Wednesday, September 30, 2015

MAONYESHO YA TEKNOHAMA KWA WANAFUNZI YAFUNGULIWA JIJINI DAR ES SALAAM

http://dewjiblog.com/wp-content/uploads/2015/09/IMG_3142.jpg
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Profesa Sifuni Mchome akizungumza kabla ya kuzindua rasmi maonesho ya Tehama yanayoendelea katika ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
IMG_3000
Kamishina wa Elimu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Eusella Bhalalusesa akizungumza kabla ya kumkaribisha Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Profesa Sifuni Mchome kuzindua maonesho ya Tehama  yanayoendelea katika ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

Serikali ya Tanzania imeeleza kuwa jumla ya  wanafunzi 60,000 katika shule 150 nchini humo wamepitiwa na mafunzo ya programu ya Bridge IT yenye lengo la kuongeza ubora wa elimu kwa kutumia teknolojia ya kisasa ya kidijiti (digital technology) katika ufundishaji na ujifunzaji wa Hisabati,Sayansi na Stadi za Maisha.

Kamishina wa Elimu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Eusella Bhalalusesa ameeleza hayo wakati akimkaribisha Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Profesa Sifuni Mchome kuzindua  maonesho ya Tehama.

Amesema  kutokana na mafanikio yaliyotokea sasa wanatanua wigo baada ya kuwezeshwa kifedha na Shirika la Kimataifa la Maendeleo ya elimu (Global Partnership For Education) kwa ajili ya kuendeleza teknolojia hiyo katika kujifunza na kufundisha katika shule za msingi na hasa darasa la awali la kwanza hadi la nne.

Maonesho hayo yanayofanyika katika ukumbi wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere yana lengo la kuonesha ubunifu ambao upo tayari kutumika kufanikisha  mafunzo hayo.

Pia maonesho hayo yanatarajia kujadili na kuangalia mbinu za kielektroniki zitakazoweza kuendana na mazingira ya Tanzania katika ufundishaji na kujifunza kwa gharama nafuu.

Pia wanatarajia kuangalia utayari wa walimu na namna ya kuwabadilisha mtazamo ili waweze kufundisha na kufundishika.

Katika maonesho hayo serikali imesema inatarajia kuanza kutumia rasmi Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tekinohama) katika kufundishia wanafunzi kuanzia ngazi ya chini kabisa ya elimu ambayo ni chekechea.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Sifuni Mchome alisema matumizi ya Tehama katika ufundishaji wa wanafunzi wa chekechea yataimarisha kiwango cha elimu.

IMG_3089
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Profesa Sifuni Mchome akifuatilia kwa makini risala Kamishina wa Elimu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Eusella Bhalalusesa (hayupo pichani).

IMG_3160
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Profesa Sifuni Mchome akijianda kuzindua rasmi maonesho ya Tehama yanayoendelea katika ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
IMG_3161

IMG_3214
Ofisa Miradi  ya Elimu kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Faith Shayo akitoa maelezo ya shughuli mbalimbali zinazofanywa na shirika lake katika kuendeleza sekta ya elimu nchini kwa Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Profesa Sifuni Mchome (kushoto) mara baada ya kuzindua maonesho hayo ambapo pia UNESCO inashiriki. Katikati ni Kamishina wa Elimu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Eusella Bhalalusesa.
IMG_3217
Ofisa anayeshughulikia masuala ya Elimu Kitaifa wa UNESCO, Tumsifu Mmari (katikati) akimsikiliza mmoja wa wadau wa elimu aliyetembelea banda la UNESCO kwenye maonesho ya TEHAMA yanayoendelea katika ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Ofisa Miradi  ya Elimu kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Faith Shayo.
IMG_2982
Ofisa anayeshughulikia masuala ya Elimu Kitaifa wa UNESCO, Tumsifu Mmari (kulia) akiwa na wadau wengine wa elimu wakipitia makbrasha mbalimbali katika mkutano huo.
IMG_3006
Pichani juu na chini ni baadhi wadau wa elimu waliohudhuria uzinduzi wa maonyesho hayo.
IMG_3004
IMG_3028
Baadhi ya wanafunzi kutoka shule mbalimbali za msingi jijini Dar walioshiriki hafla hiyo.
IMG_3105
Mkurugenzi Mkuu wa Shule Direct, Faraja Nyalandu akipozi na wadau kwenye ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere jijini Dar es Salaam yanakoendelea maonesho ya TEKINOHAMA

Thursday, September 24, 2015

DAR ES SALAAM:BASATA LATAKA KUONDOLEWA/KUSITISHWA MARA MOJA KUCHEZWA KWA NYIMBO ZOTE ZILIZOKINYUME CHA MAADILI, SHERIA NA TARATIBU



 
Baraza la Sanaa la Taifa nchini Tanzania (BASATA) limetoa siku saba kwa wasanii,vituo vya radio,runinga wamiliki wa tovuti na wale wenye wasifu kwenye mitandao ya kijamii kuondoa nyimbo zote au maudhui yenye muelekeo unaoenda kinyume na maadili,  matusi  na kashfa mbalimbali.

