Thursday, January 31, 2013

GHARAMA ZA KUPIGA SIMU ZASHUSHWA TANZANIA

 Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), imetoa viwango vipya vya bei elekezi ya gharama za kupiga simu kwa mwingiliano wa mitandao ya mawasiliano katika kampuni mbalimbali za simu nchini. Bei hizo zitakazoanza kutumika kuanzia Machi mosi mwaka huu, zitadumu hadi Desemba 31, mwaka 2017.

Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Profesa John Nkoma, aliwaambia waandishi wa habari jana, kwamba lengo na uwepo wa gharama hizo ni kuwapunguzia gharama watumiaji wa mitandao ya simu.


Kwa mujibu wa Profesa Nkoma, viwango hivyo vitasaidia kupunguza gharama za kupiga simu kwa mitandao yote ya simu bila kujali ukubwa wa kampuni.

Chini ya gharama hizo mpya, alisema kuanzia Machi Mosi, gharama za kupiga simu kwa dakika moja kutoka kampuni moja ya simu kwenda mtandao wowote itagharimu Sh 34.92.badala ya Sh 112 kwa dakika.

“Kuanzia Januari mosi mwaka 2014, zitakuwa ni shilingi 32.40, Januari mosi mwaka 2015, itakuwa ni shilingi 30.58, Januari mosi mwaka 2016, itakuwa ni shilingi 28.57 na hadi kufikia Januari mosi mwaka 2017, gharama ya kupiga simu kutoka mtandao mmoja kwenda mtandao mwingine itakuwa shilingi 26.96 kwa dakika badala ya Sh 112 ya sasa.

Profesa Nkoma alisema kwamba, kutokana na kupanuka kwa sekta ya mawasiliano nchini, kumesababisha liwepo ongezeko la watumiaji wa simu na kwamba hatua hiyo imeifanya TCRA kuangalia jinsi ya kuwasaidia watumiaji wa simu.

"Ingawa siyo kazi yetu kupanga viwango vya gharama za kupiga simu, inapofika hatua fulani ni lazima tuwajibike kwa kuwa sisi ni kama mdhibiti mkuu wa mawasiliano nchini, ingawa pia jambo hili linapaswa kushughulikiwa na wenye kampuni husika.

"Kwa kuwa wenye kampuni za simu walishindwa kukubaliana ndani ya muda tuliowapangia, tumeamua kupanga viwango hivi sisi wenyewe, kwani tumeona jinsi wananchi wanavyopata shida katika kuwasiliana pindi mmoja wapo anapokuwa mtandao wa simu tofauti na wa mwenzake.

“Tumelazimika kufanya hivi kwa sababu mtu anapokuwa katika mtandao fulani na kumpigia aliye mtandao mwingine, anakatwa kiwango kikubwa cha fedha, hii siyo sawa.

“Tunaamini viwango hivi nafuu vya gharama za kupiga simu kwa mitandao tofauti vitawasaidia watumiaji wengi wa simu, kwani wengi wao wamejikuta wakiingia gharama zisizo na ulazima kutokana na kuwepo kwa makato makubwa ya gharama za kupiga simu pindi wanapofanya mawasiliano ya kuingiliana na kampuni tofauti za simu.

"Unakuta mtu mmoja ana zaidi ya simu mbili na anafanya hivyo kwa lengo la kuepuka gharama za makato kutoka kwenye mitandao hiyo, kwani unakuta gharama za kupiga simu kutoka mtandao mmoja hadi mwingine ni kubwa ukilinganisha na gharama za kupiga mtandao huo huo.

"Kwa hiyo, punguzo hili litamsaidia mtumiaji wa simu awe na uhuru wa kutumia simu moja au laini ya mtandao mmoja kwa ajili ya mawasiliano na mtu wa mtandao mwingine kwa gharama hizi kulingana na dakika atakayoongea.

“Wananchi wajue kwamba, hii ni mara ya tatu tangu tuanze kutoa viwango vipya vya mabadiliko ya gharama za kupiga simu kwa mwingiliano wa mawasiliano katika kampuni za simu hapa nchini.

