Saturday, October 26, 2013

TAKWIMU ZA MATUMIZI YA INTANETI BARANI AFRIKA


Friday, October 25, 2013

MKONGO WA TAIFA WAINUFAISHA SERIKALI YA TANZANIA

 
Zaidi ya shilingi bilioni 41.4 zimepatikana kutokana na malipo ya huduma za Mkongo wa Taifa ambapo hadi Agosti mwaka huu kampuni 16 zikiwamo 9 za nje zimeunganishwa kwenye mtandao huo imara kwa mawasiliano.

Pia mipango inafanywa kuunganisha vituo mbalimbali vya luninga na raedio kwenye huduma hiyo.Hayo yamebainishwa kwenye juzi na Ofisa Mtendaji wa Kampuni ya Simu ya Tanzania (TTCL),Kamugisha Kazaura katika taarifa yake aliyoitoa kwa Kamati ya Bunge la Tanzania ya Miundombinu.

Amesema ni kampuni saba pekee za ndani zilizounganishwa ni kampuni hizo ni TTCL yenye jukumu la kusimamia mkongo huo,zingine ni Zantel,Simbanet,Airtel,Tigo,Infinity Africa na Vodacom.

Kampuni za nje ni pamoja na MTN-Zambia hadi Malawi,MTN-Rwanda,Airtel Rwanda,KDN,RDB,Econet,BCS na UCOM-Burundi

chanzo:Gazeti la Mwananchi

WAZIRI AITAKA SAMSUNG NA VODACOM TANZANIA KUWEKA VIZUIZI VYA TOVUTI ZISIZOFAA

Waziri wa Mawasiliano Sayansi na Teknolojia Tanzania Pro Makame Mbarawa ameitaka kampuni ya Simu ya SamSung na Vodacom kuhakikisha inazuia mifumo inayozuia kuonekana kwa tovuti zisizofaa katika mtandao wa intaneti ambao unaziunganisha shule za sekondari nchini Tanzania nchini ya mkongo wa taifa wa mawasiliano aliouzindua katika shule ya sekondari ya Kambangwa ilipo Kinondoni,Dar es salaam oktoba 22 mwaka huu.

"Nachukua fulsa hii kumwomba mwalimu Mkuu,Vodacom na Samsung kuhakikisha kuwa tovuti ambazo hazifai na zisizo na maslahi kwa watumiaji zinazuiwa kuonekanakwenye mfumo huo hilo halina mjadala"amesema waziri huyo

Amesema ni kosa kubwa kuingia katika mitandao ya ajabu na hivyo serikali ya Tanzania haitokubaliana na suala hilo na serikali iko tayali kushirikiana na walimu katika kuhakikisha suala hilo linazuiwa kwa kushirikiana na wataalamu wa wizara.

Kampuni ya Vodacom Tanzania kwa kushirikiana na kampuni ya Samsung  zimeungana katika kuunganisha shule za sekondari nchini Tanzania kupitia mkongo wa Taifa ambao utawezesha kupata mawasiliano ya intaneti kwa ajili ya kujifunza masuala mbalimbali ya kielimu ambayo baadhi yake hayawezi kupatikana darasani au kwenye vitabu na wameanza majaribio na shule ya sekondari ya Kambangwa .

Katika ufunguzi huo ambao ni sehemu ya mradi wa Tanzania ya Kesho Waziri Mbarawa aliwataka walimu na  wanafunzi wote kutumia maabara za komputa zitakazoweka katika kutumika kwenye utaratibu huo.




Saturday, October 19, 2013

KOREA YA KUSINI NA JAPAN ZAONGOZA KWA KASI YA INTANETI DUNIANI



Kwa muda sasa Korea ya Kusini imeonekana kuwa na asilimia kubwa ya uwezo wa kasi ya intaneti duniani.
 Katika robo ya pili ya mwaka 2013, Watumiaji wa intaneti wa Korea ya Kusini wametumia huduma hiyo kwa wastani wa kasi ya 13.3 Mbps, ambayo ni asilimia 53 zaidi ya ile ya Marekani ambayo kiwango chake ni asilimia 8.7 Mbps.

