Tuesday, January 7, 2014

WATAALAM WA TEKNOHAMA KATIKA NGAZI YA DUNIA WAKUTANA KUJADILI MASWALA MBALIMBALI

Mkutano Mkuu uliowashirikisha wataalam wa sekta ya teknolojia ya habari na mawasiliano katika ngazi ya kidunia umemalizika salama na kuna mengi ambayo yamepata kujadiliwa kwa kina .
Kwa kifupi yaliyojiri katika mkutano huo ni pamoja na :-

1.Mapitio ya takwimu za makosa mtandao kwa kina katika mwaka huu. Mjadala ulibobea zaidi katika, nini hasa sababu ya makosa haya kuonekana kukua na nini kifanyike ili kupunguza kasi ya ukuwaji makosa haya.

2.Namna ya utumaji wa “Key” ambazo zimetumika kuficha maneno “Encryption Key” ili kuweza kuongeza wigo wa usiri katika taarifa zinazo safirishwa kupitia mitandao.
3.Hali halisi katika Teknologia mpya ya “CLOUD COMPUTING” na wasi wasi uliozuka juu ya usalama wa taarifa zinazopokea huduma kupitia teknologia hiyo. Pali jadiliwa kwa kina usahihi wa hilo na nini kifanyike
Bwana Yusuph Kileo akiwa na Steven “FOUNDER” NA “CEO” wa Cloud perspectives (Cloud computing) Nje ya Ukumbi wa mkutano mara baada ya kumaliza sehemu ya kwanza ya kikao hicho
5.Mjadala wa kina kuhusiana na “Social media” na jinsi inavyoweza kusaidia kuelimisha jamii na kuleta mabadiliko chanya. Pia Namna ya kusaidia kuboresha na kuhimiza matumizi bora ya mitandao hiyo ya kijamii “Control mechanism to social media”4.      Changamoto zilizopo katika ukusanyaji na uchunguzi salama wa vidhibiti vya makosa ya Digitali “Digital forensics collections and investigations”
6. Mjadala wa kina katika matumizi ya Open source security info management (OSSIM) ambapo inatoa msaada mkubwa katika ulinzi wa mtandao ambapo mjadala huu ulifunguliwa na mhakiki mkuu “Chief editor” wa kitabu maarufu kinacho tumika sana katika ulinzi mtandao kiitwacho “Cyber security standard”.

7. Mjadala Mwingine Kuhusiana na Teknolojia Mpya ya Miwani ambayo inauwezo wa kuchukua taarifa kwa njia ya sauti na video na kuzisafirisha taarifa hizo kwenda sehemu nyingine. Waliangalia jinsi gani wahalifu sasa wameanza kuitumia vibaya teknolojia hiyo na umakini unahitajika kiasi gani.
8. Mkuu wa MENA, alifafanua juu ya ukuaji wa teknolojia kwa sasa na kusisitiza mafunzo ya mara kwa mara ili kwenda sambamba na ukuaji wa teknolojia.
9.Umuhimu wa kuelimisha jamii kua swala la ulinzi mtandao si jukumu la kundi Fulani bali ni jukumu la kila mmoja ilitumika kauli “ inaanza na wewe mimi na wengine wote, kwa pamoja tutaweza kupunguza hali mbaya ya makosa mtandao”
 0.Aidha mjadala shirikishi kuhusiana na “Kifaa kipya kilichoko katika hatua za awali katika utafiti ambacho kitatumia teknologia kuweza kutoa tiba ya ugonjwa wa saratani “Cancer” ambacho kinategemea kupunguza madhara mengi yaliyopo kwa sasa ikiwemo kuondoa swala la mgojwa kunyolewa kipara.

Saturday, January 4, 2014

WAHALIFU WATUMIA VIRUSI VYA KOMPUTA KUIBA PESA KATIKA ATM


Woman at cash machine
USB stick
Virusi wa  malware waliwekwa kwenye ATM kwa kutumia flash za USB

Mwishoni mwa mwaka 2013 watafiti wamegundua namna wahalifu  kwa njia ya mtandao walivyotumia mbinu ya virusi vya komputa waitwao malware  na  kuzifanya pesa zitoke zenyewe katika mashine za ATM.


Taarifa ya watafiti hao iliyotolewa katika kongamano la wataalamu wa mifumo ya komputa lililofanyika  Disemba  28,2013 huko Hamburg,Ujerumani inaonesha kuwa wezi hao walifanya wizi huo katika banki ambazo hazikutajwa majina katika nchi za Ulaya mwanzoni mwa mwaka 2013 ambapo walikuwa wakitoboa matundu na kuweka flash USB zenye namba maalum( code) katika mashine hizo za banki za kutolea pesa.