"Kwa mara ya kwanza kufanya mabadiliko haya ilikuwa mwaka 2004, mara ya pili ilikuwa 2008 na mara ya tatu imekuwa ni mwaka huu,” alisema.

Pamoja na TCRA kupanga viwango hivyo, alisema kampuni za simu za mkononi zinatakiwa kuchukulia uamuzi huu kama changamoto katika soko la ushindani wa biashara kwa kuwa zina ushindani wa kibiashara.

"Kampuni za simu zinatakiwa kuboresha huduma na kubuni njia mbadala za kuweza kukabiliana na ushindani wa soko kwa kipindi hiki, kwa kuwa bado tumetoa fursa kwa kampuni hizo kuwasilisha makubaliano yao kwetu juu ya viwango hivyo vipya tulivyovitoa na mwisho wa kufanya hivyo ni Machi 31, mwaka 2013.

 Hatua hiyo ya TCRA, imekuja baada ya kampuni za simu za mikononi kushindwa kukubaliana namna ya kurejesha makubaliano waliyoyafikia juu ya upangaji wa viwango vipya vya bei za kupiga simu kutoka mtandao mmoja kwenda mtandao mwingine.

Chini ya makubaliano hayo, kampuni za simu zilitakiwa kurudisha majibu kabla ya kuanza kwa mwaka 2013 viwango halisi vya gharama hizo vipatikane.

Saturday, January 26, 2013

MICROSOFT TO TURN OFF WINDOWS MESSENGERS ON 15 MARCH

Windows Live Messenger 


Microsoft is switching off its Windows Live Messenger service on 15 March.

On that date Messenger log-ins will no longer work and users must turn to Skype, said Microsoft in an email sent to all Messenger users.

The email also encouraged users to update to Skype and familiarise themselves with the service before the switch-off.
The service switch is a consequence of Microsoft's acquisition of Skype in October 2011 for $8.5bn (£5.3bn).

In November 2012, Microsoft announced that it was switching off Live Messenger in early 2013 but gave no firm date. At the same time, Microsoft made it possible for Messenger users to talk to and swap messages with contacts via Skype.

To help people migrate before 15 March, Microsoft has added an upgrade button to its desktop Messenger that when clicked uninstalls Messenger and puts Skype in its place.
Until the switch-off date Messenger would work as it always did, said Microsoft.

The Windows Live Messenger instant messaging program was known as MSN Messenger when it first launched in 1999. The service is believed to be used by about 300 million people every month.
China is the only nation in which Messenger will keep operating, because it is run under licence there.
Source:BBC

MATUMIZI YA TABLETS SASA YASHIKA KASI

Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Konferensi ya Mashariki mwa Tanzania Mchungaji Mark Warwa Marekana, Mchungaji L.Cooper  ambaye ni Makamu wa Kiongozi wa Mkuu katika kanisa la Waadventista wa Sabato Ulimwenguni (GC) kutoka nchini Marekani akiwa na Mkurugenzi wa mawasiliano Tanzania Mchungaji Mussa Mika wakiwa na tablets zao kwenye  mkutano wa viongozi wa kanisa hilo toka katika kanda tatu nchini Tanzania uliofanyika Morogoro,matumi ya vifaa hivyo vya kiteknohama sasa yanaonekana kushika kasi kwa watu wa kada mbalimbali

Friday, January 25, 2013

MITAMBO YA ANALOJIA TANGA,DODOMA KUZIMWA JANUARI 30

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), inaendelea kutoa elimu kwa umma ikiwa ni maandalizi ya zoezi la uzimaji wa mitambo ya analojia kwa mikoani.
Januari 30, mwaka huu, itakuwa ni zamu ya mikoa ya Tanga na Dodoma.

Hii ni baada ya zoezi hilo kuanza na Kanda ya Dar es Salaam, Desemba 31, mwaka jana.

Mbali ya Dar es Salaam, maeneo mengine kulikozimwa mitambo ya analojia siiku hiyo ni katika miji ya Kibaha, Bagamoyo, Kisarawe na Mkuranga mkoani Pwani.

