Wednesday, April 8, 2015

UTAFITI:SIMU ZINACHANGIA UMASKINI NA MIGOGORO KATIKA MAHUSIANO


 
Wataalamu wa Saikolojia kutoka Chuo Kikuu cha Pennsylvania na Chuo Kikuu cha Vijana cha Bringman nchini Marekani wamebaini kuwa matumizi ya simu ni chanzo cha kutofurahia maisha na kuongeza msongo.
Utafiti uliofanywa na wataalamu hao chini ya usimamizi wa Brandon McDaniel,Mkufunzi kutoka Chuo Kikuu cha Pennsylvania,ulibainisha kuwa watu wengi wanaongeza umaskini wa kujitakia kwa kutumia muda mwingi kwenye simu.
Wanazungumzia maisha ya watu,mafanikio yao,kushindwa kwao badala ya kuangalia vitu vitakavyowaingia fedha zaidi,inaeleza sehemu ya utafiti huo.
Utafiti huo ulibainisha kuwa mbali na umaskini wa kujitakia,matumizi ya simu kupita kiasi huchangia kwa asilimia 75 ndoa kuvunjika pia hatari ya kupata msongo wa mawazo.
Utafiti huo uliohusisha watu wazima 867 wenye umri wa miaka 30 hadi 45,ulibainisha kuwa kama wasingekuwa na simu,robo tatu ya watu hao wangekuwa wamefanya mambo mengi kuboresha maisha yao ikiwemo utendaji bora wa kazi.
Majibu ya utafiti huo yalionesha kuwa wanandoa wengi wangepata muda wa kujadili namna ya kumaliza tofauti zao,kufikia mafaniki,kutimiza malengo hata kuboresha penzi kama wasingetumia simu.
Takwimu za Mamlaka ya Mawasiliano nchini Tanzania (TCRA) zinaonesha kuwa mwaka 2014 kulikuwa na laini za simu za mkononi zipatazo 31,862,656,ikilinganishwa na laini 2,963,737 mwaka 2005,watumiaji wa intaneti wameongezeka hadi kufikia 11,000,000 Desemba mwaka 2014 kutoka 3,563 waliokuwepo mwaka 2008
Chanzo:Gazeti la Mwananchi

Thursday, April 2, 2015

DAR ES SALAAM:MATANGAZO YA TV YA ANALOJIA MWISHO JUNI 17,2015 NCHINI



Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA) na Shirika la umoja wa mataifa la Mawasiliano ya simu ulimwenguni ITU kwa  pamoja wameridhia makubaliano ya kusitisha Mfumo wa utangazaji wa televisheni unaotumia teknolojia ya analojia  katika miundombinu ya minara ifikapo juni 17,2015 na kuanza kutumia mfumo wa utangazaji wa kidijitali pekee.


Akizungumza na waandishi wa habari  hii leo jijini Dar es salaam Meneja mawasiliano wa TCRA Innocent  Mungy  amesema  makubaliano hayo ya jumuiya za ushirikiano wanchi mbalimbali zimechukua hatua za pamoja kuhakikisha uhamaji kutoka mfumo wa utangazaji wa anolojia kwenda dijitali unafanikiwa.


Mungy amesema Tanzania imekuwa nchi ya kwanza kutekeleza maazimio ya nchi wanachama na uzimaji wa mitambo ya televisheni inayotumia teknolojia ya analojia  Tanzania Bara ilianza kufanyika desemba  31,2012 .

Amekuwa Mamlaka kwa kushirikiana na Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Wizara ya Habari Utamaduni na michezo na  wadau wengine itaendelea kutoa elimu kwa umma ili kuhamasisha uhamaji pamoja na kuwaelewesha watumiaji haki zao za msingi.  

