Naibu
Kamishna wa Polisi na Kamanda wa Kikosi cha Polisi Usalama Barabarani
nchini ambaye pia ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Usalama
Barabarani, Mohamed Mpinga (wa pili kushoto) akifurahi jambo na baadhi
ya wafanyakazi wa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini. Kushoto ni
Mratibu wa Mradi wa kuboresha Demokrasia na Amani (DEP) kutoka ofisi ya
Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Bi. Beatrice Stephano, Afisa
Mfawidhi Ofisi ya Msajili wa vyama vya siasa kanda ya ziwa Mwanza, Bw.
Ludovick Ringia (wa pili kulia) nje ya ukumbi wa mikutano Ofisi ya
Waziri Mkuu mara baada ya kuwasili katika warsha ya siku nne ya wadau wa
utekelezaji wa mradi wa uchaguzi unaolenga kuboresha Demokrasia na
Amani nchini (DEP) kuelekea uchaguzi mkuu ujao iliyoandaliwa na Shirika
la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) na
kufadhiliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia maendeleo
(UNDP). (Picha zote na Zainul Mzige wa MOblog).
Na mwandishi wetu, Dodoma
Naibu
Kamishna wa Polisi na Kamanda wa Kikosi cha Polisi Usalama Barabarani
nchini ambaye pia ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Usalama
Barabarani, Mohamed Mpinga, amekubaliana na haja ya kuanzisha
mafunzo katika vyombo vya habari vya kijamii kama facebook ili kutanua
uwanja zaidi wa elimu ya usalama barabarani hasa kwa vijana ambao ndio
waathirika wakubwa wa ajali.
Aidha
amesema Polisi wanafikiriia kuanzisha mfuko wa kielektroniki wa ulipaji
wa faini kwa makosa ya barabarani ili kuongeza kasi ya udhibiti na
kuondoa tuhuma za rushwa.
Kauli
hiyo ameitoa mwishoni mwa wiki wakati akizungumza na wanahabari na
watendaji kutoka redio za jamii nchini mjini Dodoma, katika warsha ya
siku nne ya wadau wa utekelezaji wa mradi wa uchaguzi unaolenga
kuboresha Demokrasia na Amani nchini (DEP) kuelekea uchaguzi mkuu ujao
iliyoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na
Utamaduni (UNESCO) na kufadhiliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa
linaloshughulikia maendeleo (UNDP).
washa
ya siku nne ya wadau wa utekelezaji wa mradi wa uchaguzi unaolenga
kuboresha demokrasia na amani nchini kuelekea uchaguzi mkuu ujao.
Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa Unesco , Bw. Al Amin Yusuph, akisalimiana na Naibu Kamishna wa Polisi
na Kamanda wa Kikosi cha Polisi Usalama Barabarani nchini ambaye pia ni
Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mohamed
Mpinga, mara baada ya kuwasili kwenye warsha hiyo iliyomalizika mwishoni mwa wiki mjini Dodoma.
Kauli
yake hiyo ilifuatia hoja iliyotolewa na Afisa Miradi ya Mawasiliano,
Habari na Tehama wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni
(UNESCO), Bw. Al Amin Yusuph, ambaye aligusia redio za jamii katika
kusambaza habari zenye kulenga kuokoa maisha na mali kwa ajili ya
maendeleo ya taifa.
Mpinga
ambaye pia ni kamanda wa kikosi cha usalama barabarani alisema katika
mada yake kwamba changamoto kubwa ni kutekeleza sera ya kuhakikisha
kwamba hakuna kifo wala majeruhi katika ajali za usalama barabarani.
Akielezea
hali halisi ya ajali barabarani huku akikariri takwimu za Benki ya
Dunia na Shirika la Afya Duniani (WHO) kamanda Mpinga alisema kwamba
utafiti unaonesha katika kila wakazi 100,000 duniani 24 hufa katika
ajali za barabarani ambapo vijana na watu maskini ndio wapo katika
hatari kubwa zaidi.
Aidha
alisema takwimu zaidi kutoka WHO zinasema kwamba watu million 1 na laki
tatu hufa kila mwaka duniani hapa kwa ajali huku ikibainisha kwamba
asilimia 75 ya watu wanaojeruhiwa na kufa wanatoka katika nchi maskini
ambazo hazina magari mengi kama zile zilizoendelea.
