Thursday, May 30, 2013

MATAPELI WANATUMIA NAMBA ZA SIMU ZENYE MAJINA YA UONGO

Polisi kanda maalumu ya Dar es salaam wamezungumzia utapeli unaofanywa kwa kutumia simu za mkononi na kusema wengi wanaofanya hivyo husajili laini kwa majina ya uongo.

Kamishna Msaidizi wa Polisi na Mkuu wa Upelelezi Kanda Maalumu ya Dar es salaam,Ahmed Msangi amehadharisha wananchi kwa kutaka kuwa makini katika kutuma fedha kwa njia ya simu.

Alikuwa akizungumza na mwandishi wa habari wa gazeti la Habari Leo juu ya utapeli uliohusisha kampuni ya ndege ya kimataifa ya Qatar ambao baadhi ya watu wameibiwa pesa zao baada ya kuzituma kwa watu waliojifanya ni maofisa wa kampuni hiyo kwa ahadi ya kupatiwa kazi.

Kaimu meneja Mawasiliano Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA,Semu Mkwakanjala anasema alisema wanafanya mikutano kadhaa na kampuni za simu za mikononi kukumbusha kufuata utaratibu wa usajili wa namba unaozingatia sheria ili kuepusha kuendelea kutokea kwa uhalifu kupitia simu za mkononi.

Wednesday, May 29, 2013

MATUMIZI YA NAMBA ZA SIMU ZISIZOSAJILIWA NCHINI TANZANIA MWISHO JUNI 1,2013


 

Mamlaka ya Mawasilino Tanzania, TCRA, imesema watumiaji wa namba za simu ambazo hazikusajiliwa, watakatiwa mawasiliano ifikapo Juni Mosi mwaka huu. 

Tamko hilo lilitolewa jijiji Mbeya na Mkurugenzi wa Sheria na Leseni wa mamlaka hiyo, Elizabeth Nziga wakati wa semina kuhusu utekelezaji wa sheria mpya ya mawasiliano ya elektroniki na posta ya mwaka 2010 kwa wadau mbalimbali.
Hiyo ni awamu nyingine katika mipango ya TCRA, kwani awali ilikuwa na kampeni za kuzima mitambo ya analogia nchi nzima na kuwataka wananchi kuingia katika mfumo wa dijitali ulioanzia katika Mkoa wa Dar es Salaam Desemba 31, mwaka jana.
Mikoa mingine iliyoingia kwenye mfumo wa dijitali ni Arusha, Tanga, Dodoma, Mbeya na Mwanza. Nziga alisema mamlaka hiyo inasisitiza kuwa hatua hiyo ni utekelezaji wa makubaliano kati yake na watoa huduma za mawasilino ya simu na kufikia usiku wa Juni Mosi, namba za simu ambazo hazikusajiliwa zitakoma. Mmiliki wake hataweza kuitumia kupiga wala kupokea siku.
Alisema kuwa ni muda mrefu umepita ambao ulitolewa kwa ajili ya kusajili namba za simu lakini watu wengi hawakuweza kufanya hivyo kwa wakati na badala yake wamekuwa wakitumia simu vibaya ikiwa ni pamoja na kufanya uhalifu na kutoa lugha chafu.
Katika hotuba yake Mkuu wa Mkoa wa Mbeya,Abbas Kandoro, ilisema vyombo vya mawasiliano vimesaidia kukua kwa sekta mbalimbali..

Saturday, May 25, 2013

PROGRAM TUMISHI 5 ZA KUKUSAIDIA KUIPATA SIMU YAKO YA ANDROID ILIYOPOTEA

Simu za Android kwa sasa zimekuwa na watumiaji wengi na inawezekana ndio zinaongoza kwa kuwavutia wezi. Lakini bila kujali kuwa simu yako imeibiwa au umeisahau sehemu kuna umuhimu wa kuhakikisha unachukua tahadhari ili inapotokea tukio linalokufanya usijue simu yako iko wapi uweze kuifatilia. Hizi ni baadhi ya software ambazo unaweza kuweka kwenye simu yako na kukusaidia pale inapopotea au kuibiwa:


1. Anti Theft Droid 
anti-theft droid

Hii ni App inayokuwezesha kufuatilia simu yako pale inapokuwa imepotea au kuibiwa. Unapoiweka katika simu yako unakuwa na uwezo wa kuifuatilia kupitia browser ya internet kama Mozilla au google chrome na inaweza kukutumia email pale inapotokea simcard ya simu yako kubadilishwa na kuwekwa nyingine. Pia inakuwezesha kuona picha ambazo zimepigwa kwenye simu yako pale unapokuwa umeipoteza.


