Saturday, September 28, 2013

SEMINA YA ACMS YAMALIZIKA

Semina kuhusu mfumo wa utunzaji wa taarifa za washiriki katika Kanisa la Waadventista Wa Sabato (ACMS) imemalizika jijini Arusha Septemba 26,2013.

Semina hiyo iliyohudhuriwa na Makatibu wakuu pamoja na Wakuu wa Teknohama kutoka majimbo yote ya Kanisa la Waadventista Wa Sabato nchini Tanzania imekuwa na mafanikio makubwa kutokana na wahusika wote kuhudhuria kikamilifu. 

Akizungumza katika kuhitimisha semina hiyo, Msimamizi wa mfumo huo kutoka Makao Makuu ya Kanisa la Waadventista Wa Sabato Ulimwenguni Bi. Sherri Ingram-Hudgins, ametoa shukrani zake kwa Uongozi wa Tanzania Union pamoja na washiriki wote wa semina hiyo kwa ushirikiano waliouonyesha kwa muda wote wa semina.

Pia Katibu Mkuu wa Tanzania Union, Mchungaji Davis Fue, amewashukuru wakufunzi pamoja na wote waliohudhuria semina hiyo, huku akiwataka Makatibu Wakuu pamoja na Wakuu wa Teknohama kuharakisha upatikanaji wa taarifa za washiriki wa Kanisa ili matumizi ya mfumo huo yaanze kwa ufanisi.

Mfumo huo uliobuniwa na wataalamu watano wa program za komputa unakadiliwa kutumia dola za kimarekani milioni 5.

Sherri Ingram-Hudgins ambaye ni msimamizi wa mfumo wa ACMS kutoka Makao Makuu ya Kanisa la Waadventista Wa Sabato Ulimwenguni akitoa maelezo ya kuhitimisha semina hiyo.

Mr. Haggai Abuto ambaye ni Mkuu wa Teknohama kutoka Divisheni ya Afrika Mashariki na Kati akitoa shukrani zake katika kuhitimisha semina hiyo.

Mchungaji Davis Fue ambaye ni Katibu Mkuu wa Kanisa la Waadventista Wa Sabato, Tanzania Union akitoa shukrani zake katika kuhitimisha semina.

Washiriki wa semina ambao ni Makatibu Wakuu na Wakuu wa Teknohama wakiwa katika picha ya pamoja.

Popular Posts

Labels