Huu ni mfululizo wa vipindi vya Serikali Mtandao hapa utaona kwa namna gani TANAPA inavyotumia TEHAMA katika utoaji huduma kwa umma.
Monday, March 20, 2017
Tuesday, March 14, 2017
SERIKALI YA TANZANIA YASISITIZA MATUMIZI YA MITANDAO YA KIJAMII KWA OFISI ZAKE ZA UMMA
Serikali yasisitiza matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano hasa Mitando ya Kijamii katika ofisi mbalimbali za Umma nchini Tanzania katika kutoa habari na taarifa mbalimbali.
Thursday, December 15, 2016
YAHOO YASEMA WATUMIAJI BILIONI 1 WA MTANDAO HUO WAMEATHIRIWA NA WAVAMIZI WA MITANDAO
Kampuni ya Intaneti ya Yahoo inasema wavamizi wa mitandao waliiba data za zaidi ya ya watumiaji wake bilioni moja. Tukio hilo linaaminika kufanyika mnano mwaka 2013.
Katika taarifa yake, Yahoo inasema uvamizi huo wa taarifa muhimu ni
tofauti na ule ulioripotiwa mwezi Septemba mwaka huu, ambapo wavamizi
hao waliiba taarifa kutoka kwenye akaunti mbalimbali za watumiaji zaidi
ya milioni mia tano.
Imeongeza kuwa data zilizoibiwa zinajumuisha majina, anuani, namba za simu,tarehe za kuzaliwa pamoja na nywila (namba za siri).
Lakini kadi za malipo sambamba na akaunti za benki hazikuingiliwa.
Wednesday, December 14, 2016
KAGOYA YASHAMBULIWA KIMTANDAO – TANZANIA NAYO YAASWA KUFUNGA MIKANDA
Kampuni
Maarufu ya KAGOYA ya Nchini Japan Imeshambuliwa kimtandao ambapo taarifa
binafsi na za kibenki za wateja wake zimedukuliwa.
Uhalifu
huu umegundulika mwezi huu (Desemba, 2016) na tayari kampuni husika imesha toa
taarifa kwenye vyombo vya usalama vya Nchini humo - Ambavyo pia vimeanza
uchunguzi rasmi.
Kampuni
hiyo imesema, Wateja wake waliotumia "Credit card " zao baina ya Aprili
Mosi , 2015 hadi september 21, 2016 wameathiriwa na uhalifu huu na imewaasa
wateja wake wafatilie taarifa za utoaji pesa wa kadi zao.
Mjumuiko wa taarifa zilizo ibiwa ni, majina , barua pepe, Namba za simu, Namba za kadi za benki, maneno ya siri (Nywila) pamoja na taarifa nyingine za wateja wake.
Hii
si mara ya kwanza kwa Nchi ya JAPANI kupata shambulio kubwa la kimtandao kwa
mwaka huu (2016) pekee - Itakumbukwa, Mwezi May mwaka huu (2016) zaidi ya Yuan
Bil. 1.5 sawa na Dola Milioni 13 ziliibiwa katika ATM zaidi ya 1400 ndani ya
masaa mawili na nusu.
Aidha,
TANZANIA hali ya uhalifu mtandao bado ni changamoto inayo hitaji suluhu ya
kudumu. Kuibiwa kwa Fedha na Taarifa , Matumizi mabaya ya mitandao, Tovuti
kudukuliwa ni miongoni mwa matukio yaliyo jitokeza kwa mwaka huu 2016.
Akizungumza
wakati wa uzinduzi Bodi ya TCRA (Mamlaka ya Mawasiliani Tanzania) Mheshimiwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa ameitaka Bodi mpya ya TCRA, kuhakikisha
wanapata mwarobaini wa kudhibiti ongezeko la wizi wa mitandao unaoendelea
kukithiri hapa nchini.
Prof.
Mbarawa amesema watanzania wameibiwa kwa muda mrefu kupitia njia ya ujumbe
mfupi na kushawishiwa kutoa fedha kwa njia ya udanganyifu na hivyo kuitaka bodi
hiyo kutofumbia macho changamoto hiyo.