Watafiti wawili ambao wamegundua mbinu zilizotumika kufanikisha uhalifu huo ambao wameomba kutotajwa majina yao wameeleza kuwa uhalifu huo unaonesha kuwa wezi hao hawakuwa wakiaminiana .


ATM hizo zilikuwa zikitumia Windows XP. Ambapo wamiliki wa banki waligundua kuwa wahalifu walikuwa wakituma virusi kwenye komputa na kuiharibu mifumo ya faragha na kusababisha kuingia katika komputa za benki mara kwa mara bila kugundulika.


Shirika la Utangazaji la BBC limeeleza kuwa wahalifu hao walikuwa walitumia namba maalum zenye tarakimu 12 ambazo ziliruhusu kiwango cha pesa kiweze kutoka kupitia ATM na taarifa za kibenki kurudi katika komputa ambapo ATM ilitoa mwongozo wa kile kilichotakiwa na wahalifu.


 Watafiti wamesema iwapo namba hizo hazikuwa zimeingizwa mara tatu, mashine ilirudi katika mwongozo wake wa kawaida  hii inaonesha kuwa kulikuwa na kutoaminiana miongoni mwa wahalifu hao.



HIZI NI BAADHI YA PROGRAM TUMISHI ZA KUZUIA WIZI WA SIMU ZA KISASA ZILIZOTENGENEZWA KWA MFUMO WA ANDROID





Unaweza kufanya vitu vingi vya maana kwa kutumia simu yako iliyotengenezwa kwa mfumo wa Android  mbali na kupiga,kupokea simu,huduma ya ujumbe mfupi wa simu na intaneti.


Mojawapo ya mambo ya kuvutia katika simu za Android ni kuitumia kuwa na mfumo wa mlio wa kuzuia wezi,kama ilivyo katika simu za iphone ambayo hutumia program tumishi ya Find My Iphone.


Kuna program tumishi nyingi ikiwemo ya Google iitwayo  Android Discovery Manager ambayo inafanya kazi kwa watumiaji wa simu walio na barua pepe za google ambayo huwezesha kufahamu eneo ilipo simu yako.


Pia kuna program tumishi ambayo huwezesha simu yako kutoa mlio iwapo mtu atahamisha simu yako mahali ilipo,nyingine ni ile inayopiga picha kwa camera ya mbele kwa mtu atakayejaribu kufungua simu yako kwa kuuingiza neno la siri la uongo.


Kuna program tumishi iitwayo Anti Theft Alarm inayopataika katika  Google Play Store ambao inazuia simu yako ya  Android katika aina mbalimbali za wizi.Program hii tumishi ya kuzuia uhalifu na inaelezwa kuwa ni miongoni mwa program tumishi bora za kuzuia wizi wa mitandao ambapo mtu anaweza kutumia kuzuia wizi wa komputa mpakato,nyaraka,barua pepe n.k ambapo nayo huwezesha simu kutoa mlio mtu anapoihamisha ilipowekwa.

Friday, January 3, 2014

JESHI LA POLISI TANZANIA LAANZA OPERASHENI DHIDI YA WANAOTUMIA VIBAYA MAWASILIANO YA SIMU NA INTANETI

Hatimaye, Jeshi la Polisi nchini, limeanzisha operesheni maalumu ya kuwabaini na kisha kuwachukulia hatua za kisheria wale wote wanaotumia vibaya mitandao ya kijamii kama vile Twitter, Facebook pamoja na laini za simu.

Jeshi la Polisi limeamua kuchukua hatua hiyo baada ya kuona teknolojia hizo zinatumiwa vibaya na watumiaji ikiwa ni pamoja na kuhamasisha vitendo vya uvunjifu wa amani ya nchi, kutishia usalama wa maisha ya watu na kutengeneza njama ovu za matukio ya kijambazi.

Baadhi ya hatua ambazo jeshi hilo limepanga kuwachukulia wote watakaobainika kutumia vibaya mitandao hiyo ni pamoja 
na kuwapeleka mahakamani.

Akizungumza na gazeti la NIPASHE jumahili, Mratibu Msaidizi wa Polisi kutoka Makao Makuu ya Jeshi hilo, Kitengo cha uhalifu wa mitandao,Joshua Mwasungasa, alisema operesheni hiyo ni endelevu kwa nchi nzima, lakini kwa sasa wameanza na Jiji la Dar es Salaam kuanzia mwezi disemba 2013 hadi Aprili,2014.

