Thursday, October 29, 2015
TWEET MBILI ZA DR JOHN POMBE MAGUFULI KABLA NA BAADA YA KUTANGAZWA KUWA RAIS WA TANZANIA WA AWAMU YA TANO
Dr John Pombe Magufuli leo Oktoba 29,2015 alitweet kwenye account yake ya twitter ya https://twitter.com/MagufuliJP @MagufuliJP
kabla ya kutangazwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, miongoni mwa wagombea 8 waliokuwa wakigombea nafasi hiyo katika uchaguzi Mkuu wa Tanzania uliofanyika Oktoba 25,2015
Katika account yake Dr John Pombe Magufuli ambaye anakuwa Rais wa Tanzania awamu ya tano alitweet kwa mara ya mwisho Oktoba 24 ukiondoa zile alizoretweet za account ya twitter ya chama chake cha Siasa.
Saturday, October 17, 2015
POLISI NCHINI UJERUMANI WAONYA WAZAZI WANAOWEKA PICHA ZA WATOTO FACEBOOK
Polisi nchini Ujerumani wameonya wazazi dhidi ya kuweka picha za watoto wao hadharani katika mtandao wa kijamii wa Facebook.
Katika ujumbe kwenye ukurasa wao wa Facebook, polisi wa eneo la Hagen wametahadharisha wazazi kuwa picha hizo zinaweza kunakiliwa au kubadilishwa na kutumiwa vibaya na watu wanaovutiwa kimapenzi na watoto.
Aidha, watoto wahusika huenda wasipendezwe na picha hizo kuwa wazi mitandaoni watakapokomaa na kuwa watu wazima. Wazazi wameshauriwa kuhakikisha kuwa picha hizo, ikilazimu, zinatazamwa na marafiki zao pekee na si kila mtu mtandaoni.
Ushauri huo wa polisi hao umeenezwa sana mtandaoni na kuvutia hisia mseto. Afisa msemaji wa Polisi wa Hagen ameiambia BBC kwamba walishangazwa na jinsi ujumbe huo wa tahadhari ulivyopokelewa. Amesema wanakadiria kuwa umesomwa na watu zaidi ya milioni 12.
Bw Hanki ameongeza kuwa ujumbe huo haujaongozwa na matukio yoyote mapya ya kesi za uhalifu au watu wanaovutiwa na watoto kimapenzi huko Hagen.
Picha zilizobadilishwa
Shirika la kujitolea linalohusika na ulinzi wa watoto NSPCC katika taarifa yao wamesema: " Wazazi wote wanapaswa kujisikia huru na kufurahia kuchukua picha za watoto wao na kushirikiana nao na marafiki na familia. Hata hivyo, tunapaswa wote kuwa makini wakati wa kuziweka picha hizo mitandaoni."Tunajua kwamba wahalifu wa ngono wana uwezo wa kubadilisha picha za watu wasiokuwa na hatia, na maendeleo katika programu za kuhariri picha zimefanya hili kuwa rahisi sana.
" Hivyo kama wazazi watachapisha picha za watoto wao kwenye mitandao, wanapaswa kuchukua hatua ili kuhakikisha kwamba wanachunguza hali yao ya faragha na kuhakikisha wanaridhishwa na watu watakaotazama picha hizo."
Shirika hilo limeongeza kuwa iwapo wazazi wana wasiwasi kuwa picha ya mtoto wao imeanguka mikononi mwa watu wabaya, wanapaswa kuwasiliana na Internet Watch Foundation, Child Exploitation na Online Protection Centre (Ceop) au kuwasililiana na NSPCC kupitia numbari ya msaada ya simu ya 0808 800 5000 ambapo watapokeza usaidizi.
Tuesday, October 13, 2015
DAR ES SALAAM :TTCL WALIVYOZINDUA WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA
![]() |
![]() |
![]() |
![]() |
| Meneja wa Kanda ya TTCL Dar es Salaam Kati, Jane Mwakalebela (kushoto) akimlisha keki Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Dk. Kamugisha Kazaura kwenye hafla ya uzinduzi wa wiki ya huduma kwa wateja. |
![]() |
| Ofisa Mkuu wa Mauzo na Masoko wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Peter Ngota akifafanua jambo kwa wageni waalikwa kwenye hafla fupi ya uzinduzi wa wiki ya huduma kwa wateja jijini Dar es Salaam. |
![]() |
| Hapa ni wakati wa kugonganisha glasi za mvinyo kutakiana afya njema na utendaji bora...! |
![]() |
Akizungumza na baadhi ya wateja wa TTCL, maofisa na wafanyakazi jijini Dar es Salaam Mkuu wa Idara ya Huduma kwa Wateja TTCL, Laibu Leonard alisema ndani ya maadhimisho hayo maofisa wa TTCL watapita kuwatembelea wateja ofisini na majumbani kuwasikiliza maoni yao ikiwa ni pamoja na kupata mrejesho juu ya huduma wanazozitoa.