KAMATI YAPENDEKEZA SERIKALI KUONGEZA ADHABU KWA WATAKAOTUMA TAARIFA ZA UONGO KWENYE MITANDAO

Kamati ya kudumu ya Bunge ya miundombinu imependekeza kwa serikali iongeze adhabu ya faini kutoka shilingi milioni tatu na kifungo kisichopungua miezi sita na kuwa faini ya shilingi milioni tano na kifungo kisichopungua miezi sita kwa wale wote watakaotuma katika mtandao taarifa za uongo.

Aidha kamati hiyo ilipendekeza katika adhabu kwa watu wanaonyanyasa wenzao kupitia mtandaoni adhabu yao iongezwe kutoka kifungo cha cha mwaka mmoja na kuwa kifungo cha miaka mitano.

Awali akiwasilisha maelezo ya muswada huo,Waziri wa Mawasilino,Sayansi na Teknolojia Profesa Makame Mbarawa alisema kutokana na kukua kwa matumizi ya teknolojia ya Habari na Mawasiliano kumesababisha kuwepo kwa changamoto mbalimbali ikiwemo kuibuka kwa makosa ya mtandao.

Alitaja makosa ya mtandao yaliyokithiri kwa sasa kuwa ni makosa dhidi ya faragha,usalamana upatikanaji wa taarifa za kompyuta na mifumo ya kompyuta,makosa yanayohusu maudhui,makosa dhidi ya mifumo ya kompyuta na makosa ya kawaida yanayofanywa kwa kutumia mitandao.

Profesa Mbarawa alisema kuwa takwimu kutoka jeshi la polisi zinaonesha kuwa makosa ya uhalifu wa mtandao yaliyoripotiwa na kuchunguzwa kati ya mwaka 2012 hadi Agosti mwaka jana ni 400.

Alisema katika kipindi cha mwaka 2000 hadi mwaka 2013,makosa ya uhalifu wa mitandao yalisababisha hasara ya zaidi ya shilingi bilioni 9.8 kwenye taasisi za fedha.
 


Tuesday, March 24, 2015

TEKNOLOJIA YA KUHAKIKI DAWA BANDIA AMA HALISI YABUNIWA GHANA




Wataalamu wa Teknolojia nchini Ghana wamebuni teknolojia ya kuhakiki ikiwa dawa ni bandia au ni halisi. 

Teknolojia hiyo iliyozinduliwa juma hili  na Rais wa Umoja wa wamiliki wa maduka ya dawa nchini Ghana (PSHG),James Ohemeng Kyei,inamwezesha mnunuzi kukwaruza kikaratasi kilichoko kwenye pakiti ya dawa kupata nambari maalum , kisha akatuma nambari hiyo kama ujumbe wa simu ya mkononi kwa mitandao yote ya simu nchini humo kwenda kwa namba 1393.

A prospective buyer or user is expected to scratch the seal off the secret code and text it to the short code 1393 on all networks to authenticate the drug. - See more at: http://graphic.com.gh/news/health/29319-technology-to-detect-fake-drugs-launched-in-accra.html#sthash.bEGTIGx9.dpuf
A prospective buyer or user is expected to scratch the seal off the secret code and text it to the short code 1393 on all networks to authenticate the drug. - See more at: http://graphic.com.gh/news/health/29319-technology-to-detect-fake-drugs-launched-in-accra.html#sthash.bEGTIGx9.dpuf
A prospective buyer or user is expected to scratch the seal off the secret code and text it to the short code 1393 on all networks to authenticate the drug. - See more at: http://graphic.com.gh/news/health/29319-technology-to-detect-fake-drugs-launched-in-accra.html#sthash.bEGTIGx9.dpuf
A prospective buyer or user is expected to scratch the seal off the secret code and text it to the short code 1393 on all networks to authenticate the drug. - See more at: http://graphic.com.gh/news/health/29319-technology-to-detect-fake-drugs-launched-in-accra.html#sthash.bEGTIGx9.dpuf
A prospective buyer or user is expected to scratch the seal off the secret code and text it to the short code 1393 on all networks to authenticate the drug. - See more at: http://graphic.com.gh/news/health/29319-technology-to-detect-fake-drugs-launched-in-accra.html#sthash.bEGTIGx9.dpuf
A prospective buyer or user is expected to scratch the seal off the secret code and text it to the short code 1393 on all networks to authenticate the drug. - See more at: http://graphic.com.gh/news/health/29319-technology-to-detect-fake-drugs-launched-in-accra.html#sthash.bEGTIGx9.dpuf
Kwa mujibu wa mtando wa graphic.com teknolojia hiyo iliyopewa jina la PREVENT inaweza kutoa majibu baada ya sekunde 10  ikiwa ni dawa bandia au halisi ambayo imewezeshwa kutumiwa katika mitandao ya simu za mkononi na mitandao ya kijamii.