2. Snuko – Android Anti Theft Security

snuko anti-theft

Snuko ni App inayokuwezesha kuifuatilia simu yako ya android kwa kutumia GPS, Wi-Fi na mnara wa simu inayotumia. Snuko pia inaweza kuizima simu yako pale unapogundua kuwa imeibiwa na uwezekano wa kuipata haupo na inaweza kukupa taarifa pale simcard inapobadilishwa.


3. Total Equipment Protection App
Total Equipment Protection App

Hii inafanya kazi kama nyingine zilizotajwa hapo juu ikikuwezesha kujua simu yako iko maeneo gani lakini ikiwa na kitu cha ziada ambacho ni uwezo wa kufuta data zako zote zilizokuwa kwenye simu inapotokea ukashindwa kuipata simu yako..
4. Cerberus Anti Theft
Cerberus Anti Theft

Cerberus Anti Theft inaweza kutumika kuzilinda simu hadi 5 kwa wakati mmoja, pia inakutumia taarifa kupitia ujumbe mfupi “SMS”. Kitu kingine kizuri kuhusu App hii ni kuwa inaweza kufuatilia simu yako iko maeneo gani kwa kusikiliza mazungumzo kupitia microphone ya simu yako hata kama alieichukua haitumii kupiga simu.


5. Lost Droid 

lost droid


Lost Droid ni App ambayo inakusaidia kuitafuta simu yako iliyopotea kwa kutumia computer yako. Inaweza kukutumia taarifa ya mahali simu yako ilipo kupitia SMS bila kusahau kuizima simu yako kwa kutumia SMS.
  Chanzo:tanganyikanblog

Saturday, May 18, 2013

YALIYOELEZWA KWENYE KONGAMANO LA GOOGLE I/O 2013 KUHUSU TEKNOHAMA

Google I/O  ni kongamano linalofanyika kila mwaka California kwa kuwakutanisha Developers wa bidhaa za Google kama  Android, Chrome, Chrome OS, Google APIs, Google Web Toolkit, App Engine  na nyinginezo. Google I/O ilianza 2008 na I/O inamaanisha Input and  Output na Innovation in the Open.  Mwaka huu imefanyika Moscone Center, San Francisco. Chini ni baadhi ya vitu vilivyoongelewa.Tukio hilo lilioneshwa duniani live kwa kupitia YouTube na hapa Dar es salaam wanateknohama walikutana katika ofisi za KINU kushuhudia tukio hilo.

Android

Google million 900

Mwaka huu Google imeanza kutangaza kuwa na watumiaji milioni 900 kwa watumiaji wa simu za android huku program tumishi ( Apps) zaidi ya bilioni 48 zikiwa zimetumiwa. Hili ni ongezeko la zaidi ya mara mbili tofauti na mwaka jana ambao watumiaji walikuwa milioni 400 huku kwa mwaka huu pekee programa tumishi bilioni 48 zikiwa zimetumika.

Games

google gamer
Google wameiboresha Play Store kwa upande wa games ili ishindane na Apple’s Game Centre. Kwa sasa unaweza kucheza games na kulinganisha namba yako na ile ya marafiki zako ambao nao pia wameshacheza kabla yako.

Google Play Music

google music

Google Play inaonekana kulenga kushindana na spotify ambayo ndio kwa sasa inaonekana kuongoza. Hii itawawezesha watu kucheza wimbo wowote katika simu zao au computer kwa kulipia $9.999 kwa mwezi ambayo ni kama Shilingi 16,000 za kitanzania  kwa mwezi.


Google+

google hangout

 
Google Plus ambayo ilianza kwa kishindo lakini kujikuta ikishindwa kukabiliana na ushindani wa Facebook nayo imefanyiwa mabadiliko makubwa. 

 Imebadilishwa kutoka kwenye muonekano wake wa tovuti na kuifanya ionekane kama program tumishi nzuri ambayo kila mtu anapenda kuitumia. 

Hii inafanywa kukabiliana na Facebook ambao baada ya kuinunua Instagram wameongeza idadi ya watu waliokuwa wameanza kuikimbia kutokana na kuonekana haina jipya, Google+ inaonekana kujaribu kuongezea pale ambapo Facebook wameishia mfano katika picha wameongeza kitu kinachoitwa “Auto-Enhance” inayofanana sana na instagram filters.