Alisema maofisa waandamizi wa kampuni hiyo watashiriki moja kwa moja katika zoezi hilo la kutoa huduma pamoja na kuwatembelea wateja kupata maoni yao na pia kutoa shukrani kwa wao kukubali kuhudumiwa na kampuni hiyo ya simu ya kizalendo nchini Tanzania.
"...Mbali na kutoa huduma zetu katika matawi mbalimbali katika kipindi hiki maofisa waandamizi wa TTCL watawatembelea wateja moja kwa moja katika ofisi zao au majumbani kwa ajili ya kuwasikiliza na pia kupokea naoni yao," alisema Leonard akizungumza katika hafla hiyo.
Katika uzinduzi wa hafla hiyo TTCL ilitoa zawadi kwa wateja watano wa mwanzo waliofika katika vituo vya huduma kwa wateja leo asubuhi kuhudumiwa na kampuni hiyo pamoja na kuwazawadia maofisa wa TTCL waliofanya vizuri zaidi katika idara ya huduma kwa wateja ya kampuni hiyo, ikiwa ni motisha ya kuchochea utendaji bora zaidi. *Imeandaliwa na www.thehabari.com
Saturday, October 10, 2015
IFAHAMU NJIA MADHUBUTI YA KUKABILIANA NA UHALIFU MTANDAO
Tukio la kipekee katika anga ya
usalama mitandao ambalo limekualiki azimishwa kila mwaka katika mwezi
wa Oktoba ambapo mataifa yanaadhimisha siku ya uelewa wa maswala ya
usalama mitandao duniani kote.
Na imani
Mwaka huu Tanzania itauchukulia mwezi huu kinamna ya kipekee ili
kuweza kukuza uelewa kwa watu wake Tukio ambalo nategemea makampuni
mbali mbali na maeneo mengine yataandaa program mbali mbali za kukuza
uelewa wa maswala ya usalama mitandao ili kuweza kufikiwa malengo
yaliyokusudiwa na wanausalama wote mitandao duniani kote.
Aidha, inaaminika kama ilivyo katika uhalifu mwingine wowote ni vigumu kumaliza kabisa tatizo ila kuna njia kadhaa ambazo kwa umoja wake zikifanyiwa kazi vizuri zinaweza kabisa kupunguza kwa kiasi kikubwa sana tatizo la uhalifu mtandao.
Aidha, inaaminika kama ilivyo katika uhalifu mwingine wowote ni vigumu kumaliza kabisa tatizo ila kuna njia kadhaa ambazo kwa umoja wake zikifanyiwa kazi vizuri zinaweza kabisa kupunguza kwa kiasi kikubwa sana tatizo la uhalifu mtandao.
Tatizo kubwa kubwa ni kuwa njia hizi zimekua zikiishia katika maandishi baada ya kujadiliwa na wanausalama mitandao ambapo mimi binafsi nilikua miongoni mwao.
Kwa kupata elimu hii wale wote waliokua wakifanya uhalifu mtandao pasi na kujua wanakua na ufahamu wa kutosha na hatimae kundi hili linakua limeondokana na uhalifu mtandao. Aidha, kundi la pili ambalo ni lile linalofanya uhalifuu huu wa mtandao wakiwa hawana namna kwa kutokujua athari zake baada ya kujua athari za uhalifu mtandao kwao na kwa wengine na pia kujua njia mbadala wanazoweza kutumia kuepukana na uhalifu huu kupitia elimu ya uelewa ya usalama mitandao kundi hili linaweza pia likapunguzwa hadi asilimia 84% kwa mujibu wa wataalam wa usalama mitandao.
Kundi
la mwisho ambalo ni wahalifu wanaofanya uhalifu huu makusudi ingawa wanajua
wakifanyacho na hawana utayari wa kuepukana na uhalifu huu mtandao nalo
linapunguzwa nguvu kwani watumiaji mitandao wanakua na uelewa wa namna wahalifu
hawa wanavyo fanya uhalifu na njia sahihi za kujilinda hatimae kundi hilipia
linakosa watu wengi wanaoweza kuingia katika mtego wao wa uhalifu mtandao na
kupungukiwa kasi na nguvu ya usambazaji wa uhalifu huu.
Inaaminika
asilimia zaidi ya 37% ya wahalifu wa kundi hili la tatu wanapokosa watu
wanoweza kuingia mtegoni wanajikuta wanakata tama na kujishughulisha na mambo
mengine tofauti na uhalifu mtandao.
