Wakati matukio ya wizi wa fedha katika mashine maalumu za kutolea fedha katika benki maarufu kwa jina la ATM yakiendelea kuripotiwa na vyombo vya usalama nchini Tanzania,Benki Kuu ya Tanzania (BOT) imesema kuwa licha ya kuwepo kwa wizi huo kamwe haitazuia huduma hiyo kwani ni mkombozi mkubwa kwa wateja.
Gavana wa BOT Profesa Benno Ndulu amekaririwa na Gazeti la Jambo leo akieleza kuwa huduma hiyo haiwezi kufutwa badala yake wataendelea kutafiti njia za kuwabana wahalifu hao.
Kauli hiyo ya gavana Ndulu imekuja siku moja baada ya jeshi la polisi
wilayani Rungwe, mkoani Mbeya,kuwanasa watu wanne akiwamo mwanafunzi
aliyemaliza kidato cha nne mwaka jana, wilayani Bunda, mkoani Mara,
baada ya kukutwa wakiiba fedha Benki ya NMB tawi la Tukuyu kupitia
mashine za kutolea fedha (ATM).
Watuhumiwa walikutwa
wakiwa na kadi bandia za ATM 150 za watu tofautitofauti na kwamba, hadi
wanatiwa mbaroni tayari walikuwa na Sh20.5 milioni mkononi,
kadi zote ni za NMB na kwamba, zilikuwa zinaonyesha wateja wote ni
walimu kutoka wilayani Mbozi.
Thursday, February 28, 2013
Tuesday, February 26, 2013
TCRA KUZIMA ANALOJIA MWANZA
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imetangaza kuzima rasmi mitambo ya kurusha matangazo ya televisheni kupitia mfumo wa utangazaji wa analojia katika baadhi ya maeneo mkoani Mwanza kuanzia Machi 1,mwaka huu na kuwasha digitali.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Huduma za Utangazaji wa TCRA,Habi Gunze,mitambo hiyo itazimwa februari 28,mwaka huu majira ya saa 6:00 usiku katika maeneo ya jiji la Mwanza,Wilaya ya Sengerema,Wilaya ya Ukerewe na Kijiji cha Kisesa.
Amesema maeneo mengine ya mkoa huo yataendelea kutumia mfumo wa analojia hadi mitambo ya digitali itakapofungwa rasmi katika maeneo hayo na mamlaka hiyo imekamilisha maandalizi yote ili wateja wa mawasiliano ya televisheni kwa njia ya analojia waingie katika mfumo mpya wa digitali.
Monday, February 25, 2013
KATIBU KIONGOZI ASEMA WIZI KATIKA ATM NI TATIZO LA DUNIA
Katibu Mkuu Kiongozi wa Tanzania,Balozi Ombeni Sefue amesema tatizo la wizi katika mashine za kutolea fedha (ATM), la dunia nzima.
Sefue alitoa kauli hiyo alipokuwa akijibu maswali ya waandishi wa habari wakati alipotembelea Tawi la Benki ya Posta Tanzania (TPB) tawi la Kariakoo.
Katibu huyo alisema tatizo la wizi katika ATM si la Tanzania pekee ni la dunia nzima na akatoa wito kwa benki za hapa nchini kuweka mifumo ambayo itasaidia kudhibiti wizi huo.
Friday, February 22, 2013
MITANDAO YA INTERNET NA SIMU ZA MKONONI ZATUMIKA KUZUSHA KIFO CHA NDESAMBURO
Mbunge wa Moshi vijijini,Philemon Ndesambulo (CHADEMA) amezushiwa kifo kutokana na baadhi ya watu kusambaza habari hizo kupitia ujumbe mfupi wa maandishi wa simu za mkononi (sms) na simu huku watu mbalimbali huko Moshi,Tanzania wakiulizana kama kweli mbunge huyo amefariki dunia.
Mwandishi wa habari wa gazeti la mwananchi Daniel Mjema ni miongoni mwa watu waliokuwa katika wakati mgumu kutokana na kupokea simu nyingi kutoka ndani na nje ya mkoa wa Kilimanjaro wakiuliza ukweli wa taarifa hizo.
Kutokana na taarifa hizo za uzushi Mbunge Ndesambulo alisema jana kuwa alimfahamu mtu aliyesambaza taarifa hizo kuwa ni mwanammke mmoja ambaye ni mwanachama wa chama kimoja cha siasa.
Ndesambulo alisema alimtafuta mama huyo na kumwuliza kwa nini amemzushia kifo wakati yu hai akasema eti na yeye kuna mtu alimsikia akisema amesoma kwenye mtandao kuwa mbunge huyo amefariki dunia.
"Ni watu wabaya sana hao hivi sasa nikipita barabarani naonekana kama ni msukule uliofufuka lakini nataka niwahakikishie watanzania kuwa niko hai na nachapa kazi kama kawaida"alisema
MBUNGE AIBIWA SHILINGI MILIONI 6 BENKI
Mbunge wa Biharamulo Magharibi, Dk Gervas Mbasa |
Sakata la wizi wa fedha katika akaunti za wateja wa benki, sasa
limeingia katika sura mpya baada ya Mbunge wa Biharamulo Magharibi, Dk
Gervas Mbasa (Chadema) naye kuibuka na kudai kuwa ameibiwa Sh6 milioni
kutoka kwenye akaunti yake.
Akizungumzia wizi huo, mbunge huyo alisema fedha zake ziliibwa kwa nyakati tofauti kati ya Desemba 20 mwaka jana na Januari 3, mwaka huu.
Alisema kitendo hicho kilifanywa na mtu mmoja aliyempigia simu na mtu mmoja aliyejitambulisha kuwa ni mfanyakazi wa Makao Makuu ya Kampuni ya Airtel na kwamba alikuwa katika zoezi la kuhakiki namba zote za zamani.
“Alinieleza kwamba kwa niaba ya Airtel yupo katika zoezi la kuhakiki namba zote zilizosajiliwa zamani na yangu ilikuwa ni ya miaka 10 na akaniuliza namba ya mwisho kuwasiliana na mtu kupitia simu yangu. Nilimtajia namba ya mke wangu na baada ya maelezo hayo aliniomba nisizime simu yangu wakati wakiwa wanashughulika na kuisajili na kwamba muda wowote nitapatiwa maelekezo,” alieleza mbunge huyo.
