Tuesday, August 11, 2015

SHULE YA MSINGI MLIMANI KUNUFAIKA NA HUDUMA YA INTANETI YA BURE



Shule ya Msingi ya Mlimani iliyopo Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kuanzia wiki hii itaanza kunufaika na huduma ya intaneti bure inayofungwa shuleni hapo na Kampuni ya Vodacom Tanzania.

Akizungumza na waandishi wahabari Jijini Dar es salaam Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Upendo Kujerwa ameshukuru msaada huo na kusema kuwa ni muhimu na utawawezesha wanafunzi katika shule yake kuingia katikaulimwengu wa sayansi na teknolojia ya kompyuta.

Kujerwa amesema, sasa wataweza kumudu vizuri kusoma kwa kutumia kompyuta kwani sasa wataweza kupata elimu kwa nadharia na vitendo ikiwemo kupata maarifa kutoka kwenye mtandao wa intanenti.

Aidha amesema pamoja na athari za matumizi mabaya ya teknolojia, lakini ina mengi mazuri hivyo watahakikisha wanatumia msaada huu kuwapatia maarifa mazuri wanafunzi wao maarifa ambayo yatawafaa katika siku za usoni kwa kuwa miongoni mwa wataalamu wanaohitajika kwenye fani mbalimbali ilikuendeleza taifa.

Akizungumza kwa niaba ya wanafunzi wenzake, mwanafunzi Rose Mfinanga ameshukuru kwa msaada huo na kusema utawasaidia kujua somo la kompyuta na kupata maarifa kupitia mtandao wa intaneti.

Monday, August 10, 2015

FACEBOOK,TWITTER NA GOOGLE KUONDOA PICHA ZA UTUPU ZINAZOWADHALILISHA WATOTO



Programu ya Swetie inayowatambua watu wanaowadhalilisha watoto kingono

Kampuni kubwa zaidi duniani za mitandao ya kijamii Google,Facebook na Twitter zimekubaliana kuondoa picha za utupu katika mitandao yao.

Hii inafuatia kuenea kwa picha za utupu za watoto kwenye mitandao ya kijamii.

Mashirika hayo kwa ushirikiano na shirika la kijamii linalopigania haki za watoto 'Internet Watch Foundation' (IWF) sasa yameanza kuorodhesha picha za utupu wa watoto kwa nia ya kuziondoa.

Wakitumia mbinu mpya ya kufichua watu wanaoshiriki ngono na watoto , IWF inakusudia kukomesha kudhalilishwa kwa watoto.

Hata hivyo mbinu hiyo imekosolewa na wadau wa maswala ya mtandao wa intaneti ambao wanasema kuwa bado kuna mbinu fiche ya kusambaza picha hizo nje ya mitandao hiyo kubwa ya kijamii. 

Wakitumia mbinu mpya ya kufichua watu wanaoshiriki ngono na watoto wanalenga kuondoa mamilioni ya picha za utupu wa watoto mitandaoni
Mwaka uliopita waziri mkuu wa Uingereza David Cameron alionya kuwa shirika la kijasusi nchini humo litaanza ushirikiano na mashirika ya kijamii kukabiliana na kuenea kwa maeneo fiche kwenye mitandao ya intanet kwa nia ya kuwakamata watu wanaowadhalilisha watoto kingono.
Chanzo:BBC

Thursday, August 6, 2015

WANAHABARI WATAKIWA KUWA MAKINI NA HABARI KUHUSU UCHAGUZI WA MWAKA HUU





Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya kati imewataka watangazaji wa radio, luninga na mitandao ya kijamii kuwa makini na habari wanazotoa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu wa madiwani, wabunge na Rais. 


Rai hiyo imetolewa na Meneja wa TCRA Kanda ya kati, Maria Sasabo wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye maonyesho ya wakulima na wafugaji nanenane yanayofanyika katika viwanja vya Nzuguni mjini Dodoma. 