Kumekua
na wimbi kubwa la makampuni mengi mbali na kua na teknolojia nzuri ya kuzuia
uhalifu mtandao bado yameendelea kugubikwa na uhalifu mtandao kutokana na
kutowekea mkazo swala hili la kukuza uelewa wa maswala haya ya usalama
mitandao. Pia mataifa mengi yameendelea kujipanga kwa kua na vitengo kadhaa vya
udhibiti uhalifu pamoja na kua na sharia sahisi za kudhibiti uhalifu huku bado
wimbi kubwa la wahalifu mtandao bado likiendelea kua kubwa.
Tatizo
ni kukosekana na njia sahihi na namna madhubuti ya kuendea njia hii ya kukuza
uelewa wa maswala ya usalama mitandao ambapo kama nilivyo fafanua awali
ingeweza kabisa kupunguza kwa kiasi kukubwa swala hili la uhalifu mtandao.
Kumekua
na jitihada nyingi za kuhamasisha kuanzia ngazi ya mtu binafsi, Makapuni ,
Nchi, Bara na hatimae Dunia nzima kujenga tamaduni ya kukuza uelewa wa matumizi
salama ya mitandao ili kukabiliana na wimbi kubwa la uhalifu unaoendelea kukua
kwa kasi hivi sasa.
Swali
linaloulizwa ni kwamba pamoja na jitihada nyingi za wanausalama mtandao ambapo hadi sasa pamoja
na mambo mengine, tayari kuna mwezi wa Kumi ambao unafahamika kama mwezi maalum
wa maswala ya uelewa wa usalama mitandao yaani “OCTOBER" – Cybersecurity
Awareness Month” na kupatikana kwa
tamthilia maalum ambazo zipo kukuza uelewa wa usalama mitandao.
Jibu
ni kwamba, Jitihada hizi zimebaki kwa wanausalama mitandao na wananchi
wakawaida bado imekua ni vigumu sana kufikiwa na kuelewa pamoja na kua miongoni
mwa jitihada hizi.
Wengi
bado wamebaki wakijua swala la ufahamu na uelewa wa maswala ya usalama mitandao
ni swala la wanausalama mitandao pekee huku wengine wakiamini pia wana TEKINOHAMA
ndio pia wanausika.
Inasahaulika
kabisa swala la kubaki salama kimtandao ni swala linalo takiwa kuanzia katika
ngazi ya mtu binafsi sawa kabisa na swala la ulinzi wa uhalifu mwingine wowote.
Tumekua na utamaduni wa pamoja na mambo mengine, kufunga milango, kuwa na
walinzi katika nyumba zetu na kuweka taa za nje tukiamini zinauwezo wa kusaidia
upungufu wa uhalifu majumbani mwetu.
Cha
kushangaza zaidi, Jitihada hizi binafsi huzioni zikiamishiwa katika udhibiti wa
uhalifu huu wa mitandao ambapo vitu kama Antiviruses, Maneno ya siri na
mengineyo ni ya kuanzia katika ngazi ya mtu binafsi.
Kuna
Kila namna ya kufahamu kua pale swala la uelewa wa maswala ya usalama mtandao
litakapoweza kufanyiwa kazi kwa kiwango kizuri basin i wazi kabisa linaweza
kusaidia kila mmoja kuelewa na kuhimili ipasavyo uhalifu huu mtandao katika
ngazi ya mtu binafsi, pamoja na kukuza utamaduni wa kila mmoja kujua anajukumu
ssi tu la kujilinda binafsi kimtandao bali na kulinda wengine ipasavyo kuhakiki
taifa, bara na hatimae dunia inabaki salama kimtandao.
Kwa
ufupi nimefafanua kwa kina faida zinazoweza kupatikana pale uelewa sahihi wa elimu
ya usalama mtandao itapatikana kwa jamii zetu na katika maofisi yetu (Makampuni)
Maelezo hayo yanawea kusomeka kwa ku “BOFYA HAPA” Wakati huo huo nilipozungumzia
mambo muhimu yanayo paswa kuenda sambamba na uwepo wa sharia mpya ya usalama
mitandao niliainisha kwa kina swala la uelewa sahihi wa maswala ya usalama
mitandao pamoja na ujuzi wa kufanyia kazi uchunguzi wa uhalifu mtandao na
ushirikiano kama inavyoweza kufatiliwa katika video hii hapo chini.
Leo
nitaangazia njia ambayo imeshika nafasi ya juu na imeonekana na uwezo mkubwa wa
kuhimili uhalifu mtandao ambapo imeaminika inauwezo wa kupunguza aina mbili za
wahalifu mtandao pamoja na kusababisha aina ya tatu kupungua makali. Kwa ujumla
wake imezungumzwa inaweza kupunguza hadi asilimia 71% ya uhalifu wote mtandao
kama itafatwa vizuri na kupewa uzito wa kipekee katika mataifa yote.