Afisa
Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa Unesco , Bw. Al Amin Yusuph
(kushoto) akizungumza machache kabla ya kumkaribisha Naibu
Kamishna wa Polisi na Kamanda wa Kikosi cha Polisi Usalama Barabarani
nchini ambaye pia ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Usalama
Barabarani, Mohamed Mpinga, kutoa mada kwa watendaji wa redio za jamii
nchini. Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa mtandao wa redio za jamii nchini
(COMNETA) ambaye pia ni Meneja wa redio jamii Sengerema FM ya mkoani
Mwanza Bw. Felician Ncheye.
Alisema
pamoja na takwimu hizo za kutisha za duniani, nchini kwetu pekee watu
4000 hufa kila mwaka kutokana na ajali na mwaka uliopita walikufa watu
4002.
Akitoa
mada katika mafunzo hayo alisema kwamba ajali nyingi zinazotokea
zinasababishwa na binadamu ambapo asilimia 75 za ajali zote husababishwa
na makosa ya kibinadamu.
Alisema
utafiti unaonesha kwamba makosa hayo chanzo chake ni uzembe, ulevi,
mwendo kasi, kutozingatia sheria, uchovu wa madereva na matumizi ya
vyombo vya moto.
Aidha uzembe wa waendesha pikipiki ndio unabeba asilimia 20 hadi 30 ya ajali zote.
Alisema
kufunguliwa kwa biashara ya pikipiki kubeba abiria kumewaingiza vijana
wengi ambao wengi wao si wataalamu wakikosa sifa ya kuendesha vyombo
hivyo vya moto huku wakiwa vinara wa kuvunja sheria barabarani kwa
vitendo.
Naibu
Kamishna wa Polisi na Kamanda wa Kikosi cha Polisi Usalama Barabarani
nchini ambaye pia ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Usalama
Barabarani, Mohamed Mpinga, akiwasilisha mada
kwa watendaji wa redio jamii nchini (hawapo pichani) waliokuwa
wakihudhuria warsha ya siku nne ya wadau wa utekelezaji wa mradi wa
uchaguzi unaolenga kuboresha Demokrasia na Amani nchini (DEP) kuelekea
uchaguzi mkuu ujao iliyoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la
Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) na kufadhiliwa na Shirika la Umoja
wa Mataifa linaloshughulikia maendeleo (UNDP) iliyoamlizika mwishoni mwa
wiki mjini Dodoma. Kushoto ni Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na
Tehama wa Unesco , Bw. Al Amin Yusuph na Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa
mtandao wa redio za jamii nchini (COMNETA) ambaye pia ni Meneja wa redio
jamii Sengerema FM ya mkoani Mwanza Bw. Felician Ncheye.
Madereva hao alisema wanaendesha kasi, hawavai kofia ngumu na kubeba abiria kwa mtindo wa mishikaki.
Akifafanua
zaidi amesema kwamba pamoja na madereva wa pikipiki kuongoza kwa
kuvunja sheria hali za barabara kama kukosekana kwa alama, muundo wa
barabara zenyewe, utelezi , uchakavu wa vyombo na hali ya hewa vimekuwa
visababishi vya ajali.
Kamanda
alitaka vyombo vya habari vya redio za jamii kuelimisha madereva
matumizi sahihi ya barabara kwa kuwaita wataalamu kuelezea mambo hayo
bila chumvi wala kuharibu nidhamu na maisha .
Alisema
mathalani maeneo ya mnadani madereva wamekuwa wakivunja sheria hasa
upakiaji wa mizigo isiyozingatia usalama wa abiria waliomo.
Alisema
jeshi la polisi limechukua mikakati kadhaa kuwezesha kukabiliana na
hali ya usalama barabarani hasa kwa kuanzisha ukamataji wa makosa
hatarishi katika usalama wa barabara.
Makosa
hayo ni mwendokasi, ulevi, uendeshaji wa hatari na uzidishaji wa abiria
alisema faini zinazotolewa zimefanya kupungua kwa ajali kutoka elfu 17
hadi elfu 11.
Alisema
mikakati mingine ni utoaji wa elimu kwa kupitia vyombo vya habari na
kushukuru kwamba elimu hiyo anaona inasaidia. Alisema wanatoa elimu
kupitia televisheni , redio na vyombo vya habari vya kijamii.
Aidha wamekuwa wakishiriki kutoa mafunzo wakishirikiana na wadau wengine.