Amesema  vyombo vya habari nchini vinatakiwa kutoa haki sawa kwa pande zote mbili ili kuepusha mgongano wa kimaslahi unaoweza kujitokea kwa kutangaza habari za upande mmoja.


Kwa upande wa wananchi waliotembelea banda hilo walitoa akiwemo bwana Elieshiwakwe Malima amesema malalamiko yao kuhusiana na baadhi ya mitandao kuwatumia ujumbe mfupi wa maandishi kwenye simu zao za mikononi bila ridhaa yao. 


Aidha Malima ameiomba TCRA kuwadhibiti watangazaji hao na ikibidi wawe wanatumia namba zinazofahamika ili kama kuna mtu anataka kujitoa kwenye huduma hizo aweze kutumia namba husika kujitoa.






ZAIDI YA WATU MILIONI MBILI WAJIANDIKISHA KUPIGA KURA KWA MFUMO WA BVR JIJINI DAR ES SALAAM



Wapiga kura 2,845,256 wameandikishwa katika Daftari la Kudumu la Wapigakura kwa mfumo wa kielektroniki wa utambuzi wa mwili wa binadamu wa Biometric Voters Registration (BVR), mkoani Dar es Salaam.


Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Mstaafu Damian Lubuva, wapiga kura hao ni sawa na asilimia 101.2.

 Dar es salaam inaelezwa kuwa na wakazi wapatao 4,364,541 kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2012.


 Jaji Lubuva ametaja idadi ya walioandikishwa katika wilaya za jiji hilo hadi Agosti 04 mwaka huu na idadi yao kuwa ni Kinondoni 1,157,142 sawa na asilimia 105 wakati makadirio yalikuwa ni watu 1,101,565,Temeke lengo lilikuwa watu 896,142, lakini walioandikishwa ni 886,564 sawa na asilimia 98.9 wakati Ilala lengo lilikuwa 811,716, lakini  walioandikishwa ni 886,564 sawa na asilimia 98.9.


Kwa mujibu wa Jaji Lubuva, uwekajiwazi wa daftari la kudumu la wapigakura kwa mikoa iliyokwishapokea daftari utaanza Agosti saba na utadumu kwa siku tano.


Amesema lengo la uwekaji wazi huo ni kutoa fursa kwa wale wote waliojiandikisha kusahihisha taarifa zao, kuhamisha taarifa za wapiga kura waliohama toka kata au jimbo kwenda kata  au jimbo jingine kutoa kadi kwa wapiga kura waliopoteza kadi zao, kuangalia iwapo taarifa za mpiga kura aliyejiandikisha zipo kwenye daftari na kuweka pingamizi kwa jina au taarifa za mpiga kura asiye na sifa ya kuwamo katika daftari.

Saturday, August 1, 2015

KONGAMANO LA C2C LAKAMILIKA – USALAMA MITANDAO WAJADILIWA SIKU ZOTE MBILI

 Na Yusuph Kileo
Nchi ya Tanzania yabahatika tena kwa mara ya tatu kuwa mwenyeji wa mkutano wa “Connect 2 Connect” ambapo kauli mbiu ya mwaka huu imekua ni Kuunganisha bara la afrika mwambao hadi mwambao. Katika hotuba iliyotolewa siku ya kwanza katika ufunguzi wa mkutano huo ili elezea changamoto kubwa za usalama mitandao na namna unavyoweza kuleta athiri kwa kiwango kikubwa endapo usalama huu mtandao hautaangaziwa macho. Hotuba hiyo pamoja na mjadala nilio ongoza kwa siku ya kwanza unaweza kusomeka na kuonekana kwa “KUBONYEZA HAPA”.

Mkutano huu wa mara hii uliokusanya washiriki kutoka katika mataifa 30 duniani kote  ulihusisha wafanya maamuzi ya juu, watengeneza sera na wadau wengine kadhaa ambapo Mawaziri na Manaibuwaziri  wa Nchi kadhaa wkiwa ni miongoni mwa waliopata kuongoza mijadala pamoja na kuunganisha mawazo katika maswala mbali mbali ya barani Afrika.