Akizungumza na NIPASHE kwa njia ya simu jana, Mkurugenzi wa Mawasiliano TCRA, Innocent Mungy, alisema tayari ratiba ya mikoa mingine itakayofuatia katika zoezi hilo, imeshatolewa kupitia vyombo vya mbalimbali vya habari. 

“Tarehe 30 tunatarajia kuzima mitambo ya analojia mkoa wa Dodoma na Tanga  na baada ya hapo Februari 28 , mwaka huu itakuwa zamu ya mkoa wa Mwanza, Machi 31 ni zamu ya Arusha na Moshi na Aprili 20 itakuwa ni kanda ya Mbeya. Tutaendelea na utaratibu huo ili kuhakikisha mpaka ifikapo Juni, 2015, tumekamilisha zoezi hilo kwa mikoa yote,” alisema Mungy.

Alisema licha ya changamoto ya uelewa mdogo wa watu juu ya matumizi ya ving’amuzi, bado mamlaka inaendelea na zoezi la kutoa elimu kwa jamii kupitia matangazo, vipindi katika redio na kufanya mikutano mbalimbali.

"Hivi sasa ninavyoongea nipo Dodoma kwa ajili ya maandalizi ya uzimaji wa mitambo ya analojia kwa mkoa huu. Moja ya vitu tunavyo vifanya, ni utoaji wa elimu kwa wananchi," alisema.

"Tunawaelekeza wananchi kuhakikisha kwamba wanakuwa na uelewa  juu ya mfumo mpya wa dijitali pamoja na matumizi ya ving’amuzi," alisema.

Naye Afisa Mauzo wa kampuni ya Starmedia inayotoa  ving’amuzi vya Startimes,  David Kisaka, alisema kwa sasa kampuni hiyo imejipanga vizuri kwa kuongeza idadi ya wafanyakazi katika matawi yake yote ikiwamo kuweka wafanyakazi katika idara kulingana na ujuzi.

Kisaka aliwaomba wananchi kufanya manunuzi ya ving’amuzi mapema kabla ya siku ya uzimaji wa mitambo kufika katika eneo husika, ili kuepuka usumbufu kama uliojitokeza jijini Dar es Salaam.

“Tumepata usumbufu mkubwa sana hapa Dar es Salaam sababu watu wengi walisubiri mpaka mitambo izimwe ndipo wanunue ving’amuzi.  Sasa nawaomba sana wananchi wa Tanga na Dodoma wanunue ving’amuzi hivi mapema ili hata kama kuna matatizo yoyote, tuwasaidie badala ya kusubiri mpaka siku ya uzimaji,” alisema.
 

CHANZO: NIPASHE

Thursday, January 24, 2013

KENYA KUJENGA MJI WA KITEKNOLOJIA

Nchi ya Kenya imechukua hatua ya kwanza katika ujenzi wa kile kinachotarajiwa utakuwa mradi mkubwa zaidi barani Afrika wa mji wa kiteknolojia (Silicon Valley) au unaotegemea sana vifaa vya electroniki katika kuendeleza teknolojia ya habari na mawasiliano.

Rais Mwai Kibaki alizindua rasmi mradi huo katika eneo la Konza,mtaa mdogo kusini mwa Nairobi,ambako mji huo mpya wa kiteknolojia utajengwa katika muda wa miaka 20 ijayo.Rais Kibaki ambaye alizindua mradi huo muda mfupi kabla ya kuondoka madarakani mwezi machi alieleza mji wa Konza utasaidia kubadili uchumi wa Kenya kwa kiasi kikubwa.

Mradi huu wenye thamani ya Dola bilioni kumi na nne na nusu upo chini ya mpango wa Wizara ya Habari na Mawasiliano.Mradi huo unasemekana kutoa nafasi zaidi ya 100,000 za ajira ifikapo mwaka 2030 pamoja na kuendelea kudumisha ukuaji wa pato la nchi la jumla ya aslimia 10 katika kipindi cha miaka 18 ijayo.