Kilichotokea baada ya muda ni kwamba simu yangu, haikuweza kufanya kazi, hatua hiyo iliyonilazimisha kuwasiliana na watoa huduma wa kampuni hiyo huko jimboni ili kujua tatizo ni nini, lakini kila aliyejaribu kuirejesha katika mawasiliano alinijibu kuwa haiwezekani mpaka makao makuu,” alisema Mbasa.
“Kila wakala wa Airtel niliyemfuata na kumweleza kuwa simu yangu haifanyi kazi, alipoingia kwenye mtandao wao kwa ajili ya kuirejeshea mawasiliano alinijibu kuwa hiyo haiwezekani mpaka makao makuu ya kampuni hiyo,” alisema.
Mbunge huyo alisema majibu hayo yalimlazimisha kutulia bila mawasiliano hadi Januari mwaka huu alipokwenda katika Makao Makuu ya Aritel na kufanikiwa kuirejeshea simu yake mawasiliano.
Dk Mbasa alisema baadaye aligundua kuwa wakati simu yake ikiwa imekosa mawasiliano watu hao walikuwa wakishughulikia kuhamisha fedha zake kutoka katika akaunti yake.
Alisema Januari 6, mwaka huu alifanikiwa kwenda Tawi la Benki ya NMB la Mazengo ambapo baada ya kuangalia salio katika akaunti yake, alibaini kuwapo kwa wizi huo na baadaye aliwasiliana na maofisa wa benki hiyo ambao walimthibitishia kuwa ameibiwa.
Kwa mujibu wa mbunge huyo, maofisa hao walimpatia fomu za kujaza, ili kusitisha kutumia huduma ya `Sim Banking’ katika akaunti yake.
Dk Mbasa alisema baadaye aliwasiliana na meneja wa benki hiyo na kutakiwa kuandika maelezo ya wizi ikiwa ni pamoja na kukabidhiwa kwa wataalamu wa masuala ya ufuatiliaji wa uhalifu kwa njia ya mitandao.
Alisema baada ya kuangalia katika mtandao, wataalamu hao walibaini kuwa fedha zake zilitolewa na wahusika katika kipindi cha kati ya Desemba 20 mwaka jana na Januari 3, mwaka huu.
“Kwa mujibu wa mtandao wa Benki inaonyesha fedha zangu zilitolewa kwa kutumia huduma ya `Sim Banking’ ya NMB Mobile ambapo zilikuwa zikihamishwa kutoka katika akaunti yangu kwenda `Pesa Faster Collection’ na kwa watu wengine wawili,” alifafanua.
Alisema kutokana na maelezo hayo ya NMB, alilazimika kufungua jalada katika Kitengo cha Polisi cha Kupambana na Wizi kwa Njia ya mtandao lakini, hadi sasa hakuna lolote lililofanyika.
Kamanda wa Polisi mkoani Dodoma, David Misime alisema hana kumbukumbu kuhusu madai ya mbunge huyo kuibiwa na kuomba muda ili afuatilie kwa maofisa wake.
Meneja wa Kanda ya Ziwa wa Kampuni ya Simu ya Mkononi Airtel, Ally Maswanya alisema hakuna zoezi la uhakiki wa namba lililoendeshwa na kampuni yake na kwamba anavyotambua kuna watu wahuni ambao wamekuwa wakijifanya kuwa ni maofisa wa kampuni na kisha kuziingilia namba za wateja wao.
Chanzo:Gazeti la Mwananchi
VODACOM YATOA KOMPUTA 10 KAHAMA
Mfuko wa kusaidia jamii wa Vodacom Foundation,umetoa msaada wa komputa 10 zenye thamani ya shilingi milioni saba kwa shule ya sekondari ya Mt Theresa wa Avila wilayani Kahama,Shinyanga.
Msaada huo wa komputa ni kama sehemu ya mfuko huo katika kuchangia kuboresha sekta ya elimu na kusaidia matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Teknohama)nchini.
Akipokea msaada wa komputa hizo kutoka kwa Mkuu wa Kitengo cha Kusaidia Jamii wa Vodacom Tanzania,Yessaya Mwakifulefule,Mwalimu Mkuu wa shule hiyo,Joyce Martin aliishukuru Vodacom kwa msaada huo.Alisema kuwa komputa hizo zitasaidia kuboresha mahitaji ya Teknohama shuleni hapo.
Aidha alisema msaada huo utasaidia kupunguza tatizo la uhaba wa komputa uliopo shuleni hapo sambasamba na kukabiliana na changamoto za utandawazi zilizopo.
Wednesday, February 20, 2013
JESHI LA POLISI TANZANIA LAANZA KUNASA WALIOMTUKANA SPIKA WA BUNGE KWA KUTUMIA SIMU
Jeshi la Polisi Tanzania limeanza kunasa watu wanaodaiwa kutuma ujumbe wa matusi na wengine kupiga simu kwa spika wa Bunge la nchi hiyo Anne Makinda na Naibu wake,Job Ndugai.
Hatua ya jeshi hilo imekuja siku chache,baada ya ofisi ya Bunge kudai kuwa namba zilizohusika kutuma au kupiga simu na kutoa matusi wanazo na kwamba,tayari wameziwasilisha kwenye mamlaka husika kwa hatua za kisheria.
Akizungumza Dar es salaam juzi Msemaji wa Polisi,Advera Senso alisema hivi sasa wanakusanya taarifa kutoa mikoa tofauti ili kujua takwimu halisi za watu waliokamatwa.
Advera alisema kutokana na hali hiyo wananchi wanapaswa kuwa makini na matumizi ya simu,ili kuondoa matatizo yaliyojitokeza ikiwemo kutumia ujumbe ama kupiga simu za matusi zinazoweza kuwasababisha kufikishwakwenye vyombo vya sheria
Hatua ya jeshi hilo imekuja siku chache,baada ya ofisi ya Bunge kudai kuwa namba zilizohusika kutuma au kupiga simu na kutoa matusi wanazo na kwamba,tayari wameziwasilisha kwenye mamlaka husika kwa hatua za kisheria.