Tovuti ya statista imeeleza kuwa 8.7 Mbps, ambapo inatumika muda mfupi chini ya saa moja kupakua filamu ya masaa mawili yenye ubora wa HD ambayo ni sawa a GB 3- GB 4.

Marekani iko katika nafasi ya nane  kwenye tawimu za dunia za intanet zenye kasi kubwa ambapo Korea ya Kusini ndio inayoongoza,Japani ikiwa katika nafasi ya pili ya tatu ni Uswizi,huku Hong Kong ikiwa katika nafasi ya nne.

Thursday, October 17, 2013

WAMOJA ICT CONSULTING LIMITED KUSHIRIKI KATIKA KIPINDI CHA MAISHA NA TEKNOHAMA

Maofisa wa WAMOJA ICT Consulting Limited



Mtangazaji Maduhu na WAMOJA ICT Consulting Limited


Kampuni ya WAMOJA ICT Consulting Limited ya jijini Dar es salaam inayojihusisha na utoaji wa mafunzo ya teknohama nchini Tanzania imekubali kushirikiana na kipindi cha Maisha na Teknohama cha Morning Star Radio kinachosikika kila jumapili saa 3:00- saa 4:00 asubuhi kwa saa za Afrika Mashariki kushiriki katika kipindi hicho kila jumapili ya tatu ya kila mwezi.

Wakizungumza na mtangazaji wa kipindi cha Maisha na Teknohama, Mtangazaji Maduhu katika ofisi za kampuni hiyo zilizopo Mwenge,maofisa wa kampuni hiyo inayoundwa vijana wa kitanzania wakishirikiana na kijana toka Korea wamesema hiyo itakuwa fursa nyingine kwa wasikilizaji wa kipindi hicho kupata maarifa kuhusu teknohama.

Friday, October 11, 2013

TABITI ZAPUNGUZA SOKO LA KOMPYUTA


 

Kuna sababu nyingi za kushuka kwa kiwango cha uzalishwaji na  utumiaji wa kopyuta za mezani,wengine wanatoa lawama kwa toleo jipya la Window 8,wengine wanatoa sababu za kushuka kwa soko kutokana na kudolola kwa uchumi duniani

Hata hivyo ukiangalia kiuhalisia waweza gundua kuwa kupungua kwa matumizi ya kompyuta za mezani kulianza katika robo ya pili ya mwaka 2010 na sababu kubwa inayoelezwa ni baada ya kuwa sokoni kwa kifaa cha mawasilino cha iPad .

Tovuti ya statista imeeleza kuwa toka kampuni ya  Apple  ilipoingiza sokoni tabiti kwa kutoa  iPad ya kwanza Aprili 2010, usambazwaji  wa kompyuta za mezani umeshuka PC ambapo sasa umeshuka na kufikia kiwango cha asilimia 8.6.

Apple ilifanikiwa kuuza iPad milioni 20 kwa mara ya kwanza ilipoingiza sokoni vifaa hivyo. 

 Mtandao wa Gartner umekadiria kuwa ukuaji wa usafirishaji wa tabiti duniani kote utakua kutoka tabiti milioni 76 kwa mwaka 2011 na itafikia mara tano zaidi ifikapo mwaka 2017

 Katika robo ya tatu ya mwaka  2009, Toshiba ilisafirisha kompyuta za mezani  milioni  4.01 duniani idadi ambayo ni sawa na ile ya robo ya kwanza ya mwaka  2013, Hewlett-Packard (HP) ndio iliyokuwa ikiongoza kwa kusafirisha idadi kubwa ambapo inakadiriwa kusafirisha komputa za mezani milioni 11.69 katika kipindi hicho cha mwaka. 