Alisema jeshi hilo linafanya operesheni hiyo kwa ushirikiano na kampuni mbalimbali za simu pamoja na Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA), na kwamba wote watakaobainika kutumia mitandao hiyo kwa matukio yoyote ya kiuhalifu, watachukuliwa hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kupelekwa mahakamani bila kujali hali au mahali alipo mtuhumiwa.

Kwa mujibu wa Mwasungasa, wanayo idadi ya watuhumiwa wanaotumia vibaya teknolojia hizo za mawasiliano, lakini alisema asingeweza kuiweka wazi ili isivuruge zoezi hilo ambalo wanaendelea nalo kwa sasa na kwamba wameamua kuanzisha operesheni hiyo mapema kwa ajili ya kuzuia athari kubwa ambayo ingeweza kujitokeza hapo baadaye baada ya kuonekana kwa dalili za vitisho vya uvunjifu wa amani kutokana na watu wanaotumia vibaya teknolojia hizo.

“Zoezi hili si la muda mfupi, ni la muda mrefu. Hatuwezi kusubiri mpaka uharibifu utokee ndipo tuanze. Tumeona vyema tuanze sasa kwani kuna ‘threats’ (vitisho) mbalimbali vinakuja kutokana na matumizi mabaya ya laini za simu na mitandao ya kijamii. Ni lazima tuwe na ‘Line Patrol’ kabla ya kitu kutokea na kuleta uvunjifu wa amani,” alisema na kuongeza:

“Kutumia laini za simu kwa mambo ya kiuchochezi ni kosa kisheria, na Sheria ipo ya EPCO inayosimamia matumizi ya mtandao hiyo. Kama mtu anatumia mtandao wa simu kwa kukashifu mtu ni kosa, na siyo simu tu bali hata mitandao ya kijamii.

Kutokana na hili, tumeanzisha operesheni maalumu inayoitwa ‘Line Patrol’ kwenye simu na mitandao ya kijamii na endapo tutakutana na kitu ambacho kinakiuka sheria ya matumizi ya mitandao hiyo, tutamchukulia hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kupelekwa mahakamani mhusika.”

Aliongeza kuwa mtu yeyote atakayetuma meseji za uchochezi kwa mwingine kupitia mitandao hiyo ya mawasiliano, atakuwa hatiani na yule atakayepokea na kurusha kwa mwingine bila kuifuta, naye pia atakuwa ameshiriki vitendo hivyo vya uhalifu kwani atakuwa ameingizwa na kuonekana kuwa ni mmiliki wa meseji hizo za kiuhalifu.

Alitaja baadhi ya matumizi mabaya ya mitandao hiyo kuwa ni pamoja na kuzungumza au kuandika ujumbe wa uchochezi, kukashfu, kutengeneza njama za matukio ya uhalifu na kuchochea uvunjifu wa amani.

Aliwaasa Watanzania kuwa makini na matumizi ya teknolojia hizo kwani kwa mujibu wa sheria zinazosimamia matumizi ya mitandao hiyo,mtu yeyote akipokea ujumbe wa uchochezi bila kuufuta na kuurusha kwa mwingine, tayari ameshashiriki kosa hilo.

Alisema baada ya kumalizika kwa awamu ya kwanza ya uchunguzi huo katika Jiji la Dar es Salaam ifikapo Aprili 2014, watafanya tathmini na kisha kuwachukulia hatua za kisheria wote watakaobainika, na kisha kuendelea na maeneo mengine.

Aliongeza kuwa katika zoezi hilo, pia wanalenga kutoa elimu kwa Watanzania na watumiaji ambao hawana uelewa wa kutosha kuhusu matumizi ya mitandao hiyo kwani wengi wameingizwa kwenye matukio ya uhalifu kwa sababu ya kutokuwa na elimu hiyo.
Kutolewa kwa taarifa hiyo ya Jeshi la Polisi, kunafuatia malalamiko mengi kutoka kwa watumiaji wa mitandao nchini kutokana na kukashfiwa, kutishiwa usalama wa maisha yao na kudhalilishwa.

Baadhi ya viongozi ambao kwa siku za hivi karibuni walipewa vitisho kupitia mitandao hiyo ni pamoja wabunge akiwamo Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema; Mbunge wa Viti Maalum, Esther Bulaya; Spika wa Bunge, Anne Makinda na Naibu wake, Job Ndugai. 