Akizungumza Dar es salaam juzi Msemaji wa Polisi,Advera Senso alisema hivi sasa wanakusanya taarifa kutoa mikoa tofauti ili kujua takwimu halisi za watu waliokamatwa.
Advera alisema kutokana na hali hiyo wananchi wanapaswa kuwa makini na matumizi ya simu,ili kuondoa matatizo yaliyojitokeza ikiwemo kutumia ujumbe ama kupiga simu za matusi zinazoweza kuwasababisha kufikishwakwenye vyombo vya sheria
Friday, February 15, 2013
WIZI WA KUTUMIA ATM WATIKISA TANZANIA
Jeshi la Polisi mkoani Mwanza kwa kusaidiana na maofisa wa Benki ya NMB imewatia mbaroni watu watatu ambao wanadaiwa kuiba kiasi cha Sh700 milioni kwa nyakati tofauti.
Watuhumiwa hao wamenaswa baada ya kuwekewa mtego na maofisa wa benki na polisi kwenye saa 6.00 usiku wa Februari 10, mwaka huu na mtuhumiwa mmoja alibambwa akichukua fedha katika ATM ya NMB kwenye Tawi la PPF Plaza Mwanza.
Baada ya kunaswa kwa mtuhumiwa huyo, alisaidia kuwaelekeza polisi walipo wenzake, ambao walikutwa katika hoteli moja jijini Mwanza wakiwa wamejipumzisha.
Akizungumza na waandishi wa habari, Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi Mwanza, Christopher Fuime alisema pia walikamata vifaa mbalimbali ambavyo walikuwa wakitumia kwa ajili ya kufanyia uhalifu huo.
“Kwa muda mrefu sasa Jeshi letu lilikuwa likihangaika na wahalifu wa aina hiyo kwani tangu Oktoba 2012 tumekuwa tukipokea kesi mbalimbali za wizi wa fedha katika akaunti zao, lakini tumefurahi tumewatia mbaroni,” alieleza Fuime.
Kamanda Fuime alidai kuwa tangu kutiwa mbaroni kwa watuhumiwa hao, hawajasikia malalamiko ya wizi tena.
Alisema polisi walikuwa wakipata wastani wa malalamiko 15 katika kipindi cha siku 14.
“Hawa jamaa inaelekea ndiyo vinara wa wizi huu, ingawa haina maana kwamba kukamatwa kwao uhalifu huu utapungua. Wizi huu una mtandao mpana sana kwa vile hata wahalifu hao wamedokeza kuwa wamekuwa wakishirikiana na wataalamu wa kompyuta kutoka nchini Bulgaria,” alisema.
Vifaa walivyokamatwa navyo
Vifaa vilivyokamatwa navyo ni kadi za bandia 194 za kuchukulia fedha katika ATM za Benki ya NMB, ambapo kati yake kadi 95 zilikuwa na namba 0225152975 zinazotumia namba ya akaunti ya 2258103695 zenye jina na picha ya mtu anayedaiwa kuwa ni mtumiaji mwenye jina la Molely L. P. Kadi nyingine 99 zilikuwa na namba 0506056317 za akaunti namba 5068000322 zikitumia jina moja la Mnuo Z. E na picha moja.
Mbali na kadi hizo pia waliweza kunasa kadi 36 za Benki za DTB, ambazo kati yake kadi 18 zilikuwa na jina moja la Kelvin G. Gratias na namba 20497883, kadi 12 zikitumia jina la John J. Paul zenye akaunti namba 2049783 huku kadi sita zikitumia jina moja la Joseph Donald akaunti namba 2049783.
Kadi nyingine tatu zenye maandishi ya Download List na nyingine ikiwa ni kadi ya Visa ya Benki ya KCB yenye namba 4183546040003827 zikitumia jina la Elikana Zacharia. Kadi nyingine zilikuwa ni tupu zisizo na maandishi wala nembo ya benki yoyote na nyingine zikiwa ni Soviet Royalty, kadi ya raia ya Urusi ikiwa na namba 000724.
Pia walikutwa na kadi ya Benki ya Amerikani yenye namba 549012345678 zilizokuwa zikitumia jina la Richard Croswell.
Walikamatwa pia wakiwa na vifaa mbalimbali vya kielektroniki ikiwamo kamera za siri tatu za kienyeji ambazo zimetengenezwa kwa kufungwa betri za simu ya mkononi na pia walikamatwa na kifaa cha kutengenezea kadi bandia (Magnetic Card reader), mikebe mitatu ya rangi za kupulizia kamera za usalama katika ATM ili wasionekane wakati wa wizi wao, ‘printer’ pamoja na kifaa cha kuchomea vifaa vya umeme.
Wizi ulivyofanyika
Wahalifu hufika katika mashine za kutolea fedha ambapo hatua ya kwanza ni kuzima kamera za usalama za eneo husika kwa kuzipulizia rangi maalumu ili kuzitia ukungu hivyo kuharibu mwonekano wake na kuruhusu wao kuingia eneo hilo bila ya kuonekana na kufanya wizi wao.
Mara baada ya kuziharibu kamera za usalama, walikuwa wakianza kwa kuweka kamera zao za siri ili kunasa namba za siri za kufungulia akaunti ambazo huzisoma katika ‘kompyuta’ na kuzinakili katika daftari lao maalumu na kisha kuchukua kadi zao bandia na kuchukua fedha.
Wizi huo wa kuchukua fedha waliufanya nyakati za usiku saa sita hadi saa tisa usiku wakati ule wa kutegea kamera zao ulifanyika muda ambao huwa na wateja wengi hasa siku za mapumziko.
Hatua za benki kuzuia wizi huo:
Meneja wa Benki ya NMB, Kanda ya Ziwa, Straton Chilongola alipoulizwa kuhusiana na wizi huo alisema kwamba jambo hilo linashughulikiwa na Polisi, hivyo yeye hana maelezo ya ziada.