Teknolojia hiyo ambayo imebuniwa kutokana na mkakati wa PSHG wa kuisaidia serikali kupambana na uuzwaji wa dawa bandia na zilizo chini ya kiwango itawezeshwa na Wizara ya Afya ya Ghana,Mamlaka ya Chakula na Dawa na wadau mbalimbali nchini humo.

WABUNGE WA TANZANIA WAITAKA SERIKALI KUZIBANA KAMPUNI ZA SIMU NA BENKI

Wabunge wa Tanzania wameibana serikali wakiitaka iboreshe muswada wa sheria ya mifumo ya malipo ili kuzibana kampuni za simu na mabenki,kutokana na kushamiri kwa wizi katika mifumo ya malipo kwa njia ya kielekroniki kwenye simu za kiganjani na miamala ya fedha ya benki.

Wakizungumzia bungeni jana wakati wakichangia muswada huo,wamesema kampuni za simu zinawakata wananchi fedha katika simu zao za kiganjani bila ridhaa yao na hakuna sehemu yoyote wanayoweza kufikisha malalamiko yao ili warejeshewe fedha hizo.

Katika muswada huo uliowasilishwa na Waziri wa Fedha,Saada Mkuya Salum,Serikali imependekeza kuboresha usimamizi na kuongeza udhibiti,kuimarisha mifumo ya malipo,pia kuzuia na kudhibiti athari zinazoweza kujitokeza katika mifumo hiyo na kuongeza faini kwa kampuni za simu na benki zitakazokiuka sheria na utaratibu.

Saturday, March 14, 2015

MTANZANIA ABUNI NA KUTENGENEZA PROGRAM TUMISHI YA KITABU CHA NYIMBO ZA KRISTO KATIKA VIFAA VYA APPLE






Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Union Konferensi ya Kaskazini mwa Tanzania katika Kanisa la Waadventista Wa Sabato Tanzania Gideon Msambwa ameweka historia ya kuwa mtanzania wa kwanza kubuni na kutengeneza program tumishi ya kiswahili ya kitabu cha nyimbo za Kristo zinazotumiwa na waumini wa kanisa hilo ambayo ni program pekee  ya nyimbo za injili kwa lugha hiyo kubuniwa na kutumiwa katika vifaa vya mawasiliano vya kampuni ya Apple duniani.

Gideon Msambwa ameiambia blog hii kuwa  program hiyo iliwezeshwa na Apple kupatikana katika vifaa vya mawasiliano vinavyoendeshwa na program ya endeshi ya iOS ambavyo ni iPhone,iPad na iPod na imeanza kutumika rasmi Machi 12,2015.

Tuesday, February 24, 2015

GOOGLE KUWABANA BLOGGER WANAOWEKA PICHA NA VIDEO ZA NGONO KUANZIA MACHI 23,2015

 Image result for google

Kampuni ya mtandao ya Google imetoa tangazo kwa watengenezaji wa blog  kuwa kuanzia Machi  23, 2015, hawataruhusiwa kuweka ama kutangaza picha na  video za ngono ama zenye mwelekeo huo katika blog wanazozimiliki.