Thursday, January 17, 2013

WAKAZI WA DAR ES SALAAM WATAHADHARISHWA NA WIZI KWA NJIA YA MTANDAO



MAARIFA:KUUNGANISHA MARAFIKI WA FACEBOOK NA GOOGLE + ANGALIA VIDEO HII

Wednesday, January 16, 2013

WAKULIMA NIGERIA KUGAWIWA SIMU ZA MIKONONI


 

Wakulima nchini Nigeria wamepewa bure simu za mikononi,Ingawa vyama vya upinzani vinakandia hali hiyo wananchi wengi wanaamini huo ni mkakati mzuri wa kuwasaidia wananchi.

Katibu Mkuu wa Chama cha upinzai cha All Nigeria Peoples Party (ANPP) Tijani Tumsa,alisema kuwa mpango huo ni njama ya serikali kuvutia wapigakura kwa uchaguzi utakaofanyika mwakani.

Hivi karibuni Waziri wa Kilimo nchini humo,Akinwumi Adesina alisema simu hizo za mkononi zitawasaidia wakulima kuleta mageuzi katika kilimo.

Adesina anasema Nigeria inaidadi kubwa ya watumiaji wa simu za mkononi wanaokadiriwa kufikia milioni mia moja na kumi,lakini wanigeria wengi waishio vijijini hawana huduma hizo.

Alisema simu milioni tano kati ya milioni kumi zitatolewa kwa wanawake.

Monday, January 14, 2013

TCRA YASEMA MIKOA IJIANDAE KWA MATUMIZI YA DIGITALI



Mkurugenzi wa Mawasiliano TCRA, Innocent Mungy
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imewataka wananchi wa mikoani kujiandaa na matumizi ya dijitali kwa kununua ving’amuzi miezi mitatu kabla ya kuzimwa kwa mitambo ya analojia nchi mzima Julai mosi, mwaka huu.
Mkurugenzi wa Mawasiliano TCRA, Innocent Mungy, alisema hayo wakati wa mahojiano yake na kituo kimoja cha redio jijini Dar es Salaam na kufafanua kuwa wananchi wanapaswa kujiandaa mapema ili kuepusha usumbufu kama ulio jitokeza kwa Mkoa wa Dar es Salaam.

“Tumeshuhudia usumbufu mkubwa ulio jitokeza hapa Dar, watu wengi walikuwa bado hawana uelewa wa jinsi ya kuvitumia ving’amuzi na wengine mpaka siku ya kuzima mitambo inafika bado hawajanunua,” alisema na kuongeza: “Wengine tulikwenda kuwatembelea  na kukuta hata umeme hajawasha ukutani, mwingine hajui  kuchomeka zile nyaya, Kwa kweli ni changamoto kubwa.”

Mungy alisema licha ya changamoto ya uelewa mdogo wa watu, kwa sasa wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa kwani yamebaki maeneo machache yenye matatizo madogo madogo na baada ya kukamilisha itafuatia mikoa ya Tanga na Dodoma.

“Bahati mbaya jiji la Dar limekuwa la kwanza katika zoezi hili, lakini tunaenda hatua kwa hatua baada ya kukamaliza hapa tutahamia Tanga na Dodoma hivyo wananchi wa mikoa hiyo watakuwa wamejifunza kutoka kwa wenzao wa Dar es Salaam,” alisema.

“Masuala ya malipo ya kila mwezi ya king’amuzi siyo ya lazima, kitu cha lazima ni malipo ya kusaidia kuiruhusu kadi ya mteja kufanya kazi, endapo atahitaji kuona chanali za ziada, atalazimika kulipia ili aweze kuzipata,” alisema Mungy.


Chanzo: NIPASHE

BOT YAUNDA KIKOSI KAZI KUKABILIANA NA WIZI WA KUTUMIA ATM

Kufuatia wizi wa fedha za wateja unaofanywa kupitia mashine za kuchukua fedha za ATMs, Benki Kuu (BoT) imeunda kikosi kazi kinachohusisha taasisi kadhaa zikiwamo benki na jeshi la polisi kuchunguza na kushughulikia uhalifu huo.

