Wednesday, August 28, 2013

MAARIFA:NAMNA YA KUUNGANISHA TWITTER NA FACEBOOK YAKO

Tuesday, August 27, 2013

ANGALIA VIDEO YA TIM RAINS WA MICROSOFT AKITOA TAHADHARI KWA WATUMIAJI WA WINDOW XP

TAHADHARI KWA WATUMIAJI WA KOMPYUTA ZENYE WINDOW XP

 

Watumiaji wa  programu ya komputa iitwayo Window XP wamepewa tahadhari na kampuni ya Microsoft ambayo ndiyo iliyotengeneza program hiyo kuwa hapatakuwa na matoleo mapya (updates) zaidi kuhusu Window XP Service Pack 3 baada ya mwezi wa nane mwaka 2014.

Akizungumza na wataalamu mbalimbali wa masuala ya ulinzi mtandao Agosti 16,mwaka huu Mkurugenzi wa kitengo kijulikanacho kwa jina la Microsoft Trustworthy Computing,Tim Rains anasema kuwa ingawa Window XP wakati inatolewa ilikuwa na ubora huku ikipendwa na watumiaji wengi wa kompyuta,kwa sasa imeonekana kuwa dhaifu kutokana na kuongezeka kwa uhalifu wa kimtandao.

Amesema kumekuwepo na wimbi kubwa la wahalifu wanaotumia mianya mbalimbali kuingilia kompyuta za wateja wanaotumia Window XP na kuongeza kuwa hali hiyo ya uhalifu itaendelea hasa kwa wale wataoendelea kutumia aina hiyo ya window.

Rains amesema wanaendelea kutafuta ufumbuzi pale itakapobainika wahalifu wameweza kupenya katika kompyuta za wateja wao wanaotumia aina mpya za window ambapo kwa sasa kupitia kituo cha kuangalia usalama wa kompyuta cha kampuni hiyo kinaendelea kutoa maelezo ya jinsi ya kuwalinda wateja wao.

Amesema kampuni ambazo bado zitakuwa zinatumia Window XP,zitasababisha wahalifu kutafuta mapungufu katika window hiyo na kuleta athari ambapo kampuni ya Microsoft haitakuwa na msaada ama wa bure au wa kulipia dhidi ya hali hiyo,kwani itakuwa imeshaacha kutoa msaada wa kuhusu Window XP

Chanzo:Gazeti la Mwananchi


Sunday, August 25, 2013

NAMNA YA KUWEKA PICHA NA VIDEO KWENYE FACEBOOK KWA KUTUMIA IPHONE

Saturday, August 24, 2013

WASHA YA TEKNOHAMA NA VYOMBO VYA HABARI YAFANYIKA COSTECH JIJINI DAR ES SALAAM

Photo: Audience at the Mass Media and ICT Workshop..
Mwezeshaji wa kipindi cha Maisha na Teknohama cha Morning Star Radio,Johnson Mziray akichangia jambo kwenye warsha hiyo,pembeni yake mwenye miwani ni Mtangazaji wa Kipindi cha Maisha na Teknohama,Mtangazaji Maduhu
Photo: ICT and Mass Media workshop at the Buni Space Day 3 of the Workshop Sama Jahanpour instructing audience on proper filming techniques...
Sama toka Kampuni ya E Media akifundisha jinsi ya kupiga picha za Video

FACEBOOK YAWEKA UWEZO WA KU EMBED MAPACHIKO MBALIMBALI




Saturday, August 17, 2013

TWITTER YAONESHA KUWAVUTIA VIJANA

 


Facebook ni mtandao wa kijamii ambao unaendelea kuongoza kwa kuwa na watumiaji wengi duniani hata hiyo utafiti unaonesha kuwa vijana sasa wanahama kutoka mtandao huo na kujiunga na mtandao wa kijamii wa Twitter .

Kuna mamia ya watu ambao haiwezi kupita siku bila kutembelea facebook,lakini sasa inaonekana twitter ikipata watumiaji kutoka facebook hasa ikiwavutia zaidi vijana ambao wengi wao wanatumia facebook.

Twitter inaruhusu mtumiaji kufahamu kile ambacho hadhira katika mtandao huo inakizunguzia na kuruhusu kufahamu kinachoendelea na kumpatia anachokihitaji.