Taarifa hiyo ambayo imetolewa juma hili kwa blogger inaeleza kuwa picha na video zenye mwelekeo huo hazitaruhusiwa kuonekana kama ilivyosasa kuanzia siku hiyo.

Google imeeleza mabadiliko haya ya sera zake yanawataka wote walio kinyume na sera hiyo kuhakikisha wanafanya mabadiliko kwenye aina ya habari wanazozichapicha kwenye blog zao kabla ya muda huo ambapo wanatakiwa kuondoa picha na video za ngono ama kuzifanya blog binafsi na wasipofanya hivyo google watafanya mabadiliko ama kuiondoa blog hiyo.



Saturday, February 21, 2015

UINGEREZA NA MAREKANI ZINADUKUA SIMU YAKO

 

Majasusi wa Uingereza na Marekani walikiuka sheria na kudakua kampuni inayotengeneza kifaa kinachotumika kwa simu za mkononi yaani ''Sim Card''Tovuti moja ya habari za teknolojia imeripoti huko Marekani.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo Majasusi hao waliiba mfumo na data inayowaruhusu kusikiza mawasiliano mbali na kujua alipo mmiliki wa simu hiyo lengwa.

Habari hiyo ambayo chanzo chake inasemekana kuwa ni aliyekuwa mfanyikazi wa shirika la ujasusi la Marekani CIA, Edward Snowden
inaziwezesha mashirika hayo mawili ya kijasusi kudukua mamilioni ya simu za mkononi kote duniani.

Kampuni hiyo lengwa Gemalto imesema kuwa imeshtuliwa na madai hayo na kuwa inayachunguza kwa kina.

Kampuni hiyo inahudumia mataifa 85 kupitia mashirika 40.
Aidha kampuni hiyo inahudumia makampuni 450 kote duniani.

Habari hiyo inaeleza kuwa wateja wa kampuni ya simu ya AT&T, T-Mobile, Verizon, Sprint na kampuni zingine 450 kote duniani zimeathirika.

Taarifa hiyo inasema kuwa udukuzi huo ulifanyika tangu mwaka wa 2010.

Mwandishi wa BBC aliyeko mjini Washington Marekani Naomi Grimley anasema wizi huo umewawezesha majasusi wa Marekani na Uingereza
kudukua simu za wateja mataifa ya kigeni na hata kunakili jumbe zinazotumwa kutoka kwa simu hizo bila ya kuomba ruhusa kutoka kwa serikali ama makampuni ya simu.
Chanzo:BBC

Friday, February 20, 2015

MAMILIONI YA DOLA YAIBIWA KATIKA MABENKI KUPITIA WIZI MTANDAO

 https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiwlH1_FOWfTK23Qkcj-cH5PXpc0lBlTtvhbPTNnjPWj3yHfeYc3Ps6g7YndYyH9Nz0BZnDVt6MsdbbekgUwB-PHSNBIIAICHqBuCl41GV9KC30WWWzA1tB3rpPh7yHNJCwXDLXJxTzWe7K/s1600/ATM-Theft.jpg
Baada ya kikao kilichofanyika juma liliyopita katika Chuo Kikuu cha Stafford ambapo Rais Obama wa Marekani alikutana na wafanya biashara, Wanasheria na wasimamizi washeria kujadili hali ya mtikisiko wa maswala ya usalama mitandao, Inadhihirisha wazi bado kuna safari ndefu kukabiliana na wimbi hili la uhalifu mtandao duniani kote.

Hii ni kutokana na ukweli kwamba Tishio la uhalifu mtandao na utayari wa kukabiliana nao bado kuna kutowiana ipasavyo ingawa jitihada bado ni kubwa kuweza kukabiliana na uhalifu huu unaokua kwa kasi ya pekee duniani kote.

