Watu wa TEKINOHAMA haswa wanaohusika na masuala ya
Ufundi au kusimamia masuala ya usalama huwa wanaulizwa maswali 2 sana .
Hivi naweza kutumia Kompyuta yangu bila kufanya
updates ?
Naweza kupata Antivirus ambayo hainiulizi/Haitaki
updates ?
UPDATES KATIKA KOMPYUTA/SIMU NI NINI ?
Updates ni zile programu zinazoingizwa au ingia
kwenye kompyuta yako au simu yako kwa ajili ya kuboresha programu za kompyuta
yako au simu yako .
Kama ulinunua kompyuta ikawa na programu
inayoitwa UJAMAA 1.2 , Baada ya mwaka au miezi kukiwa na UJAMAA 1.3 basi hii
ndio update ya toleo 1.2 , update hii unaweza kuipata bure au kulipia kulingana
na Kampuni yenyewe lakini update nyingi ni bure .
Kuweka updates ni sawa na mwanadamu anavyokula
vyakula ili aweze apate afya aweze kuendelea kuishi na kufanya shuguli zake
mbalimbali za kujipatia kipato .
UPDATES ZINAPATIKANAJE ?
Kuna njia 2 za kupate updates :-
1 - Kwa Njia ya Mtandao( Moja Kwa moja ) - Hii
inatumika kama kifaa chako kimeunganishwa kwenye mtandao na umekiruhusu kupokea
updates kwa njia za mtandao , mara nyingi updates hizi kufanya moja kwa moja
ikimaliza inaingiza yenyewe kwa kuinstall .
Njia hii inakuunganisha moja kwa moja na
mtengenezaji wa programu husika .
2 - Kwa Njia ya Download - Hii ni kwa watu
wasiokuwa na huduma ya mtandao lakini wanataka kupata update fulani au wakati
mwingine mtu shirika lina kompyuta 200 na zote wanataka kuweka update moja
lakini bila kuunganisha kwenye mtandao , unachofanya ni kwenda kwenye tovuti
husika ya programu utapata update hiyo na utapata maelezo ya jinsi ya kuitumia
.
Hii unaweza kufanya hata kwenye internet cafe
yenye kompyuta nyingi au ofisi zenye kompyuta nyingi kwa kudownload file moja
ambalo utaweza kutumia kwenye zote .
3 - PATCH - Hizi ni updates pia lakini lengo lake
haswa ni kurekebisha kosa ambalo lilifanyika wakati wa utengenezaji wa programu
hisika , hii nayo ni bure kwa programu nyingi .
4- Plugins - Hivi ni viongo/Viongezeo katika
programu mbalimbali za kompyuta au simu kwa ajili ya kuboresha utendaji wa kitu
fulani , hizi zinatumika zaidi kwa watu wa uhandisi na uchoraji au uchanganyaji
picha , utakuta kuna kitu anahitaji kufanya kutumia programu yake badala ya
kuwa na programu fulani kubwa basi ataweza kupata Plugin moja ndogo ya kufanya
kitu hicho specific .
Tafadhali usitumie Plugin kama hujui unachofanya
ni rahisi kukuharibia mambo yako
UPDATE HUFANYIKA BAADA YA MUDA GANI ?
Kila kampuni inayotengeneza bidhaa ina sera zake
kuhusu updates lakini kila zinapotoka huwa kwenye mtandao wa kampuni husika
kama ulikosa unaweza kutafuta ukapata lakini kama umenunua kompyuta leo au simu
ukijiunga tu utalazimika kupata updates zote zilizopita mpaka leo vile vile kwa
antivirus na Simu .
Mara nyingi
Zaidi unaweza kufuatilia vyombo vya habari na
kusoma kwenye mitandao kama kuna updates zozote kuhusu programu husika .
MUHIMU
Kompyuta nyingi zenye programu ambazo sio halali
wanaogopa kufanya updates kwa hofu kwamba atakamatwa au itafanya hili na lile ,
bora upate ujumbe kwamba unatumia programu bandia na uendelee kuitumia kuliko
kutokufanya updates kabisa kwa sababu utakuwa unabadilisha mafundi kila siku na
itakuwa rahisi kwa kifaa chako kushambuliwa au watu kutumia kama mlango wa
kufanya mashambulizi kwenye mitandao mingine .
Kama mko maofisini au majumbani ni vizuri muwe na
sheria kali kuhusu kufanya updates za vitu mbalimbali vinavyotumia programu
maana itakuwa nafuu na ulinzi tosha kwako na kwa mali zako .
Kuna watu wanaibiwa data zako kwenye kompyuta kwa
sababu tu hakufanya updates kwenye antivirus yake matokeo yake alipoingia
kwenye kompyuta spyware wakaingia wakaweza kutumiwa kuhamisha taarifa au mambo
mengine .
YONA F MARO
0786 806028