“Changamoto
ya wizi wa mitandao inagusa watanzania wengi, mkiwa na jukumu la kudhibiti mna
wajibu wa kuwalinda wananchi”, amesema Waziri Prof. Mbarawa.
Ameongeza
kuwa bodi hiyo ihakikishe inasimamia kwa karibu sheria, kanuni na taratibu
zilizowekwa katika kudhibiti ubora wa masuala ya mawasiliano ikiwa ni
teknolojia inayokuwa kwa kasi kubwa.
Aidha
Prof. Mbarawa ameitaka bodi hiyo kuendelea kudhibiti wimbi la meseji za
uchozezi zinazotumwa na baadhi ya wananchi kwa kukosa maadili.
Katika
kuimarisha huduma ya teknolojia ya habari na mawasiliano nchini Waziri Prof.
Mbarawa ameikata TCRA kufanya maamuzi ya haraka na kuwa wabunifu ili kuweka
mazingira endelevu ya kukuza sekta hiyo.
Aidha,
Mwenyekiti wa Bodi mpya ya TCRA Dkt. Jones Kilimbe amesema kuwa pamoja na
changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta hiyo, Bodi itahakikisha inapata
suluhu ya changamoto hizo ndani ya muda mfupi.
Hatuna
Budi kutambua kua janga la uhalifu mtandao ni kubwa na athari zake zimekua
zikionekana situ kwa nchi zisizo na teknolojia nzuri ya kukabiliana na uhalifu
mtao bali pia Nchi zilizo endelea zimekua wahanga wa janga hili.
Taifa
la Tanzania halina budi bali kuanza na utayari uliombatana na kujipanga upya na
vizuri kukabiliana na Wimbi la uhalifu mtandao nchini.
Changamoto
za urasimu, matumizi makubwa ya pesa kwenye kampeni za kukuza uelewa zinazokosa
matokeo chanya pamoja na kutojiongezea elimu ya mara kwa mara ya kukabiliana na
uhalifu huu mtandao lazima ipaiwe suluhu.
Sheria
Mtandao pekee haziwezi kutuvusha kwenye wimbi hili la ukuaji wa uhalifu mtandao
nchini, Lazima mambo mengine muhimu ya kukabiliana na uhalifu mtandao yafanyiwe
kazi.
Naziasa
taasisi binasfi na za serikali kujenga tabia ya kutoa taarifa ya matukio ya
kishambulizi mtandao mara tu yanapo gundulika ili iwe rahisi kupatiwa suluhu.
Bila kufanya hivyo wahalifu mtandao wataendelea kupata nguvu.
Kwa
sasa Tanzania, Hatujafikia pabaya sana kulinganisha na mataifa mengine – Ila,
Kama hatua za haraka na za dhati za kujipanga na kufunga mikanda
hazitachukuliwa mapema, Mbele yetu ni mbaya Mno.
Na:Yusuph Kileo
Tuesday, December 6, 2016
TUZO ZA UMAHILI KWA WAANDISHI WA BLOG ZAJA
Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na wamiliki wa blog nchini humo inatarajia kuanzisha tuzo za umahiri kwa waandishi wa habari wa mitandao ya kijamii (blogs) nchini kuanzia mwaka 2017.
Katika hotuba yake ya kufunga Mkutano Mkuu na semina ya wanachama wa umoja wa waendeshaji wa
blog nchini jijini Dar es salaam leo Waziri wa Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo, Nape Nnauye (Pichani)amesema kuwa lengo la tuzo hizo ni kuzisaidia blogs za Tanzania kubobea
katika nyanja tofauti ikiwemo kilimo, mifugo, viwanda, hifadhi ya jamii
kwa nia ya kuipa heshima tasnia ya habari nchini.
Waziri Nape alisema kuwa tayari Serikali imeanza mazungumzo na
makampuni na taasisi mbalimbali kwa ajili ya kudhamini tuzo hizo ili
kuhakikisha kuwa washindi wanapatikana kwa uwazi.
Waziri Nape pia amewataka wamiliki na watendaji wa blogs nchini kushirikiana na Serikali ili kuweza kuijenga nchi.
