Thursday, June 16, 2016
MWANZA:KAMATI YA MAWASILIANO MKOA YATOA ELIMU KWA WATUMIAJI WA HUDUMA ZA MAWASILIANO
Tuesday, May 24, 2016
UfUNGWAJI WA SIMU BANDIA JUNI 16, 2016
Hadi kufikia juni 16 mwaka 2016 , Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) itakua imeshafunga simu nyingi bandia pamoja na vifaa vingine vya mawasiliano ambavyo havikidhi viwango na mahitaji ya soko la tanzania . Kama mtanzania kuna mambo kadhaa unatakiwa kujua kuhusu simu bandia na vifaa vya mawasiliano
Simu zote na vifaa vyake wakati vinatengenezwa mpaka kupitishwa kutumiwa huwa vinapitia katika taratibu kadhaa zinazohusu ubora na mahitaji ya kibinadamu ambayo hayaleti madhara yoyote kwa afya na mazingira . Simu bandia hazipitii utaratibu huu wala ukaguzi na wala hazijulikani watengenezaji wake wala zilipotoka ili kufuatilia . matokeo yake zinaweza kuleta athari za kiafya na mazingira kama nilivyosema hapo awali .
Kama simu itakuletea madhara ya kiafya ina maana utatumia muda na gharama nyingi kujipatia matibabu yaliyotokana na madhara kadha wa kadha hapo sio kila mtu ana uwezo wa kugharamia au kugharamiwa , kama ulikua umajiajiri basi biashara au mengine yanaweza kufa kwa sababu ya matibabu na mengine lakini ungekua na kifaa kizuri shida hii usingeweza kuipata kwa sababu ingekua na viwango vya kutosha .
Hapo pia kuna suala la kupeleka simu kwa fundi mara kwa mara kwa sababu ya ubovu au mengine ambayo simu haiwezi kufanya kutokana na viwango vyake havifu kwa mwananchi wa kawaida hii pigo kwake , wengine wanaweza kuamua kununua nyingine tu maana gharama zake pia ni nafuu kulinganisha na zile halisi zenye vitu vinavyolingana .
Simu bandia na vifaa vyake huingizwa nchini kupitia njia za panya maana kama zikikaguliwa zitagundulika na kuharibiwa na wahusika kufikishwa katika vyombo vya sheria , hii ina maana serikali ina kosa mapato kutokana na kodi , ajira zinapungua na huduma nyingine zinakosekana kutokana na hujuma kama hii .
Kumbuka kwamba wauzaji wote wa vifaa vya mawasiliano kama simu husajiliwa TCRA ambapo ada yake kwa mwaka ni laki 5 kwahiyo huwa na kibali Fulani , kama mtu hana kibali cha kuuza vifaa hivi maana yake unatakiwa kuwa na mashaka nae ni vizuri ukafikisha taarifa kwa mamlaka ya mawasiliano haraka ili hatua kuchukuliwa .
Kiusalama wa kawaida pia matumizi ya simu bandia na vifaa vyake yanaweza kuleta mambo mengi mfano ni suala la wizi wa mtandao kwa kuwa simu inakua haina mfumo mzuri na wa uhakika wa kujilinda na kwa hizi za kisasa hata antivirus na nyingine hautaweza kuweka , mhalifu anaweza kuingilia kwa urahisi hata kutokea maeneo mengine .
Kuna tukio lilitokea Saudi Arabia mwaka jana ambapo gaidi alifanikiwa kuingia katika kambi ya polisi akajitoa mhanga na kuua wengine 30 . katika tukio hili iligundulika kwamba gaidi huyu na mtandao wake walikua wanatumia simu bandia na kujisajili line kutumia majina ambayo sio yao na matokeo yake ni kufanikiwa kupita vizuizi vyote mpaka eneo nyeti la kambi ya polisi .
Kuanzia tukio hilo Serikali ya Saudi Arabia ilitoa tangazo la kufungwa wauzaji wote wa simu bandia na laini zisizosajiliwa .
Tukio kama la Saudi Arabia linaweza kutokea hata Tanzania na maeneo mengine mengi kama matumizi ya simu bandia na vifaa vyake yakiendelea bila kikomo .
Mwanzo wa Mwaka 2016 , Benki moja maarufu ilitaka kuibiwa milioni 900 kwa njia ya mtandao baada ya kununua kifaa bandia cha mawasiliano ya kiofisi , wahalifu walitumia kifaa hiko kuingilia akaunti za benki ili kuhamisha fedha ila kuna vitu walikwama na miongoni ni ujuzi wao katika matumizi ya Lugha lakini suala ni ununuzi wa kifaa bandia cha mawasiliano .