Saturday, December 28, 2013

NAMNA YA KUWEKA ULINZI WA KUKIFUATILIA KIFAA CHAKO CHA MAWASILIANO CHA APPLE KILICHOPOTEA

Umepoteza  iPhone ama kifaa chochote cha mawasiliano cha  Apple iOS? Kabla yakutoa taarifa kwa vyombo vya usalama ama kufanya lolote unapaswa ufuate hatua za kiulinzi ambazo zimewekwa na Apple ili kukusaidia kufahamu iPhone, iPad na iPod iliyopotea.

 iPhone 5S iliyotoka mwaka huu imetengenezwa mfumo wa kiusalama wa utambuzi wa alama za vidole,inahitaji kidole cha mmiliki kufungua simu,mfumo huu unasaidia kuzuia mwizi kuifungua simu ili kuitumia,simu hiyo pamoja na vifaa vingine vya mawasiliano vya Apple vinapopotea waweza kufahamu vilipo kwa kufuata hatua zifuatazo

Hatua # 1 – Seti na uactivate “Find My iPhone” katika kifaa chako

Hatua hii inahitajika uifanye mara unaponunua kifaa chako iwe ni Iphone,Ipad n.k.
Hakikisha umepada ID yako ya Apple ambayo inahusiana na kitambulisho cha kifaa ulichokinunua,ID ambayo pia itakusaidia wakati wa matumizi katika iCloud na upakuaji wa program tumishi toka Apple.
Nenda Settings ==> iCloud ==> angalia kama “Find My App” iko ON


iphone_find_my_iphone


 ipad_find_my_iphone

Utakapoweka ON “Find My iPhone” kama kifaa chako kitaibwa ama kupotea kitakusaidia kukutafuta na kufahamu kilipo .

Hatua #2 – Jiunge na  iCloud.com kwa kutumia  Apple ID yako

Unaweza kukitafuta na kukipata kifaa chako kilipo kwa kutumia iCloud.com iwapo utakuwa umefanya setting ya kwanza ya hatua ya kwanza kwa kufungua tovuti hiyo kwenye komputa yako na kuingia kwa kutumia Apple ID ile uliyosajili kifaa chako.Inakubali katika komputa za Window na Mac


 sign_in_icloud

Hatua   #3 –Fungua “Find My iPhone” na chagua palipoandikwa Device to Track

Bofya kwenye alama ya  “Find My iPhone” katika ukurasa wa  iCloud.com


 icloud_find_my_iphone

Hatua # 4 – Tafuta eneo kilipo kifaa chako. Kama ni eneo la karibu na ulipokipoteza ama ni ofisini,nyumbani n.k bofya palipoandikwa "play sound to find"

Chagua picha ya miongoni mwa kifaa kilichopotea Iphone,iPad n.k mahali palipoandikwa  “My Devices”. Baada ya kuchagua hapo, itaonekana ramani ya mahali kifaa kilipo ama muda wa mwisho kifaa hicho kilipokuwa.
icloud_select_device

Hatua # 5 – Ruhusu “Lost Mode”. Subiri mlio wa simu na endelea kuifuatilia ilipo

Baada ya kuchagua  “Find My iPhone”  program tumishi kwenye  iCloud itakuonesha mwongozo mwingine wa hatua zifuatazo,
# Play Sound – Hapa kifaa kitaanza kitatoa mlio na kama umepoteza nyumbani,ofisini n.k utausikia mlio
# Lost Mode –Kama unauhakika kuwa umeisahau simu yako ya iphone mahali utakaoruhusu hatua hii itumike itakuomba uweke namba ya simu ambapo watu watakupata,ama unaweza kuweka sentensi ama kuacha vivyo hivyo na kubofya "Done" na ujumbe utatokea kwenye simu yako iliyopotea hata kama umeifunga na utasomeka "Hii Iphone imepotea tafadhari nipigie "Namba yako"
# Erase iPhone – Hatua ya mwisho.Kwa kutumia iCloud na Find My iPhone unaweza kufuta ama kuondoa taarifa zako katika kifaa chako kilichoibwa ambapo utaondoa email zako,program tumishi ulizoweka n.k Kumbuka hatua hizi zote zinahitaji upatikanaji wa intaneti




TFF KUANZA KUTUMIA TEKETI ZA ELEKTRONIKI

 
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) litaanza kutumia tiketi za elektroniki kwenye uwanja wa Azam uliopo Chamazi,Dar es salaam wakati wa mechi za Ligi Kuu za Ashanti United na JKT Ruvu  zitakazopambana Januari Mosi 2014, kati moja ya mechi za kujaribio ya  matumizi ya mfumo huo nchini Tanzania.