Monday, December 5, 2016
SERIKALI YAITAMBUA RASMI MITANDAO YA KIJAMII (BLOG)
Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji wa Serikali Dk. Hassan Abbas (kulia), akihutubia wakati wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Tanzania Bloggers Network (TBN), Dar es Salaam leo asubuhi. Kushoto ni Mwenyekiti wa muda wa TBN, Joachim Mushi.
Mwanahabari na Blogger Frederick Katulanda (kulia), akiuliza swali.
Mwenyekiti wa muda wa TBN, Joachim Mushi (kushoto), akiwaelekeza jambo mablogger
Mkutano ukiendelea.
Mablogger kazini
Blogger Baraka kutoka Bukoba akiuliza swali.
Mwezeshaji wa mkutano huo Maxsence Mello akitoa mada.
Bloggers wakifuatilia mada.
Mwendeshaji wa mtandao wa FullShangwe, John Bukuku akichangia jambo kwenye mkutano huo.
Maofisa wa Kitengo cha Uhusiano wa Benki ya NMB wakibadilishana mawazo. Kushoto ni Doris na Joyce Nsekela.
Blogger kutoka mkoani Arusha, Tumaniel Seria (kulia), akiuliza swali. Kusho ni William Malecela mmiliki wa mtandao wa Mwananchi na katikati ni mmiliki wa Blog ya Michuzi Issa Michuzi.
Mmiliki wa mtandao wa Kamanda wa Matukio, Richard Mwaikenda akichangia jambo.
Picha ya pamoja na mgeni rasmi.
Serikali imetangaza rasmi kuitambua mitandao ya Kijamii (Bloggers) kuwa chombo cha habari nchini.
Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji wa Serikali Dk.Hassan Abbas Dar es Salaam leo wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Tanzania Bloggers Network (TBN).
"Serikali sasa inaitambua rasmi mitandao ya kijamii kuwa ni chombo cha habari kama ilivyo vyombo vingine nchini hivyo nawaomba wakuu wa vitengo vya habari serikalini kushirikiana na wanamitandao hiyo katika kutoa taarifa mbalimbali" alisema Abbas.
Abbas alivitaka vyombo vya habari hasa magazeti pale wanapotumia picha kutoka mitandao ya kijamii kueleza chanzo cha picha hiyo tofauti na ilivyo hivi sasa ambapo picha zao zinatumika bila ya kutaja chanzo.
Katika hatua nyingine Abbas alisema Bloggers haina tofauti na vyombo vingine hivyo ni vema wanapotoa habari zao kuzingatia sheria na weredi wa kazi vinginevyo sheria itawakumba kama ilivyo kwa magazeti na vyombo vingine.
Abass aliwataka wanamitandao hao kujiunga na TBN ili iwe rahisi kutatuliwa changamoto walizonazo kuliko kila mmoja kuwa kivyake.
Wanamitandao hao wakizungumzia changamoto waliyonayo walimwambia mkurugenzi huyo kuwa wamekuwa wakibaguliwa na maofisa habari wa serikalini ikiwa pamoja na kunyimwa 'Press Card' jambo linalokwamisha utendaji wao wa kazi.
Picha na Habari:Dotto Mwaibale
Sunday, December 4, 2016
YUSUPH KILEO MTANZANIA ALIYETWAA TUZO YA MWAKA YA USALAMA MTANDAONI
![]() |
| Yusuph Kileo baada ya kukabidhiwa tuzo |
Mtaalamu wa masuala ya usalama mtandaoni Yusuph Kileo hivi karibuni alipata Tunzo ya "Cybersecurity expert of the year" Ikiwa ni katika kutambua mchango wake katika mataifa ya Afrika.
Tuzo hizo zilitolewa Nairobi nchini Kenya ambapo Mgeni rasmi alikua ni PS au KM wa wizara ya mipango na Majimbo (Ugatuzi) - Kenya Mheshimiwa Saitoti Torome.Kwa ujumla zilitolewa tunzo 31 katika makundi tofauti.
CHAMA CHA WAMILIKI NA WAENDESHA MITANDAO YA KIJAMII KUFANYA MKUTANO WAKE MKUU
-->
Chama cha
Wamiliki/Waendeshaji wa Mitandao ya Kijamii nchini 'Tanzania Bloggers Network' (TBN) kitafanya mkutano wake kwa siku mbili kuanzia kesho jijini Dar es salaam ukiwahusisha wanachana wake toka mikoa mbalimbali nchini.