“Naomba kama mnataka suala hili fuatilieni polisi kwa vile wahalifu wote na kesi kwa jumla inashughulikiwa huko, kwa upande wangu mimi siyo msemaji wa benki kulingana na uzito wa suala hili,” alisema.
Hata hivyo, habari kutoka ndani ya benki hiyo zilieleza kwamba kutokana na kuongezeka kwa malalamiko ndani ya wateja wao walilazimika kuweka watu katika mitambo yao ya kamera ikiwa ni pamoja na kufuatilia kwa ukaribu nyendo za wizi huo ambapo waliweza kubaini muda na wakati ambao wamekuwa wakiingia na hivyo kuwasiliana na maofisa wa Polisi kwa lengo la kuweka mtego.
Idadi ya malalamiko ya wateja
Kaimu Kamanda Fuime alieleza kwamba, tangu kipindi cha Oktoba 5, 2012 hadi Februari 10, mwaka huu kitengo cha jeshi hilo kwa njia ya uhalifu wa njia ya mtandao (Cyber Crime) kiliweza kupokea jumla ya malalamiko 135 na kuyafungulia majalada ya uchunguzi wa wizi huku wastani wa kupokea malalamiko kwa siku moja ukiwa ni kesi 15.
Chanzo:Gazeti la Mwananchi
Wednesday, February 13, 2013
TAHADHARI KUHUSU KUPANDISHWA VYEO KUPITIA UJUMBE WA SIMU
Serikali ya Tanzania
inapenda kuufahamisha umma wa Watanzania kuwa hivi karibuni kumezuka
kundi la Watu wadanganyifu ambao wamekuwa wakitumia majina ya viongozi
waandamizi wa serikali na Taasisi nyeti ikiwemo Usalama wa Taifa
kujipatia fedha kwa madai ya kutumwa na viongozi hao.
Watu hao wamekuwa wakituma ujumbe mfupi wa simu (SMS) kwa maofisa mbalimbali wa wizara, mashirika ya umma na Idara za Serikali zinazojitegemea kuomba pesa ili wawafanye mipango ya kupandishwa vyeo.
Utapeli huo umekuwepo nchini kwa kipindi kirefu sasa, ambapo watu huwapigia simu viongozi wa Taasisi za fedha, Mifuko ya Taasisi za Jamii na watu binafisi wakiomba fedha kwa madai ya kutumwa na viongozi waandamizi Serikalini wakati si kweli.
Watu hao wamekuwa wakiwatapeli maofisa mbalimbali kuwa wanaweza kuwafanyia mipango ya kupandishwa vyeo endapo watawapatia kiasi cha fedha jambo ambalo halipo katika taratibu za utumishi wa umma.
Utumishi wa umma unazo taratibu zake za kuwapandisha vyeo watumishi wake kulingana na sifa za kada zao na wala haiwezekani kwa viongozi waandamizi kuwachangisha fedha kwa ajili ya kuwapandisha vyeo. Serikali inawataka wananchi kuwapuuza matapeli hao na watoe taarifa katika vyombo vya dola na usalama mara wapatapo ujumbe wa aina hiyo ili hatua zichukuliwe dhidi yao.
IMETOLEWA NA:
IDARA YA HABARI (MAELEZO)
DAR ES SALAAM. 12.02.2013
Chanzo:wanabidii googlegroups.com
Watu hao wamekuwa wakituma ujumbe mfupi wa simu (SMS) kwa maofisa mbalimbali wa wizara, mashirika ya umma na Idara za Serikali zinazojitegemea kuomba pesa ili wawafanye mipango ya kupandishwa vyeo.
Utapeli huo umekuwepo nchini kwa kipindi kirefu sasa, ambapo watu huwapigia simu viongozi wa Taasisi za fedha, Mifuko ya Taasisi za Jamii na watu binafisi wakiomba fedha kwa madai ya kutumwa na viongozi waandamizi Serikalini wakati si kweli.
Watu hao wamekuwa wakiwatapeli maofisa mbalimbali kuwa wanaweza kuwafanyia mipango ya kupandishwa vyeo endapo watawapatia kiasi cha fedha jambo ambalo halipo katika taratibu za utumishi wa umma.
Utumishi wa umma unazo taratibu zake za kuwapandisha vyeo watumishi wake kulingana na sifa za kada zao na wala haiwezekani kwa viongozi waandamizi kuwachangisha fedha kwa ajili ya kuwapandisha vyeo. Serikali inawataka wananchi kuwapuuza matapeli hao na watoe taarifa katika vyombo vya dola na usalama mara wapatapo ujumbe wa aina hiyo ili hatua zichukuliwe dhidi yao.
IMETOLEWA NA:
IDARA YA HABARI (MAELEZO)
DAR ES SALAAM. 12.02.2013
Chanzo:wanabidii googlegroups.com
Tuesday, February 12, 2013
MADAKTARI NCHINI TANZANIA KUWASILIANA BURE KUPITIA VODACOM
Waatalamu wa afya nchini Tanzania wakiwamo madaktari, wataanza kupata huduma ya kupiga simu na kutuma ujumbe mfupi wa maneno bila malipo yoyote kwa wataalam wenzao popote nchini humo na kupokea taarifa, maelekezo na ushauri unaohitajika kupitia mtandao wa mawasiliano ya simu za mkononi wa Vodacom.
Mtandao kwa ajili ya mawasiliano ya wanataaluma wa afya Health Network Programme, umeanzishwa kwa lengo la kurahisisha utendaji kazi wa madaktari na kuboresha kiwango cha mawasiliano ya wenyewe kwa wenyewe.
Usajili wa mtandao huo kuanzia sasa unatarajia kuhusisha wataalam wa afya wapatao 9,000 nchi nzima, wakiwamo madaktari wa meno na wasaidizi wao, tabibu na tabibu wasaidizi popote alipo, serikalini na binafsi.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Vodacom Foundation, Yessaya Mwakifulefule, kwa vyombo vya habari jijini Dar es Salaam jana, ili mtaalam wa afya ajiunge kwenye programu hiyo, atatakiwa kutumia simu yake ya mkononi ambayo itakuwa na kadi ya simu (simcard) ya Vodacom.