Taarifa ya TFF kwa vyombo vya habari imeleza kuwa
Viingilio katika mechi hiyo itakayoanza saa 10 kamili jioni ni sh. 1,000 na sh. 2,000 ambapo tiketi zinapatikana kupitia M-Pesa na mawakala wa CRDB Fahari Huduma. Tiketi zitaendelea kuuzwa hadi kipindi cha kwanza cha mechi hiyo kitakapomalizika.


Mawakala 18 wa Fahari Huduma wanaouza tiketi hizo ni ABC Computer- Mtaa wa Samora, Abraham Anangisye Mwampetele- Maji Matitu, Apex Security Services- Mtaa wa Mibega, Kinyerezi, Athuman Fakhi Adam- Kongowe Mbagala, Fedha Investment Limited- Pamba Road na Fuya Godwin Kimbita- Tegeta Block.


Ghomme Health & Education Limited-Bahari Beach, Herman Arbogast Tarimo- Kigamboni, K- Finance Limited- Shekilango, Sinza, Koli Finance Limited- Mtaa wa Samora, LB Pharmacy- Mtoni Kijichi, Lista Phares Barnabas- Tabata Segerea na Maly Investment Company Limited- Mtaa wa Sikukuu, Kariakoo.


Wengine ni Micu Enterprises- Mtaa wa Congo, Kariakoo, S&D Collection Company Limited- Mikocheni, Shoppers Plaza, Therry Investment Limited- Tegeta Kibaoni, TSHS Distributors Limited- Mtoni kwa Aziz Ali na Wemerick Independent Vehicle- Mtaa wa Boko.


Pia mshabiki anaweza kununua tiketi kwa njia ya simu- mtandao wa Vodacom kwa kupiga *150*03*02# ambapo atapata namba atakayoitumia kufanya malipo kupitia MPESA. Katika MPESA namba ya malipo kwa TFF ambayo ndiyo mshabiki ataitumia kufanya malipo ya tiketi (business number) ni 888800. Vilevile mteja wa CRDB aliye katika mtandao anaweza kufanya malipo kupitia CRDB simbanking.


Baada ya kufanya maombi kupitia njia yoyote ya hizo tatu; MPESA, Fahari Huduma na CRDB simbanking, mshabiki atapata namba ambayo ataitumia ku-print tiketi yake kupitia mashine maalumu za kuchapia Tiketi ya TFF zilizo katika ATM za CRDB kwenye maeneo yafuatayo;


Benki ya CRDB tawi la Azikiwe, tawi la Holland House ambapo kuna mashine mbili, tawi la Vijana, tawi la Kariakoo, ATM ya Mtaa wa Shaurimoyo ambapo kuna mashine mbili na ATM ya CRDB iliyoko kituo cha mafuta cha Kobil Sabasaba, Mtoni kwa Aziz Ali.

HACKER NI NINI?

 
KAMA HAUKUJUA BASI JUA
Na MBUKE TIMES
Neno HACKER makusudio yake haswa sio kumaanisha mtu anayefanya vitendo vya kihalifu kwa kutumia kompyuta, yaani kama vile kuiba password za watu, kusoma emails za watu n.k. Bali neno HACKER kiasili lina maana ya mtu mwenye uwezo wa kipekee wa kutafuta suluhu ya tatizo kwa haraka, kwa mbinu za ubunifu ambazo pengine si mbinu rasmi, ila zinaleta suluhu ya haraka.

--Hata hivyo kwakuwa HACKER ana ujuzi wa hali ya juu wa matumizi ya kompyuta na ni mtundu, basi wapo Hackers walioamua kutumia ujuzi huo kufanya uhalifu, na ndipo jina lilipoharibika.

--Hata hivyo jamii ya hackers na wanateknolojia wengi wameendelea kuelimisha matumizi sahihi ya jina HACKER na neno HACKING. Mifano ya wazi ni :-
1. Facebook: Kuta za ofisi za FB zimeandikwa neno HACK. Kusisitiza umuhimu wa kuandika codes kwa haraka na kutafuta kwa ubunifu na kwa haraka suluhu ya matatizo.
Hata mfumo mzima wa uendeshaji wa FB umepewa jina THE HACKER WAY.

2. Makampuni mengi yamekuwa yakiandaa mikutano ya siku moja au zaidi kwa ajili ya kukutanisha HACKERS ili kubuni bidhaa na kutatua matatizo mbalimbali. Mikutano hiyo huitwa HACKATHONS
-- Kwa maelezo zaidi search Google maneno HACKER, FACEBOOK THE HACK WAY na HACKATHONS.