Kongamano hili la mwaka huu lililoandaliwa kwa kushirikiana wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia  pamoja na kampuni ya simu ya TTCL limeonyesha mafanikio makubwa sana kwa kuwezesha kauli mbiu ya mwaka huu kufikiwa kwa kiasi kikubwa kupitia mijadala mbali mbali iliyo jadiliwa katia kongamano hili.

Mbali na mada nyingine mbai mbali – Kwa siku zote mbili za mkutano huu mijaadala mizito ya usalama mtandao ilipata kujadiliwa kwa kina ambapo nilipata bahati ya kuongoza mjadala wa siku ya kwanza na kuhutubia kwa siku ya pili juu ya maswala ya usalama mitandao. 

Katika hotuba yangu ya siku ya pili katika mkutano huu nilipata kuangazia hali ilivyo duniani kote na kueleza kwa kifupi kuhusiana na Mkutano mkuu wa mwaka ulioangazia maswala ya usalama mitandao jijini Johannesburg ambapo pia nilihutubia kwa niaba ya Bara la Afrika tulipo kutana wataalam wa maswala haya katika ngazi ya dunia. Zaidi niliweza kuainisha mapungufu makuu tuliyo nayo yanayo sababisha vita dhidi ya uhalifu mtandao kuenekana kutushinda kutokana na uhalifu huu mtandao kuendelea kushamiri.


Msisitizo mkuu niliotoa mbali na kuhimiza ushirikiano na kutumia vizuri wenye ujuzi na elimu hii ya usalama mitandao, Nilipata kuainisha makundi ma nne ambayo ni Mtu binafsi, kundi la Watu ( Wana usalama mitandao), Kampuni , pamoja na serikali na kueleza kuna dhana potofu inayo dhani makundi matatu kati ya hayo manne ndio yenye dhamana ya usalama mtandao na kusahau kabisa kua lazima usalama mtandao uanzie katika ngazi ya MTU BINAFSI.

Nikitolea hili ufafanuzi – Nilielezea mtu binafsi anakila sababu ya kuhakiki usalama wake uko vizuri kwa kuhakiki neno la siri “Password” Matumizi ya salama ya mitandao na kuhakisha kila hatua za kujilinda dhidi ya uhalifu mtandao kama ilivyo katika hali ya kawaida ya kulinda makazi yetu zina angaziwa vizuri kwani  jukumu la kulinda usalama mtandao si la kundi flani la watu pekee.

Nikiwa na waziri wa TEKINOHAMA - BURUNDi

Waziri wa TEHAMA wa Burundi katika mazungumzo yake mkutanoni na baadae tulipo kutana  kwa mazungumzo baina yetu alionyesha dhahiri matumizi mabaya ya mitandao hasa hii ya kijamii ilivyo changia kuyumbia taifa la Burundi huku akiendelea kutoa wito juu ya matumizi salama ya mitandao ya kijamii ili kuweza kuchochea usalama wa taifa lolote duniani – Katika kuumunga mkono nilimpatia mifano kadhaa ya Nchi kama Misri, Libya na nyinginezo ambazo ziliyumba na kuanguka huku sababu kuu ikiwa ni mitandao ya kijamii kuchochea fujo katika nchini hizo.

Niliwa na Waziri wa TEKINOHAMA -  LETHOSO

Nilifarijika kuona Nchi ya LETHOSO pamoja na NAMIBIA kuonyesha dhamira yao ya dhati ya kutaka kujifunza kutoka kwetu kwenye maswala haya ya usalama mitandao na kupongeza hatua nzuri tuliopiga hadi leo. Katika mazunungumzo yangu na Waziri wa TEHAMA wa LESOTHO alinieleza wimbi kubwa na matumizi mabaya ya mitandao nchini mwake ndio limeendelea kua kikwazo na ana mikakati ya kuandaa sera pamoja na sheria mitandao ili kuhakiki ana himili vishindo vya ukuaji wa matumizi mabaya ya mitandao.