Akizungumza katika uzinduzi wa huduma hiyo jijini Dar es Salaam, Mwakifulefule, alisema huduma hiyo muhimu na yenye tija siyo tu itawanufaisha madaktari na sekta ya afya, bali pia Watanzania wote mijini na vijijini.
Alisema mbali ya kupiga simu bure, wanachama wa mtandao huo kwa kushiriki katika programu hiyo watakuwa na uwezo wa kutuma ujumbe mfupi wa maneno 50 bure kila mwezi kuwasiliana na wenzao waliojisajili ndani ya programu hiyo.
Awali, Taasisi ya Kimataifa inayoshughulika na huduma za mawasiliano (Switchboard) kupitia taarifa yake kwa vyombo vya habari, imewasihi madaktari kujumuika katika program hiyo ili kutathmini mafanikio ya utendaji wao kama wadau na wataalamu ndani ya sekta ya afya.
Alisema suala la upungufu wa madaktari na wataalam wa afya katika mataifa mengi limesababisha daktari au muuguzi mmoja kujikuta akihudumia wagonjwa kati ya 5,000 hadi 150,000.
Programu hiyo inadhaminiwa na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Switchboard na Kampuni ya simu za mikononi ya Vodacom.
TCCL YAKABIDHI MRADI WA MAWASILIANO KWA CAG
Kampuni ya Simu nchini Tanzania (TTCL) jana imekabidhi mradi wa mawasiliano utaotumiwa katika mikoa 12 ya Tanzania kwa ofisi ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa lengo la kuboresha kazi za ofisini hiyo ambao utagahrimu zaidi ya shilingi milioni 477.
Mikoa hiyo ni Manyara,Kilimanjaro,Arusha,Singida,Dodoma,Tanga,Morogoro,Mbeya,
Dar es salaam,Lindi,Shinyanga na Ofisi za NAOT zilizopo Kamata.
Akizungumza katika makabidhiano ya mradi huo Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali ya Tanzania Ludovick Utouh,amesema ofisi yake ilifanya makubaliano na TTCL katika awamu tatu huku awamu mbili ikilipa asilimia 90 ya fedha za mradi.
Utouh anasema kukamilika kwa mradi huo kutainufaisha ofisi yake katika mambo matano yakiwamo kuimarisha mawasiliano ya ndani na nje ya nchi,intaneti,ofisi kutumia mtandao mmoja na kuweka miundombinu mizuri ya kiukaguzi.
MAKINDA ASHAMBULIWA KUPITIA SIMU
Spika wa Bunge la Tanzania Anne Makinda |
Chanzo kilichopo karibu na Spika kimesema kuwa tangu chama hicho
kilipotangaza namba hizo za simu, jumla ya simu 200 za kumtukana Spika
zilipigwa.
Hali kadhalika, katika kipindi hicho jumla ya ujumbe 400 mfupi wa
simu za mkononi (sms), uliokuwa ukimtukana ulipokelewa katika simu zake.
“Simu hizo walikuwa wameshika wasaidizi wake, kila aliyepiga simu
kwa lengo la kutukana, amekuwa akiachwa kutukana hadi anapomaliza na
kisha kuambiwa sawa,” kilisema chanzo hicho ambacho hakikutaka jina lake
liandikwe gazetini.
Hata hivyo, NIPASHE ilimtafuta Spika Makinda jana kuzungumzia suala
hilo bila mafanikio na kuelezwa kuwa ofisi ya Bunge itafanya mkutano na
waandishi kati ya leo ama kesho kulizungumzia sakata hilo.
Viongozi wa Chadema waligawa namba za viongozi hao wa juu wa Bunge
Jumapili iliyopita katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja
vya Temeke Mwisho, jijini Dar es Salaam.
Monday, February 11, 2013
FACEBOOK DEVELOPING APP THAT WILL TRACK YOUR EVERY MOVE
Facebook is developing a new smartphone app to track the location of users in an effort to target them with localised adverts, according to reports.
The app will help users to find friends who are nearby, alert them when it detects one in close proximity even when the app is not open on the handset, it is claimed.
It will be just one of a whole suite of mobile apps Facebook is building up to help it profit from the increasing proportion of its users who access the social network on the go.
But privacy campaigners warned it was another example of 'profit trumping privacy' and called the function 'intrusive'.
Read More here:Mail Online
SOFTWARE THAT MINES SOCIAL NETWORKS USERS
New software which mines data from
social networks to track people's movements and even predict future
behaviour poses a 'very real threat to personal freedom', civil rights
groups warned today.
Multinational defence contractor Raytheon has developed the 'extreme-scale analytics' software which can sift through vast quantities of data from services like Facebook, Twitter and Google.
Critics have already dubbed it a 'Google for spies' and say it is likely to be used by governments as a means of monitoring and tracking people online to detect signs of dissent.
Source:Mail Online
Multinational defence contractor Raytheon has developed the 'extreme-scale analytics' software which can sift through vast quantities of data from services like Facebook, Twitter and Google.
Critics have already dubbed it a 'Google for spies' and say it is likely to be used by governments as a means of monitoring and tracking people online to detect signs of dissent.
'Google for spies': A screengrab of a video
demonstrating Raytheon's Riot software, which mines the personal data
from social networking websites to track people's movements and even
predict their future behaviour
Source:Mail Online
Saturday, February 9, 2013
MISRI YAPIGA MARUFUKU YOUTUBE
Mahakama
moja ya Misri imepiga marufuku kwa mwezi mmoja tovuti ya kusambaza
video ya Youtube kwa kuonesha filamu iliyotusi Uislamu na kuzusha
maandamano ya ghasia katika sehemu kadha za nchi za Kiislamu.
Mahakama
ya utawala ya Cairo yaliamua kuwa wakuu lazima wachukue hatua kupiga
marufuku Youtube nchini na tovuti nyengine yoyote iliyoruhusu filamu
hiyo kuoneshwa.