Wakati haya yakijiri na mikakati zaidi ikiendelea ya kukabiliana na wimbi kubwa la uhalifu mtandao hivi sasa makampuni yanayojihusisha maswala ya fedha yameonekana yakiathirika zaidi na uhalifu mtandao – Hii ni kwamujibu ya ripoti maalum iliyotolewa na kampuni ya Kaspersky Lab.

Taarifa inaeleza kwamba genge la wahalifu mtandao limefanikiwa kuiba Mamilioni ya Dola za kimarekani kutoka kwenye akaunti za wateja wa mabenki 100 katika mataifa 30 kati ya mwaka 2014 na 2015.

Ripoti hiyo inaelezea mbinu mpya za wahalifu mtandao wanazotumia kudukua nambari za akaunti za wateja za siri kabla ya kuingia na kuiba pesa.

Kaspersky imesema kuwa wizi huo ulianza mwaka wa 2013 na bado unaendelea hata leo kwani mabenki yote yalioathirika hayana uwezo wa kuwazuia wezi hao.

Hadi kufikia sasa ripoti hiyo inadai kuwa takriban dola bilioni moja zimeporwa kutoka kwenye akaunti za wateza.

Genge hilo la wezi, lililoanzia shughuili yake nchini Urusi, Ukraine na pia Uchina ndilo linalolaumiwa kwa wizi huo.

Kampuni hiyo ya Kaspersky inasema inafanya juhudi za kuzima wizi huo kwa ushirikiano na polisi wa kimataifa Interpol na polisi wa bara ulya Europol.
 
Kwa mujibu wa ripoti hiyo mabenki katika mataifa 30 yakiwemo, Russia, Marekani , Ujerumani , Uchina, Ukraine na Canada yameathirika pakubwa.

Kamanda wa kikosi cha polisi wa kimataifa Interpol bwana Sanjay Virmani, amesema kuwa wezi wataendelea kutumia upungufu wa miundo msingi katika sekta ya uchumi wa mataifa husika hadi pale kutaibuka umoja wa kuzuia mapengo.

Kaspersky hata hivyo inasema kuwa genge hilo linalenga mabenki bila ya kuwaibia watu binafsi.

genge hilo kwa jina Carbanak, linatumia mbinu ya kuambukiza virusi kwenye mashine za benki ikiwemo kamera za CCTV ilikunakili kila kitu kinachoandakiwa kwenye kompyuta.

Kutokana na uweledi wao genge hilo lilituma pesa kwenye account zao huku wengine wakiamrisha mmitambo ya kutoa pesa ATM kumimina pesa bila kikomo.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo kila tukio la wizi lilihusisha takriban dola milioni kumi.

Kwa Tanzania Hali inaweza kubadilika kabisa siku za usoni kwani tayari mipango na mikakati ya dhati ya kukabiliana na uhalifu huu wa kuibia watu pesa zao kupitia ATM inaendelea kwa kasi na hatima ya kupata muarobaini stahiki unategemewa kutatua hali husika.
Na:Yusuph Kileo

 

Friday, February 13, 2015

WANATEKNOHAMA WA KANISA LA WAADVENTISTA WA SABATO WATAKIWA KUTUMIA USALAMA MTANDAO NA PROGRAM TUMISHI KATIKA UTUME


Baadhi ya Wataalamu wa Teknohama wa Taasis za Kanisa la Waadventista


Wataalamu wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano wa Kanisa la Waadventista Wa Sabato wametakiwa kutumia utaalamu wao katika masuala ya usalama kwenye mtandao,ubunifu wa program tumishi na program za komputa za utambuzi wa maeneo katika kufanikisha utume duniani.

Akitoa mada kwenye mkutano wa wataalamu wa intaneti wa kanisa la waadventista duniani (GAiN) ulioanza Februari 11 mwaka huu unaofanyika kwa njia ya mtandao na  unaoratibiwa toka Marekani yalipo makao makuu ya kanisa hilo na kuwakutanisha  washiriki toka nchi 70 duniani Mkurugenzi wa Teknohama wa Divisheni ya Marekani ya Kaskazini David Greene amewaasa wanateknohama kuhakikisha tovuti wanazosimamia na kuzitumia zina ulinzi wa kutosha.