Mtandao wa solidtechreview umeeleza kuwa mwishoni mwa mwaka  2012, inakadiliwa kuwa asilimia  21 ya watumiaji wa intaneti duniani walikuwa walikuwa wamejiunga na twitter na kila mwezi kulikuwa na watu milioni  288 waliokuwa wanajiunga na mtandao huo.

Utafiti unaonesha kuwa facebook ina asilimia 34 ya watumiaji ambao umri wao ni chini ya miaka  30 na asilimia 45 zaidi ya miaka  45. Wakati ni asilimia 30 tu ya watumiaji wa twitter ambao wanaumri zaidi ya miaka  45.

Twitter inaelezwa kuwa ni rahisi kutumiwa na watu ambao hawana muda mwingi wa kukaa na kuandika mambo mengi kwenye mitandao ya kijamii,rahisi kukuunganisha na watu wengi maarufu duniani, rahisi kuwasilianana kubadilishana mawazo mbalimbali kuliko facebook.

GOOGLE YAANZISHA HUDUMA YA KUKUPATIA RATIBA YA USAFIRI WA NDEGE


Kampuni ya Google kupitia huduma yake ya kutafuta jambo sasa imeanzisha utaratibu wa kutoa majibu ya moja kwa moja kwa maswali kuhusu ratiba ya ndege unayotaka kuitumia kwa kusafiri.

Huduma hiyo ambayo mtumiaji anaweza kuuliza swali na akapata jibu kwa mfano Je ndege yangu ni ya hadhi gani moja moja google itakuonyesha juu ya ukurasa ndege unayohitaji kusafiri nayo.
  Google inaeleza kuwa kipengele hiki kinatoa majibu ya haraka kwa mtumiaji kuliko kusoma  ujumbe wa barua pepe ama kalenda.

Huduma hii ilianza huko Marekani kwa ajili ya kuweka booking ya ndege ama hoteli kwa kutumia sauti ama kwa kuandika.Hata hivyokipengele hiki kimeelezwa kuwa si vyema kukitumia kwa watu ambao wanahitaji faragha katika mambo yao.

Friday, August 16, 2013

JINSI YA KUONDOA UJUMBE USIOKUHUSU KWENYE WASIFU WAKO WA FACEBOOOK


Je, Unasumbuliwa na MESSAGE usizozitaka kuziona, hususani toka kwa watu usiowajua ?

Nenda sehemu ya Settings, kisha chagua kuwa Unataka kupokea message za Walio FRIENDS zako tuu.

Message nyingine zote zitaingia kama SPAM, hivyo hazitokuja INBOX yako. Zitapelekwa kwa Folder maalum la SPAM, ni mpaka ulitafute hilo folder la Spam ndio utaziona message nyingine kama hizo za kukusumbua.


 
Kama unataka kuangalia Messages ambazo zimeingizwa kwenye folder la SPAM, unachotakiwa kufanya ni kuenda sehemu ya MESSAGE (Kushoto mwa profile yako),  kisha bofya hapo juu kama unavyoona kwenye kielelezo hapa chini 

Unaweza kufanya hivi, kwani pengine kuna mtu muhimu ambaye si rafiki yako amekutumia ujumbe ambao ungependa kuusoma. -


 


chanzo:Mbuke blog

TAHADHARI:USITUMIE SIMU YAKO IKIWA KWENYE CHARGER


Apple Opens Store In Berlin

Wengi tuna tabia ya kutumia simu zetu zinapokuwa kwenye charger, hasa tunapopigiwa simu wakati betri imekaribia kuisha au tunapolazimika kupiga simu muda wakati charge haitoshi. Hii sio tabia nzuri na imethibitika hivyo baada ya msichana raia wa China kufa baada ya kupigwa shoti wakati akitumia simu yake.

Ma Ailun, mdada mwenye miaka 23 alikuwa akitumia iPhone5, na mara baada ya kifo chake dada yake aliamua kuwapa onyo watumiaji wengine wa iPhone kuhusu hilo tatizo kupitia weibo ambayo ndio kama twitter ya China na baada ya habari kusambaa Apple ambao ndio watengenezaji wa iPhone walitoa pole kwa familia na kuahidi kufuatilia tatizo lilikuwa nini, mwanzoni msemaji wa Apple alisema alisema inawezekana charger iliyotumika ilikuwa feki lakini ikathibitika kuwa simu ilinunuliwa kwa wakala aliethibitishwa na ilikuwa haina muda mrefu.