Chanzo:Chingaone
Friday, February 8, 2013
WANAOTAZAMA RUNINGA KWA MUDA MREFU HUPOTEZA NGUVU ZA KIUME
Wanaume wanaotumia muda wa saa tatu na zaidi kwa siku kutazama runinga wanapoteza nguvu za kiume ukilinganisha na wale wanaotazama runinga mara chache.
Utafiti uliofanywa na Chuo Kikuu cha Afya ya Umma cha Havard (HSPH) kilichopo Boston nchini Marekani, umebaini kuwa kuporomoka kwa kiwango cha mbegu za kiume kunahusiana moja kwa moja na kutofanya mazoezi na kutazama runinga kwa muda mrefu.
Imeelezwa kuwa wanaume wanaotazama runinga kwa zaidi ya saa 20 kila wiki wanapoteza asilimia 44 ya mbegu za kiume ukilinganisha na wale wasiotumia muda mrefu katika runinga.
Vilevile, wanaume wanaofanya mazoezi kwa zaidi ya saa 15 kwa wiki, wana uwezo wa kuongeza asilimia 73 ya mbegu zao ukilinganisha na wale wasiofanya mazoezi au wanaofanya mazoezi chini ya saa tano kwa wiki.
Kiongozi wa utafiti huo, Dk Audrey Gaskin alisema mtindo wa maisha unachochea zaidi upungufu wa mbegu za kiume na uzalishwaji wa mbegu za kiume.
Wanaume hao walihojiwa kuhusu kiwango cha ufanyaji wao wa mazoezi, muda wanaotumia katika kutazama runinga au filamu katika kipindi cha miezi mitatu.
“Baada ya utafiti huo, nusu ya wanaume wasiofanya mazoezi na waliotumia muda mrefu katika runinga walikuwa na kiwango hafifu cha uzalishaji wa mbegu,” alisema Dk Gaskin.
Dk Gaskin alisema: “Masuala mengine ya kiafya yanayoweza kuathiri kiwango cha mbegu za kiume ni chakula, msongo wa mawazo na uvutaji wa sigara,” alisema.
Daktari huyo alisema mwanamume anapokaa kwa muda mrefu katika sofa mbegu za kiume zinapata kiwango kikubwa cha joto ambalo huathiri uzalishwaji wa mbegu.
Alisema wanaume wanaohitaji watoto wanatakiwa kuacha kuvaa nguo za ndani zinazobana ili kuimarisha kiwango cha mbegu za kiume huku madereva na waendesha baiskeli wakionywa kuwa katika hatari ya kupungukiwa kutoa mbegu nyingi.
Mhadhiri Mkuu katika Chuo Kikuu cha Sheffield nchini Uingereza, Dk Allan Pacey anasema matokeo ya utafiti wake yatasaidia kuelimisha umma.
Hata hivyo, Daktari bingwa wa Uchunguzi wa Magonjwa kwenye Kitengo cha Patholojia katika Hospitali ya Muhimbili, Henry Mwakyoma aliyewahi kufanya utafiti kuhusu ugumba kwa wanaume, alisema bado utafiti wa Dk Gaskin una maswali mengi.
“Siwezi kuukubali au kuukataa utafiti wake, inawezekana ni mionzi au joto ndilo linalosababisha udhaifu wa mbegu hizo, lakini bado utafiti wake una maswali mengi,” alisema Dk Mwakyoma.
Alisema mazingira ya eneo husika na hali ya hewa na mlo vinaweza kusababisha mabadiliko ya kiafya, ikiwemo uzalishwaji wa mbegu za kiume.
Dk Mwakyoma aliwahi kufanya utafiti katika kipindi cha Oktoba 2009 hadi Septemba 2010 na kubaini kuwa kati ya wanaume 221 waliopimwa, asilimia 17.2 walikuwa hawana mbegu za kiume kabisa na asilimia 30.03 walikuwa na mbegu dhaifu na chache.
Hivyo basi, asilimia 47.05 ya wanaume waliokwenda kupima katika hospitali hiyo, waligundulika kuwa na matatizo ya ugumba.
Dk Mwakyoma alisema sababu za ugumba kwa wanaume huweza kusababishwa na kuambukizwa kwa vijidudu vya bakteria au virusi katika tezi inayozalisha mbegu za kiume au magonjwa ya zinaa.
“Baadhi wamezaliwa hivyo, miili yao haizalishi mbegu au walipata maambukizi ya vijidudu wakati wa kuzaliwa,” alidokeza Mwakyoma.
Alitaja sababu nyingine zinazosababisha ugumba kwa wanaume ni kuziba kwa mirija inayosafirisha mbegu za kiume kutoka katika korodani hadi katika uume na kwenda kwa mwanamke.
Sababu nyingine ni mionzi, hasa kwa watu wanaofanya kazi migodini, jeshini kutokana na baadhi ya kemikali zinazopatikana kwenye shughuli zao na hasa kuathiri watu wenye umri kuanzia miaka 50 hadi 59.
‘Pia, wanaume waliowahi kuugua ugonjwa wa matezi nao huathirika katika nyumba ya kuzalisha mbegu,” alisema Dk Mwakyoma.
Naye Injinia John Ben Ngatunga wa Tume ya Mionzi Tanzania, (TAEC) alisema mionzi iliyopo katika runinga nyingi za kisasa haziwezi kuleta madhara katika mwili wa binadamu.
“Pengine utafiti wake unaweza kuwa na ukweli iwapo kutazama runinga kutamwathiri mtu kisaikolojia.
Runinga nyingi ni zile zenye LCD (Liquid Crystal) ambazo hazina athari za mionzi,” aliongeza Ngatunga.
Alisema runinga nyingine zinaweza kuwa na mionzi, lakini ni pale ambapo mtu ataikaribia kwa umbali wa kati ya inchi saba hadi 12.
