Nimekamilisha
vikao vya usalama mitandao vilivyofanyikia jijini Nairobi kufuatia
mualiko maalum nilioupata. Katika vikao hivyo niliwasilisha mada mbili
(ya kwanza ikiwa ni namna ya kukabiliana na uhalifu mtandao na mada ya
pili ikiwa ni namna ya uchunguzi wa makosa ya digitali kitaalam) katika
mada hizo mbili ambazo zilipokelewa vizuri na kupelekea mijadala ya
kipekee kuna mengi nikajifunza kutoka kwa washiriki. Aidha, nilishiriki
mijadala duara iliyojikita katika changamototo mbali mbali za uhalifu
mitandao na kuiangazia sharia mtandao ya nchi ya Kenya.
Kenya
ni miongoni mwa nchi tatu barani afrika ambazo zimeorodheshwa kuwa na
uhalifu mkubwa sana wa kimtandao nyingine ni Nigeria pamoja na Afrika ya Kusini. Tukijadili takwimu za kutisha duniani kote, tulishuka na
kuangazia bara la Afrika na baadaye Afrika Mashariki na hatimae kujikita
na twakwimu za nchi ya Kenya.
Kwa
upande wa Kenya kwa mujibu wa takwimu zilizowasilishwa katika mkutano,
hadi kufikia Mwezi wa saba mwaka huu (2015) kuna simu 34.8 Milioni
huku watumiaji wakiwa ni 26.0 Milioni. Aidha, matumizi ya intaneti ni
29.1 milioni ambayo ni sawa na 65% “penetration”. Takwimu hizo
zinasindikizwa na upotevu wa dola za kimarekani 20 milioni ($20 Mil)
kila mwaka kutokana na uhalifu mtandao.
Palizungumzwa
matukio ya kudukuliwa kwa tovuti nchini humo ambapo, tovuti za serikali
103 ziliathiriwa mwaka 2013, na 3 kwa mwaka wa 2014 huku twitter ya
serikali mwaka jana (2014) ikiwa ni miongoni mwa zilizo dukuliwa na
kutumiwa vibaya. Nilihoji tofauti kubwa ya udukuzi wa tovuti na
kujulishwa baada ya tukio la aina yake la mwaka 2013 serikali iliamua
kuzifunga tuvuti zake nyingi hasa zile zilizo onekana hazina umuhimu
sana kua hewani kitu ambacho kilichangia kupunguza namba kubwa ya
udukuzi kwa mwaka 2014.
Kwa
upande wa pesa zinazopotea kwa nyia ya simu – Miamala inayofanywa kwa
njia ya simu ni asilimia kumi (10%) ya fedha za miamala yote kila mwezi
huku idadi hiyo kuonekana kushtusha wengi.
Ikumbukwe
nchi ya Kenya, matumizi mabaya ya mitandao yalisababisha kuchochea na
kutokea vurugu zilizosababisha matatizo makubwa sana kipindi cha
uchaguzi kilichopita ambapo kwa mujibu wa mchambuzi mmoja wa maswala ya
uchanguzi alichapisha andiko na kueleza mitandao ilikua chanzo kikubwa
cha kueneza chuki na fujo kipindi cha uchaguzi uliopita.
Yote
hayo – Takwimu zote hizi kwa nchi ya Kenya zimesababishwa na jambo moja
zuri sana ambapo ni kua na uwazi wa takwimu na taarifa za kihalifu
mtandao ambapo kwa Afrika imekua ni nchi pekee iliyofanikisha swala
hili. Itakumbukwa nilitoa pongezi kwa nchi hiyo baada ya ku ainisha
takwimu zake kwa mara ya kwanza mwaka jana (2014) na kufanya iwe ya
kwanza Afrika katika hili.
Kilicho
nifurahisha zaidi ni hatua taifa hilo limechukua kukabiliana na uhalifu
mtandao. Tayari nchi hiyo ina “National cybersecurity master plan” na
sheria mtandao ambapo kosa la udukuzi adhabu ni miaka kumi (10) jela,
faini ya KSH 10,000 au vyote kwa pamoja. Pia ina strategy ya maswala ya
usalama mitandao na kupitia mamlaka ya TEHAMA “ICT Commission” wamesha
zindua andiko linalotoa muongozo wa kuwalinda watoto katika mitandao.
Hayo
ni uchache katika mengi ambayo tayari taifa limeweka katika mikakati
yake. Zaidi ni mikakati ya kukuza uelewa na ujuzi kwa watu wake ili
kuweza kuendelea kutumia vizuri mitandao pamoja na namna ya kukabiliana
na uhalifu mtandao.Aidha, Mpango wa serikali kuimarisha ushirikiano
ambapo CERT – KENYA inajumuisha vyombo vyote vya ulinzi na usalama huku
mashirika binafsi yakiwa na nafasi kubwa kuisaidia ili kukabiliana na
uhalifu mtandao. Mfano wa Hili ni mshiriki kutoka Microsoft alipo tolea
ufafanuzi kampuni hiyo inavyo fanya kazi karibu na serikali ya kenya
kukabiliana na uhalifu mtandao nchini humo kupitia CERT –KENYA.
