Friday, October 11, 2013
TABITI ZAPUNGUZA SOKO LA KOMPYUTA
Kuna sababu nyingi za kushuka kwa kiwango cha uzalishwaji na utumiaji wa kopyuta za mezani,wengine wanatoa lawama kwa toleo jipya la Window 8,wengine wanatoa sababu za kushuka kwa soko kutokana na kudolola kwa uchumi duniani
Hata hivyo ukiangalia kiuhalisia waweza gundua kuwa kupungua kwa matumizi ya kompyuta za mezani kulianza katika robo ya pili ya mwaka 2010 na sababu kubwa inayoelezwa ni baada ya kuwa sokoni kwa kifaa cha mawasilino cha iPad .
Tovuti ya statista imeeleza kuwa toka kampuni ya Apple ilipoingiza sokoni tabiti kwa kutoa iPad ya kwanza Aprili 2010, usambazwaji wa kompyuta za mezani umeshuka PC ambapo sasa umeshuka na kufikia kiwango cha asilimia 8.6.
Apple ilifanikiwa kuuza iPad milioni 20 kwa mara ya kwanza ilipoingiza sokoni vifaa hivyo.
Mtandao wa Gartner umekadiria kuwa ukuaji wa usafirishaji wa tabiti duniani kote utakua kutoka tabiti milioni 76 kwa mwaka 2011 na itafikia mara tano zaidi ifikapo mwaka 2017
Katika robo ya tatu ya mwaka 2009, Toshiba ilisafirisha kompyuta za mezani milioni 4.01 duniani idadi ambayo ni sawa na ile ya robo ya kwanza ya mwaka 2013, Hewlett-Packard (HP) ndio iliyokuwa ikiongoza kwa kusafirisha idadi kubwa ambapo inakadiriwa kusafirisha komputa za mezani milioni 11.69 katika kipindi hicho cha mwaka.
Takwimu za awali zilionesha kuwa hadi kufikia robo ya nne ya mwaka 2012 inakadiriwa kuwa kompyuta zilizosafirishwa kwenda sehemu mbalimbali duniani toka kwa makampuni yanayozitengeneza zilikuwa milioni 90.
Tabiti zimewapa watumiaji wa kompyuta nafasi nyingine ya kuchagua njia mbadala ya matumizi sawa na yale wanayoweza kuyapata toka katika kompyuta hasa katika suala la matumizi binafsi na bei ya vifaa hivyo.