Wednesday, October 2, 2013

VIBER KUTOZA MALIPO YA HUDUMA ZA STIKA

 viber

Program tumishi ya viber ambayo iliahidi kutoa huduma ya ujumbe mfupi wa maneno na kupiga simu bure kupitia simu,tabiti na kompyuta,hatimaye septemba 30,2013 imetangaza hatua nyingine ya 
kibiashara.
 
Viber ambayo imekuwa na ushindani na program tumishi za mawasiliano za WhatsApp, MessageMe, na  Facebook, sasa imepanga kutumia huduma yake ya stika,alama za hisia zinazoambatana na maandishi kwa ajili ya kupata mapato.

Kampuni hiyo itakuwa ikitengeneza bidhaa za kulipia na kupata leseni kutoka katika vyanzo vingine ikiwemo vipindi vya televisheni,nembo za biashara,japo kuwa sio bidhaa zote za stika zilizopo sokoni zitalipiwa ingawa baadhi zitakuwa zikipatikana katika program tumishi za kulipia.

Viber ilianza huduma ya stika disemba 2012,na imekuwa ikitoa huduma hiyo bure kwa watumiaji wake na kutangazwa kwa huduma hii ya kulipitia kutaanza hivi karibuni japo haijaelezwa siku rasmi. 

 Kinachosubiriwa na ni kuona huduma hii ya soko la stika katika kampuni hii ambayo inawatumiaji zaidi ya milioni 200.

Popular Posts

Labels