Kwa mujibu wa maelezo ya Lucy Kinunda, Mkurugenzi wa Masuala ya Malipo wa BoT kikosi kazi kinaundwa na BoT, Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA), Chama cha Mabenki nchini (TBA) na Idara ya Polisi ya Upelelezi wa Jinai inayoshughulikia vitengo vya uhalifu wa fedha na wa mtandao.

Katika muendelezo huo Kinunda alisema BoT imeziagiza benki zote kutoa mafunzo ya wafanyakazi ya kutunza siri na taarifa za ndani za wenye akaunti ili kuzuia uhalifu dhidi ya amana zao.

Pia BoT imeagiza wafanyakazi wasiowaaminifu wanaoshirikiana na wahalifu kuadhibiwa kikamilifu pia kufanya mchujo wa wafanyakazi kabla ya kuwaajiri.

Pia imewataka kuwahamasisha wateja kutunza neno ama namba ya siri na kuacha kuzitoa kwa jamaa na ndugu zao, pia wametakiwa kufuatilia usalama kwenye ATMs na kuanzisha mifumo ya kurekodi matukio ya wanaotoa fedha kwenye mashine hizo na kuhimizwa kuweka kamera za CCTV.

BoT imeyaagiza mabenki kupambana na kudhibiti wajanja wanaotumia mbinu za kuchota taarifa za wateja kwenye mashine hizo.

Baadhi ya mbinu zinazotumiwa ni kukamata kadi , kuweka vifaa vya kunakili na kunasa namba ya siri na utambulisho wao ili baadaye waweze kuandaa mbinu za kuiba kwa njia ya mtandao.

Kinunda alisema BoT imewashauri wenye mabenki kutumia viwango vya kimataifa vya kuhakikisha usalama wa kadi za ATMs za Visa na Master Card vya EMV.

EMV ni mikakati ya kimataifa ya kuziwezesha kadi za Master Card na Visa kuwa na usalama na kuziepusha zisitumiwe kihalifu na kuzilinda ili zibakie kuwa kadi zinazoweza kuingilia kwenye ATM ya benki yoyote ya kimataifa
.
Pia Benki Kuu kwa mujibu wa Kinunda itaendelea kupitia sheria za malipo ya kimtandao ili kudhibiti upungufu na kujiimarisha zaidi ili kuepusha uhalifu unaoweza kutokana na malipo ya mtandao.
Baadhi ya mbinu za wizi wa mtandao ni kupachika kifaa kama film inayoweza kurekodi taarifa za mteja kuanzia namba au neno la siri, kiasi cha fedha, jina na kumbukumbu zote.

Kikaratasi hicho huwekwa juu ya eneo ambapo kadi ya ATM huingizwa. Mteja anapochomeka kadi film husoma taarifa zake na kuzibakiza mikono mwa wezi ambao huzitumia kuchonga kadi mpya na kumwibia licha ya kwamba ametunza kadi yake.

Lakini pia wafanyakazi wa mabenki wa idara za teknolojia ya habari na mawasiliano (Teknohama) wanadaiwa kushirikiana na wezi hao .

Pia zipo taarifa kuwa baadhi ya watumishi wasio waaminifu wa kampuni zinazotengeneza kadi za ATM hushirikiana na wezi wa mtandao kuandaa kadi mpya ili kufanikisha wizi wa ATMs.
CHANZO: NIPASHE JUMAPILI

Friday, January 11, 2013

WATIWA MBARONI KWA TUHUMA ZA KUIBA KWA KUTUMIA KADI ZA ATM

 


Watu wawili wametiwa mbaroni kwa tuhuma za kukutwa wakiiba fedha kwa kutumia kadi 30 kwenye mashine ya kutolea fedha (ATM) ya Benki ya Afrika (Boa) eneo la Sinza jijini Dar es Salaam. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyela, alisema kadi hizo ni za wateja mbalimbali wa benki ya Barclays na walitaka kuiba fedha hizo kwa kutumia kadi hizo katika benki ya Boa. Kamanda Kenyela alisema watuhumiwa hao ambao walikamatwa jana saa 6:00 mchana, wametambuliwa kuwa ni raia wa Msumbiji lakini hakuwataja majina yao.