Natoa wito kwa kila mmoja wetu kukuza upendo wa kufatilia na kutaa kujua namna mbali mbali za kuweza kujilinda katika ngazi ya mtu binafsi na uhalifu huu mitandao unaokua kwa kasi zaidi hivi sasa huku makampuni kua na tamaduni ya kuwa na mafunzo maalum ya maswala haya na taifa kwa ujumla kuhakiki linaongeza jitihada katika kukuza uelewa kwa wananchi katika maswala ya usalma mitandao ili kukabiliana na ongezeko la uhalifu mtandao nchini.
Na:Yusuph Kileo
ANAYETUHUMIWA KUENEZA TAARIFA ZA UONGO KWENYE MITANDAO YA KIJAMII KUHUSU MKUU WA MAJESHI NCHINI TANZANIA AFIKISHWA MAHAKAMANI
Serikali ya Tanzania imemfikisha Mahakamani Bernedict Angelo Ngonyani kwa tuhuma za kutumia mtandao wa Facebook na WhatsApp kueneza taarifa za uongo kuwa mkuu wa majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange amelazwa Nairobi kwa madai ya kulishwa chakula chenye sumu.
Akizungumza kwenye eneo la mahakama ya kisutu jijini Dar es Salaam ambako mtuhumiwa huyo alifikishwa kwa ajili ya kusomewa mashitaka, wakili mkuu wa serikali Joanes Karungura amesema, mtuhumiwa huyo amefikishwa mahakamani hapo kwa kuvunja kifungu namba 16 cha Sheria ya Makosa ya Kimtandao ya mwaka 2015.
Sheria hiyo ijulikanyo kwa lugha ya Kiingereza, Tanzania Cybercrime Act
2015, inakataza kusambaza ujumbe, taarifa au data za uongo au
zisizothibitishwa kwa njia ya mtandao.
Ngonyani ambaye amenyimwa dhamana kutokana na aina ya kosa alilofanya la kuvunja sheria ya mtandao ya mwaka 2015 alikamatwa Septemba 25 mwaka huu kwa ushirikiano wa mamlaka ya mawasiliano nchini, Jeshi la Polisi na vyombo vya ulinzi na usalama.
Wakati huo huo serikali imewafikisha watuhumiwa watano katika mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam, mmoja raia wa Afrika ya Kusini, mmoja raia wa China na watatu kutoka Pakstani, kwa kosa la kuiba kwa njia ya kimtandao wizi wenye thamani ya karibu shilingi billion moja, fedha za Kitanzania.
Mhandisi wa Mamlaka ya Mawasiliano nchini, TCRA anasema watuhumiwa hao walikutwa na laini zaidi ya mia moja zenye usajili bandia ambazo walikuwa wanazitumia kufanya biashara ya kupiga simu Kimataifa kinyume cha sheria.
Mtuhumiwa wa makosa ya mtandao Benedict Angelo Ngonyani (24) (wa kwanza kulia) anayetuhumiwa kusambaza taarifa za uongo zinazomhusu Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, akiwa katika mahakama ya hakimu mkazi ya Kisutu akisubiri kusomewa mashitaka.
Wengine ni watuhumiwa wa wizi kwa kutumia mitandao ya simu (fraud and use of telecommunication network) Ally Hamze (53) raia wa Afrika Kusini (wa pili kulia), Huang Kun Bing (26) Raia wa China (wa tatu kulia) Irfan Mirza Baig (46) (wa kwanza kushoto) Hefeez Irfan (32) (wa pili kushoto) na Mirza Rizwan Baig (41) (wa tatu kushoto) wote watatu raia wa Pakistani wakiwa katika Mahakama ya hakimu mkazi Kisutu wakisubiri kusomewa mashitaka ya wizi kwa kutumia mitandao ya simu (fraud and use of telecommunication network).
Kesi zote zimeahirishwa hadi Oktoba 23 mwaka huu na watuhumiwa wote wamepelekwa rumande huku uchunguzi ukiendelea.
Ngonyani ambaye amenyimwa dhamana kutokana na aina ya kosa alilofanya la kuvunja sheria ya mtandao ya mwaka 2015 alikamatwa Septemba 25 mwaka huu kwa ushirikiano wa mamlaka ya mawasiliano nchini, Jeshi la Polisi na vyombo vya ulinzi na usalama.
Wakati huo huo serikali imewafikisha watuhumiwa watano katika mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam, mmoja raia wa Afrika ya Kusini, mmoja raia wa China na watatu kutoka Pakstani, kwa kosa la kuiba kwa njia ya kimtandao wizi wenye thamani ya karibu shilingi billion moja, fedha za Kitanzania.