Takwimu za awali zilionesha kuwa hadi kufikia robo ya nne ya mwaka  2012 inakadiriwa kuwa kompyuta zilizosafirishwa kwenda sehemu mbalimbali duniani toka kwa makampuni yanayozitengeneza zilikuwa milioni 90.
 
Tabiti zimewapa watumiaji wa kompyuta nafasi nyingine ya kuchagua njia mbadala ya matumizi sawa na yale wanayoweza kuyapata toka katika kompyuta hasa katika suala la matumizi binafsi na bei ya vifaa hivyo.

GOOGLE YAENDELEA KUONGOZA KATIKA KIPATO TOKA KUANZISHWA KWAKE MIAKA 15 ILIYOPITA

 
Google ni kampuni ya teknolojia ya habari na mawasiliano, makao yake makuu yakiwa huko Mountain View,California,Marekani.Kampuni hiyo hutoa huduma za mawasiliano ya intaneti ,matangazo ya biashara kupitia mitandao,compyuta na program za kompyuta.

July 2012 Google.com ilikuwa ni tovuti iliyokuwa imetembelewa na watu wengi duniani huko Marekani ambapo walifikia watu milioni  166.47 nchini humo na kujipatia kiasi cha mapato ya mtaji wake wa dola bilioni 184.5 .

Ikiwa na miaka  15  sasa  baada ya kampuni hiyo iliyoanzishwa kwenye karakana huko Menlo Park, Septemba 4, 1998,Google imekuwa maarufu katika ulimwengu wa mtandao wa intaneti.

Takwimu toka tovuti ya mashable  zinaonesha kuwa mwaka 2013 Google wamepata dola za kimarekani bilioni 36.9  kutokana na matangazo ya biashara ambapo Facebook ambao ni washindani wake wao walipata dola za kimarekani bilioni 6.4

Kwa upande wa mgawanyo wa mapato toka matangazo kwenye simu za mkononi Google wamepata asilimia 53 na facebook wao wamepata asilimia 13 ya matangazo hayo kwa mwaka 2013.

Katika matangazo yanayowekwa katika vivinjali,Google kupitia kivinjali cha chrome wamepata mgawanyo wa  mapato ya asilimia 43 wakati kivinjali cha internet explorer cha kampuni ya  Microsoft  kikipata mgawanyo huo kwa  asilimia 26 

Kwa upande wa  kutafuta mambo mbalimbali  kwa mwezi wa disemba mwaka 2012 kupitia tovuti ya Google  ilitumiwa na watu milioni 1,168 waliotafuta masuala yapatayo bilioni 114.7,wakati mtandao mwingine wa Baidu ulioko China ulitumiwa na watu milioni 293 katika kutafuta masuala mbalimbali kwenye mtandao yapatayo bilioni 14.5. 

Katika mgawanyo wa mapato yatokanayo na program za kutengenezea simu katika robo ya pili ya mwaka 2013 Google walipata asilimia 79 kutoka kwa program ya Androd na iOS wao walipata asilimia 14,ambapo pia walifanikiwa kuongoza kwa asilimia 54 kutokana na programu yao  tumishi ya google maps ikifuatiwa na facebook iliyopata asilimia 44 katika kipindi hicho cha mwaka 2013
 

Thursday, October 10, 2013

CHINA YAONGOZA KWA BIASHARA MTANDAO

Takwimu za wanunuzi kupitia mtandao kwa mwaka 2012 (Vipimo viko katika milioni) Chazo:eMarketer

Kwa namna mabadiliko ya digitali yanavyoongezeka siku kwa siku ndivyo mabadiliko hayo yanavyowafanya watu wengi na wafabiashara duniani kufanya biashara kupitia mtandaoni.

Takwimu zinaonesha kuwa hadi kufikia juni 2012 watumiaji wa intaneti huko China walikuwa milioni 537. 

Hali hii imesaidia sana kukua kwa soko la biashara mtandano nchini China ambalo linaelezwa kukua mara tatu zaidi ya soko la biashara mtandao lile la Marekani ifikapo mwaka 2015. 