Taarifa ya BASATA iliyotiwa saini na Katibu Mtendaji wa Baraza hilo Godfrey Mngereza imevitaka  pia vyombo vya habari zikiwemo radio na luninga kuondoa na kuacha mara moja kucheza au kurusha nyimbo zote zenye maudhui hayo.

Mngereza amesema maudhui ya kashfa,matusi,kejeli,udhalilishaji zinatishia kuigawa jamii ya watanzania katika kipindi hiki ambacho taifa linaendelea na kampeni za kujiandaa na uchaguzi mkuu tarehe 25 mwezi wa kumi mwaka huu.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa  kifungu namba 118 [a-d] cha sheria ya bunge namba 9 ya mawasiliano ya mtandao ya mwaka 2010 vinaelekeza kuwa ni marufuku kwa njia yoyote kwa mtu au chombo chochote kutengeneza ujumbe ambao unamlengo wa matusi ,dharau,uzushi au jinai kwa lengo la kutukana ,kutisha, kusumbua au kushusha hadhi  ya mtu mwingine.



WIZARA YA ULINZI YA UINGEREZA YATOA NGUO ZA WANAJESHI WAKE ZENYE MFUMO WA KISASA WA MAWASILIANO




Wizara ya Ulinzi wa Uingereza imetoa Nguo za kisasa kwa ajili ya wanajeshi wake wa miaka ijayo . Picha unayoiona ni mfano wa nguo hizo na huo ni ubunifu wa njia ya kompyuta,mradi huo unaitwa Future Soldier Vision kwa ufupu FSV .

Taarifa zinasema nguo hizo zitakuwa na mfumo wa kisasa wa mawasiliano na mfumo wa biometriki ambao utamfanya mwanajeshi wa Uingereza kuwa salama zaidi kushinda wakati wowote atakapokua kwenye uwanja wa vita .

Katika vita upande wenye taarifa nyingi ndio huwa na uwezekano wa kushinda kwa urahisi . FSV ni mpangilio wa vifaa vya kisasa vya mawasiliano na silaha zinazovaliwa mwilini mwa mwanajeshi . kutakua na sensa itakayowezesha wanajeshi wote kujuana wakiwa uwanja wa vita au kokote bila kuchanganyana , mfumo wa mawasiliano ambao utaweza wanajeshi kutumiana taarifa kwa mfumo wa picha , sauti na video .

Wakati wizara imetoa mchoro huu wa ubunifu na kuuelezea , kampuni , taasisi na watu binafsi wameanza utafiti ambao utawezesha kutengeneza vifaa vingi vitakavyofanya kazi sambamba na wanajeshi hao muda ukifikia kwa ajili ya soko la ndani ya Uingereza na maeneo mengine ulimwenguni.

KAMPUNI YA APPLE KUANZA KUUZA MAGARI YA YAKE YANAYOTUMIA UMEME IFIKAPO MWAKA 2019

 

Baada ya kuwepo kwa uvumi wa kipindi kirefu kuwa kampuni ya Apple inampango wa kutengeneza magari yake hatimaye siri zimeanza kuvuja.  

Kulingana na ripotI iliyochapishwa katika tovuti ya The Wall Street Journal, vyanzo vya kuaminika kutoka kampuni hiyo inayofanya vizuri katika vifaa vya teknolojia za mawasilianio na elektroniki, vimesema kuwa kampuni hiyo itaanza kuuza magari yake yanayotumia nishati ya umeme ifikapo mwaka 2019.

Licha ya kuwepo na kampuni nyingine nyingi kama Tesla ambazo tayari zinatengeneza magari yanayotumia nishati ya umeme, Apple imedhamiria kujiingiza katika biashara hiyo.

Je, wataleta mapinduzi yoyote kama yale waliyo fanya katika Kompyuta na simu za kiganjani?