Chanzo:Gazeti la Mwananchi
Wednesday, February 6, 2013
ISACA -TANZANIA NA MAKUBALIANO YA USALAMA WA INTANET TANZANIA
Rais wa Taasisi inayojihusisha na Usimamizi na Ukaguzi wa Mitandao Duniani (ISACA)yenye makao makuu yake huko Marekani Bw.Boniphace Kanemba (Kushoto) akiwa na Mtangazaji Maduhu wa Kipindi cha Maisha na Teknohama Morning Star Radio baada ya kufanya naye mahojiano kuhusu usalama katika mitandao mwaka 2012 kwenye semina iliyoandaliwa na taasis hiyo jijini Dar es salaam
Norway Registers Development (NRD) AS,ambayo kwa sehemu fulani imefadhiliwa na Norwegian Agency for Develepment Cooperation (NORAD) imemaliza kazi yake nchini Tanzania ambapo katika ziara yake ilikuwa kupanua shughuli zake nchini humo na Jumuia ya Afrika Mashariki kupitia ubia na kuanzisha chombo cha Tanzania kwa kutoa huduma bora za kitaaluma katika maeneo ya usalama wa intaneti,utekelezaji wa ulinzi mipango ya mwendelezo wa kibiashara,utekelezaji wa udhibiti wa usalama wa teknolojia ya habari na ukaguzi.
Wakati wa ziara,semina ya usalama wa intaneti ilifanywa Dar es salaam na mkataba wa makubaliano na Taasisi inayojihusisha na Usimamizi na Ukaguzi wa Mitandao Duniani ISACA tawi la Tanzania ulitiwa saini.
Madhumuni ya mkataba huo ni kueleza maslahi ya kawaida ya na dhamira ya taasis hizi kaushiriki katika maendeleo ya mashauriano ya mfumo wa kitaifa wa usalama wa intaneti nchini Tanzania na utekelezaji wake katika sekta ya umma na binafsi ili kulinda mali ya thamani zaidi ya nchi,mazingira salama ya teknolojia ya habari na mawasiliano na kuendeleza kufanyakazi ni sehemu muhimu ya mfymo wa usalama wa taifa.
Mpango huu nchini Tanzania sehemu yake imefadhiliwa na kuungwa mkono na NORAD,ambapo ina mipango ya kuchochea maendeleo ya sekta binafsi katika nchi zinazoendelea.
Katika vita vya kimatifa dhidi ya uhalifu kwenye intaneti NRD kwa kushirikiana na Taasisi inayojihusisha na Usimamizi na Ukaguzi wa Mitandao Duniani ISACA zote zinategemea wataalamu wenye uwezo mkubwa wa habari.
TEKNOHAMA NA UTENDAJI WA IDARA YA UHAMIAJI
Idara ya Uhamiaji nchini Tanzania imeeleza kujivunia mabadiliko ya utumiaji wa Teknohama katika utendaji wake wa kazi katika kipindi cha miaka saba iliyopita ndani ya idara hiyo iliyopo chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani.
Majukumu ya idara hii ni kuwezesha kudhibiti ujangili,utokaji wa watu na ukaazi wa wageni nchini Tanzania,kutoa huduma ya hati za kusafiria na hati nyingine za safari kwa raia wenye sifa na kuratibu mchakato wa maombi ya uraia wa Tanzania kwa wageni wanaoishi nchini Tanzania kihalali.
Moja ya maeneo yanayopewa kipaumbele katika kuboresha utoaji wa huduma za uhamiaji ni matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano.Kati ya mwaka 2006 na 2012,idara hii imefanikiwa kuboresha utendaji kazi kwa kutumia mifumo ya komputa na mitandao yake katika utoaji wa huduma.
Jumla ya Mifumo minane imefungwa na inaendelea kutumika katika utoaji wa huduma katika sehemu tofauti tofauti za idara hii.
Kwanza mfumo wa utoaji wa hati za kusafiria huu ulifungwa mwaka 2005 katika ofisi za makao makuu ya uhamiaji Dar es salaam na Zanzibar huu unatumika katika kutoa hati za kusafiria kwa wananchi wa Tanzania,Mwingine ni mfumo wa utoaji wa Viza ambao unahusika na utoaji wa visa kwa wageni wanaohitaji kuja Tanzania pamoja na kutunza kumbukumbu zao ambao ulifungwa mwaka 2006 katika balozi 33 za Tanzania nje ya nchi na katika vituo vikubwa 19 vya kuingia na kutoka Tanzania.
Mfumo mwingine ni wa udhibiti na kutunza kumbukumbu za wasafiri ambao umefungwa mwaka 2003 na uliboreshwa mwaka 2010 ili kuongeza uchukuaji wa taarifa nyingine muhimu za wasafiri.
Pia kuna mfumo wa kudhibiti na kutunza kumbukumbu za wasafiri ambao umefungwa mwaka 2008 katika vituo 13 kwa ajili ya kutunza kumbukumbu za wasafiri na umeunganishwa na makao makuu ya mikoa na makao makuu jijini Dar es salaam.
Pia idara ya Uhamiaji ina mfumo wa utunzaji wa majalada,huu ulifungwa mwaka 2007 makao makuu ya uhamiaji na unatumika kutunza kumbukumbu za majalada kwa njia ya kielektroniki.Baada ya mfumo huu kuna mwingine ambao unahusika na utoaji wa vibali vya ukaazi ambao ulifungwa mwaka 2012 makao makuu ya idara hiyo jijini Dar es salaam na Ofisi Kuu ya idara hiyo huko Zanzibar,huu ni mfumo ambao unatumika kuchapisha vibali na kutunza kumbumbu za wageni wanaoomba kuishi Tanzania japo bado unahitaji maboresho ili ulete mafanikio.
Kuna mfumo wa kutoa vyeti vya uraia wa Tanzania kwa wakimbizi 2009 huu huhusika kusimamia wanaoomba huduma nao umefungwa yalipo makao makuu mwaka 2012 huu ni kwa ajili ya kusimamia utoaji huduma kwa kujali muda aliofika mteja,huu umerahisisha ufuatiliaji na tathmini ya utendaji kazi wa maofisa wanaohudumia wateja.
Taarifa ya idara hiyo inaonesha kuwa hadi kufikia Desemba 2012 ilikuwa imetoa hati za kusafiria 537,426 kati ya hizo hati za kusafiria za kawaida ni 518,561,za kidiplomasia 4753,za kiutumishi 1499 na hati za kusafiria za Afrika Mashariki 12,613.