Aidha, Kwa upande wa NAMIBIA – Mbali na kunipongeza walionyesha dhamira ya yadhati ya kufanyia kazi ushauri niliotoa katika mkutano huu, huku wakisisitiza kua wanaamini kabisa tatizo kubwa ni upungufu wa ukuzaji wa uelewa juu ya mambo ya usalama mitandao pamoja na serikali nchini afrika kutoona Usalama mitandao ni kipa umbele na wakisahau Uhalifu mtandao unauwezo mkubwa wa kuangusha taifa lolote.


Mwisho, Nitoe wito kwa serikali ya Tanzania na wadau mbali mbali kutambua athari kubwa katika Nyanja zote kuanzia kiuchumi hadi kisiasa zinazoweza kuonekana kama usalama mtandao hauta angaziwa macho ipasanyo. Wakati huu tukiwa tunaelekea uchaguzi mkuu lazima tujue mitandao ya kijamii inaweza kabisa kuyumbisha taifa letu hivyo hakuna budi kuwa na umakini madhubuti katika hili. Tayari nimesha lizungumzia hili mara kadhaa na zaidi unaweza kupitia Andiko linalosomeka kwa “KUBOFYAHAPA”

USHIRIKIANO NI MUHIMU KATIKA UTHIBITI WA UHALIFU MTNDAO

Itakumbukwa Mwishoni mwa mwezi wa tano mwaka huu katika hotuba yangu niliyo iwasilisha kwa wanausalama mitandao tulipo kutana  jijini Johannesburg mbali na mambo mengine nilihimiza sana ushirikiano baina yetu kwani wahalifu mtandao wameendelea kua mbele yetu kutokana na ushirikiano mkubwa waliokua nao. Ushirikiano unao mabatana na kusambaza vitendea uhalifu mtandao bure auu kwa gharama nafuu mitandaoni.

Baada ya kulizungumza hili laushirikiano wazungumzaji wengine wote walionekana kuniunga mkono na hatimae kuonekana ni swala muhimu lakufanyiwa kazi mapema. Nafarijika kuona Uingereza tayari mukuu wake wa CERT ametilia mkazo kauli hii (Ya ushirikiano) kupitia kikao kilicho malizika London ambapo taarifa kamili kuhusiana na hili inaweza kusomeka kwa “KUBOFYA HAPA”

Aidha, Marekani na Israel baada ya kutia saini makubaliano ya kuboresha ushirikiano katika maswala ya usalama mitandao paliambatana na kuhimiza mataifa mengine kuona umuhimu wa kushirikiana katika vita hii ya uhalifu mtandao.

Nilipata kuzungumza tena katika mkutano wa wanausalama Nchini Cyprus ambapo pia nilizungumza kwa mara ya kwanza kuhusiana na ushirikiano huku nikipongeza umoja wa ulaya kwa kuungana kwao katika hili la usalama mitandao kupitia chombo chao kiitwacho ENISA kinacho hudumia mataifa yote yaliyo ndani muungano wa nchi za ulaya katika maswala ya Usalama mitandao.

Tayari kume endelea kuonekana jitihada mbali mbali zikifanyika kupitia majukwaa yetu ya kimtandao ambapo tunajadili mambo mbali mbali na kuu limekua kukumbushia ushirikiano huku wengi wakionekana kuelezea wazo hili la ushirikiano nililo litoa mkutanoni limeendelea kusikilizwa na mataifa makubwa huka mataifa mengine yakihamasishwa kuiga mfano.

Tanzania kumekua na Kauli kama Umoja ni nguvu, Kidole kimoja hakifunji chawa, Umoja ni ushindi na nyinginezo zinazo hamasisha ushirikiano katika nyanja mbali mbali lakini katika hili la kuunganisha nguvu katika maswala ya uthibiti wa uhalifu mtandao bado naona safari ni ndefu.