Pia suala la Ushindani wa kibiashara na Ubinifu hupotea na kufa kabisa katika maeneo ambayo biashara za vitu bandia hushamiri , mtu mwenye simu bandia ya Nokia 200 kwa mfano atauza shilingi 4 wakati ile halisi ni 8 hii ina maana baada ya muda mfupi Yule wa 8 anaweza kufunga biashara yake na kufuta wafanyakazi waliobuni kifaa husika , kukijaribu , kukitafutia masoko na mengine mengi . sasa muwekezaji hatapenda kuwekeza Tanzania akijua kuna soko kubwa la vitu bandia .
Kama unafanya kazi zako kutumia simu , ukiwa na simu bandia utaweza kuona ubora wa picha , sauti , cover , kioo na vitu vingine unavyokua mbaya kulinganisha na vile vilivyoko katika simu original yenye ubora wa uhakika . kwahiyo utaweza kukosa kazi kwa kuharibu kazi kwa kutumia vifaa bandia visivyokidhi mahitaji .
Suala la vitu bandia liko katika vitu vingi tu ambavyo tunajua madhara yake kama spea za magari ambazo huchangia katika ajali za mara kwa mara , vifaa vya ujenzi ambavyo huchangia majengo kuporomoka au kuwaka moto .
Vita dhidi ya vifaa bandia viko dunia nzima , sio Tanzania tu , kwahiyo tuunge mkono jitihada hizi za serikali chini ya TCRA , POLISI , TBS na mamlaka nyingine zenye uwezo huo kisheria ili kulinda nchi na watu wake .
Mwandishi wa makala hii hana uhusiano na kampuni yoyote ya simu wala mamlaka ya mawasiliano tanzania . Ulichomaliza kusoma ni kwa ajili ya kujifunza ili kuelimika kisha usaidie wengine .
YONA FARES MARO
0786 806028
Sunday, April 24, 2016
WIZARA YA UJENZI ,UCHUKUZI NA MAWASILIANO YAENDELEA NA MCHAKATO WA UKUSANYAJI MAONI JUU YA UBORESHAJI SERA YA TAIFA YA (TEHAMA)MKOANI MBEYA
Mkurugenzi
Msaidizi anayeshughulikia masuala ya Simu katika Wizara ya Ujenzi
,Uchukuzi na Mawasiliano Ndugu John Mwera akizungumza na wanahabari
katika viwanja vya Chuo Cha Uhasibu jijini Mbeya( TIA ) juu ya zoezi la
uchukuaji maoni na ushauri kwa wadau katika kuboresha sera ya Taifa ya
Habari ,Teknologia na Mawasiliano (TEHAMA).
|
Mhandisi
Enock Mpenzwa Idara Mawasiliano toka Wizara ya Ujenzi ,Uchukuzi na
Mawasiliano akizungumza na wanafunzi wa shule ya sekondari ya Forest
jijini Mbeya waliofika kwa ajili ya zoezi la utoaji maoni na ushauri juu
ya uboreshaji wa sera mpya ya Taifa ya TEHAMA katika viwanja vya Chuo
Cha Uhasibu TIA jijini Mbeya April 22 ,2015.
|
Baadhi
ya wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Forest jijini Mbeya wakiwa katika
foleni ya kujiandikisha ili kutoa maoni yao na ushauri juu ya
uboreshaji wa sera ya Taifa ya TEHAMA,zoezi ambalo limefanyika katika
viwanja vya Chuo Cha Uhasibu Mbeya (TIA) April 22 ,2015.
|
Mwanafunzi
shule ya sekondari Forest jijini Mbeya Mariam Jordan akijiandikisha kwa
ajili ya kutoa maoni yake katika zoezi la uboreshaji wa sera ya Taifa
ya TEHAMA zoezi ambalo limeratibiwa na Wizara ya Ujenzi ,Uchukuzi na
Mawasiliano ,katika viwanja vya Chuo Cha Uhasibu Jijini Mbeya( TIA)
|
Baadhi
ya wanafunzi wa Chuo Cha Uhasibu Jijini (TIA)wakijibu baadhi ya Maswali
kama sehemu ya ukusanyaji maoni ili kuboresha sera ya TEHAMA .
|
Baadhi
ya wanafunzi wa Chuo Cha Uhasibu Jijini (TIA) na wadau mbalimbali
kutoka Mkoani Mbeya wakijibu baadhi ya Maswali kama sehemu ya ukusanyaji
maoni ili kuboresha sera ya TEHAMA .
|
Thursday, April 7, 2016
WHATSAPP YALINDA UJUMBE WA WATUMIAJI WAKE
Hatua hiyo itaufanya ujumbe huo kutosomeka iwapo mhalifu ama hata maafisa wa polisi wanajaribu kuingilia simu bila idhini.