Kati ya mwaka 2006 hadi Desemba 2012,Waziri wa Mambo ya Ndani amekubali maombi ya wageni 1,027 walioomba uraia wa Tanzania..
Tuesday, February 5, 2013
SAFER INTERNET DAY 2013
Over the years, Safer Internet Day (SID) has become a landmark event in the online safety calendar. Starting as an initiative of the EU SafeBorders project in 2004 and taken up by the Insafe network (www.saferinternet.org) as one of its earliest actions in 2005, Safer Internet Day has grown beyond its traditional geographic zone and is now celebrated in more than 90 countries worldwide, and across six of the world’s seven continents.
From cyberbullying to social networking, each year Insafe aims to be at the forefront of emerging online issues and chooses a topic reflecting current concerns. For SID 2012 we focused on connecting generations, as we invited people of all ages from very young children to parents and grandparents to “discover the digital world together… safely”.
Insafe, a network set up within the Safer Internet Programme
In 1999, the European Commission (EC) created the Safer Internet Programme, with the aim of promoting safe, responsible use of the internet by children and young people, and protecting them from illegal and harmful content and conduct online. The programme is managed by the Directorate General for Information, Society and Media and highlights the shared responsibility of NGOs, educational establishments, law enforcement bodies, industry and families in online safety initiatives across the European Union member states. In 2004, the Insafe network was set up to spearhead awareness activities within the Safer Internet Programme.
Safer Internet Centres and Committees
Today Insafe comprises 30 Safer Internet Centres, one in each of the 27 EU member states as well as in Iceland, Norway and Russia. Most Safer Internet Centres are composed of an awareness centre, helpline, hotline and youth panel. The helplines offer information and advice to children, young people, parents and teachers about how to stay safe online.
However, Safer Internet Day is also celebrated outside Europe. In 2009, the concept of Safer Internet Day Committees was introduced, to strengthen the bonds with countries outside the network and invest in a harmonised promotion of the campaign across the world. There are around 30 committees working closely with the Insafe coordination team, which is based at the heart of the European Union in Brussels.
Supporting SID
Saferinternetday.org provides a global online community platform where countries and international organisations can showcase events and actions conducted locally, nationally and internationally for Safer Internet Day.
Within these pages you will find a wealth of multilingual resources empowering young people, their teachers and their families to make the best possible use of online technology. It is a space where leaders in the internet safety community can communicate with the public and exchange ideas, knowledge and experience with each other.
Saturday, February 2, 2013
VYOMBO VYA HABARI VYATAKIWA KUTOA ELIMU KUHUSU MKONGO WA TAIFA
Ofisa Biashara wa Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano, Thomas Lemunge akitoa ufafanuzi katika semina kwa wahariri juu ya mkongo wa taifa katika Hoteli ya New Afrika jijini Dar es Salaam |
Vyombo vya habari nchi vimeombwa
kutoa elimu kwa jamii juu ya manufaa ya uwepo wa Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano
(National ICT Broadband Backbone-NICTBB) ili wananchi wauelewe na kuulinda
kutokana na umuhimu wake.
Changamoto hiyo imetolewa hivi karibuni jijini Dar es Salaam naMeneja
Uendeshaji wa NICTBB, Adin Mgendi alipokuwa akizungumza na wahariri wa vyombo
anuai vya habari juu ya utendaji kazi wa mkongo huo na manufaa yake kwa taifa.
Mgendi alisema manufaa ya ujenzi wa Mkongo wa mawasiliano nchini yameanza
kujitokeza hivyo Watanzania wana kila sababu ya kuulinda mtandao huo kwani
unaumuhi mkubwa kwa jamii na taifa.
Alisema kwa sasa jumla ya nchi sita, ambazo ni pamojana Malawi, Zambia,
Rwanda, Burundi, Uganda na Kenya zimeunganishwa na Tanzania hivyo nchi yetu
ikibeba dhamana ya kuwahudumia kupitia mtandao wa Mkongo.
Mtalamu huyo alivitaka vyombo vya habari kuendelea kutoa elimu kwa wananchi
hasa waliopo karibu na njia ya mkongo ili wasiuharibu kupitia shughuli
mbalimbali za kijamii zinazofanyika ardhini.
Akifafanua zaidi kwa wahariri wao, Ofisa Biashara wa Mkongo, Thomas Lemunge
alisema kwa sasa mikoa yote ya Tanzania Bara tayari imeunganishwa na mkongo
hivyo kurahisisha miundobinu ya mawasiliano.
Aidha aliongeza kuwa mtandao wa mkongo ambao ujenzi wake uaendelea umepita
maeneo anuai; ikiwemo ardhini pembezoni mwa barabara, mashambani, juu ya nyaya
za umeme na kwenye maji huku ukiwa na mizunguko mitatu yaani wa Kaskazini,
Magharibi na Kusini.
Awali akizungumza na washiriki hao, kabla ya kufungua warsha hiyo,
Mkurugenzi wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano nchini (TEKNOHAMA), Mhandisi
Zaipuna Yonah alisema mkongo unamanufaa makubwa kwani hadi sasa matumizi ya
intaneti yameongezeka tofauti na awali.
“Ongezeko la matumizi na faida za mkongo zinaongezeka siku hadi siku na
hivyo kukidhi matarajio ya Serikali ya kuziba pengo la matumizi ya TEKNOHAMA
kwa wananchi katika maeneo ya mbalimbali ya nchi yetu na hatimaye kukuza
uchumi,” alisema Yonah.
Wahariri hao walipata fursa ya kutembelea kituo kikuu kinachoratibu shughuli
za mkongo maeneo mbalimbali ya nchi na kuona namna wataalamu wanavyofanya kazi
eneo hilo.
Mkongo wa taifa ambao kwa sasa unategemewa na nchi jirani za Tanzania na makampuni binafsi katika usabazaji huduma za mawasiliano unasimamiwa na Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) huku wakiwa ndio meneja wa Mkongo huo.
Chanzo:The Habari.com