Watu wanne huko
nchini Marekani wameushitaki mtandao wa kijamii wa LinkedIn unaowaunganisha
wanataaluma kuwa umekuwa ukiingilia wasifu wao kwa kutuma maombi kwa marafiki zao kujiunga na mtandao huo.
Tuhuma
hizo zimeeleza kuwa LinkedIn imekiuka sheria ya shirikisho pamoja na sheria
ya faragha ya jimbo la California,ambapo
imedaiwa kuwa mtandao huo unapoomba
anuani ya barua pepe kwa mtumiaji hauweki wazi kuwa itatumika kuwaomba watu wengine kujiunga na
LinkedIn kupitia anuani ya barua pepe ya mhusika.
Madai mengine yanayoelezwa ni kuwa kwa muda wa miaka mine watu
wamekuwa wakilalamikia utaratibu wa masoko unaotumiwa na mtandao huo.