Akitoa taarifa ya mkutano huo iliyoambatana na upokeaji wa hundi ya shilingi milioni 10 toka NMB Mwenyekiti wa muda wa TBN Joachim Mushi amesema lengo la mkutano huo ni wanatasnia kupewa semina juu ya uendeshaji mitandao ya jamii kwa manufaa, upashaji habari kwa kutumia mitandao yao kwa kuziangatia maadili na namna ya kunufaika na mitandao hiyo kwa waendeshaji (kujipatia kipato) hasa ukizingatia kuwa wapo baadhi yetu tunaifanya kama ajira nyingine.
-->
![]() |
| Mwenyekiti wa muda wa Chama cha Wamiliki wa Blog (TBN),Joachim Mushi akizungumza na waandishi wa habari |
Akitoa taarifa ya mkutano huo iliyoambatana na upokeaji wa hundi ya shilingi milioni 10 toka NMB Mwenyekiti wa muda wa TBN Joachim Mushi amesema lengo la mkutano huo ni wanatasnia kupewa semina juu ya uendeshaji mitandao ya jamii kwa manufaa, upashaji habari kwa kutumia mitandao yao kwa kuziangatia maadili na namna ya kunufaika na mitandao hiyo kwa waendeshaji (kujipatia kipato) hasa ukizingatia kuwa wapo baadhi yetu tunaifanya kama ajira nyingine.
-->
Thursday, November 3, 2016
TTCL NA HUAWEI WAZINDUA MTANDAO WA 4.5 G
Kampuni ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano ya Huawei Tanzania na Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) zimeungana na kuzindua mtandao wa 4.5 utakaokuwa wa kwanza kwa mitandao yote nchini Tanzania.
Mkurugenzi Mtendaji wa Huawei Tanzania Bruce Zhang amesema uzinduzi huo unadhihirisha mafanikio ya TTCL kwenye safari ya mabadiliko ya kukua kibiashara nchini.
Hivi karibuni serikali ya Tanzania ilitangaza kumiliki hisa zote za TTCL baada ya kuchukua asilimia 35 zilizokuwa zinamilikiwa na Kampuni ya Bhart Aitel.
DAR ES SALAAM:RAIA WATATU WA PAKSTANI WAHUKUMIWA KWA KOSA LA KUMILIKI MITAMBO YA MAWASILIANO BILA LESENI
Raia watatu kutoka Pakstani wamehukumiwa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kulipa faini ya shilingi milioni 120 na iwapo watashindwa watatumikia kifungo cha mwaka mmoja jela kutokana na kosa la kula njama,kuingiza nchi Tanzania vifaa vya kielektroniki vya mawasiliano bila kuwa na leseni ya TCRA,kuvisimika,kuendesha huduma za mawasiliano ya simu za kimataifa bila kibali kutoka TCRA,kukwepa malipo na kusababishia serikali na mamlaka hiyo hasara ya shilingi milioni 140,049,000.
Raia hao wa Pakstani ni Hafeez Irfan (32),Mirza Baig (41) na Irfan Baig (46) na wakidaiwa kutenda makosa hayo katika Hoteli ya Butterfly iliyoko Kariakoo,Wilaya ya Ilala katika chumba namba 905.
Raia hao wa Pakstani ni Hafeez Irfan (32),Mirza Baig (41) na Irfan Baig (46) na wakidaiwa kutenda makosa hayo katika Hoteli ya Butterfly iliyoko Kariakoo,Wilaya ya Ilala katika chumba namba 905.
Wednesday, October 26, 2016
WATEJA WA TIGO PESA KUVUNA BILIONI 6.04 GAWIO LA KUMI LA ROBO MWAKA
Mkuu wa Huduma za Fedha kwa njia ya simu wa Tigo Ruan Swanepoel (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam kuhusu, Wateja Tigo Pesa kuvuna 6.04bn/- (dola 2,763,636) gawio la kumi la robo mwaka. Kulia ni Meneja Masoko na Usambazaji Huduma za Kifedha wa Tigo, Catherine Rutenge.