Tuesday, September 22, 2015

SERIKALI YA TANZANIA YAVITAKA VITUO VYA RADIO NA TV KUEPUKA KURUSHA HABARI ZA UCHOCHEZI



Mkurugenzi  Mkuu wa TCRA Dr Ally Simba
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), imevitaka vituo vya redio na televisheni nchini Tanzania kuepuka kurusha habari za uchochezi hasa katika kipindi hiki cha kampeni kuelekea uchaguzi mkuu.
Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Dk. Ally Simba ameeleza kuwa  vyombo vya habari vinatakiwa kuepuka kurusha na kuandika habari zitakazochochea vurugu na uvunjifu wa amani kwan jamii ina imani kubwa na vyombo vya habari na waandishi wa habari, hivyo hawana budi kutumia weledi katika utoaji wa taarifa katika kipindi hiki cha kampeni kuelekea uchaguzi mkuu.

Radio 106 na televisheni 28, zimesajiliwa nchini Tanzaia na kwamba katika kuelekea uchaguzi mkuu, tayari vituo vitano vya televisheni vimekuwa na makosa yaliyosababisha kupewa adhabu na onyo.

MICROSOFT YAWATAKA WATUMIAJI WA KOMPYUTA KUTUMIA PROGRAM ZENYE VIWANGO


 

Kampuni  ya Microsoft imesema kuwa watumiaji wa program za kompyuta, wanapaswa kutumia program zenye viwango na kujiepusha na zisizo na viwango.

Akizungumza hii leo katika mkutano wa matumizi ya program za kompyuta,Afisa mtendaji na msimamizi wa Hakimiliki wa COSOTA, Dorine Sinare amesema kuwa, kutumia program za kompyuta zilizo bora zitasaidia kuepuka uharamia katika mitandao na serikali kuweza kuongeza mapato yaliyotokana na program hizo.

Dorine amesema kuwa wameanza kushirikiana na Microsoft katika kuweza kutoa elimu juu ya matumizi ya program ambazo halisi na kuachana na ambazo si halisi kwani zinaweza kuharibu program zingine.

Njiru ameongeza kuwa Microsoft inafanya kazi katika kuhakikisha watu wanapata mawasiliano yenye kiwango kutokana na utoaji wa huduma za program za komputa zenye kiwango.

ARUSHA:TCRA YASEMA BADO KUNA MATATIZO YANAYOTOKANA NA WATUMIAJI WA MAWASILIANO


 

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA) Dr. Ally Yahaya Simba(Pichani),amesema pamoja na mafanikio katika sekta ya mawasiliano nchini Tanzania lakini bado kuna matatizo  yanayojitokeza ikiwemo ukiukwaji wa kwa sheria za mawasiliano.

Ameyasema hayo jijini Arusha alipofanya ziara yake fupi ya utambulisho katika kanda ya kaskazini huku kaiwataka wadau wa mawasiliano na vyombo vya Habari nchini kumpa ushirikiano ili kuboresha sekta hiyo katika kipindi cha uongozi wake.

Dr. Ally Simba amesema pamoja mafanikio yaliyopo katika sekta ya Mawasiliano nchini lakini bado kuna matatizo yanayojitokea kutokana na  watumiaji wa huduma ya mawasiliano ikiwemo ukiukwaji wa masharti ya leseni na matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii.

Aidha amewapongeza wadau wa Mawasiliano na vyombo vya habari kwa kuzingatia sheria na kanuni za utoaji wa Habari na utangazaji katika msimu huu wa kampeni za uchaguzi mkuu.



Friday, September 18, 2015

NDEGE MAALUM ZISIZO NA RUBANI SASA KUTUMIKA KUPAMBA NA UJANGILI NCHINI TANZANIA

Ndege isiyotumia rubani aina ya Super Bat DA-50 katika majaribio.Ndege hii na nyingine nyingi zitatumika katika kuimarisha vita dhidi ya ujangili nchini.Zitakuwa zinaruka katika maeneo mbalimbali ya Mbuga za wanyama,misitu na meeneo mengine kuimarisha usalama wa wanyama

 
 


Natumaini umeshasikia kuhusu ndege ambazo hazina rubani maarufu kama drones.

Kwa siku za karibuni zimekuwa maarufu kwani zinatumika kupeleka misaada mbalimbali hata katika maeneo hatari ya vita ambako hakufikiki kirahisi.


Nchini Tanzania tumeanza kuitumia teknoloia hii yanaweza kuwa maendeleo mengine mapya.

 Phil Jones ni ofisa mwendeshaji wa mitambo  kutoka kampuni ya MartinUAV ya Marekani iliyotengeneza ndege hiyo aina ya Super Bat DA-50 UAV 

Ndege hiyo  haihitaji kuwa na rubani, inaongozwa kwa kompyuta maalum, ina antenna mbili, ina kamera maalum ambazo zinaweza kupiga picha usiku na hata mchana.

