Friday, October 11, 2013

GOOGLE YAENDELEA KUONGOZA KATIKA KIPATO TOKA KUANZISHWA KWAKE MIAKA 15 ILIYOPITA

 
Google ni kampuni ya teknolojia ya habari na mawasiliano, makao yake makuu yakiwa huko Mountain View,California,Marekani.Kampuni hiyo hutoa huduma za mawasiliano ya intaneti ,matangazo ya biashara kupitia mitandao,compyuta na program za kompyuta.

July 2012 Google.com ilikuwa ni tovuti iliyokuwa imetembelewa na watu wengi duniani huko Marekani ambapo walifikia watu milioni  166.47 nchini humo na kujipatia kiasi cha mapato ya mtaji wake wa dola bilioni 184.5 .

Ikiwa na miaka  15  sasa  baada ya kampuni hiyo iliyoanzishwa kwenye karakana huko Menlo Park, Septemba 4, 1998,Google imekuwa maarufu katika ulimwengu wa mtandao wa intaneti.

Takwimu toka tovuti ya mashable  zinaonesha kuwa mwaka 2013 Google wamepata dola za kimarekani bilioni 36.9  kutokana na matangazo ya biashara ambapo Facebook ambao ni washindani wake wao walipata dola za kimarekani bilioni 6.4

Kwa upande wa mgawanyo wa mapato toka matangazo kwenye simu za mkononi Google wamepata asilimia 53 na facebook wao wamepata asilimia 13 ya matangazo hayo kwa mwaka 2013.

Katika matangazo yanayowekwa katika vivinjali,Google kupitia kivinjali cha chrome wamepata mgawanyo wa  mapato ya asilimia 43 wakati kivinjali cha internet explorer cha kampuni ya  Microsoft  kikipata mgawanyo huo kwa  asilimia 26 

Kwa upande wa  kutafuta mambo mbalimbali  kwa mwezi wa disemba mwaka 2012 kupitia tovuti ya Google  ilitumiwa na watu milioni 1,168 waliotafuta masuala yapatayo bilioni 114.7,wakati mtandao mwingine wa Baidu ulioko China ulitumiwa na watu milioni 293 katika kutafuta masuala mbalimbali kwenye mtandao yapatayo bilioni 14.5. 

Katika mgawanyo wa mapato yatokanayo na program za kutengenezea simu katika robo ya pili ya mwaka 2013 Google walipata asilimia 79 kutoka kwa program ya Androd na iOS wao walipata asilimia 14,ambapo pia walifanikiwa kuongoza kwa asilimia 54 kutokana na programu yao  tumishi ya google maps ikifuatiwa na facebook iliyopata asilimia 44 katika kipindi hicho cha mwaka 2013
 

Popular Posts

Labels