Meneja Masoko na Usambazaji Huduma za Kifedha wa Tigo, Catherine Rutenge (kulia), akizungumza katika mkutano huo.
Meneja Masoko na Usambazaji Huduma za Kifedha wa Tigo, Catherine Rutenge (kulia), akizungumza katika mkutano huo.
Kampuni inayoongoza kwa mtindo wa maisha ya kidijitali Tigo imetangaza gawio jingine la robo mwaka la shilingi bilioni 6.04 (sawa na dola za Marekani 2,763,636) kwa watumiaji wa Tigo Pesa ikiwa ni mara ya kumi katika mfululizo wa kampuni hiyo ya simu kugawa faida hiyo kwa watumiaji wake wa huduma ya fedha kwa njia ya simu.
Akizungumza katika mkutano wa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Mkuu wa Huduma za Fedha kwa njia ya simu wa Tigo Ruan Swanepoel alisema kwa ujumla kampuni hiyo imeshawalipa watumiaji wake wa huduma za fedha kwa njia ya simu jumla ya shilingi bilioni 52.28 (sawa na dola za Marekani 23,763,636) ikiwa ni malipo ya robo mwaka ya kumi tangu kuzinduliwa kwa huduma hiyo Julai 2014.
Hii ni mara ya tatu kwa mwaka huu kwa Tigo kulipa gawio kwa wateja wake.
Swanepoel alisema kuwa katika robo ya tatu ya mwaka huu kiwango cha faida kilipanda na kufikia asilimia 9 ikiwa kimepanda kwa asilimia 1 kutoka robo ya pili ambako kumechangiwa kwa kiwango kikubwa na kiwango kizuri cha riba katika mifuko ya dhamana ndani ya benki mbalimbali za biashara.
Aidha alidokeza kuwa ongezeko kubwa katika kiwango cha gawio kumechangiwa na kuongezeka kwa faida, kuboreshwa kwa mazingira ya soko na kukua kuliko imara kwa idadi ya watumiaji wa Tigo Pesa kama nyenzo kuu katika ongezeko kubwa la kiwango cha faida hususani katika kundi la wafanya biashara. Tigo Pesa hivi sasa ina mtandao mkubwa wa wafanya biashara zaidi ya 50,000.
Mwaka 2014 Tigo Tanzania ilikuwa kampuni ya kwanza ya simu duniani kugawa faida iliyozalishwa na fedha za simu zilizopo katika Akaunti ya Udhamini kwa kipindi cha robo mwaka kwa wateja wake.
Popular Posts
-
Mkurugenzi Msaidizi anayeshughulikia masuala ya Simu katika Wizara ya Ujenzi ,Uchukuzi na Mawasiliano Ndugu John Mwera akizungumza ...
-
Kanisa la Waadventista Wa Sabato mwaka huu litashiriki mkutano wa Waadventista watalaamu wa mawasilino ya Intaneti duniani (GAiN) kwa k...
-
Mkuu wa Huduma za Fedha kwa njia ya simu wa Tigo Ruan Swanepoel (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam...
-
Shule ya Msingi ya Mlimani iliyopo Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kuanzia wiki hii itaanza kunufaika na huduma ya intaneti bure inayofung...
-
Imeelezwa kwamba kadri teknolojia inavyoongezeka, inatengeneza fursa ya kukua kwa Shirika la Posta Duniani. Hayo yamesemwa na Kai...
-
Mkuu wa wa Kitengo cha Huduma za Kifedha wa Tigo, Ruan Swanepoel (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es ...
-
Na Yusuph Kileo Nchi ya Tanzania yabahatika tena kwa mara ya tatu kuwa mwenyeji wa mkutano wa “Connect 2 Connect” ambapo kauli mbiu ya...
-
Wapiga kura 2,845,256 wameandikishwa katika Daftari la Kudumu la Wapigakura kwa mfumo wa kielektroniki wa utambuzi wa mwili wa binada...
-
John Sculley aliyewahi kuongoza kampuni ya Apple kwa muda wa miaka 10 (muongo mmoja) tangu mwaka 1983 amezindua simu ya...




