Takwimu za wanunuzi kupitia mtandao kwa mwaka 2012 (Vipimo viko katika milioni) Chazo:eMarketer |
Kwa namna mabadiliko ya digitali yanavyoongezeka siku kwa siku ndivyo mabadiliko hayo yanavyowafanya watu wengi na wafabiashara duniani kufanya biashara kupitia mtandaoni.
Takwimu zinaonesha kuwa hadi kufikia juni 2012 watumiaji wa intaneti huko China walikuwa milioni 537.
Hali hii imesaidia sana kukua kwa soko la biashara mtandano nchini China ambalo linaelezwa kukua mara tatu zaidi ya soko la biashara mtandao lile la Marekani ifikapo mwaka 2015.
Takwimu za karibuni zilizotolewa na eMarketer zinaonesha kuwa watu wanaonunua bidhaa kupitia mtandaoni walikuwa ni milioni 219.8 kwa mwaka 2012, ambalo ni ongezeko la asilimia 23 toka mwaka 2011 wakati huko Marekani kulikuwa na wanunuzi kupitia mtandao wapatao milioni 150 kwa mwaka huo japo nchi hiyo inabakiwa kuongoza kuwa na soko kubwa la mauzo kupitia mtandao.
Inakadiliwa kuwa wanunuzi kupitia mtandao wapatao milioni 193 huko China wataongezeka na kufikia milioni 350 ifikapo mwaka 2015 ambapo watakuwa wametumia kiasi cha yuani trioni 2.6 na hii inaonekana biashara kupitia mtandao imekuwa ikiongeza mapato makubwa kwasasa.
Kampuni maarufu na iliyofanikiwa kwa biashara ya mtandao nchini China ni Alibaba.com