Nalisema hili kwa sababu bado uhalifu mtandao unaendelea kukua na ki uhalisia vitengo vinavyo husika na hili nchini bado vimekua havionekani kuungana na kua na uwezo mmoja madhubuti kwa kuhimili uhalifu huu. Kuungana ninaotegemea mimi ni pamoja na kushirikiana katika taarifa, Vitendea kazi pamoja na wataalam ambapo kwa ujumla wake yote matatu yame gawanywa inayopelekea kuto onyesha matunda tegemewa.

Nitatolea mfano uhalifu mpya uliokuja kwa kasi nchini na wengi wamonekana kuathirika huku athari ya uhalifu huu baada ya kujaribu kujadiliana na wngine wameweza kueleza athari kubwa ipo kwa Tanzania na isipo angaziwa baadae inaweza kuibua uhalifu mwingine ambao utakua ni matunda ya huu ulioko sasa na pengine kua na madhara makubwa sana kwa taifa kiujumla.

Nitoe wito katika hili kwa watumiaji wa mitandao ya kijamii kufahamu ya kua hawana buni kuhakiki wanaendelea kua na tabia ya kujijengea ulinzi katika ngazi ya mtu binafsi mtandaoni huku wakiwa makini sana na kutafakari sana kabla ya kuandika “THINK BEFORE YOU INK” huku umakini na kubadilisha maneno ya siri kua ni moja ya tabia ya watumiaji mitandao kwani neno la siri madhubuti na linalo badilishwa itakikanapo husaidia kuzuia uhalifu wa udukuzi.

Matumizi salama ya mitandao ya kijamii na kutambua utumiapo mtandao wa kijamii kusemea wengine vibaya au kutumia lugha zisizo rafiki kwa wengine inasababisha uhalifu aina ya Cyberbulling ambao umeendelea kugharimu sana uhai wa watu duniani kote.kuendelea kuangaza macho kwenye mifumo yetu yote ya digitali pia ni muhimu sana kwani ukuaji wa matumizi ya digitali katika maisha yetu lazima tujue yanakuja na changamoto za ukuaji wa uhalifu mtandao hivyo hatuna budi kuongeza umakini katika usalama mitandao.

Faragha zetu katika mitandao ya Kijamii nazo ni zakuangaliwa sana kwani baadhi ya malalamiko ya kihalifu mitandao inatokana na faragha kua na mapungufu ambapo inatoa fursa kwa wahalifu mtandao kupata taarifa za watu binafsi mitandaoni kirahisi sana. Hili linapelekea wengine kutumia mapungufu hayo kutengeneza mitandao ya kijamii feki yenye taarifa za watu wengine na picha zao walizo zipata kupitia mitandao ya kijamii iliyo wazi (faragha dhaifu).
Na:Yusuph Kileo

POSTA NCHINI YAELEZA UMUHIMU WA MATUMIZI YA TEKNOHAMA



Imeelezwa kwamba kadri teknolojia inavyoongezeka, inatengeneza fursa ya kukua kwa Shirika la Posta Duniani.

Hayo yamesemwa na Kaimu Mkuu wa Shirika la Posta nchini, Fortunatus Kapinga wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ukuaji wa Teknolojia.

Kapinga amesema  kuwa teknolojia inaleta fursa na sio tishio ila inategemea imetumiwaje katika eneo husika na kuongeza kuwa biashara ya mtandao imeimarisha biashara ya shirika hilo ikiwa ni pamoja na kutoa teknolojia mpya.

Aidha amesema kutokana na kuongezeka kwa biashara ya mtandao barani Ulaya, mapato yamekuwa kwa asilimia 1.4, Asia na Amerika ya Kaskazini asilimia 3.9 na ameongeza kwa kusema kuwa shirika limefanikiwa kutekeleza miradi mbalimbali ya matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano(Teknohama) ili kuongeza ubora wa huduma zake.

Popular Posts

Labels