Mahakama ya kimataifa ya ICC imetoa onyo kali kwa wanablogu nchini
Kenya,wanaotoa taarifa kuhusu mashahidi waliofika mbele ya mahakama ya
ICC.
Hii ni baada ya taarifa kuhusu shahidi wa kwanza mbele ya
mahakama hiyo kujitokeza kwenye mitandao hasa kwenye blogu, twitter na
Facebook kumhusu.
Blogu hiyo ya udaku pia ilichapisha picha ya mwanamke huyo
Baadhi
ya taarifa zilisema kuwa amewahi kutoa ushahidi wake ambao
haukutofautiana na alioiambia mahakama ya ICC, katika mahakama nchini
Kenya lakini ukapuuziliwa mbali na mahakama.
Mashahidi hao wanatoa
ushahidi wao ndani ya mahakama ila wamefichwa nyuso zao hatua
iliyochukuliwa ili kuwalinda kutokana na tisho lolote dhidi ya maisha
yao.
ICC huenda ikachukua hatua za kisheria dhidi ya wanaosambaza taarifa kuhusu mashahidi wanaofika mbele ya mahakama hiyo.
Jaji
anayeongoza vikao hivyo, Chile Eboe-Osuji, alisema kuwa ni makosa
kisheria kuwafichua mashahidi wakati mahakama imebana kuwatambulisha.
Shahidi
huyo ambaye wenye blogu wanasema wanamfahamu, ni mwanamke mwathiriwa wa
shambulizi dhidi ya Kanisa la Kiambaa ambako yeye na wanakijiji wenzake
walitafuta hifadhi wakati wa ghasia za baada ya uchaguzi kutokota
katika mkoa wa Rift Valley.
Watu zaidi ya thelathini waliteketezwa wakiwa hai ndani ya kanisa hilo.
Chanzo:BBC
Popular Posts
-
Kampuni ya Simu nchini Tanzania (TTCL) jana imekabidhi mradi wa mawasiliano utaotumiwa katika mikoa 12 ya Tanzania kwa ofisi ya Mkaguzi na ...
-
Miaka michache iliyopita kulikuwa na changamoto ya kuhifadhi vitu sehemu ambayo mtu anaweza kutumia akiwa popote duniani akiwa ame...
-
Ofisa Biashara wa Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano, Thomas Lemunge akitoa ufafanuzi katika semina kwa wahariri juu ya mkongo wa taifa katika...