Kuna Utapeli umeanza kusambaa saa chache zilizopita kupitia CRDB INTERNET BANKING .
Anayefanya utapeli huu ametengeneza majina bandia ya watu maarufu
kama wanasiasa na wanamuziki kisha anaingiza watu kwenye orodha ya namba za mawasiliano alizohifadhi halafu anawatumia ujumbe huu kama vile yeye ni mtu halisi .
Mtu anapokubali anampa huyu jamaa taarifa zake za benki halafu
mwisho wa siku hela zake zinaweza kuhamishwa kwa njia ya mtandao .
MFANO WA UJUMBE NI HUU
------------------------------ -----------------------
Habari za wakati ndugu watanzania! Kwa yoyote ambae amejiunga na
huduma ya CRDB Bank kupitia Online. Internet Banking sio SIM BANKING
alie jiunga na Internet Banking. Tafadhali naomba tuwasiliane kuna
project maalum yenye faida kwangu nakwako pia kwa kushirikiana nao CRDB
Bank. Malipo ni kila wiki katika hiyo project. Nitumie meseji inbox kama
umejiunga na internet banking na unahitaji kushiriki katika hii project
============================== ============================== ==
Mpaka sasa hivi nimegundua majina 2 ya Kala Jeremia ambaye ni mwanamuziki na Jerry Silaa ambaye ni mwanasiasa .
Tuchukuwe tahadhari na tusambaze ujumbe huu .
Na:Yona Maro