Pia
aliutaja mkakati mwingine ni kuboresha mifumo ya utendaji kwa kuainisha
maeneo yanayotokea ajali mara kwa mara, ukusanyaji wa takwimu na
kubadili mfumo wa ukaguzi barabarani kwa kuanzisha maeneo maalumu ya
kukagulia magari kwa undani.
Pia kunatengenezwa mfumo wa nukta ambapo dereva anapofanya makosa pointi zinaondolewa na zikimalizika anapokonywa leseni.
Kuhusu
ulipaji wa faini kupitia benki na njia nyingine za elektroniki alisema
zitarahisha utendaji wa polisi na kuondoa tuhuma za rushwa na pia
kuwafanya watu kuwa waangalifu zaidi.
Aidha
amesema wanatengeneza utaratibu kwa kushirikiana na wadau wengi
kutengenezwa kanuni ya ulazima wa madereva kurejea shule kwa mafunzo
hasa kutokana na kubadilika mara kwa mara kwa miundombinu ya barabara na
teknolojia ya magari.
Sehemu
ya wadau/watendaji wa redio jamii wa utekelezaji wa mradi wa uchaguzi
unaolenga kuboresha Demokrasia na Amani nchini (DEP) kuelekea uchaguzi
mkuu ujao wakifuatilia kwa umakini mada iliyowasilishwa na Kamanda
Mpinga kwenye warsha hiyo.
Hata
hivyo alisema pamoja na mikakati hiyo na mingine Jeshi la Polisi
linakabiliwa na changamoto zinazoambatana na bajeti ndogo ya kuiwezesha
kununulia vifaa vya kazi kama speed radar za kisasa na mifumo muafaka ya
kusimamia usalama barabarani ambapo kwa sasa kila tatizo wanasukumiziwa
polisi iwe ni taa mbovu za barabarani au mashimo.
Changamoto nyingine ni wananchi wenyewe kukosa utamaduni wa kuheshimu sheria mpaka waone polisi.
Alivitaka
vyombo vya redio jamii kufundisha wananchi na wala sio kuchochea wao
wazidi kuvunja sheria na kuitoa mfano wa matuta barabarani ambayo
yanadaiwa na wananchi na kusema hiyo si dawa bali elimu kwa wananchi
kuhusu usalama barabarani na namna ya kudhibiti ajali.
Naye
Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa Unesco , Bw. Al Amin
Yusuph akimkaribisha Kamanda Mpinga azungumze alisema mafunzo hayo
yameandaliwa kwa ajili redio za jamii kujiuza kw apamoja katika
kuhudumia umma na kujiendeleza.
Alisema
redio ndio njia pekee ya kuwafikia watanzania wengi hasa kwa kuzingatia
kwamba watumiaji wa vyombo vingine ni wachache hasa kutokana na
kukosekana kwa nishati na pia kuwa mbali na maeneo yanayotangaza habari.
Wasaidizi
wa Kamanda Mpinga wakigawa machapisho mbalimbali yanayotoa elimu ya
usalama barabarani kwa washiriki wa warsha hiyo iliyomalizika mwishoni
mwa juma mjini Dodoma.
Reportuer
wa warsha ya wadau wanaotekeleza mradi wa uchaguzi iliyomalizikia
mwishoni mwa juma mjini Dodoma Mchungaji Privatus Karugendo akihoji
suala la baadhi ya watumiaji wa vyombo vya moto wanaotumia simu za
viganjani pindi wawapo barabarani kitu ambacho ni hatari kwa usalama
wao.
Baadhi ya machapisho yaliyogawiwa kwa watendaji wa redio jamii nchini yanayotoa elimu ya usalama barabarani.
Baadhi
ya washiriki wa warsha hiyo wakipitia machapisho hayo yaliyotolewa
na Kitengo cha Polisi Usalama Barabarani kwenye warsha hiyo.
Naibu
Kamishna wa Polisi na Kamanda wa Kikosi cha Polisi Usalama Barabarani
nchini ambaye pia ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Usalama
Barabarani, Mohamed Mpinga, akipata picha ya kumbukumbu na Mshiriki wa warsha hiyo Prosper Kwigize.
Naibu
Kamishna wa Polisi na Kamanda wa Kikosi cha Polisi Usalama Barabarani
nchini ambaye pia ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Usalama
Barabarani, Mohamed Mpinga, akifurahi jambo na Mkurugenzi wa redio jamii Uvinza Fm, Alhaji Ayubu Kalufya.