Mhandisi wa Mamlaka ya Mawasiliano nchini, TCRA anasema watuhumiwa hao walikutwa na laini zaidi ya mia moja zenye usajili bandia ambazo walikuwa wanazitumia kufanya biashara ya kupiga simu Kimataifa kinyume cha sheria.
Mtuhumiwa wa makosa ya mtandao Benedict Angelo Ngonyani (24) (wa kwanza kulia) anayetuhumiwa kusambaza taarifa za uongo zinazomhusu Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, akiwa katika mahakama ya hakimu mkazi ya Kisutu akisubiri kusomewa mashitaka.
Wengine ni watuhumiwa wa wizi kwa kutumia mitandao ya simu (fraud and use of telecommunication network) Ally Hamze (53) raia wa Afrika Kusini (wa pili kulia), Huang Kun Bing (26) Raia wa China (wa tatu kulia) Irfan Mirza Baig (46) (wa kwanza kushoto) Hefeez Irfan (32) (wa pili kushoto) na Mirza Rizwan Baig (41) (wa tatu kushoto) wote watatu raia wa Pakistani wakiwa katika Mahakama ya hakimu mkazi Kisutu wakisubiri kusomewa mashitaka ya wizi kwa kutumia mitandao ya simu (fraud and use of telecommunication network).
Kesi zote zimeahirishwa hadi Oktoba 23 mwaka huu na watuhumiwa wote wamepelekwa rumande huku uchunguzi ukiendelea.
Thursday, October 8, 2015
CONNECTMOJA TECHNOLOGIES LIMITED WAZINDUA MFUMO MPYA WA SCHOOL MANAGEMENT SYSTEM
Kampuni
ya Connectmoja Technologies inayoendesha shughuli zake hapa nchini
Tanzania leo imezindua Mfumo madhubuti unaojulikana kwa jina la
KSchool Management system.
Akizungumza
na wana habari, Mtaalamu wa utafiti na ukuzaji wa Masoko Bw. Fred Crich
amewaambia wanahabari kwamba Kampuni yao ya ConnectMoja Technologies
imejikita zaidi katika kuhakikisha inasaidia sekta ya elimu na uwekezaji
kukua pamoja na maendeleo ya Teknolojia hapa Nchini.
Bw.
Crich amesema mfumo huu umewalenga wamiliki wa mashule kwani mfumo
unawawezesha kuweka rekodi sahihi za wanafunzi, kutunza kumbukumbu za
mienendo ya wanafunzi, kuweka rekodi ya matokeo ya wanafunzi na wazazi
pia wanaweza kuona rekodi hizi wakiwa majumbani au mahala popote kwa
kutumia simu za kiganjani au computer zenye internet.
Mfano. Mwanafunzi
anapotoka shule, Mzazi atakuwa na uwezo wa kuingia kwenye mfumo huu
kupitia(Parent Portal) na kujua kama mtoto alifika shuleni, na kama
alifika alifundishwa nini, pia kujua kama ana Homework ya kufanya pindi
afikapo nyumbani, pia itamwonesha matokeo yake papo hapo.
Mfumo huu una Teachers Portal na students portal ambapo Mwalimu anaweza kutuma Assignments kwa wanafunzi hata wakiwa Likizo.
Bw.
Crich ameelezea kwamba mfumo huu umeanza kutumika kwenye baadhi ya
shule hapa Nchini na kwa sasa wameuboresha zaidi ili uweze kuwanufaisha
wazazi pamoja na wadau wa sekta ya elimu.
Pia anakaribisha wamiliki wa shule wote wanaotaka kuupata mfumo huu, bei ni nafuu .
Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kupitia:
call: +255 777 88 0000 7 au 0714 215 600
TIGO YAENDELEA KUSHEREKEA JUMA LA HUDUMA KWA WATEJA
Meneja
wa duka la TigoNkurumah, Lulu Kikuli akimkabidhi zawadi ya simu Grace
Joachim mkazi wa Tandale ikiwa ni sehemu maadhimisho ya wiki ya
wateja wa
Tigo
|
Mwandishi
wa habari wa TV1 Robert Latonga akifanya mahojiano na mteja wa Tigo,
Hamadi Maliwata mkazi wa Mbagala kwenye maadhimisho ya wiki ya wateja
wa Tigo
|
Meneja
wa ubora huduma kwa wateja wa Tigo Bi. MwangazaMatotola,
akimkabidhi fulana mteja wa Tigo Nickson Mbwambo mkazi wa Mabibo,
|
Mtaalam wa huduma kwa wateja wa Tigo Jackson Jerry(kushoto),
, Halima Kasoro (katikati) na
Meneja wa ubora huduma kwa wateja wa Tigo Mwangaza Matotola(kulia) wakiwa
kwenye picha ya pamoja
|
Mteja wa Tigo Zenah Hamdi mkazi wa Tandika, akipata huduma toka kwa Mtoa huduma wa Kampuni ya Tigo
|
Thursday, October 1, 2015
KIONGOZI WA KANISA LA WAADVENTISTA WA SABATO ULIMWENGUNI TED N.C.WILSON AJIUNGA NA FACEBOOK NA TWITTER KWA AJILI YA KUWASILIANA NA WAUMINI NA WATU MBALIMBALI
![]() |
| Ted Wilson na mkewe Nancy |
Wilson anasema atatumia wasifu wake wa twitter kwa anuani yake ambayo ni @pastortedwilson na kwenye mtandao wa facebook anatumia ukurasa wake ambao ni facebook.com/pastortedwilson ambapo atakuwa akiwasiliana na watu kwa njia ya maombi,mafundisho ya Biblia na Roho ya Unabii,taarifa zake za utume,picha na habari mbalimbali za ziara zake za kikazi.
