Semina kuhusu
mfumo wa utunzaji wa taarifa za washiriki katika Kanisa la Waadventista
Wa Sabato (ACMS) imemalizika jijini Arusha Septemba 26,2013.
Semina hiyo iliyohudhuriwa na Makatibu
wakuu pamoja na Wakuu wa Teknohama kutoka majimbo yote ya Kanisa la
Waadventista Wa Sabato nchini Tanzania imekuwa na mafanikio makubwa
kutokana na wahusika wote kuhudhuria kikamilifu.
Akizungumza katika
kuhitimisha semina hiyo, Msimamizi wa mfumo huo kutoka Makao Makuu ya
Kanisa la Waadventista Wa Sabato Ulimwenguni Bi. Sherri Ingram-Hudgins,
ametoa shukrani zake kwa Uongozi wa Tanzania Union pamoja na washiriki
wote wa semina hiyo kwa ushirikiano waliouonyesha kwa muda wote wa
semina.
Pia Katibu Mkuu wa Tanzania Union,
Mchungaji Davis Fue, amewashukuru wakufunzi pamoja na wote
waliohudhuria semina hiyo, huku akiwataka Makatibu Wakuu pamoja na
Wakuu wa Teknohama kuharakisha upatikanaji wa taarifa za washiriki wa
Kanisa ili matumizi ya mfumo huo yaanze kwa ufanisi.
Mfumo huo uliobuniwa na wataalamu watano wa program za komputa unakadiliwa kutumia dola za kimarekani milioni 5.
Mfumo huo uliobuniwa na wataalamu watano wa program za komputa unakadiliwa kutumia dola za kimarekani milioni 5.
Sherri Ingram-Hudgins ambaye ni
msimamizi wa mfumo wa ACMS kutoka Makao Makuu ya Kanisa la Waadventista
Wa Sabato Ulimwenguni akitoa maelezo ya kuhitimisha semina hiyo.
Mr. Haggai Abuto ambaye ni Mkuu wa
Teknohama kutoka Divisheni ya Afrika Mashariki na Kati akitoa shukrani
zake katika kuhitimisha semina hiyo.
Mchungaji Davis Fue ambaye ni Katibu
Mkuu wa Kanisa la Waadventista Wa Sabato, Tanzania Union akitoa shukrani
zake katika kuhitimisha semina.
Washiriki wa semina ambao ni Makatibu Wakuu na Wakuu wa Teknohama wakiwa katika picha ya pamoja.