UTAFITI:FACEBOOK YAKIMBIWA NA VIJANA HUKO UINGEREZA




Utafiti unaonesha kuwa Vijana kati ya miaka 16-18 nchini Uingereza wanaonekana kutovutiwa na mtandao wa kijamii wa facebook  kutokana na kukerwa na mtandao huo. 

Tovuti ya yahoo imesema kuwa Vijana hao sasa wameonekana kuvutiwa  Zaidi na mitadao ya kijamii mingine ambayo ni  Twitter, Instagram, Snapchat  na WhatsApp.

Profesa Daniel Miller kutoka Chuo Kikuu cha London ambaye alisaidia kufanya utafiti kuhusu jambo hilo amesema wakati ambapo wazazi wamekuwa na wasiwasi kuhusu watoto wao kujiunga na face book lakini watoto wanaeleza kuwa ni familia zao ndizo zinazosisitiza wawepo kwenye mtandao huo kwa ajili ya mawasiliano.

Utafiti huo ulifadhiliwa na umoja wa ulaya na kuwahusisha vijana wenye umri wa miaka 16-18 umeonesha kuwa mitandao mingine ya kijamii na program tumishi zinaonekana si bora katika miongozo ya namna ya  kuitumika  kuliko facebook.

Utafiti huo unaonesha kuwa Facebook inawaunganisha watumiaji vyema,inatoa mpangilio mzuri wa picha na mpangilio wa mahusiano miongoni mwa watumiaji.

 WhatsApp inaonekana ni bora kwa ujumbe wa maandishi ambapo kwa sasa inaonekana kuipiku facebook na kutokana na kuonekana bora katika huduma ya ujumbe mfupi wa maneno . 

Miongoni mwa vijana wengi nchini Uingereza  sasa wanatumia  Snapchat,ambao hukuwezesha kutuma picha ambazo huondoshwa sekunde chache baada ya kuzituma.

Kumekuwa na lawama kuhusu faragha katika mtandao wa facebook hasa baada ya mwaka huu kuelezwa kuwa Wakala wa Ulinzi wa Marekani (NSA) imekuwa ikifanya  udukuzi wa taarifa zilizoko katika mtandao huo.

Utafiti huo pia unaonesha kuwa vijana hao sasa wanajiunga na Instagram mtandao unaotoa huduma ya kubadilisha picha,Mike Butcher kutoka Techcrunch.com ameiambia Sky News kuwa Facebook ilikuwa mahali tulivu na faradha hasa kwa wanafunzi wa vyuo vikuu na wahitimu kwa ajili ya kutengeneza kipato na imekuwa maarufu.
Anaeleza kinachotokea sasa ni vijana kutafuta mitandao mbadala ambayo ni  Instagram na Twitter.

Monday, December 16, 2013

TANZANIA IMEJIPANGAJE KATIKA KUKABILIANA NA UDUKUZI?

UDUKUZI NI NINI ?

Ni uchukuaji wa taarifa za mwingine kwa njia ambazo sio halali kwa kutumia vyombo vya mawasiliano anavyotumia mtu husika kama email , simu , kompyuta , tv na vingine vingi .

Taarifa hizi zinaweza kuwa kwa njia ya nyaraka zilizohifadhiwa , zinazofanyiwa kazi ( kama ziko shared ) , kusikiliza mawasiliano ya sauti kama kupiga au kupokea simu , ujumbe mfupi yaani sms na Mawasiliano ya email mtu anayofanya na watu wake au makundi .

Katika siku za karibuni wigo umepanuka kidogo sasa hivi mpaka kwenye anuani za watu kwenye mitandao ya kijamii kama facebook watu wanaouwezo wa kuiba taarifa au kuingia na kupotosha , kwenye majukwaa ya majadiliano pia watu wanaweza kuingia kuvuruga au kuiba taarifa za mtumiaji fulani bila wenye jukwaa kujua .

Kwa mataifa yaliyoendelea Aina hii ya Ujasusi ni njia moja wapo ya kujilinda dhidi ya adui wa nje na wa ndani , adui huyo anaweza kuwa gaidi , jasusi mwenzake , biashara za kimataifa , teknolojia , uuzaji na usambazi wa silaha , taarifa za afya , viwanda na nyingine nyingi .

MATUKIO MAARUFU YA UDUKUZI KIMATAIFA
1 – Miezi kadhaa iliyopita tumesikia na kusoma kwenye vyombo vya habari kuhusu Udukuzi uliokuwa unafanywa dhidi ya viongozi mbalimbali wa nchi za ulaya na amerika ya kusini na mashirika ya ujasusi ya kimarekani .

