumla
wake imezungumzwa inaweza kupunguza hadi asilimia 71% ya uhalifu wote mtandao
kama itafatwa vizuri na kupewa uzito wa kipekee katika mataifa yote.
Njia
hii si nyingine bali ni “Awareness
Program” Yaani elimu ya uelewa wa uhalufu mtandao na namna ya kujilinda.
Elimu hii inatoa fursa kwa mwananchi wa kawaida kutambua aina mbali mbali za
uhalifu mtandao, athari zake, njia ya kujilinda, Na Namna ya kulinda wenzake.
Natoa
wito kwa kila mmoja wetu kukuza upendo wa kufatilia na kutaa kujua namna mbali
mbali za kuweza kujilinda katika ngazi ya mtu binafsi na uhalifu huu mitandao
unaokua kwa kasi zaidi hivi sasa huku makampuni kua na tamaduni ya kuwa na
mafunzo maalum ya maswala haya na taifa kwa ujumla kuhakiki linaongeza jitihada
katika kukuza uelewa kwa wananchi katika maswala ya usalma mitandao ili
kukabiliana na ongezeko la uhalifu mtandao nchini. Na:Yusuph Kileo