Alisema Jeshi la Polisi linaendelea kuwatafuta watuhumiwa wengine wanaojihusisha na wizi wa namna hiyo.

Aidha, Kamanda Kenyela alisema wizi kama huo wa kutumia mashine na kadi za benki, umekuwa ukitokea mara kwa mara jijini Dar es Salaam.

Alisema wengi wanaoibiwa fedha katika mashine za ATM, hawana uelewa wa kutosha namna ya kuzitumia hivyo kuwalazimu kuomba msaada kwa jirani, jambo linalowasababishia kuibiwa namba za siri na hatimaye kuibiwa.

Kamanda Kenyela aliongeza kuwa wizi mwingine ulitokea mwaka jana ambapo  watuhumiwa wawili raia wa kigeni walikamatwa wakiwa na ATM walizokuwa wakizitumia kuibia fedha.

Mei 29 mwaka jana, Polisi jijini Dar es Salaam walimkamata raia mmoja wa Bulgaria, ambaye alinusurika kuuawa na wananchi baada ya kudaiwa kuiba dola za 23,000 za Marekani kwenye ATM.

Tukio hilo lilitokea katika benki ya Standard Chartered, tawi la Ilala jijini Dar es Salaam.

Hata hivyo, mtuhumiwa huyo aliokolewa na askari waliokuwa doria.

Tuesday, January 8, 2013

WARSHA YA MAWASILIANO YA KANISA LA WAADVENTISTA WASABATO

Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Kanisa la Waadventista Wasabato Tanzania Mch Musa Mika akizungumza na wanahabari kuhusu warsha ya Mawasiliano inayofanyika katika Hoteli ya Rombo Green View jijini Dar es salaam

 
 Kiongozi Mkuu wa Kanisa la Waadventista Wasabato Tanzania Mch Godwin Lekundayo akifungua warsha hiyo

 Daryl Gungadoo(aliyevaa miwani)toka Radio ya Waadventista Ulimwenguni  Uingereza na John Beckett toka idara ya mawasiliano ya kanisa la waadventista nchini Marekani wakiweka mambo sawa na kufuatilia kinachoendelea katika washa hiyo

Thursday, January 3, 2013

VING'AMUZI VYA DIGITALI VYAWAKOSESHA BAADHI YA WAKAZI WA DAR ES SALAAM MATANGAZO YA TELEVISHENI

Mkurugenzi wa Mawasiliano wa TCRA, Innocent Mungy
Kuzimwa kwa mitambo ya kurushia matangazo ya televisheni kwa mfumo wa analojia,na kuwa katika mfumo mpya wa digitali kumesababisha sintofahamu ya wakazi wengi wa mkoa wa Dar es Salaam kushindwa kupata matangazo. Mitambo hiyo ilizimwa saa sita usiku Desemba 31 mwaka huu kwa maelekezo ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania  (TCRA). 
 
Sintofahamu hiyo imeonekana kwa baadhi ya wakazi wa  jiji la Dar es Salaam, kwa kutopata  matangazo ya televisheni licha ya kununua ving’amuzi.

Aidha, wamesema chaneli tano zilizopewa leseni  na serikali kuendelea kurusha matangazo yao, nazo zinaonyesha chenga chenga.
Baadhi ya watu wamekaririwa na vyombo vya habari wakidai kuwa mfumo huo umeleta usumbufu mkubwa kwao.
Wakati wananchi hao wakitoa malalamiko yao, Mkurugenzi wa Mawasiliano wa TCRA, Innocent Mungy akizungumza na wanahabari amesema kuwa kinachowafanya wananchi washindwe kupata matangazo ni wao wenyewe kushindwa kuunganisha ving’amuzi.
 Mungy aliwataka wananchi kubadilika na kutumia mafundi wa kampuni zinazouza ving’amuzi badala ya wao wenyewe kujigeuza mafundi.
Alisema huduma ya kufungiwa king’amuzi inatolewa bure na hakuna haja ya mtu kupanda juu ya nyumba yake na kuanza kufunga bila kujua anachokifunga.
Kabla ya kuzimwa mitambo hiyo Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Profesa John Nkoma, akizungumza na waandishi wa habari, alisema hata kama mitambo hiyo itazimwa, lakini chaneli tano za hapa nchini zitaendelea kurusha matangazo yake kama kawaida.
  Ving'amuzi vyagombewa
  Wakati zoezi la kuhamia dijitali likiendelea, blog hii ilishuhudia mamia ya wakazi wa Jiji la Dar es Salaam walifurika katika maduka mbalimbali ya mawakala wa kampuni ya Star Times kuendelea kununua ving’amuzi kwa ajili ya televisheni zao.
 
