Friday, October 25, 2013

WAZIRI AITAKA SAMSUNG NA VODACOM TANZANIA KUWEKA VIZUIZI VYA TOVUTI ZISIZOFAA

Waziri wa Mawasiliano Sayansi na Teknolojia Tanzania Pro Makame Mbarawa ameitaka kampuni ya Simu ya SamSung na Vodacom kuhakikisha inazuia mifumo inayozuia kuonekana kwa tovuti zisizofaa katika mtandao wa intaneti ambao unaziunganisha shule za sekondari nchini Tanzania nchini ya mkongo wa taifa wa mawasiliano aliouzindua katika shule ya sekondari ya Kambangwa ilipo Kinondoni,Dar es salaam oktoba 22 mwaka huu.

"Nachukua fulsa hii kumwomba mwalimu Mkuu,Vodacom na Samsung kuhakikisha kuwa tovuti ambazo hazifai na zisizo na maslahi kwa watumiaji zinazuiwa kuonekanakwenye mfumo huo hilo halina mjadala"amesema waziri huyo

Amesema ni kosa kubwa kuingia katika mitandao ya ajabu na hivyo serikali ya Tanzania haitokubaliana na suala hilo na serikali iko tayali kushirikiana na walimu katika kuhakikisha suala hilo linazuiwa kwa kushirikiana na wataalamu wa wizara.

Kampuni ya Vodacom Tanzania kwa kushirikiana na kampuni ya Samsung  zimeungana katika kuunganisha shule za sekondari nchini Tanzania kupitia mkongo wa Taifa ambao utawezesha kupata mawasiliano ya intaneti kwa ajili ya kujifunza masuala mbalimbali ya kielimu ambayo baadhi yake hayawezi kupatikana darasani au kwenye vitabu na wameanza majaribio na shule ya sekondari ya Kambangwa .

Katika ufunguzi huo ambao ni sehemu ya mradi wa Tanzania ya Kesho Waziri Mbarawa aliwataka walimu na  wanafunzi wote kutumia maabara za komputa zitakazoweka katika kutumika kwenye utaratibu huo.




Popular Posts

Labels