 Hii inaonekana kufunika zaidi kwa sababu tofauti na kubadili rangi pia inafanya mazingira yaliyokuzunguka (Background) kuonekana kwa uzuri zaidi. Google+ imewekewa kitu kinaitwa “Auto Awesome” ambayo kazi yake ni kugundua picha ambazo umezipiga kwa wakati mmoja na kwa pozi tofauti na kukutengenezea GIF ambayo safi kulinganisha na “PicMix”.

Upande wa Google Hangout ambayo ilikuwa inapatikana kwa wanaotumia computer, sasa inahamia kwenye simu zinazotumia android  na iOS na pia itaongezwa extension yake katika google chrome. Hii inamaanisha Google Talk, Google+ Messenger na Google Hangout ya zamani zinaagwa rasmi. Google+ Hangout mpya inachukua rasmi nafasi na inaingizwa kushindana na WhatsApp na Facebook Messenger.

Galaxy S4 Kuwa Nexus
samsung nexus

Google itaanza kuuza Samsung S4 ambayo ina android. Hii itakuwa na vitu vingine ambavyo mtu mwenye S4 ya kawaida anavipata lakini itakuwa na kila kitu ambacho mtu anayetumia Nexus amezoea kukiona. Hii itaingia sokoni June 26 na itakuwa na ukubwa wa 16GB.


“OK Google”
google vs siri

Kwa waliokwishaitumia iPhone nadhani wanaifahamu Siri, app ambayo inakupa maelekezo kwa sauti. Google nao wamekuja na kitu kinaitwa “OK Google’  ambayo itakuwezesha kupata taarifa na kukukumbusha vitu kama taarifa za usafiri, miadi na hata vitu kama vipindi vyako cha TV. Pia una uwezo wa kuifungua “OK Google” na kuiuliza chochote katika computer na yenyewe itakutafutia kila kitu hata kama ilikuwa ni kwenye Google Search.


Google Play For Education
google play for education


Google imetangaza mpango wa kuhakikisha inatengeneza computer na tablet za bei rahisi kwa kila shule. Ili kufanikisha hilo imekuja na mpango inaouita Google  Play For Education ambayo ni store ya program tumishi kwa ajili ya kufundishia mashuleni. 

Kinachotakiwa ni kila mwanafunzi kuwa na account ya google na mwalimu atachagua program tumishi ipi gani inafaa kufundishia na kuiweka katika kila computer au tablet.

Asante kwa KINU waliofanya Live Streaming ya tukio zima na kukaribisha developers na wadau wengine wa Technology kuangalia moja kwa moja.

chanzo:tanganyikaniblog

Thursday, May 16, 2013

VIDEO YA MAPINDUZI YA KITEKNOHAMA YALIYOELEZWA MEI 15,2013 NA GOOGLE

Wednesday, May 15, 2013

MAFUNZO YA TEKNOHAMA KWA WASICHANA HAYA HAPA

Intro to Coding – Download pdf, print and post to places near you
Taasisi inayojihusisha na kuwawezesha wanawakike katika masuala ya teknohama duniani,Rails Girls itakuwa na maadhimisho ya juma zima la kimataifa la masuala ya teknohama  litakaloanza Mei 20,2013.

Kwa jijini Dar es salaam,Taasisi hiyo iliyoanzishwa nchini Finland itafanya maadhimisho hayo kwa kuwakutanisha wanawake wanaopenda kujihusisha na masuala ya teknohama hasa katika uundaji wa program za komputa na kuwapa mafunzo.

Mafunzo hayo yako wazi kwa mwanamke yoyote anayependa kuunda program  tu  yatafanyika zilizopo ofisi za  KINU kuanzia saa nane mchana, ili kushiriki jisajili bofya hapa

GOOGLE KUTANGAZA UTOAJI WA HUDUMA YA MUZIKI LEO?


Google Ready To Announce Streaming Music Service?

Tovuti ya readwrite inaeleza kuwa habari zilizoandikwa jana na The Verge, The Wall Street Journal na The New York Times zinaeleza kuwa Google inataraji kuanza utoaji wa huduma ya utangazaji wa Muziki mtandaoni jambo ambalo linatarajia kutangazwa leo na kampuni hiyo wakati maofisa wake watakapokutana na watengenezaji wa programu tumishi za tarakilishi leo Mei 15,2013  mkutano ambao utafanyika  Moscone Center, San Francisco utaneshwa katika sehemu mbalimbali duniani kupitia mtadaoni ambapo jijini Dar es salaam utaonekana "live" katika ofisi za KINU zilizopo barabara ya A.H.Mwinyi saa 1:00 kwa saa za Afrika Mashariki


Japokuwa Google hawajathibitisha rasmi lakini taarifa zinaonesha kuwa kampuni hiyo imeanza mchakato wa kupata leseni na  Universal Music Group, Sony Music Entertainment na tayali imeshaingia mkataba na  Warner Music Group ambazo zote ni Kampuni za Muziki duniani.