Hata hivyo, baadhi ya wakazi hao walikosoa huduma zilizokuwa zikitolewa na mawakala hao kwa madai kwamba hazikidhi kiwango kinachotakiwa.
Utafiti uliofanywa na blog hii umegundua kuwa ving'amuzi sasa vinauzwa kuanzia sh 39,000 hadi sh 62,000 za kitanzania.
 Afisa Masoko wa kampuni ya Star Times, Erick Cyprian, alisema watu walinukuu vibaya kuhusiana na suala la punguzo la manunuzi kwa kipindi cha kuelekea sikukuu.
“Punguzo la manunuzi ya king'amuzi halihusiani na muda wa hewani, hivyo wengi wao wanadhani wakishanunua king'amuzi kwa bei ya Sh. 39,0000, watapata muda wa maongezi moja kwa moja,” alisema Cyprian.
 
TCRA imekuwa ikieleza kuwa hatua ya kuhamia digital ni kufuatia Shirika la Kimataifa la Mawasiliano(ITU),kuzitaka nchi zote duniani kuhamia kwenye mfumo wa kurusha matangazo kwa njia hiyo ifikapo julai 2015.
 
Desemba 31,2012 Mamlaka hiyo inayosimamia mawasiliano nchini Tanzania ilieza kuwa mitambo ya analojia itazimwa katika mikoa ya Dar es salaam,Dodoma na Tanga ambapo zoezi hilo litahamia mkoa wa Mwanza na Machi 31,2013 itakuwa ni zamu ya mikoa ya Kilimanjaro na Arusha na mkoa wa mwisho utakuwa ni Mbeya ambako watazima Aprili 30. 
 
Kutokana na mfumo mpya wa digitali matangazo ya televisheni yanapatikana kupitia ving'amuzi ama madishi ya satalaiti. 
 
 

MKONGO AZINDUA SIMU YA KISASA

 



Kwa mara ya kwanza katika historia ya Afrika,Raia wa Afrika kutoka Congo-DRC  Verone Mankou,amezindua simu aina ya smarthphone na kompyuta za tablet.

Kampuni yake ya VMK inatumia vifaa vinavyoendeshwa kwa teknolojia ya Adroad ya Kampuni ya Google
Simu hizo za smartophone zitauzwa kwa bei ya rejareja ya dola za kimarekani 170 sawa  na shilingi 268,600 hivi za Tanzania.

Mankou aliyekuwa katika mkutano wa Tech4Afrika uliofanyika mjini Johannesburg hivi karibuni anasema ni waafrika wenyewe ndio watakaofahamu mahitaji ya afrika .

"Apple ni kampuni kubwa Marekani,Samsung ni barani Asia na tunataka VMK kuwa kampuni kubwa barani Afrika"anasema mvumbuzi huyo.


Simu hiyo ya smartphone nyumba na mbele ina kamera na skrini ya ukubwa wa inchi 3.5 sawa na sentimita 8.9,kuna mipango ya kuuza simu hizi katika nchi kumi za Afrika Magharibi pamoja na Ubelgiji,Ufaransa na India.

Mankou anasema anatajia kuzindua uuzaji wa kompyuta za bei nafuu zaidi kwa wanafunzi mapema mwaka huu.

VMK imesisitiza kuwa wakati bidhaa zake zinatengenezwa China kwa sababu za unafuu wa gharama ubunifu na uhandisi wa simu hizo ni wa kiafrika.

Popular Posts

Labels