Saturday, September 21, 2013

FACEBOOK WATAKA KUJUA MAANA YA KINA YA PACHIKO LAKO




Facebook imeanza kutumia   teknolojia iitwayo  akili bandia (AI) inayotambua maana ya kina ya pachiko la mtumiaji wa mtandao huo wa kijamii.

Mbinu hii itaweza kusaidia  Facebook kuwaelewa  watumiaji wake na data zao zilizo bora.

Facebook imeweka utaratibu huo ili kufahamu vyema watumiaji milioni 700  ambao hushiriki maelezo ya maisha yao binafsi kwa kutumia mtandao jamii kila siku.

Kikundi cha watafiti wapya  ndani ya kampuni hiyo inafanyia kazi  teknolojia inayotumia  nguvu ya akili bandia ya utambuzi inayojulikana kwa jina la  kujifunza  kwa kina, ambayo inatumia mifumo ya utambuzi wa seli za ubongo zinavyotambua mchakato wa data,Utaratibu ambao unaonekana kuisaidia Facebook kupata matangazo ya biashara kutokana na namna watumiaji wanavyowasiliana.

Ofisa wa Teknolojia wa Facebook Mike Schroepfer amesema lengo lingine la utaratibu huu ni kuweza kupunguza idadi ya mapachiko na habari zinazoonekana kwenye  mtandao huo kutoka 1500 kuwa 30 au 60 kwa zile ambazo ni muhimu tu.

Teknolojia hii pia kwa sasa tayali inatumiwa na makampuni ya google na microsoft ambapo inaelezwa ni miongoni mwa teknolojia 10 za hali ya juu zilizoibuniwa mwaka 2013.



Popular Posts

Labels