Sikiliza ujumbe wa ukaribisho wa Kiongozi huyo baada ya kujiunga na mitandao hiyo ya kijamii
Mpaka kufikia saa 6:00 usiku wa Alhamisi ya Oktoba 1,2015 tayali watu waliokuwa wameshamfuatilia kwenye twitter ni 1,435 na kwenye ukurasa wake wa facebook kulikuwa na likes 10,050
Pia kiongozi huyo atatumia ukurasa wake wa facebook kujibu maswali kuhusu kanisa la Waadventista Wa Sabato ambapo watu wataweza kumtumia maswali kupitia anuani yake ya barua pepe ambayo ni e-mail:askpastorwilson@adventist.org na atatoa majibu ya maswali matatu kila ijumaa.
Haifahamiki idadi kamili ya Waadventista Wa Sabato waliko kwenye Twitter na Facebook. Ukurasa wa Facebook wa Divisheni ya Kanisa hilo katika eneo la Kusini mwa Amerika unaonekana kufuatiliwa na watu zaidi ya 877,000 japo hakuna anayafahamu kuwa wote ni Waadventista.
Wasifu wa Kanisa la Waadventista Wa Sabato kwenye Twitter ambao ni @AdventistChurch,unafuatiliwa na watu 50,300 na kuufanya kuwa unaongoza kwa kuwa na wafuasi wengi miongoni mwa twitter zinazomiliiwa na makanisa .
Viongozi wengine wa dini walioko kwenye twitter ni Papa Francis ambaye anaidadi ya watu Milioni 25 wanaofuatilia akitumia @Pontifex ambayo inatumia lugha 9 kuwasilia na Dalai Lama ambaye anawatu wanaomfulia milioni 11.9
Sikiliza ujumbe wa ukaribisho wa Kiongozi huyo baada ya kujiunga na mitandao hiyo ya kijamii
Mpaka kufikia saa 6:00 usiku wa Alhamisi ya Oktoba 1,2015 tayali watu waliokuwa wameshamfuatilia kwenye twitter ni 1,435 na kwenye ukurasa wake wa facebook kulikuwa na likes 10,050
Pia kiongozi huyo atatumia ukurasa wake wa facebook kujibu maswali kuhusu kanisa la Waadventista Wa Sabato ambapo watu wataweza kumtumia maswali kupitia anuani yake ya barua pepe ambayo ni e-mail:askpastorwilson@adventist.org na atatoa majibu ya maswali matatu kila ijumaa.
Haifahamiki idadi kamili ya Waadventista Wa Sabato waliko kwenye Twitter na Facebook. Ukurasa wa Facebook wa Divisheni ya Kanisa hilo katika eneo la Kusini mwa Amerika unaonekana kufuatiliwa na watu zaidi ya 877,000 japo hakuna anayafahamu kuwa wote ni Waadventista.
Wasifu wa Kanisa la Waadventista Wa Sabato kwenye Twitter ambao ni @AdventistChurch,unafuatiliwa na watu 50,300 na kuufanya kuwa unaongoza kwa kuwa na wafuasi wengi miongoni mwa twitter zinazomiliiwa na makanisa .
Viongozi wengine wa dini walioko kwenye twitter ni Papa Francis ambaye anaidadi ya watu Milioni 25 wanaofuatilia akitumia @Pontifex ambayo inatumia lugha 9 kuwasilia na Dalai Lama ambaye anawatu wanaomfulia milioni 11.9
Wednesday, September 30, 2015
MAONYESHO YA TEKNOHAMA KWA WANAFUNZI YAFUNGULIWA JIJINI DAR ES SALAAM
| Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Profesa Sifuni Mchome akizungumza kabla ya kuzindua rasmi maonesho ya Tehama yanayoendelea katika ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. |
Kamishina
wa Elimu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Eusella
Bhalalusesa akizungumza kabla ya kumkaribisha Katibu Mkuu Wizara ya
Elimu na Mafunzo ya Ufundi Profesa Sifuni Mchome kuzindua maonesho ya
Tehama yanayoendelea katika ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Mwl.
Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Serikali ya Tanzania imeeleza kuwa jumla ya wanafunzi 60,000 katika shule 150 nchini humo wamepitiwa na mafunzo ya
programu ya Bridge IT yenye lengo la kuongeza ubora wa elimu kwa kutumia
teknolojia ya kisasa ya kidijiti (digital technology) katika
ufundishaji na ujifunzaji wa Hisabati,Sayansi na Stadi za Maisha.
Kamishina wa Elimu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi,
Profesa Eusella Bhalalusesa ameeleza hayo wakati akimkaribisha Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na
Mafunzo ya Ufundi Profesa Sifuni Mchome kuzindua maonesho ya Tehama.
Amesema
kutokana na mafanikio yaliyotokea sasa wanatanua wigo baada ya
kuwezeshwa kifedha na Shirika la Kimataifa la Maendeleo ya elimu (Global
Partnership For Education) kwa ajili ya kuendeleza teknolojia hiyo
katika kujifunza na kufundisha katika shule za msingi na hasa darasa la
awali la kwanza hadi la nne.
Maonesho hayo yanayofanyika katika ukumbi wa kimataifa wa Mwalimu
Julius Nyerere yana lengo la kuonesha ubunifu ambao upo tayari kutumika
kufanikisha mafunzo hayo.
Pia
maonesho hayo yanatarajia kujadili na kuangalia mbinu za kielektroniki
zitakazoweza kuendana na mazingira ya Tanzania katika ufundishaji na
kujifunza kwa gharama nafuu.
Pia wanatarajia kuangalia utayari wa walimu na namna ya kuwabadilisha mtazamo ili waweze kufundisha na kufundishika.
Katika
maonesho hayo serikali imesema inatarajia kuanza kutumia rasmi
Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tekinohama) katika kufundishia
wanafunzi kuanzia ngazi ya chini kabisa ya elimu ambayo ni chekechea.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Sifuni Mchome
alisema matumizi ya Tehama katika ufundishaji wa wanafunzi wa chekechea
yataimarisha kiwango cha elimu.
Katibu
Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Profesa Sifuni Mchome
akifuatilia kwa makini risala Kamishina wa Elimu Wizara ya Elimu na
Mafunzo ya Ufundi, Profesa Eusella Bhalalusesa (hayupo pichani).
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Profesa Sifuni Mchome akijianda kuzindua rasmi maonesho ya Tehama yanayoendelea katika ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Ofisa
Miradi ya Elimu kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi
na Utamaduni (UNESCO), Faith Shayo akitoa maelezo ya shughuli mbalimbali
zinazofanywa na shirika lake katika kuendeleza sekta ya elimu nchini
kwa Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Profesa Sifuni
Mchome (kushoto) mara baada ya kuzindua maonesho hayo ambapo pia UNESCO
inashiriki. Katikati ni Kamishina wa Elimu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya
Ufundi, Profesa Eusella Bhalalusesa.
Ofisa
anayeshughulikia masuala ya Elimu Kitaifa wa UNESCO, Tumsifu Mmari
(katikati) akimsikiliza mmoja wa wadau wa elimu aliyetembelea banda la
UNESCO kwenye maonesho ya TEHAMA yanayoendelea katika ukumbi wa mikutano
wa Kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. Kushoto
ni Ofisa Miradi ya Elimu kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu,
Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Faith Shayo.
Ofisa
anayeshughulikia masuala ya Elimu Kitaifa wa UNESCO, Tumsifu Mmari
(kulia) akiwa na wadau wengine wa elimu wakipitia makbrasha mbalimbali
katika mkutano huo.
Pichani juu na chini ni baadhi wadau wa elimu waliohudhuria uzinduzi wa maonyesho hayo.
Baadhi ya wanafunzi kutoka shule mbalimbali za msingi jijini Dar walioshiriki hafla hiyo.
Mkurugenzi
Mkuu wa Shule Direct, Faraja Nyalandu akipozi na wadau kwenye ukumbi wa
mikutano wa Kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere jijini Dar es Salaam
yanakoendelea maonesho ya TEKINOHAMA
Thursday, September 24, 2015
DAR ES SALAAM:BASATA LATAKA KUONDOLEWA/KUSITISHWA MARA MOJA KUCHEZWA KWA NYIMBO ZOTE ZILIZOKINYUME CHA MAADILI, SHERIA NA TARATIBU
Baraza la Sanaa la Taifa nchini Tanzania (BASATA) limetoa
siku saba kwa wasanii,vituo vya radio,runinga wamiliki wa tovuti na wale wenye wasifu kwenye mitandao
ya kijamii kuondoa nyimbo zote au maudhui yenye muelekeo unaoenda kinyume na
maadili, matusi na kashfa mbalimbali.