WhatsApp ambayo ina wateja zaidi ya bilioni moja duniani imesema kuwa uhamisho wa faili pamoja na sauti pia zitalindwa.
Huduma hiyo inayomilikiwa na kampuni ya Facebook imesema kuwa ulinzi wa mawasiliano ya faragha ni miongoni mwa malengo yake.
Ulinzi huo uliathiriwa wakati shirika la Marekani la FBI lilipotaka kampuni ya Apple kuisadia kuchukua data katika simu moja ya iphone iliotumiwa na muuaji Syed Farook.
Whatsapp ilisema:Wazo hilo ni rahisi, unapotuma ujumbe mtu pekee anayeweza kuusoma ni mtu ama kundi la mawasiliano ambalo umelitumia ujumbe huo.
Hakuna mtu anayeweza kuusoma ujumbe huo hata kama ni wahalifu wa mitandaoni ama hata serikali.hata sisi hatuwezi kuusoma.
Watumiaji wapya wa huduma hiyo waliarifiwa kuhusu mabadiliko hayo wakati wanapotuma ujumbe siku ya Jumanne ya April 5,mwaka huu
Wednesday, April 6, 2016
NJIA ZINAZOTUMIWA NA WAFANYABIASHARA WA SIMU KUKWEPA USHURU NCHINI TANZANIA

Utafiti uliofanywa mwaka jana na Kampuni ya Utengenezaji wa simu ya Nokia kabla haijabadilishwa na kuwa Microsoft kuhusu biashara ya mauzo ya simu katika nchi mbalimbali barani Afrika,Tanzania ikiwa ni miongoni mwao,umebaini kuwa kuna mianya ambayo imekuwa ikitumika kuingiza simu hizo kwa njia za magendo bila kulipia ushuru huku ukiikosesha Serikali ya Tanzania kiasi cha shilingi bilioni 91.23.
Utafiti huo unaeleza kuwa njia ambazo zimekuwa zikitumika ni upitishaji wa simu katika maeneo ya pembezoni mwa nchi hususani mikoa iliyoko mipakani mwa Tanzania na nchi jirani na kuingiza simu za magendo kupitia katika viwanja vya ndege vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam na ule wa Kilimanjaro ambapo wafanyabiashara hulipia kiasi kidogo cha fedha ambazo hukadiliwa bila kuangalia uzito na thamani ya mzigo alionao.
Takwimu za utafiti huo zinaonesha kuwa kwa wastani,simu za kawaida takribani 750,000 huuzwa kwa mwezi nchini Tanzania ambapo wastani wa bei kwa simu moja ni Sh 35,000 ambapo jumla ya mauzo ni Sh bilioni 26.2,huku kwa upande wa simu za kisasa kwa mwezi zikiuzwa simu 87,000 na wastani wa bei ikiwa ni Sh 250,000 ambapo mauzo yake kwa mwezi ni sawa na Sh bilioni 21.75.
Jumla ya simu zinazouzwa kwa mwezi ni 837,000 ambapo thamani yake ni Sh Bilioni 48,kama zimu zote zitalipiwa ushuru wa asilimia 18 na mianya yote kufungwa basi serikali inastahili kukusanya Sh.Bilioni 8.64 kwa mwezi.
Thursday, March 31, 2016
WAHALIFU MTANDAO WADUKUA TOVUTI 20 ZA SERIKALI NCHINI ANGOLA

Kikundi cha kihalifu mtandao cha #Anonymous kimetekeleza mashambulizi mtandao dhidi ya Nchi ya Angola na kufanikiwa kudukua na kuangusha Tovuti 20 za serikali ya Nchi Hiyo.
Hatua hiyo ya kikundi hicho imefuatia baada ya kushinikiza serikali ya Nchi hiyo kuwaachia watu 17 waliokamatwa kutokana na uasi dhidi ya Serikali ya Rais Jose Eduardo dos Santo.
Tukio hilo la Mashambulizi limepokelewa kwa masikitikomakubwa na jumuia ya wana usalama mitandao huku usaidizi wa dhati kuimarisha usalama kwa tovuti za Nchi hiyo zikichukuliwa.
Matukio ya kushambulia Serikali za Nchi za Afrika kimtandao yamepata kuonekana mara kadhaa ambapo Ghana pia ilipata kua muathirika.
