Mamlaka ya mawasiliano nchini ,TCRA, imewaonya wale wote wanaotumia mitando
kuchafua na kudhalilisha watu waache mara moja vinginevyo watakabiliwa
na mkono wa sheria.
Onyo
hilo limetolewa jana mjini Arusha na Kaimu Mkurugenzi wa mamlaka
ya mawasiliano nchini TCRA, Dkt, Raynold Mtungahema, alipokuwa akitoa
ufafanuzi wa maswali ya wanahabari kuhusu kuenea kwa picha chafu
zinazowadharirisha watu mbalimbali kwenye mitandao..
Mtungahema,
amesema matumizi ya mitandao ambayo sio sahihi ni kosa la jinai na
hivyo wale wote wenye tabia hiyo waache mara moja na akawataka
wanaochafuliwa kupitia mitandao wafungue majalada polisi na mamlaka
hiyo itasaidia kuwafuatilia wahusika na kuwafikisha mbele ya vyombo vya
sheria .
Alisema
mitandao yote imesajiliwa hata kama aliyehusika kuchafua anaishi
uvunguni atakamatwa kwa kuwa mitandao haipo kwa ajili ya matumizi yasiyo
sahihi ambayo hayaruhusiwi.
Mtungahema,
amesema atakaebainika anatumia mtandao kumchafua mtu mwingine huyo
amefanya kosa la jinai hivyo afikishwe mbele ya vyombo vya sheria kwa
kuwa tayari zipo sheria zinazotoa adhabu kwa mtuhumiwa atakaepatikana na
hatia.
Aliongeza
kuwa TCRA, imeshapokea malalamiko mengi na tayari wahusika wameshatiwa
mbaloni na ufuatiliaji utaendelea ili mradi tu mamlaka hiyo itaarifiwe .
Nchi
wanachama wa jumuia afrika mashariki zimeaanza kikao cha siku nne
mjini Arusaha kwa ajili ya kutafuta ufumbuzi wa chang moto mbalimbali
zinazoikabili sekta ya mawasiliano.
Mwenyekiti
wa jumuia hiyo ya sekta za mawasiliano, EACO, Dakta Fracis Wangusi,
amesema sekta ya mawasiliano inakabilwa na changamoto mbalimbali ambazo
zinakwamisha upatikanaji wa huduma za mawasiliano kwa haraka.
Wangusi
ambae pia ni mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya mawasiliano nchini
Kenya,amezitaja sekta hizo kuwa ni pamoja na kuhama kutoka mtandao wa
analojia kwenda digital na matumizi ya visumbusi kwa ajili ya luninga.
Aliongeza
kuwa , sekta ya simu inakabiliwa na changamoto ya kuwepo gharama kubwa
za matumizi ya simu, usambazaji barua na vifurushi kunakofanywa
namashirika ya posta unaotokana na ukuaji wa mji ambao haujapangiliwa
,matumizi ya vikwazo vya kuchelewesha huduma ya haraka ya internet .
Alisisitiza kuwa ili kupatikana kwa mafanikio hayo ni kuondoa vikwazo na kuhimiza uwekezaji kwenye sekta ya mawasiliano ICT.
Chanzo:edwinmoshi.com