2 – siku kadhaa kabla ya mkutano wa G20 NA hata wakati mkutano huo unaendelea baadhi ya wajumbe walipokea barua pepe ambazo zilikuwa na program maalumu zilizojiingiza kwenye kompyuta zao na hapo hapo walianza kufuatiliwa na kuibiwa taarifa zao haswa kile walichokuwa wanafanya na kuandika kutumia kompyuta zao na simu , uchunguzi ulipofanyika iligundulika uvamizi huu ulitokea uchina .

3 – wajumbe wa mpango wa nyuklia wa irani walipoenda uingereza kwa ajili ya mkutano Fulani nao waliingiziwa virusi walipowasha tu vifaa vyao vya mawasiliano , virusi hivi vilisambaa mpaka kwao mpaka kwenye vinu vyao vya nyuklia matokeo yake ni kwa baadhi ya vitu kutokufanya kazi sawasawa .
Hili suala kwa Irani pamoja na vikwazo ndio limesababisha uongozi mpya kutaka muafaka na mataifa yaliyoendelea , pia lilisababisha baadhi ya wanasayansi wao kuuwawa kwa njia za kigaidi haswa wale waliokuwepo kwenye mradi huu .

MATUKIO MAARUFU YA UDUKUZI NCHINI
Kwa hapa nchini kuna matukio 3 ambayo ni maarufu lakini hayajawahi kuongelewa sana .
1 – Waziri mmoja na kundi lake walikuwa wanaenda nchi Fulani ya ulaya kwa ajili ya warsha na alitarajiwa kutoa msimamo Fulani , basi alivyofika hotelini kuwasha kompyuta yake kuanza kupekua vitu hapo maharamia wa mtandao walimvamia na kuharibu hiyo kitu aliyokuwa anafanyia kazi siku zote .

2 – Mara kadhaa kumewahi kutokea udukuzi kwenye taasisi zetu zinazosimamia maswala ya mawasiliano haswa TCRA na ilipochunguzwa ikagundulika waingiliaji wengi walitokea nchi ya China , china imekuwa nchi inayongaa ulimwenguni kwenye masuala ya Udukuzi .
3 – Udukuzi uliwahi kufanywa dhidi ya shirika moja la ndege nchini halafu wahalifu wakavamia kwa nia ya kuharibu utaratibu wa urushaji ndege na uhifadhi mwingine wa taarifa , hii ilisababisha ndege moja kukaa uwanjani bila kufanya safari kwa mwezi mmoja kwa sababu za kiusalama na ndege hiyo ilikuwa inaendeshwa na mitambo maalumu kutoka nchi nyingine .

HALI YA TANZANIA
Hali ya Tanzania kusema za ukweli sio ya kuridhisha sana kutokana na mambo 3 makuu .
1 – Sheria za Mawasiliano – Sheria zetu za mawasiliano hazijitoshelezi na wahalifu wengi wanatumia fursa hiyo kufanya uhalifu wao kutoka hapa kupiga wengine au kupitia hapa kupiga wengine wa mbali , tunapenda kuwa na sheria nzuri za mawasiliano zinazoendana na wakati wa sasa na kila idara serikalini itengeneze sheria zake kwa kunukuu sheria mama .

2 – Utumiaji wa Vifaa chakavu – Tunaona watu haswa wenye fedha zao wakinunua vifaa chakavu vya mawasiliano haswa toka nchi za mbali kwa ajili ya kuja kutumia hapa nchini vifaa hivi vingi vimesababisha utengenezwaji wa njia za kivamizi na kwa sababu teknologia zake za kizamani imekuwa rahisi wa wahalifu kuzichezea na kufanya wanachojua .
3 – Vifaa visivyokidhi viwango – Tumeona watu wananunua simu ambazo hazina viwango na kuzitumia kwenye shuguli za uhalifu , simu nyingine zinapunguzwa baadhi ya vitu ili ziweze kufanya kazi nchini , watu maofisini wanaingiza programu kwenye kompyuta zao ambazo hazina leseni au leseni bandia yote hii haitakiwi .

4 – Kutokufuata taratibu za manunuzi – Hapo juu nimesema hatuna sheria za mawsiliano na tumezoea kununua vifaa chakavu , tukiwa na hivyo viwili tutaweza kuwa na utaratibu mzuri wa kununua vifaa haswa vya mawasiliano maofisini na kwenye idara za serikali utakaofuata vitu hivyo viwili .