Thursday, March 3, 2016
WHATSAPP NAYO YATANGAZA KUTOTUMIKA KATIKA BAADHI YA MATOLEO YA SIMU DUNIANI IFIKAPO DISEMBA 2016
Baada ya Serikali ya Tanzania kuanzisha kampeni ya kuondosha matumizi ya simu zisizohalisi toka Disemba mwaka jana,ambapo simu hizo hazitaendelea kutumika ifikapo Juni mwaka 2016 huku ikielezwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania kuwa kuna asimilia 40 ya simu zinazotumika nchini humo ambazo ni halisi. TCRA na Makampuni ya Huduma za Mawasiliano ya Simu za Mkononi Tanzania kwa sasa wanaendesha kampeni ya kuhakiki simu ya mtumiaji kama ni halisi ama si halisi kwa kutumia IMEI ya simu kuituma kwenda namba 15090.
Mtandao wa kijamii wa WhatsApp ulio na watumiaji bilioni moja duniani katika mawasilino miongoni mwao wakiwemo watanzania,nao hauko nyuma katika kutafuta kilichobora kwai umetangaza kuwa ifikapo Disemba 2016 hatutatumika katika baadhi ya simu zilizopo duniani.
Kampuni hiyo imejitetea na kusema kwamba haijawatupa wateja wake ambao wamechangia sana katika ufanisi wake lakini ni kutokana na mabadiliko ya teknolojia.
Orodha kamili ya mifumo ya simu ambayo wateja hawataweza tena kutumia WhatsApp ni hii hapa:
- Android 2.1 and Android 2.2
- Blackberry OS 7 and earlier
- Blackberry 10
- Nokia S40
- Nokia Symbian S60
- Windows Phone 7.1
Lakini sasa asilimia 99.5 ya simu zinatumia mifumo ya Google, Apple na Microsoft.
Chanzo:BBC
Thursday, February 18, 2016
TTCL YAKANUSHA MFUMO WAKE WA MAWASILIANO KUDUKULIWA
Tuesday, February 16, 2016
TIGO YATAHADHARISHA WATEJA DHIDI YA MATUMIZI YA SIMU BANDIA
Wednesday, February 3, 2016
TCRA YATOA SEMINA KWA WAANDISHI WA HABARI KUGUNDUA SIMU FEKI
Imetayarishwa na Othman Mapara.Blogspot
Thursday, January 28, 2016
IPHONE YAPOROMOKA SOKONI
Hii itakuwa mara ya kwanza kwa mauzo ya iPhone kushuka tangu kuzinduliwa kwa simu hizo za kisasa.
Mauzo ya iPhone yalichangia asilimia 68 ya faina ya kampuni ya Apple mwaka jana.
Kushuka kwa mauzo ya kampuni hiyo kunadaiwa kutokana na kiwango cha uchumi wa China kushuka.
Mauzo ya Apple nchini China, Hong Kong na Taiwan yaliongezeka 14%, lakini kiwango hicho cha ukuaji ni cha chini mno kikilinganishwa na ukuaji wa 70% ulioshuhudiwa mwaka mmoja uliopita.
Popular Posts
-
Mkurugenzi Msaidizi anayeshughulikia masuala ya Simu katika Wizara ya Ujenzi ,Uchukuzi na Mawasiliano Ndugu John Mwera akizungumza ...
-
Kanisa la Waadventista Wa Sabato mwaka huu litashiriki mkutano wa Waadventista watalaamu wa mawasilino ya Intaneti duniani (GAiN) kwa k...
-
Mkuu wa Huduma za Fedha kwa njia ya simu wa Tigo Ruan Swanepoel (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam...
-
If you've already bought a smart phone, you'll know the importance of choosing a good OS for it. With the versions of all the giant...
-
1.Kutune Gitaa /Kutafuta Ufunguo wa Sauti ya Gitaa Kulikuwa na wakati ambapo bei ya vifaa vya umeme kwa ajili ya kutafuta ...
-
Uchina imetaja kama kukosa kuwajibika ipasavyo kwa Marekani kudai kuwa wadukuzi wa Uchina ndio waliosababisha udukuzi wa taarifa za...
-
Serikali Mtandao inarahisisha utendaji kazi na utoaji wa huduma kwa umma. Usikose kuangalia kipindi hiki cha Seikali Mtandao katika Mamlaka...
-
Wabunge wa Tanzania wameibana serikali wakiitaka iboreshe muswada wa sheria ya mifumo ya malipo ili kuzibana kampuni za simu na mabenki,kuto...
-
Wataalamu wa Teknolojia nchini Ghana wamebuni teknolojia ya kuhakiki ikiwa dawa ni bandia au ni halisi. Teknolojia hiyo iliyozindul...
-
New software which mines data from social networks to track people's movements and even predict future behaviour poses a 'very ...