Saturday, September 21, 2013

BBM SASA KUANZA KUPATIKANA KATIKA ANDROID NA iOS



Program Tumishi maarufu ya mawasiliano ya ujumbe wa papo kwa papo katika simu za BlackBerry inayojulikana kwa jina la  BlackBerry Messenger (BBM) inaanza kupatikana mwishoni mwa juma hili  katika vifaa vya mawasiliano vilivyotengenezwa katika mfumo wa program za  Android na  iOS.

Kampuni ya BlackBerry imesema program tumishi hiyo itapatikana katika vifaa vya mawasiliano vyenye Android 4.0 na zaidi ,  iOS 6 na iOS 7,ambapo itawawezesha watumiaji wa vifaa vya Android na  iOS kuwasiliana na wale wenye  BlackBerry.

BBM ni program tumishi inayowezeshwa na intanet kuwasiliana kwa ujumbe maandishi wa papo kwa papo na simu kwa njia ya video ambapo kwa sasa takwimu zinaonesha kuwa kwa mwezi watu milioni 60 wanaotumia BlackBerry wanajiunga na huduma hiyo.

 Pamoja na hayo kumekuwa na tetesi kuwa kampuni ya BlackBerry itapunguza asilimia 40 ya wafanyazi wake kutokana na kukosa soko kwa tabiti yake mpya ya PlayBook iliyotoka hivi karibuni.

Huduma za BBM katika  Android na  iOS

-Mawasiliano ya papo kwa papo katika simu za  Android, iPhone na  BlackBerry
-Ni zaidi ya kuchat-kwani unaweza kutuma file la sauti linaloambatana na maandishi.
-Unaweza kuwasiliana na watu wengi kwa wakati mmoja kwa idadi ya watu 30

-Inakupatia neno la siri la pekee linaloimarisha faragha kwa mtumiaji bila kutumia namba ya simu ama anuani yako ya barua pepe.

Popular Posts

Labels