Taarifa ya BASATA iliyotiwa
saini na Katibu Mtendaji wa Baraza hilo Godfrey Mngereza imevitaka pia vyombo vya habari zikiwemo radio na
luninga kuondoa na kuacha mara moja kucheza au kurusha nyimbo zote zenye maudhui
hayo.
Mngereza amesema maudhui ya
kashfa,matusi,kejeli,udhalilishaji zinatishia kuigawa jamii ya watanzania
katika kipindi hiki ambacho taifa linaendelea na kampeni za kujiandaa na
uchaguzi mkuu tarehe 25 mwezi wa kumi mwaka huu.
Taarifa hiyo imeeleza kuwa kifungu namba 118 [a-d]
cha sheria ya bunge namba 9 ya mawasiliano ya mtandao ya mwaka 2010 vinaelekeza
kuwa ni marufuku kwa njia yoyote kwa mtu au chombo chochote kutengeneza ujumbe
ambao unamlengo wa matusi ,dharau,uzushi au jinai kwa lengo la kutukana
,kutisha, kusumbua au kushusha hadhi
ya mtu mwingine.
WIZARA YA ULINZI YA UINGEREZA YATOA NGUO ZA WANAJESHI WAKE ZENYE MFUMO WA KISASA WA MAWASILIANO

Wizara ya Ulinzi wa Uingereza imetoa Nguo za kisasa kwa ajili ya wanajeshi wake wa miaka ijayo . Picha unayoiona ni mfano wa nguo hizo na huo ni ubunifu wa njia ya kompyuta,mradi huo unaitwa Future Soldier Vision kwa ufupu FSV .
Taarifa zinasema nguo hizo zitakuwa na mfumo wa kisasa wa mawasiliano na mfumo wa biometriki ambao utamfanya mwanajeshi wa Uingereza kuwa salama zaidi kushinda wakati wowote atakapokua kwenye uwanja wa vita .
Katika vita upande wenye taarifa nyingi ndio huwa na uwezekano wa kushinda kwa urahisi . FSV ni mpangilio wa vifaa vya kisasa vya mawasiliano na silaha zinazovaliwa mwilini mwa mwanajeshi . kutakua na sensa itakayowezesha wanajeshi wote kujuana wakiwa uwanja wa vita au kokote bila kuchanganyana , mfumo wa mawasiliano ambao utaweza wanajeshi kutumiana taarifa kwa mfumo wa picha , sauti na video .
Wakati wizara imetoa mchoro huu wa ubunifu na kuuelezea , kampuni , taasisi na watu binafsi wameanza utafiti ambao utawezesha kutengeneza vifaa vingi vitakavyofanya kazi sambamba na wanajeshi hao muda ukifikia kwa ajili ya soko la ndani ya Uingereza na maeneo mengine ulimwenguni.
Popular Posts
-
Mkurugenzi Msaidizi anayeshughulikia masuala ya Simu katika Wizara ya Ujenzi ,Uchukuzi na Mawasiliano Ndugu John Mwera akizungumza ...
-
Kanisa la Waadventista Wa Sabato mwaka huu litashiriki mkutano wa Waadventista watalaamu wa mawasilino ya Intaneti duniani (GAiN) kwa k...
-
Mkuu wa Huduma za Fedha kwa njia ya simu wa Tigo Ruan Swanepoel (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam...
-
Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), imeendelea kukuza matumizi ya mawasiliano na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEKNOHAMA) nchini Tanzan...
-
Na Yusuph Kileo Nchi ya Tanzania yabahatika tena kwa mara ya tatu kuwa mwenyeji wa mkutano wa “Connect 2 Connect” ambapo kauli mbiu ya...
-
Wapiga kura 2,845,256 wameandikishwa katika Daftari la Kudumu la Wapigakura kwa mfumo wa kielektroniki wa utambuzi wa mwili wa binada...
-
Rais Barak Obama wa Marekani Serikali ya Marekani imekumbwa na udukuzi wa mtandao wa komputa ambapo taarifa bina...
-
Windows 10 upgrade Watumiaji wa WINDOWS , je umepata ofa ya WINDOWS 10 ya bure toka kwa Microsoft ? Jambo hili liko hivi, Microsoft ...
-
John Sculley aliyewahi kuongoza kampuni ya Apple kwa muda wa miaka 10 (muongo mmoja) tangu mwaka 1983 amezindua simu ya...


