Akasema ndege hiyo ina uwezo wa kuruka urefu wa futi 20,000 kutoka usawa wa bahari na kwenda katika nusu kipenyo cha kilometa 35 kutoka ilipo mitambo ya kuiongoza.

Jones, ambaye ni rubani wa zamani wa ndege za kijeshi katika Jeshi la Uingereza aliyestaafu mwaka 2014 ambaye kwa sasa anaishi nchini Marekani, anasema ndege hiyo inayorushwa kwa mtindo wa manati (catapult launch system), inaweza kuruka mfululizo kwa muda wa saa 10 ikiwa angani kabla ya kutua na kujazwa mafuta tena hivyo ni rahisi kubaini kama kuna majangili.


Ndege hii inatua kama ndege za kawaida , tofauti yake tu yenyewe haina magurudumu. Naam, unaweza kuwa ufumbuzi mwingine wa kupambana na ujangili nchini, tatizo ambalo haliko Tanzania tu, bali katika nchi nyingi barani Afrika.


Taasisi mbalimbali za ndani na nje zikiwemo serikali za mataifa makubwa zimekuwa zikijitahidi kusaidia mapambano hayo kama alivyofanya Rais Barack Obama wa Marekani alipoahidi kutoa Dola milioni 10 (sawa za Shs. 20 bilioni) ili kuimarisha mapambano hayo nchini.


Takwimu zinaonyesha kuwa Bara la Afrika mwaka 1930 lilikuwa na tembo 50 milioni na kwamba hadi kufikia mwaka 2013 tembo waliobakia katika bara zima ni  500,000.

Wednesday, September 16, 2015

SIKILIZA ALICHOSEMA KAMANDA WA JESHI LA POLISI KIKOSI CHA USALAMA BARABARANI KUHUSU TOZO KWA NJIA YA KIELEKITRONIKI


 
Jeshi la Polisi kikosi cha usalama barabarani mkoani Dar es salaam limeanzisha kanuni ya tozo la papo kwa hapo kwa njia ya kielektroniki na kanuni ya kuweka nukta katika lesseni za udereva.

Kamanda wa Polisi kikosi cha usalama barabarani Mohamed Mpinga ameeleza leo kuwa hii ni  kutokana na kuongezeka kwa malalamiko toka kwa wamiliki wa magari na madereva  kulipishwa faini na askari barabarani pasipo kupewa risiti halali za serikali 
Maelezo ya Kamanda Mpinga yote yako hapa

Monday, September 7, 2015

KIOTA KIPYA CHA BIASHARA MTANDAONI - MAVAZI STORE



 Kampuni ya ConnectMoja Technologies  Wamezindua tovuti mpya iitwayo Mavazi Store (www.mavazi.co.tz)  ambayo inajumuisha Mkusanyiko wa maduka mbalimbali ya mavazi ya aina zote mtandaoni. 




Kwa Mujibu wa Meneja Chapa ambaye pia ni Ambasador wa Mavazi Store bwana  Steve Seducter   mfumo huu wa kisasa umelenga  Kuondoa kero ya kutafuta bidhaa mbalimbali zinazohusiana na Urembo pamoja na Mavazi, pia kuwaokolea muda wateja  kwa kuunganisha  maduka Mengi zaidi kupitia tovuti hii ya www.mavazi.co.tz  .  Mtu yeyote mwenye simu ya kiganjani au kupitia katika kompyuta yake ataweza kutembelea Tovuti hii na kuona biashara zilizosajiliwa pamoja na Bidhaaa wanazouza. Hii itamuwezesha kuchagua  na kuwasiliana na duka husika Moja kwa moja alipo (Delivery),



Muonekano wa Tovuti ya MavaziStore  (www.mavazi.co.tz)
Pamoja na mengine Mtafiti wa Masoko na ukuaji wa biashara Bwana Fred Crich  alifafanua kwamba  kwa Sasa ConnectMoja Technologies imejikita kusaidia ukuaji wa biashara mbalimbali za kitanzania, na kuhakikisha kwamba Maendeleo yanayotokea katika Dunia hasa kupitia teknolojia yanaipa Manufaa pia jamii yetu ya Kitanzania. Crich Ameongeza kwamba  Kwa Kampuni inatoa Ofa kwa wamiliki wa maduka kutangaza katika Tovuti hii Bure kwa Mwezi Mmoja  ili kuwafikia zaidi wateja walio wengi. Ili Kutangaza Nasi Tembelea  http://mavazi.co.tz/advertise/  au Wasiliana nasi kwa Simu   0777880007  au 0714215 600  :  Office:  Oysterbay – Dar free Market Mall (GL14)

Imetolewa na  Kitengo Cha Masoko – ConnectMoja Technologies Limited



Sunday, September 6, 2015

TWEET YA SIKU

Katika ukurasa wake wa twitter Mhe Zitto Kabwe ametweet "Asanteni sana Wauza Mawese leo kwenye uzinduzi wetu Kigoma Mjini.
 