Takwimu za karibuni zilizotolewa na  eMarketer zinaonesha kuwa watu wanaonunua bidhaa kupitia mtandaoni walikuwa ni milioni  219.8 kwa mwaka  2012, ambalo ni ongezeko la asilimia  23 toka mwaka 2011 wakati huko Marekani kulikuwa na wanunuzi kupitia mtandao wapatao milioni 150 kwa mwaka huo japo nchi hiyo inabakiwa kuongoza kuwa na soko kubwa la mauzo kupitia mtandao. 

Inakadiliwa kuwa wanunuzi kupitia mtandao wapatao milioni 193 huko China wataongezeka na kufikia milioni 350 ifikapo mwaka 2015 ambapo watakuwa wametumia kiasi cha yuani trioni 2.6 na hii inaonekana biashara kupitia mtandao imekuwa ikiongeza mapato makubwa kwasasa. 

Kampuni maarufu na iliyofanikiwa  kwa biashara ya mtandao nchini China ni Alibaba.com

Saturday, October 5, 2013

UNAVYOWEZA KUJILINDA KWENYE MITANDAO YA INTANETI

TOVUTI ZINAZOTEMBELEWA ZAIDI KWA KILA NCHI

TopSitePerCountry_InternetPopulation 
Katika kile ambacho kinaelezwa kuwa ni kipindi cha himaya  enzi ya  utawala wa intaneti ramani hii inaonesha tovuti ambazo zinatembelewa mara nyingi zaidi kwa kila nchi duniani.

Ramani hii imetokana na utafiti wa takwimu unaofanywa kupitia tovuti ya Alexa na kutolewa Agosti 12,2013 ambapo kampuni hiyo ilianza kufanya uchambuzi huo toka mwaka 1996.Alexa hukusanya data kutoka katika mamilioni ya watumiaji wa intaneti wanaotumia vivinjari vya intaneti 25,000 tofauti tofauti toka katika nchi mbalimbali duniani.

Utafiti huu unaonesha kuwa Google na Facebook ndio tovuti zinazonekana kuwa na idadi kubwa ya watu wanaozitembelea,ambapo Google inaonekana kuwa na watumiaji wengi walioko Ulaya,Marekani ya Kaskazini na Oshenia,wakati Facebook inaonekana kutumiwa zaidi na watu waliko katika nchi za Mashariki ya Kati,Afrika ya Kaskazini na kwa watu wanaofahamu kuhispania walioko barani Amerika.

Hali ni ya kushangaza zaidi huko Asia kwani kumekuwa na ushindani mkubwa katika makampuni hayo ya kigeni toka Marekani kwani mtandao wa Baidu ambayo ni tovuti iliyo na umaarufu huko Uchina  katika kutafuta mambo mbalimbali kwenye intaneti katika nchi hiyo ambayo inaelezwa kuwa na idadi ya watumiaji wengi wa intaneti kuliko nchi zote duniani ikiwa na watumiaji wa intaneti wapatao nusu bilioni.Baidu pia inaonekana kutumiwa zaidi huko Korea ya Kusini.
Alexa haikuweza kutoa maelezo ya kina kuhusu watumiaji wa tovuti katika nchi zilizopo Kusini mwa Jangwa la Sahara.Japo kuna nchi zinazotumia intaneti zimeoneshwa. Kenya , Madagascar, Nigeria, na Afrika ya Kusini ziko katika utawala wa himaya ya  Google ambapo Ghana, Senegali na Sudan wanakadiriwa kuwa chini ya utawala wa Facebook.