Times linaeleza kuwa huduma hiyo inataraji kutolewa kupitia program tumishi zinazopatikana kupitia Google Play kwa simu za Android pia kwa sasa kampuni hiyo inajipanga kutoa huduma hiyo ya muziki kupitia huduma yake maarufu ya You Tube,haya yote yanataji kufafanuliwa leo.

Saturday, May 11, 2013

WAZIRI MKUU WA TANZANIA AHAMASISHA MAKTABA ZA KIELEKTRONIKI

Waziri Mkuu Mizengo Pinda
Waziri Mkuu wa Tanzania Mizengo Pinda
 Waziri Mkuu wa Tanzania Mizengo Kayanza Pinda amewasihi wadau wa elimu nchini Tanzania kujitokeza kuchangia uanzishwaji wa maktaba ya kielektroniki ili kuondoa mizigo ya ubebaji wa madaftari kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari.

Pinda ametoa kauli hiyo huko Arusha jana alipokuwa akizindua mradi wa  makataba za mkononi za kielektroniki katika shule mbili, za Nanganga na Nambala ambazo zimefadhiliwa na Chuo cha Nelson Mandela na Taasisi ya Worldreader ya Marekani iliyotoa vitabu hivyo vilivyohifadhiwa katika mfumo kama wa laptop ambavyo vinahifadhi zaidi ya vitabu zaidi ya 100 vya masomo mbalimbali

Friday, May 10, 2013

WARSHA YA MATUMIZI YA MITANDAO JAMII KATIKA KULETA TIJA YAFANYIKA JIJINI DAR ES SALAAM


 Afisa wa Taasisi ya uwezeshaji na ujengaji uwezo kwa wateknohama nchini KINU,Catherinerose Barretto akimkabidhi cheti Ally Said toka Pangani,Tanga
Washiriki wa warsha ya Matumizi ya Mitandao jamii na Maendeleo katika jamii


Wanateknohama 22 toka mashirika,asasi na Taasisi mbalimbali nchini Tanzania wameshiriki katika warsha ya siku tano iliyoendeshwa na KINU taasisi isiyo ya kiserikali inayowawezesha na kuwajengea uwezo wanateknohama nchini Tanzania katika kuleta tija ya maendeleo ya Teknohama.

Washa hiyo ilikuwa ni kwa ajili ya kujifunza namna ambavyo mitandao ya kijamii inavyoweza kutumiwa na wanateknohama katika kuleta tija ya maendeleo katika nyanja mbalimbali za maisha.

Thursday, May 2, 2013

UNAVYOWEZA KUUNGANISHA FACEBOOK NA TWITTER YAKO

 


Watengeneza wa mitandao jamii wamejaribu kurahisisha na kuunganisha mitandao yao kwa ajili ya kuleta tija ya mawasiliano mfano ni facebook,twitter na skype.Hii inamaanisha kwamba unaweza kuchagua kuandika ama kufanya mawasiliano kwa kutumia mtandao mmojawapo wa kijamii na kuhusisha mitandao yote hiyo kwa wakati huo huo.

Kama una account ya twitter ingia kwa twitter yako baada ya hapo nenda setting mkono wako wa kulia kuna kama kinyota mbele ya bar ya seach bofya hapo utaona setting baada ya hapo angalia kushoto kuna menu bofya palipo andikwa Profile,ukishabofya hapo kutatokea ukurasa kushoto chini kabisa kuna mahali pana nembo ya facebook na pameandikwa connect to facebook bofya hapo itakuletea sehemu tatu za kuchagua

Allow Twitter to:
post retweets to Facebook
post to my Facebook profile
post to my Facebook page: 


Chagua njia mojawapo ama zote kwa unavyopenda baada ya hapo save changes hapo utakuwa umefanikiwa kuunganisha twitter yako na facebook,ikiwa na maana kwamba utakachokuwa unakipachika facebook kitakuwa kinaonekana kwenye twitter yako ama kinyume chake.
Pia hata kama unaaccount ya skype inaweza kuhusianisha kama ilivyofanyika twitter na facebook.

Popular Posts

Labels