Mtu mmoja ambaye alijitambulisha kwa cheo cha Katibu wa Usaili Idara ya Uhamiaji Dr Mawazo Kaburugu anatafutwa na idara hiyo kwa tuhuma za kutoza watu sh 10,000 kwa njia za udanganyifu.
Mtu huyo ambaye alifanikiwa kutuma ujumbe kwa watu zaidi ya 900,wanaotaka kufanyiwa usaili kwenye idara ya Uhamiaji,anadaiwa kupata kiasi kikubwa cha fedha kutokana na ujumbe aliokuwa akutuma kwa watu hao.
Ujumbe huo ulisomeka "Habari ndugu,pongezi kwa kuitwa kwenye usaili kuanzia tar 9/6.Idara ya uhamiaji inakufahamisha kuwa unatakiwa kulipa sh 10,000 na haitarejeshwa kama gharama za usaili vikiwamo vitambulisho pekee ndio wataruhusiwa kuingia ukumbini,malipo yote yatumwe kwa tigo pesa kwenye namba 0715 54 62 81 kuanzia tarehe 26 hadi 30,kisha tuma sms yenye code za Tigopesa na jina lako kamili,imetolewa na Kamishna Dr Mawazo Kaburugu Katibu wa Usaili".
Mwandishi wa gazeri la Raia Tanzania aliwasiliana na mtu huyo ambapo alieleza kuwa wote ambao wameitwa kwenye usaili watume fedha hiyo kama ujumbe ulivyotolewa na kuongeza kuwa pesa hiyo inahitajika haraka sana ili iweze kufanyakazi iliyokusudiwa kwa ajili ya usaili.
Kaimu Mtendaji wa Idara ya Uhamiaji,Tatu Bruani amesema mtu huyo ni tapeli na ambao wametumiwa ujumbe wasitume pesa hizo.
Chanzo:Gazeti la RaiaTanzania
Popular Posts
-
Mamlaka ya Mawasilino Tanzania, TCRA, imesema watumiaji wa namba za simu ambazo hazikusajiliwa, watakatiwa mawasiliano ifikapo Juni M...
-
Polisi kanda maalumu ya Dar es salaam wamezungumzia utapeli unaofanywa kwa kutumia simu za mkononi na kusema wengi wanaofanya hivyo husajili...
-
Google I/O ni kongamano linalofanyika kila mwaka California kwa kuwakutanisha Developers wa bidhaa za Google kama Android , Chrome , Chrom...
-
Afisa wa Taasisi ya uwezeshaji na ujengaji uwezo kwa wateknohama nchini KINU, Catherinerose Barretto akimkabidhi cheti Ally Said toka P...
-
Picha na Salim Kikeke Kuanzia sasa kudanganya kwamba mtu hakupata ujumbe wako wa WhatsApp itakuwa historia, au kud...
-
Microsoft is switching off its Windows Live Messenger service on 15 March. On that date Messenger log-ins will no longer work a...
-
Mwezeshaji wa kipindi cha Maisha na Teknohama cha Morning Star Radio,Johnson Mziray akichangia jambo kwenye warsha hiyo,pembeni yake mweny...
-
Idadi ya watu wanaotumia huduma ya mtandao wa Intaneti nchini Tanzania imeongezeka kutoka watu 26,000 mwaka 2000 hadi kufikia watu mili...
-
Masomo kwa njia ya mtandao(Online Studies) kwa miaka ya hivi karibuni yamekuwa yakitolewa bure na baadhi ya Vyuo Duniani. Mfano katika...