Miongoni mwa nchi 50 zinaoneshwa na Facebook kuwa zinawatu wanaotumia tovuti hiyo ikifuatiwa na nchi 36 kati ya hizo zinatumia google na 14 zilizobakia zimeorodhesha kuwa zinatumia  YouTube ambayo inamilikiwa na Google.
Chanzo cha kilelezo:Creative Commons


Thursday, October 3, 2013

PROGRAM TUMISHI YA FACEBOOK YAONGOZA KUWA NA WATUMIAJI WENGI HUKO MAREKANI

PROGRAM TUMISHI ZINAZOPAKULIWA KATIKA SIMU KUFIKIA ZAIDI YA BILIONI 100 MWAKA HUU

Hadi kufikia mwishoni mwa mwaka 2013 inakadiliwa kuwa jumla ya program tumishi kwenye simu zitakazo kuwa zimepakuliwa duniani zitakuwa ni bilioni 102,idadi ambayo itakuwa imevuka lengo kwa kiasi cha milioni 268 lilokuwa linakadiriwa kufikia mwaka  2017.Ingawa ni asilimia 9 tu ya program tumishi za kulipia katika idadi hiyo.

Hii ni kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na tovuti ya mashable inayoandika habari mbalimbali za teknolojia ya habari na mawasiliano (TEKNOHAMA).

 
 2013_09_19_Apps (1)

Wednesday, October 2, 2013

VIBER KUTOZA MALIPO YA HUDUMA ZA STIKA

 viber

Program tumishi ya viber ambayo iliahidi kutoa huduma ya ujumbe mfupi wa maneno na kupiga simu bure kupitia simu,tabiti na kompyuta,hatimaye septemba 30,2013 imetangaza hatua nyingine ya 
kibiashara.
 
Viber ambayo imekuwa na ushindani na program tumishi za mawasiliano za WhatsApp, MessageMe, na  Facebook, sasa imepanga kutumia huduma yake ya stika,alama za hisia zinazoambatana na maandishi kwa ajili ya kupata mapato.

Kampuni hiyo itakuwa ikitengeneza bidhaa za kulipia na kupata leseni kutoka katika vyanzo vingine ikiwemo vipindi vya televisheni,nembo za biashara,japo kuwa sio bidhaa zote za stika zilizopo sokoni zitalipiwa ingawa baadhi zitakuwa zikipatikana katika program tumishi za kulipia.

Viber ilianza huduma ya stika disemba 2012,na imekuwa ikitoa huduma hiyo bure kwa watumiaji wake na kutangazwa kwa huduma hii ya kulipitia kutaanza hivi karibuni japo haijaelezwa siku rasmi. 

 Kinachosubiriwa na ni kuona huduma hii ya soko la stika katika kampuni hii ambayo inawatumiaji zaidi ya milioni 200.

TRA YASISITIZA TOZO LA LAINI ZA SIMU

 

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imeendelea kuzitaka kampuni za simu nchini humo kulipa tozo ya shilingi 1000 kila mwezi kwa laini moja ya simu ndani ya siku 14.

Awali tozo hiyo ilitakiwa kuanza kulipwa julai mwaka huu lakini kutokana na malalamiko ya wadau,utekelezaji huo ulisubiri  mapendekezo ya Tume Maalumu iliyoundwa na Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete kushughulikia suala hilo.

Hivi karibuni umoja wa wamiliki wa  Kampuni za simu nchini Tanzania (MOAT) ulisema asilimia 48 ya watanzania ndio wanaotumia simu za mkononi sawa na watu milioni 22.

Kutokana na tozo hiyo inakadiliwa kuwa zaidi ya asilimia 40 hadi 45  watafungiwa simu zao na kudai takribani watanzania milioni nane hushindwa kuweka shilingi 1000 kwa mwezi katika laini zao za simu.

Tume iliyoundwa na Rais Kikwete kushughulikia suala hilo ilijumuisha wajumbe kutoka TRA,Wizara ya Fedha na wawakilishi wa kampuni za simu.

Julai 19 mwaka huu,Waziri wa Fedha,Dkt William Mgimwa alisema serikali imekubali kupitia mawazo na maoni ya MOAT kuhusu kufutwa kwa tozo hiyo ambayo imelalamikiwa na wadau wengi wa sekta ya mawasiliano.



Popular Posts

Labels