 Mpaka saa 5:15 usiku tayali ilikuwa imesambazwa mara 15  huku ikiwa imependwa mara  23.

Saturday, September 5, 2015

SAMSUNG NA MIT KUTENGENEZA BETRI ZA SIMU ZINAZOTUNZA NISHATI YA UMEME KWA MUDA MREFU


 Samsung And MIT’s “Indefinite” Battery Lifetime

Huenda umekuwa ukikumbana na tatizo la betri za simu hizi za kisasa kuisha nguvu yake ya nishati ya umeme  mapema yaani kuisha chaji,watumiaji wengi wanadai kuwa simu za kisasa kuwa na program tumishi nyingi zinazfanyakazi kwa wakati mmoja yaweza kuwa ni sababu ya kuisha kwa betri katika simu za kisasa.

Tatizo hili huenda likapata ufumbuzi kwa sababu kampuni ya simu ya Samsung  kwa kushirikiana na Taasisi ya Teknolojia  Massachusetts (MIT) wameanza mpango mkakati wa kutengeneza betri za simu zisizokwisha uwezo wake wa kutoa nishati ya umeme katika simu.
Pia watafiti wanaendelea na utafiti utakaowezesha kuchaji simu za kisasa  kwa kutumia teknolojia ya WiFi.

Kwa kawaida betri ya simu imeundwa kwa vitu vitatu moja ni kimiminika kiitwacho electrolyte,wanasayansi wamegundua njia ambayo itasaidia kuunda betri iinayotumika muda mrefu kwa kutengeneza electrolyte ambayo haiko katika hali ya kimiminika.

Njia itasaidia kuondoa tatizo la betri kuisha chaji na kuzimika kwa simu.

PROGRAM TUMISHI YA KUPAMBANA NA UBAKAJI KUZINDULIWA NCHINI DRC MWAKA UJAO



MediCapt App

Shirika la kujiolea la nchini Marekani linalojihusisha na utabibu na masuala ya haki za binadamu (PHR) limetengeneza program tumishi mpya ambayo itawasaidia kupata haki za kisheria  watu waliothirika na ubakaji huko Jamhuri ya Demokrasia ya Congo (DRC).

Umuhimu wa kutengenezwa program tumishi hiyo ulianza kuonekana mwaka 2011 baada ya ripoti ya Umoja wa Mataifa kuonesha kuwa  wastani wa wanawake 48 walibakwa kila baada ya saa moja kati ya mwaka 2006 na 2007 .

Taarifa hiyo inaonesha kuwa maeneo ya vijijini huko DRC  yamekuwa yakishikiliwa na waasi ambapo waasi hao wakati mwingine wamekuwa wakichoma nyumba,kuwachukua watoto na kuwabaka wanawake.
Kutokana na hali hiyo kumekuwa na tatizo la ukusanyaji na upatikanaji wa taarifa za matukio hayo ya kuwadhalilisha watoto na wanawake katika maeneo hayo yanayokaliwa na waasi nchini humo.

PHR imekubali kushirikiana na umoja wa mataifa  na hivyo imetengeneza program tumishi iitwayo MediCapt.Ni program tumishi ambayo itakuwa na uwezo wa kupeleleza na kutunza taarifa za udhalilishaji huo na kutoa taarifa kwa wataalamu wa afya kuhusu uharifu huo wanaofanyiwa wanawake nchini humo tofauti na awali ambapo walikuwa wakitumia taaarifa za kuuliza tu.

Program tumishi hiyo itakuwa na uwezo wa kupiga picha na kuhifadhi taarifa za tukio hata kama hakuna  na mtandao wa intaneti na kutuma taarifa hizo katika kituo cha kukusanya data.Kwa sasa tayali wataalamu wa teknohama watakaoratibu program tumishi hiyo inayotumika kwa simu zenye mfumo endeshi wa androd wako nchini DRC katika kuhakikisha inaanza kutumika mapema mwakani.

Popular Posts

Labels