Saturday, October 5, 2013

TOVUTI ZINAZOTEMBELEWA ZAIDI KWA KILA NCHI

TopSitePerCountry_InternetPopulation 
Katika kile ambacho kinaelezwa kuwa ni kipindi cha himaya  enzi ya  utawala wa intaneti ramani hii inaonesha tovuti ambazo zinatembelewa mara nyingi zaidi kwa kila nchi duniani.

Ramani hii imetokana na utafiti wa takwimu unaofanywa kupitia tovuti ya Alexa na kutolewa Agosti 12,2013 ambapo kampuni hiyo ilianza kufanya uchambuzi huo toka mwaka 1996.Alexa hukusanya data kutoka katika mamilioni ya watumiaji wa intaneti wanaotumia vivinjari vya intaneti 25,000 tofauti tofauti toka katika nchi mbalimbali duniani.

Utafiti huu unaonesha kuwa Google na Facebook ndio tovuti zinazonekana kuwa na idadi kubwa ya watu wanaozitembelea,ambapo Google inaonekana kuwa na watumiaji wengi walioko Ulaya,Marekani ya Kaskazini na Oshenia,wakati Facebook inaonekana kutumiwa zaidi na watu waliko katika nchi za Mashariki ya Kati,Afrika ya Kaskazini na kwa watu wanaofahamu kuhispania walioko barani Amerika.

Hali ni ya kushangaza zaidi huko Asia kwani kumekuwa na ushindani mkubwa katika makampuni hayo ya kigeni toka Marekani kwani mtandao wa Baidu ambayo ni tovuti iliyo na umaarufu huko Uchina  katika kutafuta mambo mbalimbali kwenye intaneti katika nchi hiyo ambayo inaelezwa kuwa na idadi ya watumiaji wengi wa intaneti kuliko nchi zote duniani ikiwa na watumiaji wa intaneti wapatao nusu bilioni.Baidu pia inaonekana kutumiwa zaidi huko Korea ya Kusini.
Alexa haikuweza kutoa maelezo ya kina kuhusu watumiaji wa tovuti katika nchi zilizopo Kusini mwa Jangwa la Sahara.Japo kuna nchi zinazotumia intaneti zimeoneshwa. Kenya , Madagascar, Nigeria, na Afrika ya Kusini ziko katika utawala wa himaya ya  Google ambapo Ghana, Senegali na Sudan wanakadiriwa kuwa chini ya utawala wa Facebook.

Miongoni mwa nchi 50 zinaoneshwa na Facebook kuwa zinawatu wanaotumia tovuti hiyo ikifuatiwa na nchi 36 kati ya hizo zinatumia google na 14 zilizobakia zimeorodhesha kuwa zinatumia  YouTube ambayo inamilikiwa na Google.
Chanzo cha kilelezo:Creative Commons


Popular Posts

Labels