Kilicho
nipa faraja kubwa ni kauli ya pamoja kua Kenya imefanya mengi lakini
pakakubalika kua kuna mengi bado yakufanyia kazi ili kuweza kupiga hatua
zaidi katika maswala ya usalama mitandao nchini humo. Ni marachache
sana mataifa yanakiri kua bado safari ni ndefu ili kufikia malengo.
Pamoja na hatua kubwa nilizo ziona katika nchi hiyo lakini bado walikiri
kuna safari ya kupiga ili kusonga mbele zaidi.
Tulipata
kuangazia aina za uhalifu na namna zinavyofanyika kwa nchi ya kenya –
hakika aina hizi hapa kwetu pia ziko njiani na hofu yangu kubwa ni kwa
kiasi gani tutakua tumejiandaa? Kujua tatizo nihatua za awali za utatuzi
na wengine wakinyolewa ni vizuri tukatia nywele maji.
Kwa ufupi mambo yakufanyiwa kazi ambayo bado ni changamoto kwa mataifa yote yaliyoweza kujadiliwa ni pamoja na:-
Bado
kumekua na dhana kua swala la usalama mitandao ni la kundi fulani (
wana TEHAMA – waliojikita katika maswla ya usalama mitandao) Hili sasa
linatakiwa libadilike na katika kila kampuni au serikali lazima swala
hili lianzie katika ngazi ya juu kushuka hadi ngazi ya mmoja mmoja (Kila
mtu)
Bado
udukuzi na uhalifu mtandao kwa ujumla umeendelea kushika kasi huku
ugunduzi wa tukio kutokea kuchukua hadi siku 200 kwa wastani baada ya
tukio ambapo tumekubaliana kimsingi hii ni namba kubwa sana na kunakila
sababu ya kushusha namba hizi – pia kuwe na njia za kuzuia tatizo kabla
halijatokea ambazo ni madhubuti kwa kufanyia kazi ushauri unaotolewa
wataalam.
Uhalifu
wa ndani (Insider threats) bado ni changamoto kubwa sana katika anga ya
dunia na imeonekana kusahauliwa kabisa huku jitihada za dhati zikianza
kuonekana kukuza uelewa kwenye hili na sasa tayari “Mr. Robot” tamthilia
mpya ya kukuza uelewa wa maswala ya usalama mitandao imejikita kwenye
hili.
Uhaba
wa wataalam katika maswala ya usalama mitandao ni la kuchukuliwa hatua
za haraka kwa kuhimiza mitaala ya usalama mitandao kuingizwa vyuoni huku
wataalam wanaopatikana kutumika vizuri – Wenye ujuzi watumike mahali
husika kwani imeonekana bado kuna changaoto ya kutotumiwa vizuri wataalm
wa maswala haya inaypelekea uhalikfu kukua kwa kasi kila kukicha. Hili
limeonekana zaidi barani Afrika na mataifa kadhaa wamesha anza
kulifanyia kazi ili kuweka mabo sawa.
Sheria
mitandao kutumiwa ipasavyo lakini pia iambatane na kua na waelewa wa
uchunguzi wa makosa haya kwa kuzingatia maadili na taratibu za kitaalm
zilizo sahihi na kuhakiki uelewa unasambazwa kwa watu ili kuepusha wimbi
kubwa la wahalifu mtandao wanao fanya uhalifu huu bila kujua kuingia
matatani – Imeonekana bado kuna ugumu mkubwa wa kesi za uhalifu mtandao
kuvuka mahakamani na watuhumiwa kuwajibishwa kutokana na udhaifu mkubwa
kwa mataifa ya Afrika mashariki walionao katika kufata taratibu za
kuwasilisha kesi hizi ipasavyo mahakamani (Ujuzi bado Uko chini sana).
Ushirikiano
wa ndani ya mataifa pamoja na kuvuka mipaka bado ni changamoto inayo
onekana kuzikumba Nchi nyingi hasa barani Afrika huku Kenya ikiwa
imeliona hili na imepiga hatua nzuri kwa ndani ila bado wanakiri kuvuka
mipaka bado ni changamoto kutokana na utayari wa mataifa mengine katika
hili.
Hayo
ni kwauchache tu kwani mengi sana yamejadiliwa na nategemea kutumia
muda wangu kadhaa kuwasilisha kidogo kidogo ili tuweze kuendelea
kujifunza zaidi kupitia vyanzo mbali mbali vya habari.
NA:Yusuph Kileo