Chanzo:tanganyikan blog

Friday, August 9, 2013

SONY NA PANASONIC WAUNGANA KUTEGENEZA CD YENYE UWEZO WA HIFADHI YA GB 300.



 
 Na Brown Nyanza
Kampuni mbili maarufu duniani SONY Corporation na PANASONIC Corporation kupitia tovuti zao wametangaza kuwa wameingia katika makubaliano ya kutengeneza CD (compact disk/Optical Disc) zenye uwezo wa kuhifadhi GB 300 za data ifikapo mwaka 2015.
Kampuni zote mbili zimeongeza kwa kusema kwamba hii itakuwa ni mara ya kwanza katika historia ya CD duniani. Katika miaka ya karibuni CD zimesifika kuwa na uwezo wa kuhifadhi data kwa ulizi wa hali ya juu, hii ni kutokana uwezo mkubwa wa kuhimili  mabadiliko mbalimbali ya kimazingira, vumbi, joto, na pia CD inaweza kuhifadhi  data kwa kipindi kirefu sana iwapo ikihifadhiwa sehemu nzuri.
Kampuni hizo zimekaririwa kwa kusema kwamba wateja wao hasa wamelengwa kuwa makampuni makubwa ya kutengeneza filamu nchini marekani na duniani kote, Pia makampuni makubwa ya utangazaji, Pia (Cloud based Data centes) zinatarajiwa kuwa ndio soko kubwa katika teknolojia hii mpya ya kuhifadhi data. Katika miaka ya karibuni Kampuni ya SONY ilitengeneza CD zenye zinazotumia teknolojia ya BluRay zenye uwezo wa kutunza data kwa kiasi cha GB 25 hadi GB 50 katika CD moja tu.

HUAWEI YAIPATIA NM-AIST DOLA 30,000 ZA MAREKANI

Kampuni ya Huawei ya Tanzania imesaini makubaliano na Chuo cha Sayansi na Teknolojia cha Nelson Mandela (NM-AIST) kuhusu kukijengea chuo hicho uwezo zaidi wa kufanya tafiti katika masuala ya teknolojia ya habari na mawasiliano (TEKNOHAMA).

Katika makubaliano hayo,kampuni itakuwa ikitoa Dola 30,000 za Marekani kila mwaka ndani ya miaka mitatu,ili kusaidia chuo nyanja hiyo na hasa kwa wanachuo wa ngazi za uzamili na uzamifu.

Balozi wa China nchini Tanzania,Lu Youqing amesema moja ya mahitaji ya vyuo vinavyofanya tafiti duniani ni kupata vitendea kazi na wataalamu waliobobea.

Wednesday, August 7, 2013

MWENYEKITI WA MAKAMPUNI YA IPP,DR REGINALD MENGI AWAPONGEZA WASHINDI WA TWEET YA JULAI 2013




  
Kupitia Mtandao wa Twitter Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP,
Dr Reginald Mengi  amewapongeza washindi wa tweet bora ya julai 2013 ambao aliwakabidhi zawadi  ofisi kwake jijini Dar es salaam jana ambapo miongoni mwa waliopata zawadi ni mshindi wa tatu ambaye ni mtangazaji wa kipindi cha Maisha na Teknohama cha Morning Star Radio ambaye alijibu swali lililoulizwa na Dr Mengi kupitia twitter ambalo liliuliza "Kijana asiyekuwa na ajira wala fedha anawezaje kuanza kujijenga kiuchumi?Ambapo jumla ya tweet 1225 zilizojibu swali hilo mwezi julai.

Dr Mengi amekuwa akiuliza swali la uchumi kupitia twitter toka mwezi mei mwaka 2013 na kuchagua tweet tatu zinazojibu swali na kutoa zawadi ikiwa ni njia ya kuibua mawazo mapya katika kuondoa umaskini nchini Tanzania

Swali la tweet bora Agusti 2013 ni: Je, Nini kifanywe kuzalisha ajira nyingi kwa vijana hapa Tanzania?

Popular Posts

Labels