Greene amesema kuwa asilimia  80 ya usalama wa tovuti utakuwa  umeondoka baada ya miaka miwili na hivyo kuna umuhimu wa kuhakikisha kuongeza usalama huo,na amewahimiza wataalamu wa tovuti za kanisa kuhakikisha wanapata vikoa vyenye usajili rasmi na vinavyotambuliwa kisheria.

Mkutano wa GAiN utamalizika  February 15,huku mada na mijadala mbalimbali ya teknohama  ikifanyika  mara tatu kwa siku kwa ajili ya kuwafikia washiriki walioko kwenye maeneo mbalimbali duniani ambapo unaweza kushiriki kwa kutembea katika tovuti ya gain.adventist.org na mada zilizojadiliwa zitawekwa baada ya majuma kadhaa ya mkutano huo. 

Wednesday, February 11, 2015

KANISA LA WAADVENTISTA WA SABATO RIVER SIDE ARUSHA LASHIKA NAFASI YA KWANZA BARANI AFRIKA KUTUNZA KUMBUMBUMBU ZA WASHIRIKI KITEKNOHAMA


 

Kanisa la River Side lililopo mtaa wa Njiro jijini Arusha, Tanzania, limetangazwa kuwa ni kanisa pekee barani Afrika ambalo limefikia asilimia 80 ya kutunza kumbukumbu za majina ya washiriki kwa kutumia mfumo wa kiteknolojia ya habari na mawasiliano  wa usimamizi wa makanisa ya kiadventista.



Taarifa hiyo imetolewa  na Msimamizi mkuu wa mfumo wa Usimamizi wa makanisa ya kiadventista duniani Mrs Sherri Ingram-Hudgins Februari 9, mwaka huu wakati akitoa takwimu za mfumo mpya wa kanisa la Waadventista wa kusimamia makanisa (ACMS) kwenye mkutano wa wanateknohama wa kanisa hilo uliofanyika Maryland,Silver Spring,Marekani.

                                                                                                                                           

Takwimu hizo zinaonesha kuwa  Brazil ndio inaongoza duniani kuwa na washiriki wengi waliosajiliwa, ikifuatiwa na nchi za Peru na Argentina. Barani Afrika, Tanzania ndio inaongoza ikifuatiwa na Ghana.

Mwaka 2015, mfumo huu unategemewa kuanzishwa katika nchi za Kenya, Africa Kusini na Madagascar.


Akieleza mbele ya wajumbe kutoka division 13 duniani, Sherri alionesha jinsi mfumo huu wa kusimamia makanisa ulivyoboreshwa kwenye vipengele 5 ambapo unauwezo wa kutunza kumbukumbu za vikao vya kanisa mahalia, kupiga kura za kuchagua viongozi wa kanisa, unawezesha kanisa mahalia kuufasiri kwa lugha husika ya kanisa mahalia ,kutunza kumbukumbu za fedha za kanisa na kukusanya taarifa za kila idara kisha kuzituma konferensi, unioni, divisheni na Konferensi Kuu.



Awali mfumo huu ulipoanza kutumika ulikuwa na uwezo wa kutunza majina ya washiriki na kuhamisha jina la mshiriki toka kanisa moja kwenda jingine.



 Sherri ametoa rai kwa wajumbe wote kuusimamia mfumo huu kwa makanisa yote makubwa yaliyopo mijini kisha kwenda makanisa yaliyopo vijijini.



Divisheni ya  Afrika mashariki na kati iliwakilishwa na wajumbe watatu, Nicolas Washington (Kenya), Kelvin Opiyo (Kenya) na Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Unioni Konferensi ya Kaskazini mwa Tanzania  Gideon Msambwa.








Popular Posts

Labels