NINI KIFANYIKE
Ni wakati mzuri sasa kwa Taasisi muhimu nchini kama Mabenki , Polisi , Tume ya mawasiliano , Kampuni za Mawasiliano ya Simu na Intaneti , taasisi za elimu kama vyuo na shule kuwa na taratibu za kufundisha watu matumizi salama ya vifaa vya mawasiliano , ununuzi mzuri wa vifaa vya mawasiliano na uuzaji mzuri wa vifaa vya mawasiliano .

Tufanye hivi huku tukingoja sheria mama wa mawasiliano iboreshwe na wengi wataboresha masomo yao kuzingatia sheria mama ya mawasiliano nchini kulingana na hali tuliyonayo .

Ningependa kuona sheria mama ikiandikwa kutokana na mila na tamaduni za mtanzania sio nje ya hapo , hata pale mtu akisoma itoe harufu ya utanzania au uafrika mashariki .

Kupambana na udukuzi wote sio rahisi lakini tunaweza kupunguza uwezo wa kufanyiwa udukuzi kwa kuhakikisha tuna vifaa vizuri vya mawasiliano na kufuata taratibu za utumiaji .
YONA FARES MARO
0786 806028

Saturday, December 14, 2013

MUONGOZO WA KUTENGENEZA TOVUTI HUU HAPA

 

Kitabu hiki kipo tayari. Wasiliana kwa namba 0713 309 314 au 0763 309 314 na Mushi Richard, Mpesa: 0755872462, Tigopesa: 0713643703 lipia kitabu chako mtumie email yako kisha akihakiki hela imeingia anakutumia kitabu kilicho katika mfumo wa Soft Copy. Ni TSHS. ELFU KUMI NA MBILI TUU (12,000/=). Hata kama upo mkoani.

MICROSOFT KUWASAIDIA WANAFUNZI WA VYUO KUPITIA STUDENT ADVANTAGE




Kampuni ya Microsft Corporation imeanzisha programu mpya ambayo itawawezesha wanafunzi kufanya mazoezi yote wanayopewa shuleni kupitia teknolojia ya habari na mawasiliano.

Kampuni hiyo imebuni programu mpya ya Student Advantage ambayo itawawezesha wanafunzi kupeana kazi za shule,mazoezi ya nyumbani na masuala yote muhimu ya kitaaluma.

Mpango huo uliotangazwa hivi karibuni wakati kampuni hiyo ikitambulisha programu ya Microsoft Office 365 Education ambayo inakadiriwa kutumiwa na zaidi ya wanafunzi milioni 110 wa vyuo 35,000,idara na wahadhiri mbalimbali duniani.

Programu hiyo itawapa fursa wanafunzi kuitumia kupitia huduma zilizopo ambazo ni Microsoft Word na OneNote ambazo zinafanana na huduma za PowerPoint na Excel.

Mpango huo umeanza rasmi Desemba Mosi mwaka huu,huku vyuo mbalimbali duniani vikipewa leseni ya Office 365 ProPlus kwa wanafunzi wahadhiri pamoja na wakuu wa idara watakuwa wanatumia programu yenye leseni ya Office Proffesional Plus bila gharama zozote.Huduma hizo zote zitawapa wanafunzi nafasi wanafunzi kupata maarifa mbalimbali kupitia mtandao wakiwa nyumbani na huduma nyingine ambazo zipo kwenye programu hiyo yenye vitu vingine vitakavyomwezesha mwanafunzi kuwasiliana na wanafunzi wengine waliopo katika vyuo mbalimbali duniani.

Mkuu wa Kampuni hiyo katika nchi za Afrika Mashariki na Kati Mark Chaban anasema wamefanikiwa kutembelea vyuo 30 binafsi na vya umma pamoja na Wizara mbalimbali za elimu ili kutoa mafunzo kuhusu utumiaji wa programu hiyo ambayo ipo chini ya International Data Corporation (IDC) ambayo itakuwa ikikusanya taarifa za maendeleo ya wanafunzi watakaokuwa wakitumia ili waweze kupata ajira na kuboresha maisha yao.

Kampuni hiyo imesema inakusudia kufuatilia uwezo wa wanafunzi katika kutumia huduma hiyo ambapo watakaoonekana kuwa na kiwango cha juu watachukuliwa na kupelekwa kwenye makampuni mbalimbali na kulipwa mishahara minono.

Microsoft imepanga kutengeneza ajira kwa asilimia 28 ifikapo mwaka 2020 ambapo miongoni mwa wanafunzi milioni 115 watakaoajiriwa kwa vigezo vilivyowekwa .

Popular Posts

Labels